NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 11 Kupita siku zote, jioni hiyo nilijisikia vizuri sana, nilikula kama nilikuwa na njaa ya siku nyingi. Nililala nikiwa nimetosheka kisha nikalala usingizi mzito hadi asubuhi. Kama kawaida niliona maandishi mengine chini ya kitanda changu na nilipotazama google ilikuwa ni namba tisa ya Kiarabu. Nikaideki nikiwa nimekasirika kweli, kwa sababu mbali na Jay Love kunitisha lakini kazi ya kusafisha kila siku ilikuwa imenichosha na sikutaka tabia hiyo iendelee tena nikapata jibu (nitakwambia baadaye nilichofanya). Siku hiyo nikaamua kukumbushia siku zangu za upaparazi, nikabeba kamera yangu kwenye begi na kukodi pikipiki kama kawaida nikiwa na kofia iliyoniziba sura, nikayoyoma kuelekea mitaa ya Ubungo kumtegea Rabia, baada ya jana yake kumuona akiwa kwenye gari ya dereva yuleyule wa zamani, Devi huku wakiwa na Jay Love. Nilikaa sana upande wa pili wa ile barabara na kusikilizia ili niwaone wakiwa wanaingia. Kama nilivyotabiri, majira ya saa 8 mchana nikaiona ile taksi ikiingia ndani ya geti la Land Mark Hotel, nikachomoa kamera yangu na kupiga picha kadhaa, nikamuona Jay Love akishuka lakini siku hiyo alionekana kama mtu aliyekosa afya tofauti na nilivyomuona siku moja ya nyuma yake. Macho na lenzi ya kamera yangu zilishuhudia wakikumbatiana kisha wote wakapotelea ndani ya hoteli. Haraka nikavuka upande wa pili na kumuwahi Devi aliyekuwa akitoka na taksi yake, nikilenga kumuuliza kuhusu kila kitu kinachoendelea kati ya Rabia na yule Msomali wake. Nilipofika nilinyoosha mkono kama abiria na alisimama nikapanda akiwa hanijui kabisa kama mimi ndiye siku kadhaa nyuma niliwahi kumtishia ili anilete hapo hotelini.

at 12:59 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top