Home → simulizi
→ simulizi ya maisha. KOSA
sehemu ya tano
ILIPOISHIA
Utendaji wangu wa kazi katika siku hiyo ulikuwa tofauti sana kana kwamba nilikuwa najua kunakitu ambacho kinatokea nyumbani wakati ule. Maana hata niliwahi kutoka kazini pasipo kawaida yangu. Ndugu msikilizaji, ni kama vile nilikuwa nimeota maana kile nilichokuwa na kiona kwenye macho yangu punde nilipokuwa. Na tazama na nyumba.
Nikusihi ndugu msikilizaji, matizo ni jambo ambalo halina taarifa, hivyo ni vyema ukayakupokea katika namna ambayo itakufanya ujue ni njia gani utayakabili. Na hiii ilikuwa sehemu ya nne ya simulizi hii ya maisha.
.
NA HII NI SEHEMU YA TANO
Umati wa watu walikuwa wamejazana na ilipo nyumba yetu na kadiri nilivyokuwa nikipiga hatua nilikuwa nikikaribishwa vizuri na umati ule, huku nikipambana na sauti Kutokea kwenye umati ule kutokana na kile walichokuwa wakishuhudia. Kiukweli ndugu msikilizaji nilishanganyikwa sana.
Hofu iliongezeka kweli wakati nikipokea taarifa kwenye ngoma za masikio yangu. Kwa mara ya kwanza nilihisi mkojo ukitaka kunitoka pasipo mategemeo mbele ya umati ule, Mungu tu kwa siku ile pia alitenda miujiza yake maana jirani mmoja ambaye sikumbuki kama hapo awali niliwahi kuonana nae au la, alinishika mkono na kunisogeza nje kidogo ya umati ule na kinisihi sana nikubaliane na hali ambayo punde ningekwenda kuiyona. Mpaka dakika hiyo sikuwa najua kama kuna jambo gani ambalo linaendelea pale nyumbani. Maneno yake yalikuwa natija sana kwangu, maana yalinipa uelekeo, wa mimi kufahamu kile kilichokuwa kinaendelea.
HUwezi amini ndugu msikilizaji wa simulizi hii ya maisha ninachosema hapa ni ukweli tena ukweli mtupu, nimewahi kuona watu wakipigwa tena vipigo viisivyokuwa na makadilio maalumu, lakini kwa upande wa shemeji safari hii alikuwa amevuka mpaka kabisa. Sura yangu uliweza kuona vyema hali ya dada, ambaye alikuwa amezingiliwa na watu ambao walikuwa wakijitahidi kuokoa uhai wa dada, macho yangu yaliweza kushudia dada akipumua kwa shida sana huku akiwa ajitambui, pembeni ya watu wale pia nilimuoa mdada moja akiwa ameshika mpwa wangu Nasri.
Sikumbuki akili gani niliyokuwa nimeitumia pale kufanikisha kumpeleka dada hospitali ninachokumbuka kuna baadhi ya majirani walinisaidia sana. Ni kama Mungu vile alikuwa upande wangu siku hiyo, nilikuwa na akiba ya pesa katika chumba changu, ile ilinisaidia sana la sivyo ningedhalilika mie.
Baada ya kumfikisha hospitali dada, sikuwa na jinsi daktari alinishauri ni rudi nyumbani baada ya kusubiri sana ilikufahamu hatima yake nilitia mkazo lakini sikuwa na jinsi niliamua kutoka pale nikiwa na mpwa wangu mgongoni, mtoto nae alikuwa analia sana, kilio chake nacho kikawa kinanizidi kuniweka katika hali ya tofauti. Ikiwa imetimu saa nne usiku nilikuwa nje ya geti ya hospitali ile.
Sikuweza kuvumilia usiku ule ule nilienda kutoa taarifa katika kituo cha polisi. Baada ya kutoa taarifa polisi nilirudi nyumbani nikiwa na mpwa wangu, safari hii akiwa amelala.
Usiku wa siku hiyo nao hakuwa mfupi, nililala kwa manyanyaso sana. Asubuhi ilipowadia ya siku nyingine nikawa mgeni wa kwanza hospitali pale. Hatimaye niliweza kuona na Daktari alinieleza hali ya dada, kabla ya kuona nae. Kumbe ilimchukua masaa sita ndipo alipoweza kuzinduka.
Niliona na dada hata hivyo alikuwa akiongea kwa shida, na alinieleza ya kuwa kifua kilikuwa kina mbana sana. Ni kweli kilikuwa kinambana maana kama vile alivyokuwa akiongea nami ndio alikuwa akizidi kuumia. Aliniuliza kuhusu Nasri, hapo uvumilivu ukanishinda. Ndugu msikilizaji sikuweza kuizua hali ile nilijikuta machozi yakinitoka, ijapokuwa chozi la mwanaume kutoka ni kazi, lakini siku hiyo ni kama vile ilikuwa tembo kumuua sisimizi.
Hatakama waswahili wanasema mtoto ni baraka kutoka kwa Mungu, kwa upande wangu nilijua wazi ile haikuwa baraka bali ilikuwa kama mtihani katika ndoa ya dada. Sababu ya yote yale ni yule mtoto, lakini nawezaje kumchukia malaika wa Mungu ni sawa na bure tu. Nililia kimya kimya, japo niliweza kumjibu dada ya kuwa mtoto nilikuwa nimepatia yule dada ambaye alikuwa bega kwa bega na mie katika matatizo yale kabla sijatoka nyumbani kufika pale, alinielewa.
_________
Muda wa kukaa na wagonjwa uliisha, nami nikabidi nirejee nyumbani, hivyo mchezo ukawa huo huo kwa siku kama nne hivi hatimaye dada aliruhusiwa kurudi nyumbani, baada ya kuonekana walau afya yake imeweza kutengemaa. Wakati huo shemeji akuweza kuonekana nadhani alikuwa ameenda mahali kujificha maana nilifanya juhudi za kumsaka kwa uchungu sana. Sikufanikiwa kumpata, katika kila siku ieandayo duniani.
Mpaka aliporejea nyumbani mwenyewe, baada ya wiki mbili kupita, pasipo mimi mwenyewe mategemeo katika siku ambayo nilikuwa nimerejea mapema sana nyumbani ndio nilipokutana na ujio wa shemeji akiwa sebuleni na dada, tena akiwa wanacheka, kama vile kulikuwa hakuna jambo baya lilikuwa limetokea katika siku za karibuni.
Ndugu msikilizaji naomba ni kiri kwako ni kweli mapenzi ni upofu, tena wahali ya juu. Kamwe nakushauri tu usishadadie ugomvi wa mke na mume. Maana kile nilichokuwa na kiona kwenye macho yangu hakikuwa ndoto bali ilikuwa ni ukweli mtupu. Ni shemeji kabisa akiwa dada wakifurahi kupita maelezo, pembeni yao wakiwa wamepambwa na sauti ya mtoto mdogo ambaye kama alikuwa akitaka kusema jambo lakini lilikuwa likishindwa kutoka.
Nilijiweka katika mtazamo wa kukubali matokeo, pasipo ulazimu. Ilinibidi nitoe salamu yangu kwa shemeji kisha sikuchelewa kujitoma ndani. Dada aliweza kuibaini hali yangu nakumbuka siku iliyofatia mapema asubuhi dada aliinita kusema nami, maneno ambayo sikuona yanatija kabisa kwa upande wangu. Ndio tulikuwa tunashida zilizopitiliza lakini yule mwanaume katika mtazamo wangu wa kawaida niliona uwenda ipo siku isiyokuwa na jina, hata angeweza kulibadilisha jina la dada yangu na kuwa marehemu kutokana na vipigo vyake na hilo kwake asingejali kabisa.
_______
Baada ya mazungumzo yale siku ziliyoyoma wakati huo hapakuwa na dalili yoyote iliyoonesha yule mtoto angeweza kuongea nami kwa upande wangu sikutaka kujishungulisha sana na mambo ambayo niliona kama hayanihusu vile, katika siku hizo kuna mambo kama ya siri yalikuwa yakitendeka mule ndani lakini mimi sikuwa nikishirikishwa, nilizisikia tu habari juu juu ya kuwa shemeji na dada walikuwa wakiangahika kwa waganga wa jadi juu ya tatizo la mtoto. Kwa vile walikuwa wakinificha mimi sikushunghulika nao, niliendelea kupiga kazi huku nikiomba Mungu aweze kufungua milango yule mtoto aweze kuongea, kwa maana chanzo cha migogoro mule ndani ni yule mtoto.
Siku nazo ziliendea kwenda mambo yalikuwa yale yale. Jioni moja tulipokea ugeni nyumbani pale. Mama yake shemeji akiwa na dada yake walikuwa wamekuja kutokea kijijini kwao. Dada alikaribisha vyema ugeni ule, nyumba nayo ikaonekana kuchangamka zaidi tofauti hata na awali.
Baada ya ugeni ule mambo yalianza kubadilika nilianza kusikia minong’ono kuhusu hali ya mtoto, mara chache nikiwa narudi kazini nilikuwa nikikaribishwa na habari zile, habari ambazo zilianza kubadilisha hali ya amani mule ndani na hata muonekano wa shemeji ambaye alikuwa ametulia kweli. Ndugu asikuambie mtu maneno ni mabaya sana. Hatimaye shemeji alianza kuwaka kama pili pili, akisaidiwa na ndugu zake, yule mama yake shemeji alikuwa muongeaji mkubwa kila siku katika vikao ambavyo nilikuwa navifumania nikiwa natoka kazini. Vikao ambavyo sikuwahi kualikwa ndugu msikilizaji.
___________
Amini usiami, katika siku moja, nadhani sitoisahau ilikuwa jioni moja, niliporudi kutokea kazini nikiwa nimechoka kutokana na kazi nyingi zilizonikabili kazini. Nilikaribishwa na kikao kizito, kikao ambacho hakika sitokuja kukisahau, maana.
Ndugu, matatizo tumeumbiwa binadamu ni kuombe tu usiwe mwepesi wa kukata tamaa, pambana.
JE NINI KITAENDELEA?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: