Home → simulizi
→ Simulizi ya maisha. KOSA.
Ilipoishia.
Nilimsihi mganga ya kuwa ningempatia kiasi cha laki moja kama angeweza kufanikisha swala lile la mpwa wangu kuongea. Mganga yule hakuonekana kujali kiwango kile cha pesa alitulia kimya. Kabla kukifukuza kimya kile kwa maneno ambayo ndugu msikilizaji siku ya tegemea kabisa.
Naam!, mwanadamu ni mwanadamu tu si vyema kumuamini kwa kila kitu.
NA HII NI SEHEMU YA MWISHO
Ni kweli sikuyategemea maana hakuna kilichokuwa kimebadilika mambo yalikuwa yale yale. Ajabu sasa yule mganga alinena yakuwa hakuitaji kiasi chochote cha pesa kwajili ya kumtibia mpwa wangu kwa sababu hakuwa na uwezo wa kumfanya aweze kuongea licha ya kuwa yule mtoto alikuwa anauwezo wa kuongea kama alivyosema hapo awali. Aliongeza kuwa mwenye jukumu la kumuwezesha kuongea yule mtoto ni mama yake.
Majibu yake yaliniweka katika wakati mgumu sana, Ila sikuonesha kuyajali majibu yale ya mtaalamu kwa wakati ule maana sikutaka pengine kumweka dada katika hali ya tofauti, kama alivyokuwa akihisi labda ningemfulizia maswali. Hivyo baada ya huduma yake tulitoka kwenye chumba kile. Mwenyeji wetu alikuwa akiendelea kutusubiri.
Tulijitoa eneo lile, kijua kikianza kuwaka kweli. Nilimweleza kifupi yule bwana namna tulivyoyapata kwenye chumba kile cha mtaalamu, ndugu yule alikuwa kimya tu akinisikiliza. Baada ya kumaliza kile nilichokuwa nikiongea, nikamuomba kutusadia upatikanaji wa usafiri wa kutoka eneo lile. Juhudi za yule bwana zilifanikisha kutupatia usafiri wa kutoka mahali pale.
Saa kumi na moja jioni tulikaribisha na kiupepo cha nyumbani, nikiwa hoi bin taaban, kushuka tu kwenye pikipiki, nilipoingia ndani nilijibwaga moja kwa moja kwenye kitanda, usingizi mzito ulikuja kunichukua, na kunifikisha saa tatu usiku na dakika zake. Nyakati hizo niliamshwa na dada kwajili ya kupata chakula. Hapo ndipo Wazee wa kapata fursa ya kutuuliza juu ya safari yetu, japo nilikuwa nimechoka ilinibidi niweze kuwaeleza mwanzo hadi mwisho tulichovuna juu ya safari ile. Ila sikuwaeleza habari ya kuwa mganga alisema kuhusu tiba ya mtoto ni mama mwenyewe. Nilihofia kumweka dada katika mtihani mzito. Maana nilishanza kuhisi uwenda dada kunakitu alikuwa akificha na hakukitaka kukiweka wazi kwangu na hata kwa wazazi, maana hata habari za ile safari alinisubiri mimi kuwajuza wazazi. Tuliyamaliza mazungumzo yale yalikuwa yakisindikizwa na chakula kitamu alichokuwa amekiandaa dada.
___________
Usiku wa siku hiyo sikupata usingizi kabisa ndugu msikilizaji, maswali mengi yalijengeka kichwani mwangu pasipo kuwa na majibu ya sahihi. Na kumbuka kama sikosei saa tisa ya usiku ndio usingizi ulikuja kunichukua na kunifikisha asubuhi ya siku nyingine. Mungu alinijalia kuamka salama katika dunia yake. Ilipotimu saa saba mchana nilipata chakula cha tumbo langu likawa limeridhika kabisa, na hata mwili kuwa mwepesi kabisa, jioni nayo ya siku ya kwanza ya pili na ya tatu ikatimia.
Jioni ya siku ya nne nilimuita dada, hapo ilikuwa baada ya kuwemo katika tafakari nzito kuhusu hali ya mpwa wangu. Niliongea kwa upole sana kwa siku hiyo hali ambayo hata dada hakuwahi kuniona kwa kipindi kirefu hali ile ilimuweka katika mshangao lakini ndio tayari nilikuwa nimedhamilia. Lengo ilikuwa nikufahamu nini ambacho dada anakificha kuhusu yule mtoto. Maana yule mganga katika siku kadhaa za nyuma alitoa kauli ya kuwa mwenye jukumu la kumtibu yule mtoto ni mama mwenyewe, hivyo ndio nilikuwa nikihitaji nifahamu jukumu lipi haswa ambalo dada alikuwa nalo juu ya tiba ya mpwa wangu Nasri.
Nilizungumza kwa hisia sana ndugu msikilizaji maneno yangu yalianza kumwingia dada kidogo kidogo hatimaye dada alianza kuanguka kilio kizito. Nilitumia muda mwingi kumweka sawa, dada alikaa sawa, kipindi chote hicho katika kilio chake alikuwa akilitaja jina langu akisindikiza maneno ya kuniomba msamaha kutoka na kitendo chake cha kuniweka katika matatizo pasipo kupaswa.
Maneno yake nayo yakaanza kuniongezea udadisi. Nilitumia maneno yangu ya ushawishi sana hatimaye dada alianza kuniambia maneno ambayo sikuwahi kuhisi kipindi chote yalikuwa ndani ya kinywa cha dada.
_______
Dada anasema, alikuwemo ndani ya kosa ambalo hakuwahi kufikiria ingeghalimu maisha yake japo alitumia juhudi zote kujiondoa ndani ya lile kosa. Ilikuwa hivi.
Kabla ya kufunga ndoa na shemeji katika kipindi cha miezi miwili ya nyuma alikuwa na mwanaume mwengine akienda sambamba na shemeji Libogoma, pasipo mategemeo alishika ujauzito. Baada ya kushika ule ujauzito. Akawa mtihani kwake kubaini mwanaume gani ndio alikuwa miliki hali wa mimba ile. Katika kipindi hicho chote mawasilino ya kawa yamepotea baina ya dada na huyo mwanaume. Hivyo kutokana na vile dada akamuweka wazi shemeji Libogoma ya kuwa alikuwa na mimba yake, shemeji libogoma baada ya kusikia habari za mimba hakuchelewa moja kwa moja akatangaza ndoa.
Wakati dada alipokuwa akimalizia michakato ya ndoa yake yule mwanaume alikuja kumtafuta safari hii haikuwa kwa simu tena alifanya kuona nae kabisa na alipokuja moja kwa moja yule mwanaume alilama sana kuhusu dada kumpa damu yake mtu mwingine maana alibaini kabisa dada alikuwa na mimba yake, na kuhusu hilo dada alikana katu katu ya kuwa ile mimba haikuwa ya mwanaume yule. Hivyo kitendo cha mwanaume yule kuondoka na manungu’niko juu ya yule mtoto ndio imekuwa kama chanzo cha yule mtoto kushindwa kuzungumza, kwa maana dada anasema yule mwanaume alishawahi kumtafuta na kuzungumza na dada juu ya suala lile la mtoto na kumtadhalisha sana kuhusu yule mtoto.
Dada akuishia hapo aliongea mengi sana huku akisitiza niweze kumsamehe maana alikuwa akijisikia vibaya kwa kitendo kile. Hakusita kunigusia kitendo chake cha kumuonga daktari katika miezi kadhaa iliyopita baada ya shemeji kucharuka kutaka kupimwa damu ya yule mtoto kutokana na kuhitaji kuokoa ndoa yake. Dada aliamua kufanya vile maana alishabaini kabisa yule mtoto hakuwa mali ya shemeji Libogoma.
_________
Ukweli nilichoka ndugu msikilizaji, kwa kuwa yalikuwa yameshamfika dada, nilikuwa sina budi kulisimamia tatizo lake na kulihakikisha linatatuliwa, usiku wa siku ile niliwaeleza wazazi kwa kifupi mambo yalikuwa yakimsibu ndugu yangu. Wazazi hawakuwa na hiyana walinielewa. Taratibu za kutamfuta yule mwanaume ambaye ndio alikuwa baba halali wa mpwa wangu Nasri, tulizifanya baada ya wiki tuliweza kuona nae.
Huwezi amini ndugu msikilizaji kitendo cha yule mtoto kumuona baba yake, mdomo ulianza kuwa mwepesi, siku kadhaa baada ya kufanyiwa mila na desturi za ukoo wao. Basi yule mtoto alianza kuyachalaza maneno kama ugomvi, nami nikaitwa mjomba, wakuitwa bibi aliitwa bibi, wakuitwa babu aliitwa babu. Yule mwanaume hakuwa na hiyana aliamua kumuoa dada yangu Asha na maisha yao ya kawa na furaha tele. Wakati huo shemeji Libogoma alifahamu ukweli lakini naye alikuwa tayari anaishi na mwanamke mwingine.
MWISHO.
Mwisho
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: