_________ Simulizi ya maisha. KOSA. Sehemu ya sita. Ilipoishia. Amini usiami, katika siku moja, nadhani sitoisahau ilikuwa jioni moja, niliporudi kutokea kazini nikiwa nimechoka kutokana na kazi nyingi zilizonikabili kazini. Nilikaribishwa na kikao kizito, kikao ambacho hakika sitokuja kukisahau, maana. Ndugu, matatizo tumeumbiwa binadamu ni kuombe tu usiwe mwepesi wa kukata tamaa, pambana. NA HII SEHEMU YA SITA. Kili badilisha muelekeo wa maisha yangu na ndoa ya dada kwa ujumla, kikao kilikuwa kirefu, maneno yangu ya busara hayakutosha kuikoa ndoa ya dada, shemeji alikuwa amechachama kweli, akisaidiwa na dada yake pamoja na mama yake. Kwa wakati huo dada alikosa la kusema japo alikuwa akimpenda mwanaume yule lakini hiyo akitosha kubadili maumuzi yale. Nami manyanyaso ya yule mwanaume nikaona sawa tu ni heri tungerejea nyumbani kama walivyokuwa wakihitaji. ____________ Mapema asubuhi tulichukuzana na dada akiwa na mtoto mgongoni, mimi nikiwa na mizigo. Kuianza safari ya kurejea nyumbani Morogoro. Saa tano asubuhi tulikuwa tumeingia kijijini kwetu. Wazazi wakatupokea na kwa bahati nzuri mdogo wangu Masumbuko siku hiyo nae alikuwa nyumbani, tulizungumza mengi hapo awali kabla ya kufikia kwenye sababu haswa ya ujio ule. Niliwaeleza wazazi kwakina juu ya maisha ya dada na ndoa yake yalivyoingia dosari baada ya yule mjukuu wao kukumbwa na tatizo la kushindwa kuongea. Wakati huo yule mtoto alikuwa akikaribia kutimiza miaka miwili. Mama alimtazama yule mtoto kisha akasema, “ kuna tiba yoyote ambayo alipatiwa huyu mtoto”, alisita akatutazama. Dada alikuwa kimya tu hivyo akanibidi mimi nilijibu lile swali lake, “ha… pana, tulipokwenda hospitali mara zote walisema ya kuwa yule mtoto hakuwa na tatizo lolote”, nilinyamaza. Mama akanielekezea tena swali,… “sasa….kama hana tatizo kwani ashindwe kuongea….? Hapo kila mtu alibaki kimya, mama akaendelea kubaki kuwa mzungumzaji aliongea mengi sana na hata hapo hakusita kutupa historia ya nyuma kuhusu ukuaji wetu na kusema katika watoto wake, mimi ndio nilichelewa kuongea na hata hivyo haikuzidi mwaka na nusu, ndugu zangu wote walianza kuyatamka maneno wakiwa na mwaka tu. Kisha akagusia kuhusu kama tulitafuta tiba nyingine tofauti na hospitali, hapo kidogo ikawa ngumu dada hakuweka wazi suala lao la kutafuta tiba nyingine ambapo awali nilizisikia habari zile. Hivyo mama alipouliza swali lile nilimgeukia dada na kumtazama nilivyomuona yupo kimya nilijua kama alivyoficha hapo awali hakuwa tayari kuweka wazi jambo lile, nami nilinyamaza sikutaka kusema jambo ambalo sikuwa na uwakika nalo zaidi ya kulisikia tu. Baada ya mazungumzo yale mama na baba walishauri tuweze kuangaikia suala lile kwa wanganga wa jadi, jambo ambalo lilikuwa jipya masikioni mwangu, maana maisha yangu yote licha ya kuishi kijijini masuala ya waganga nilikuwa nayaogopa. Sikuwa na jinsi ndugu msikilizaji mimi ndio nilipewa jukumu lile la kupambania mpywa wangu. Ilinibidi kuangalia taratibu zote za kupatikana huyo mganga, nilipohakikisha mambo yamekaa sawa. _________ Jioni ya siku hiyo nilimuhita dada tukaingia kwenye mazungumzo mazito baina yangu na yake, sikiona haja ya kulazia damu jambo lile kwa maana maji nilikuwa nimeshavulia nguo sasa nilikuwa lazima niyaoge. Nilimueleza yale niliyokuwa nikayasikia kuhusu yeye kwenda kwa waganga wa kienyeji na shemeji hapo awali lakini dada alinikatalia katu katu. Na nilipogusia kama kuna jambo lolote ambalo uwenda anahisi ndio chanzo cha mwanae kushindwa kuongea dada napo hakuwa na jibu, na hata pale nilipomuliza ya kuwa anaamini tunaweza kupata tiba ya mwanae kupitia waganga wa kienyeji pia alishia kujing’ata nga’ta. Kwa vile wazazi walikuwa wameshaamua vile asubuhi na mapema tulikuwa njiani kuelekea kwa mganga ambaye alikuwa amejizoelea sifa sana kutokana na tiba zake. Safari ilikuwa ndefu masaa matatu tulikuwa juu ya pikipiki, hatimaye tuliweza kufika nyumbani kwa yule mganga, hapo tulikaribishwa na umati wa watu ndugu msikilizaji, vilio navyo vikawa vinapenya sawia ndani ya ngoma za masikio yetu kadiri tulivyokuwa tukisogelea nyumba ya mganga yule. Loo! uwezi amini ndugu kumbe roho ya yule mganga ilikuwa imeshaacha mwili zamani. Ghafla tumbo la kuharisha lilinishika nikiwa pale, nikaanza kutafuta msaada… dakika tatu nilikuwa nikipata huduma ndani ya choo katika nyumba zile za karibu na pale. Baada ya hapo yule mwenyeji aliyenipatia msaada aliniletea vimajani fulani akaniambia nitafune, kihoro kinashika lakini niliamua kufanya kama vile alivyokuwa ameniagiza kweli baada ya nusu saa tumbo lilituliaa hata ule mchafuko wa tumbo sikuweza kuusikia tena. Wakati huo yule mwenyeji alitufahamisha kile kilichokuwa kinaendelea ya kuwa muda mchache walikuwa wakielekea kumzika mganga, lakini yule mwenyeji hakutuweka wazi juu ya nini haswa kilichosabisha kifo cha mganga yule. Miguu yote ilikosa nguvu, hatukuwa na jinsi ilibidi nasi twende kumsindikiza yule mganga katika safari yake ya mwisho. Kweli zoezi lile tulifanikisha ikiwa muda umeenda sana. Safari ya kurudi nyumbani haikuwepo tena ilitubidi tulale pale pale. Hatukuwa na jinsi tukajumuhika na watu wakijiji kile katika kuombeleza. Asubuhi na mapema nilirudi nilimtafuta yule mwenyeji aliyekuwa amenipatia msaada, dakika tano tu zilitosha kumpata. Sikumficha kitu nilianza kumweleza kitu kilichotuleta pale alinisikiliza kwa makini sana, akaomba kumwona yule mtoto, hivyo nikaenda kumtoa dada mahali alipokuwa amekaa, na kwenda nae kwa yule mwenyeji. Baada ya kufika alimuangalia yule mtoto kwa muda alafu akazungumza kitu, kitu ambacho sikuweza kuamini mwanzoni na kama ningeyasikiliza maneno ya yule ndugu nadhani safari yetu ingeishia pale na kurejea nyumbani. Ubaya ningejua huja mwisho wa safari. Yule mwenyeji aliongea yakuwa kwa jinsi alivyomtazama yule mtoto hakuwa na tatizo lolote. Hakuishia hapo alituelekeza kwa mtaalamu mwingine, na uzuri yule mwenyeji alikubari kutusaidia baada ya kupata kifungua kinywa tuliongozana nae mpaka kwa mtaalamu mwingine, hapakuwa mbali sana na maeneo yale. Nusu saa tulikuwa nje ya nyumba ya mtaalamu, kwa bahati mbaya alikuwa ametoka hivyo akatupaswa kuweza kumsibiri. Ilichukua muda hatimaye yule mtaalamu aliukuta ugeni wetu. Alipoweka mambo sawa akatukaribisha katika chumba ambacho alikuwa akitolea tiba. Mimi na dada tuliingia kwenye chumba kile tukimuacha yule mwenyeji nje. Chumba kilikuwa kimesanifiwa na vitu ambavyo kiukweli vilioniogopesha na kuamini tulikuwa kwa mtaalamu haswa, wakati huo Mpwa wangu alikuwa amelala. Yule mganga alitukaribisha nasi tukaketi. Kabla hatujasema shida yetu yule mganga alianza kuongea maneno ambayo sikuwa nikiyafahamu. Kama dakika mbili alafu akanza kutajia shida yetu iliyotuleta mahali pale. Ama kwa hakika maneno aliyekuwa akiyanena yule mtaalamu, yalinifanya niamini kwa mara nyingine pale nilikuwa mahali sahihi kabisa na suala letu lilikuwa likienda kuisha kwa mganga yule. Alielezea shida yetu kwa usahihi bila ya kukosea nasi tukatingisha kisha kuashiria suala lile ndio lilituleta pale. Nilimsihi mganga ya kuwa ningempatia kiasi cha laki moja kama angeweza kufanikisha swala lile la mpwa wangu kuongea. Mganga yule hakuonekana kujali kiwango kile cha pesa alitulia kimya. Kabla kukifukuza kimya kile kwa maneno ambayo ndugu msikilizaji siku ya tegemea kabisa.

at 5:18 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top