Simulizi ya maisha. KOSA Sehemu ya nne Ilipoishia. Hamadi nilipokelewa na taswira ya daktari, wakati huo dada alikuwa ameketi kwenye moja ya kiti. Naam! mtihani tumeumbiwa binadamu, wakati mwingine unaweza ukahisi dunia inakuchukia hapana budi kupambana. NA HII NI SEHEMU YA NNE Daktari yule alituangalia mimi na shemeji kisha akatuambia tuketi kwenye viti, nasi tukaketi. Sasa yule daktari ndio alikuwa mzungumzaji kwa kina, alianza kuzungumza jambo moja moja. “Naam! tumelifanya vipimo vyote kama mlivyotaka wapendwa kwa usahihi sana. Aliongea kisha akasita na kutazama, mimi nikamtazama kwa makini, wakati huo dada alikuwa kimya sana, shemeji akiwa na shauku ya juu. Nasri kwa wakati huo usingizi ulikuwa umemchukua hivyo hakuwa akitambua jambo gani lilikuwa linaendelea, alimeza mate kidogo yule daktari akaendele kusema. “Yaa…. Kwa upande wa tatizo la mtoto kuwa na ububu hilo hatukuliona inaonesha wazi kama mara ya kwanza tulivyosema mtoto huyu anauwezo wa kuongea, lakini hatuna uwakika ni muda gani ataweza kuyatamka maneno”. Daktari aliweka kituo. Nami nilivuta pumzi ndefu kuyakabili yale majibu yake ambayo kwa upande wa shemeji kama vile alikuwa akitaka kusema jambo lakini kinywa chake kikashikwa na haya. Alitupa fursa ya kuuliza maswali kabla ajaendelea na kile alichokuwa amekipata, kwa upande wangu sikuwa na swali, kabisa ni hivyo hivyo dada hakuwa na swali, hata shemeji yeye alibaki kumwangalia tu daktari. Kutokana sisi hatukuwa na maswali dhidi yake yule daktari akamugeukia shemeji na kumuliza swali. “Bwana Kizito kwanini umetaka tufanyie vipimo vya DNA, uwenda unamashaka na damu ya huyu mtoto?” swali lile la daktari kwa upande wangu lilinishitua mno, nilijua wazi shemeji alidhamiria lile, sikuweza kulizua hali ile, nilibaki nikayasuburi majibu ya shemeji. Safari hii hakuwa na haya hata kidogo alibwabwaja sana mbele ya yule daktari ya kuwa kwa vyovyote vile yule mtoto anasilimia nyingi haikuwa damu yake. Mimi niliendelea kumsikiliza moyoni nikiwa naumizwa sana na hali ile. Daktari alimuomba atulie baada ya kuona hali ile ingeweza kuzusha mtafaruku. Shemeji alitulia wakati huo yule daktari akiomba nafasi ya yeye kuzungumza. Kweli alipatiwa, mazungumzo yalikuwa marefu kwa muda kidogo yote yakionekana kumsihi shemeji nasi tuweze kukubalina na matokea ya vipimo vile vya DNA. Hatimaye ilifika wakati wa kuyapokea yale matokeo. Alisita kidogo daktari yule akitutazama kwa makini, kisha akaanza kwa kusema. “Majibu haya ni majibu sahihi kabisa kutoka kwenye vipimo vyetu vya kisasa na uwakika kabisa. Yanasema hivi baada ya kuipima damu ya mtoto na damu yako ndugu Kizito, damu zenu zinaonesha kuendena sana, na kwa lugha nyingine zinawiyana, hivyo basi kutokana na majibu hayo inaonesha huyo mtoto ni wako kabisa ndugu kizito”. Daktari alimaliza vile. Hayakuwa majibu madogo kabisa kwa upande wa shemeji maana sura yake ilikuwa ikisita sita kunitazama mara mbili, alishikwa na mfadhahiko, alifura akionekana kama alikuwa akubaliani na yale majibu. Nilimshukuru Mungu kwa namna moja ama nyingine, nikimkumbatia dada ambaye sasa machozi yalianza kumtilika kwenye uso wake, alilia kimya kimya kiasi cha kwamba kilio chake kilikuwa kinaniumiza sana, nilijitahidi kuzuia kilio chake kwa muda wakati huo shemeji alikuwa ameshatoka kwenye chumba cha yule daktari pasipo kusemeshana na sisi. Tulitoka nje ya chumba cha daktari, lakini nje hatukumkuta shemeji, tulijaribu kumwangalia sehemu zote za hospitali ile lakini hatukumwona, ilitubidi tupande daladala kurejea nyumbani, tulikumbana na shida kidogo, mpaka tulipofika nyumbani. Ajabu sasa pasipo mategemeo shemeji hatukumkuta nyumbani. Kama tulivyokuwa tukidhani uwenda tunge kutana naye nyumbani. Kibaya zaidi shemeji hakurejea nyumbani, ilipita siku ya kwanza ya pili na hata ya tatu, hali ambayo ilitupa hofu. Ijapokuwa vituko vya shemeji lakini dada yangu alikuwa akimpenda sana mwanaume yule. Hivyo siku ya nne ilibidi tuchukuzane mimi na dada hadi kazini kwa shemeji baada ya kukosa hata mawasiliano naye kupitia njia ya simu yake ya mkononi. Pia huko atukupata taarifa zake. Mwishowe tulirejea nyumbani, safari hii dada akitoa wazo la kupigiwa simu ndugu zake uwenda ingekuwepo kwa moja ya ndugu zake, lakini ajabu taarifa zilikuwa zile zile, baada ya kufanya mawasiliano kwa wote muhimu ambao wangeweza kutupa taarifa zake. Habari zile hazikuwa njema kabisa kwa upande wetu, ilifika kipindi ilitubidi kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi, hiyo ilikuwa baada ya wiki na nusu tangia kumpoteza shemeji kwenye mboni za macho yetu. Mwishowe tulijikatia tamaa ya kumtafuta. Katika kati ya wiki ya pili katika jioni moja, shemeji alirejea nyumbani akiwa tofauti sana kuliko hata nilivyokuwa nikimjua hapo awali, tangia nikae pale sikuwahi kumwona shemeji akirudi nyumbani akiwa amekunywa vinjwaji vikali yaani pombe, hakika shemeji alilewa sana kuliko kawaida tofauti na walevi wengine.. Katika ujio wake ule, ambao hata majirani waligeuka watazamaji wa senema ile ya bure. Alitudhalilisha sana maana alitutukana vya kutosha. Ukoo wetu aukupona hata kidogo kwa mara nyingine. Nilishikwa na hasira kali sana, wakati huo nilitamani walau niweze kumpiga makofi kadhaa iliniweze kumnyaamazisha. Nikisahau kama tuliangaika si chini ya wiki kumtafuta. Kwa upande wake dada Asha, alipomkea mumewe na kumpeleka chumbani akiwa hoi bin tabani, pasipo kujielewa. Huku ikiacha minongo’no kwa majirani walikuwa wakishuhudia varangati lile. Mimi nikijitoma chumbani kwangu, baada ya kufunga mlango mkubwa wa nyumba. Giza liliingia katika siku hiyo kukiwa kimya sana, nyumbani pale maana shemeji alivyoingia ndani na dada hapakuwa na maongezi, pombe zile zilimzimisha kabisa, kiasi cha kwamba kilimpa shaka dada maana baada ya muda alikuja na kunigongea mlango wa chumbani kwangu kisha kunipa taarifa kuhusu hali ya shemeji. Japo kuwa sikuwa mzoefu sana na maswala ya ulevi lakini nilimshauri dada asiwe na hofu kuhusu jambo lile nilimwambia. Ni ulevi tu ndio ulimfanya awe vile usijali dada atakaa sawa baada tu ya ule ulevi kumtoka kwenye mwilini mwake. NI kweli kama nilivyokuwa nikisema. Nilivyomka asabuhi dada mapema tu dada alikujakunigongea chumbani kwangu, na kunipa taarifa ya kuwa shemeji ameondoka tena. Nami nilimuambia asiwe na shaka Mungu atasimamiya na kila kitu kitakwenda sawa kwenye ndoa yake, na hata kumwezesha Nasri kuweza kuongea. Kweli dada alinielewa na mimi sikurudi kulala tena, nilienda kuoga kisha kuelekea kwenye harakati zangu. Utendaji wangu wa kazi katika siku hiyo ulikuwa tofauti sana kana kwamba nilikuwa najua kunakitu ambacho kinatokea nyumbani wakati ule. Maana hata niliwahi kutoka kazini pasipo kawaida yangu. Ndugu msikilizaji, ni kama vile nilikuwa nimeota maana kile nilichokuwa na kiona kwenye macho yangu punde nilipokuwa. Na tazama na nyumba. Nikusihi ndugu msikilizaji, matizo ni jambo ambalo halina taarifa, hivyo ni vyema ukayakupokea katika namna ambayo itakufanya ujue ni njia gani utayakabili. Na hiii ilikuwa sehemu ya nne je nini kitaendelea? Usikose kesho sehemu inayofata.

at 5:17 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top