Simulizi ya maisha. KOSA Ilipoishia. Nilitulia kimya, nikimtazama dada nae alinitazama, tuliendelea kutazamana kwa muda kiasi, kabla ya kuitwa kuelekea kwenye chumba cha daktari. Majibu ya jambo lile yalikuwa tayari hadharani. NDUGU, na kusihi tena katika maisha yako unapotoa maneno yafanyie tathimini kabla ya kuyatamka, maana kwa wakati mwingine maneno yako mwenyewe yanaweza kukugharimu. NA HII NI SEHEMU YA TATU Wakati huo, tukiwa tunaelekea kwenye chumba cha daktari yule mtoto alianzisha kilio, alilia sana katika kilio ambacho sikuweza kukitafsri kwa muda ule. Dada alijaribu kuzuia kilio cha mwanae, kwa muda kidogo hatimaye alifanikiwa pindi tunatazamana na daktari. Tulitulia kimya, kila moja akiwa na shauku ya kufahamu ni nini ambacho kilikuwa kinasababisha yule mtoto ashindwe kuongea, wakati ulikuwa umri sahihi wa kuanza walau kumtaka maneno japo kwa kukosea kosea kisha kukaa sawa. Hofu nayo haikuwa mbali sana ilikuwa karibu nasi. Nilitazama daktari kwa makini nadhani kushinda hata Shemeji na dada, katika mtazamo ambao hakuweza hata kubadilisha majibu yake. Na yeye hakuwa akiteteleka alianza kusema kile ambacho kilichopatikana. Pasipo mategemeo yetu yule daktari aliongea ya kwamba hakuwa na tatizo kabisa yule mtoto na hakuna kitu chochote ambacho kimeonesha ya kuwa yule mtoto alikuwa anakabiliwa na tatizo la ububu, labda ndio lilikuwa likifanya ashindwe kuongea. Alichosisitiza tu mtoto aweze kupatiwa muda ataweza kuongea. Katika siku ambazo hakusema zingekuwa ngapi, lakini yeye alisisitiza baada ya mwezi tungerejea kama hatakuwa bado aongei, iliaweze kufanyiwa uchunguzi wa kina. Maneno ya yule daktari yalileta kidogo faraja kwa upande wangu, na pia ya kutuletea amani ambayo ilionekana kuwa mbali tangu jambo lile kutokea. Safari ya kurudi nyumbani haikuwa ya tabu. Tuliweza kufika nyumbani, mchana ikiwa imetimia, kufika shemeji aliniomba tuzungumze, wakati huo dada akijishughulisha kuandaa chakula kutokana hali ya matumbo yetu yalikuwa yakipata upinzani mkali wa njaa iliyokuwa imechukua nafasi. Kutokana tulitoka asubuhi bila ya kupata kitu kwenye matumbo yetu. Kweli tulitulia mezani pale sebuleni, sauti ya runinga ikawa inasindikiza maongezi yetu. Shemeji aliongea sana katika yale mazungumzo akiomba msamaha kwa kile kilichokuwa kinatokea katika siku zote mule ndani, na kuahidi kuwa mvumilivu kwenye jambo lile na kamwe hatuweza kuongea mambo mabaya kuhusu familia yetu. Nilimsikiliza kwa makini sana maneno yake, nikiizuia hasira yangu, hilo nilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kulizua nikiwa mbele yake sikutaka kuonesha tofauti na jinsi nilivyolichukulia. Kwa upande wangu, nilimuambia ya kuwa kila kitu kipo sawa, hakuna kilichohalibika. Ni kiongeze ya kuwa ile ilikuwa mitihani tu katika maisha hakuna budi kukabiliana nayo kwa namna moja ama nyingine, pia ni vyema tungeendelea kumuomba Mungu aliaweze kutatulia mtihani ule. Shemeji alinielewa sana. Muda ulizidi kwenda tukiwa katika mazungumzo ambayo mada zilibadilika, baada ya ile ya msingi kuwa tumeizungumzia. Hatimaye tulipata chakula. Jioni nayo haikuwa mbali, baada ya chakula kile cha mchana muda ulienda haraka sana, na siku hiyo sikuwa na sehemu ya kwenda nilishinda nyumbani muda wote. Usiku wa siku nyingine ulitimia, amani ikiwa imetawala sana. Siku nazo hazikuwa nyuma wiki, wiki mbili, wiki ya tatu ilitimia hapakuwa na mabadiliko yoyote kwa Nasri. Hakuna kilichokuwa kimebadilika, mdomo wake ulikuwa mzito vile vile hakuweza kuzungumza zaidi ya kulilia tu kama ilivyokuwa hapo awali. Jambo ambalo hata mimi sasa ilianza kunijengea shaka juu yake. Lakini sikutaka kuiweka wazi, wakati huo Dada muonekano wake ulikuwa ukionesha kuna jambo ambalo lipo ndani yake ila alikuwa akishindwa kuliweka wazi. Nami sikutaka kuusemea moyo wa mtu, niliendelea kumuomba Mungu aweze kumwezesha Nasri aweze kuzungumza. Na kumwepusha dada yangu katika janga lile. Mwezi ulitimia Shemeji akiwa kimya kabisa, wakati nikiwa na hofu juu ya kupotea amani tena kwa mara nyingine nyumbani pale, pasipo mategemeo, wiki ya mwezi ule ikawa imekwisha, na wiki ya pili nayo ilikuwa inakaribia kupotea katika uso wa dunia. Amani ikiwa imetawala pale nyumbani, huku hakukuwa na mabadiliko yoyote kwa yule mtoto. Ghafla mambo ya kabadilika kwenye usiku moja, ikiwa mapema zaidi kuliko mategemeo, safari hii shemeji alienda mbali zaidi baada ya zogo lile nililoanza kulisikia taratibu nikiwa chumbani kwangu. Alienda mbali na kusema kuwa uwenda yule mtoto hakuwa wake, maana kwao hakuna hali kama ile, na katika ukoo wao, mtoto anaanza kuongea kabla hata ajafikisha mwaka moja. Hakuishia hapo alichachama zaidi, pale nami nilipotoka kwenye chumba changu, kwenda kugombelezea hali ile. Akitaka mapema kabisa tuelekea hospitali kwa jili ya vipimo vyote ikiwemo kupima damu, maana alisema ana wasi wasi inawezekana ile damu haikuwa yake. Katika kuhakisha amani inarejea, nilitamka Shemeji aweze kutulia ili kesho yake tuweze kuelekea hospitali. Japo jambo lile la Shemeji kusema yule mtoto si damu yake liliniumiza sana, lakini sikuwa na jinsi maana alishamua kusema nami nisingewe kuyarudisha maneno yale kwenye kinywa chake. Baada ya muda niliweza kuzuia hali ile. Na kurejea kwenye chumba changu. ________ Mapema asubuhi, tulikuwa watu wa kwanza kabisa kufika katika ile hospitali, nayo ikatupokea, katika mshangao wa baadhi ya wale wafanyakazi wa hospitali ile, lakini hakuna mtu aliyekuwa akijali. Kama kawaida yake shemeji alikuwa mtu wa kwanza kuingia kwenye chumba cha daktari, safari hii akitumia muda mwingi kuzungumza na daktari. Muda huo nilipata nafasi ya kumsihi dada kwa mara nyingine awe mvumilivu katika kipindi kama kile, na achukulie jambo la kawaida sana. Dada alikubalina na maneno yangu akitangisha kichwa akishiria amenielewa. Shemeji alirejea na kumchukua dada na mtoto baada ya muda. Mimi nikibaki nje kwenye benchi la kusubiri huduma. Nilikaa pale kwa muda mrefu, nikimomba Mungu aweze kuijelesha amani katika ndoa ya dada, kwa kumuwezesha yule mtoto kuongea, maana ndio chanzo cha amani kupotea, huku nikimsihi Mungu yule mtoto awe damu ya Shemeji na isiwe vinginevyo maana ingezidi kuleta hali mbaya zaidi kwa dada. Ilipita kama lisaa limoja ni kiwa katika maombi mazito, nilikuja kushtuliwa na sauti ya shemeji, ikinitika nimfate kule alipokuwa anaelekea. Nilipiga hatua kuelekea kule alipokuwa akienda kisha nilijitoma kwenye chumba ambacho hakikuwa kigeni kwangu, ni mara yangu ya pili nilikuwa ndani ya chumba kile, nikiwa na Shemeji. Hamadi nilipokelewa na taswira ya daktari, wakati huo dada alikuwa ameketi kwenye moja ya kiti. Naam! mtihani tumeumbiwa binadamu, wakati mwingine unaweza ukahisi dunia inakuchukia hapana budi kupambana. Na hii ilikuwa sehemu ya tata ya simulizi yetu ya maisha, je nini kitaendelea? Usikose kesho saa kumi na mbili jioni

at 5:17 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top