NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 12 “Habari yako bwana Devi! Nilimsalimia akaniitikia bila kuniangalia lakini kuna kitu kama alishtuka akageuka na kunitazama, sasa akaonesha kunikumbuka. “Mwandishi! Nini kimekukuta, mbona upo hivyo!” aliniuliza harakaharaka ikabidi nimdanganye kuwa nilikuwa ninaumwa ghafla hivyo nilikuwa hapo ili kukamilisha uchunguzi wangu. Nikamkumbusha uongo wangu wa mwanzo kuwa ni kuhusu jambazi ambalo dakika chache zilizopita alikuwa amelileta mle hotelini likiwa na mwanamke (Rabia) lakini kama kawaida sikumtaja kuwa huyo mwanamke ni mke wangu. Cha kushangaza yule dereva alishtuka akasema kuwa mle ndani hakuwa amemuingiza mwanaume yoyote zaidi ya Rabia, nikabaki nimestaajabu, kuwa inawezekana huyo Msomali, Jay Love ninamuona mimi peke yangu. Nikashuka kutoka kwenye ile taksi nikiwa nimejishika kichwa baada ya kuona kitendawili kinazidi kuwa kigumu. Kuhakikisha maneno ya dereva nikampigia simu yule mdada mhudumu wa pale mapokezi niliyemuachia namba yangu kipindi kile nataka kumfumania Rabia. Nikamuuliza kama mke wangu alikuwa ameingia na mtu yoyote pale hotelini akanijibu kuwa kama kawaida Rabia alifika peke yake na kujifungia chumbani kwake. Baada ya kusema hayo nikagundua kuwa nimekuwa na uwezo wa kuuona mzimu, sikujua nimewezaje ? Kichwani nikaanza kufikiri jinsi ambavyo Rabia alivyokuwa na Jay Love siku zote alizoingia pale hotelini nikidhani alikuwa peke yake. Akili yangu ikaanza kuumba mawazo; huenda hata wakawa wanafanya mapenzi huko ndani mmoja akiwa binadamu na mwingine ni mzimu. Hata hivyo pia ilinifanya nione wivu kwa kiasi kikubwa, “Haiwezekani!” nilizungumza kwa hasira lakini nilijilazimisha kurudi nyumbani moyo wangu wote ukipaa na kuingia chumba alichokuwa Rabia na Jay Love nikawa kama naona naumizwa na hisia za chochote walichokuwa wakikifanya. Itaendelea kesho.

at 12:59 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top