NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 10 Wakati nikiendelea kushangaa akanitaka niiname na kufanya ishara kama natua mzigo chini, nikainama nakufanya kama alivyonielekeza nikafanya mara tatu, kisha akaniambia nisimame na kujaribu kutembea, nikashangaa nikijiona mwepesi kuliko, ilikuwa kama vile nimeshusha mzigo wa lumbesa niliokuwa nimeubeba mgongoni. “shehe kwani umenifanyia nini? mbona najisikia mwepesi hivi?” nilimuuliza. Badala ya kunijibu akacheka kwanza na kunionesha kwa kidole, tazama hapo; nikageuka na kutazama pale nilipofanyia ishara kama nashusha mzigo, nikashangaa kuliona dubwana kubwa kama pipa lenye shepu ya luba likiwa na damu nyingi ndani yake. Nikaruka nyuma ya Shehe kwa woga, lakini mwenyewe hakuwa na hofu hata kidogo akaniambia; “huo ndiyo mzigo uliokuwa ukiubeba muda wote huo na ndiyo ulikuwa ukikunyonya uhai na kumpatia Jay Love.” Aliponiambia hivi nilijikuta nikipata hasira maradufu nikamuuliza shehe, nini nifanye ili kulipiza kisasi kwa Jay Love. Akaniambia ili kupambana naye inabidi nivifute viapo alivyokula na Rabia au kuhakikisha jina la Jay Love linasahaulika kabisa kwa sababu kadri linavyotamkwa au kukumbukwa ndipo mzimu wake unazidi kuwa na nguvu. Alipomaliza kusema hayo akaniambia maneno yaliyonivunja moyo, kuwa hadi hapo hawezi kuendelea mbele tena kwa kuwa uwezo ulifikia mwisho, hata hivyo alinitaka niendelee kumshirikisha kila kinachonisibu ili ajaribu kunisaidia. Nilimshukuru kwa ukarimu wake na nafuu niliyoipata, nikaelekea nyumbani kupambana na matatizo yangu peke yangu.

at 12:58 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top