Home → simulizi
→ KIAPO CHA SIRI
(Damu yangu haipotei)
Mtunzi : ZAYNABTALY
0625756953
SEHEMU YA 4.......
Ilipoishia......
" We Koma wewe mimi sio mama yako nataka changu ". Yalikuwa maneno yaukali ambayo yalimchoma moyo na kumfanya akose cha kukiongea mbele ya mama yule ambaye jaziba zake aliamini zingetulia kwa pesa tuu na sio vinginevyo.
*******SONGA NAYO********
Wakati akiwa anahaha asijue chakumpa yule mama mara alisikia sauti ambayo aliwahi kuisikia siku zilizo pita. "Habari zenu..? " ilikuwa nisauti nzuri yenye kupendeza Kutoka kwa Stellar.
"Salama ".
Aliitikia huku akiwa hamkumbuki mwanadada yule aliwahi kumuona wapi Wala kuisikia sauti yake.
"vipi Mbona hapa Kuna tatizo? ".aliuliza ilikuona namna atakavyoweza kusolve tatizo lile.
"yaani Dada angu acha tuu ".
Kabla ya yule kijana kutia neno lolote mara yule bibi akadakia. "Kama wewe ndo Hawala yake haya msaidie kulipa pango sasa sio kukitumia tuu chumba changu na kukiacha hata gest wanalipa pango eeeh... ".
Maneno ambayo yalimfanya stellar staajabu kwa yale maneno yaliyomshukia ila hakuwa na jinsi akaingiza mkono wake katika pochi yake kisha akatoa noti za elfu kumi na kuanza kuhesabu.
Kisha akampatia yule mama "nimekulipia na miezi miwili ijayo ".
"Ooh asante Sana Dada angu nashukuru Sana kwa msaada wako ".
"Usijali ".
"naushukuru huyu malaya wako Kaja kukupa msaada leo saa sivyo pangechimbika hapa leo maana habari zako zote ninazo mpuuzi wewe kukicha kuleta wasichana wa ajabu ajabu nyumbani kwangu na sijui hata utakuwa lini maana hela yenyewe huna hae hohe tuu kama mimi ila msumbufu mtaa mzima huu wanakujua wewe kwa jinsi ulivyokicheche na mwizi na sikia hata juzi ukitoka kuuliwa tandika lakini Mi hata sijali hayo muhimu umenipa pesa yangu "
Yalikuwa maneno ya mama mwenye nyumba huku taratibu akikanyaga hatua kuondoka eneo lile.
"Daah niwie radhi tafadhali maana bila mimi yote haya Sidhani kama yangekusulubu. "Aliongea yule kijana mwenye sauti ya upole ambayo ilienda sambamba na sura yake.
Macho yake ya aibu yasiyo na hata chembe ya ukaidi ndio yaliyokuwa yakitalii kwa kuibia juu ya mwanadada yule aliyemsaidia kutoka katika sakata lile huku machozi yakimlenga katika macho yake juu ya lile tukio la muda mfupi lililotokea.
"usijali ila nilikuwa naomba wasaa wakuongea na wewe kwa uchache? ".
"Aah usijali Karibu ndani ".
"Naitwa Stellar "alijitambulisha baada ya kuingia ndani ya chumba cha kijana yule kilicho pambwa na kitanda kimoja kikubwa cha Ukubwa wa tano kwa sita, kiti cha plastiki, meza ndogo iliyopangwa vyombo vichache chini yake. kwa chini kulikuwa na jiko la mafuta pamoja na sufuria mbili chafu.
Baada ya kukamilisha kutembeza macho yake ndani ya chumba kile sasa macho yake yalikutana na macho ya yule mvulana.
"Mi naitwa Sam Karibu kwangu".
"Asante, sijui unanikumbuka..? "aliuliza ilikuweza kutambua uhai wakumbukumbu juu ya tukio lile la kukutwa ndani ya gari la watu na kuhitajia msaada.
"Hapana Labda unikumbushe tulionana wapi ".
"any way kunasiku nilikukuta katika gari yangu ukaniomba msaada Nikulete mpaka mitaa hii.
"Ooh Nimekukumbuka ila Samahani Sana kwa lile tukio sikuwa na jinsi ".
Aliongea huku akipiga goti kwa nidhamu kumshukuru mwanadada yule ambaye kwa mara ya pili sasa alikuwa msaada mkubwa mno kwake.
Baada ya muda wakautengeza urafiki ambao chanzo chake ilikuwa ngumu mno kwa watu kutambua. Uwepo wa Sam Ulifanya furaha ya stellar kuongezeka mara dufu kila leo na hasa pale alipokawa akiona mipango yake ya kila siku ikiwa na director katika kila hatua aliyokawa akiipiga.
Jioni moja walipanga Kutoka ilikuweza kutalii manzari ya jiji kwa Masaa kadhaa kisha kila mtu angerejea kujipumzisha. Muda wa miadi ukifika na kila mmoja aliwasili kwa wakati huku nafsi ya stellar ikiwa na furaha zaidi kuwa Karibu na Sam kila pale anapohitaji.
"Sam...? ".Alimuita jina lake ilikumpa utayari wakumsikiliza juu ya nini ambacho stellar alikuwa akihitaji kukiongea ,Ilikuwa ni baada ya kimya cha muda mrefu ambacho kilitawala baina ya watu wale wawili huku kila mtu akiwa busy kutazama mazingira ya sehemu ile.
"Naam... ".
"Tumejuana kwa bahati mbaya Sana uwenda bila mimi Kuwepo eneo lile la tukio siku ile basi ingekuwa bahati mbaya zaidi kwa wako lakini pia sitamani iwe bahati mbaya zaidi kuishi na rafiki nisiyejua hata historia yake kwa ufupi ya hapo awali mpaka sasa, Kwetu mimi ndo mtoto wapekee wakike baba angu mzee SUDDEIS anao uwezo wakifedha Kiasi Fulani ameunga ubia na baadhi ya makampuni makubwa hapa nchini mbali na hivyo yeye sio mtu wakutulia Sana nyumbani na mama yangu ni mama tuu wanyumbani tunaishi Mbezi siku moja nitakuchukua na kukupeleka kwetu ukapaone".
Alimaliza kumueleza kuhusu yeye na familia yake huku akijiweka sawa kuyasikiliza kwa upande wa Sam.
Itaendelea......
Naam hiyo nisehemu ya nne usikae mbali na sehemu ya tano inakuja hivi punde huyu ni Stellar usikose sehemu ijayo iliuweze kumjua Sam ni nani hasa na hiki kiapo ni cha Nani na iweje Damu yangu haipotei.... Ulikuwa nami mwanadada ZAYNABTALY usisahau kulike na kushusha comments ya nguvu katika page hii iliniweze kuendelea kukuletea simulizi maridhawa kupitia mkono wangu page........
KIAPO CHA SIRI (Damu yangu haipotei) Mtunzi : ZAYNABTALY 0625756953 SEHEMU YA 4....... Ilipoishia...... " We Koma wewe mimi sio mama yako nataka changu ". Yalikuwa maneno yaukali ambayo yalimchoma moyo na kumfanya akose cha kukiongea mbele ya mama yule ambaye jaziba zake aliamini zingetulia kwa pesa tuu na sio vinginevyo. *******SONGA NAYO******** Wakati akiwa anahaha asijue chakumpa yule mama mara alisikia sauti ambayo aliwahi kuisikia siku zilizo pita. "Habari zenu..? " ilikuwa nisauti nzuri yenye kupendeza Kutoka kwa Stellar. "Salama ". Aliitikia huku akiwa hamkumbuki mwanadada yule aliwahi kumuona wapi Wala kuisikia sauti yake. "vipi Mbona hapa Kuna tatizo? ".aliuliza ilikuona namna atakavyoweza kusolve tatizo lile. "yaani Dada angu acha tuu ". Kabla ya yule kijana kutia neno lolote mara yule bibi akadakia. "Kama wewe ndo Hawala yake haya msaidie kulipa pango sasa sio kukitumia tuu chumba changu na kukiacha hata gest wanalipa pango eeeh... ". Maneno ambayo yalimfanya stellar staajabu kwa yale maneno yaliyomshukia ila hakuwa na jinsi akaingiza mkono wake katika pochi yake kisha akatoa noti za elfu kumi na kuanza kuhesabu. Kisha akampatia yule mama "nimekulipia na miezi miwili ijayo ". "Ooh asante Sana Dada angu nashukuru Sana kwa msaada wako ". "Usijali ". "naushukuru huyu malaya wako Kaja kukupa msaada leo saa sivyo pangechimbika hapa leo maana habari zako zote ninazo mpuuzi wewe kukicha kuleta wasichana wa ajabu ajabu nyumbani kwangu na sijui hata utakuwa lini maana hela yenyewe huna hae hohe tuu kama mimi ila msumbufu mtaa mzima huu wanakujua wewe kwa jinsi ulivyokicheche na mwizi na sikia hata juzi ukitoka kuuliwa tandika lakini Mi hata sijali hayo muhimu umenipa pesa yangu " Yalikuwa maneno ya mama mwenye nyumba huku taratibu akikanyaga hatua kuondoka eneo lile. "Daah niwie radhi tafadhali maana bila mimi yote haya Sidhani kama yangekusulubu. "Aliongea yule kijana mwenye sauti ya upole ambayo ilienda sambamba na sura yake. Macho yake ya aibu yasiyo na hata chembe ya ukaidi ndio yaliyokuwa yakitalii kwa kuibia juu ya mwanadada yule aliyemsaidia kutoka katika sakata lile huku machozi yakimlenga katika macho yake juu ya lile tukio la muda mfupi lililotokea. "usijali ila nilikuwa naomba wasaa wakuongea na wewe kwa uchache? ". "Aah usijali Karibu ndani ". "Naitwa Stellar "alijitambulisha baada ya kuingia ndani ya chumba cha kijana yule kilicho pambwa na kitanda kimoja kikubwa cha Ukubwa wa tano kwa sita, kiti cha plastiki, meza ndogo iliyopangwa vyombo vichache chini yake. kwa chini kulikuwa na jiko la mafuta pamoja na sufuria mbili chafu. Baada ya kukamilisha kutembeza macho yake ndani ya chumba kile sasa macho yake yalikutana na macho ya yule mvulana. "Mi naitwa Sam Karibu kwangu". "Asante, sijui unanikumbuka..? "aliuliza ilikuweza kutambua uhai wakumbukumbu juu ya tukio lile la kukutwa ndani ya gari la watu na kuhitajia msaada. "Hapana Labda unikumbushe tulionana wapi ". "any way kunasiku nilikukuta katika gari yangu ukaniomba msaada Nikulete mpaka mitaa hii. "Ooh Nimekukumbuka ila Samahani Sana kwa lile tukio sikuwa na jinsi ". Aliongea huku akipiga goti kwa nidhamu kumshukuru mwanadada yule ambaye kwa mara ya pili sasa alikuwa msaada mkubwa mno kwake. Baada ya muda wakautengeza urafiki ambao chanzo chake ilikuwa ngumu mno kwa watu kutambua. Uwepo wa Sam Ulifanya furaha ya stellar kuongezeka mara dufu kila leo na hasa pale alipokawa akiona mipango yake ya kila siku ikiwa na director katika kila hatua aliyokawa akiipiga. Jioni moja walipanga Kutoka ilikuweza kutalii manzari ya jiji kwa Masaa kadhaa kisha kila mtu angerejea kujipumzisha. Muda wa miadi ukifika na kila mmoja aliwasili kwa wakati huku nafsi ya stellar ikiwa na furaha zaidi kuwa Karibu na Sam kila pale anapohitaji. "Sam...? ".Alimuita jina lake ilikumpa utayari wakumsikiliza juu ya nini ambacho stellar alikuwa akihitaji kukiongea ,Ilikuwa ni baada ya kimya cha muda mrefu ambacho kilitawala baina ya watu wale wawili huku kila mtu akiwa busy kutazama mazingira ya sehemu ile. "Naam... ". "Tumejuana kwa bahati mbaya Sana uwenda bila mimi Kuwepo eneo lile la tukio siku ile basi ingekuwa bahati mbaya zaidi kwa wako lakini pia sitamani iwe bahati mbaya zaidi kuishi na rafiki nisiyejua hata historia yake kwa ufupi ya hapo awali mpaka sasa, Kwetu mimi ndo mtoto wapekee wakike baba angu mzee SUDDEIS anao uwezo wakifedha Kiasi Fulani ameunga ubia na baadhi ya makampuni makubwa hapa nchini mbali na hivyo yeye sio mtu wakutulia Sana nyumbani na mama yangu ni mama tuu wanyumbani tunaishi Mbezi siku moja nitakuchukua na kukupeleka kwetu ukapaone". Alimaliza kumueleza kuhusu yeye na familia yake huku akijiweka sawa kuyasikiliza kwa upande wa Sam. Itaendelea...... Naam hiyo nisehemu ya nne usikae mbali na sehemu ya tano inakuja hivi punde huyu ni Stellar usikose sehemu ijayo iliuweze kumjua Sam ni nani hasa na hiki kiapo ni cha Nani na iweje Damu yangu haipotei.... Ulikuwa nami mwanadada ZAYNABTALY usisahau kulike na kushusha comments ya nguvu katika page hii iliniweze kuendelea kukuletea simulizi maridhawa kupitia mkono wangu page........
Artikel Terkait
MUUZA MAZIW EP 07 “aaaaahh!! Jamani wifi wao!!” Aliongea kwa furaha baada ya kumuona mgeni aliyekuwa akigonga ni penina. “asante wifi , shikamoo!” Penina aliongea na kisha kumkumbatia wifi yake kwa furaha. “ marhaba wifi ,vipi masomo?” Aliongea huku akiipokea mizigo aliyo ibeba “naendelea vizuri tu wifi” “haya mungu akusaidie” Aliongea lisa na kuelakea sebuleni , aliiiweka mizigo pembeni ya kochi na kasha kuelekea sehemuk ilipo friji. Penina, penina akaamua kuichukua mizigo ili aipeleke chumbani. “hapana wifi, hapana , hiyo iache hapo hapo nitaiingiza mwenyewe,, wewe kwanza kunywa juisi upumzike.“ Aliongea lisa huku akiwa ameshikilia jagi lenye juisi pamoja na glasi, alifanya hivyo kwa sababu chumba anachotakiwa kulala penina ndicho chumba ambacho amemficha muuza maziwa. “usipate tabu wifi wangu kunywa juisi upumzike, nipo kwa ajili yako “ Aliongea lisa huku akiibeba mizigo na kuelekea chumbani na kumuacha penina akinywa juisi taratibu. Alipoingia chumbani alimshutua muuza maziwa na kumweleza hali halisi. “kwahiyo nitatoka saa ngapi humu?” “ itabidi uvumilie mpaka usiku wifi akilala , mlango wa nje nitauacha wazi leo” Aliongea lisa “Sawa lakini vipi kuhusu chakula manaake niana njaa” “ usijali nitakuletea utakula humu humu , jitahidi usitoke nitajaribu kufanya mpango hata kamakabla ya usiku ikiwezekana” “poa” Muuza maziwa aliitikia “alafu nitaa……” Lisa alikatiza kauli yakebaada ya kusikia mlio wa kitasa kikifunguliwa. Haraka haraka muuuza maziwa aliingia kabatini na kisha lisa aliufunga mlango wa kabati hiyo kabla hata hajauachia mlango huo alisikia sauti nyuma yake. “wifi mbona unagombana na hilo kabati!?” Swali hilotoka kwa penina lilimfanya lisa ashikwe na kigugumizi cha ghafla huku akitoa maelezo ya kujikanyagakanyaga. “ah, mh, a-, u-n-a-j-u-a hi-li ka-ba-ti ni bo-vu” “limeharibika , ooh, mungu wangu!” Penina aliongea huku akilisogelea kabati hiloili kuiangalia sehemu ilipoaribika. “ah, hapana wifi usiiguse hapa nimeitegesha , iache hivyo hivyo mpaka atakapokuja fundi kulirekebisha” Aliongea Lisa haraka haraka. “okey”[sawa] Aliongea Penina huku akitikisa kichwa kuonyesha kwamba ameelewa. “nataka kuoga wifi” “na kweli manaake umechoka kweli kweli wifi yangu” Aliitikia Lisa haraka haraka kwani alijua huo ndio upenyo wa kumtoa muuza maziwa. Na kweli penina alipoingia bafuni lisa aliufungua mlango wa kabati haraka na kumtoa muuza maziwa , akala chakula haraka na kuanza safari ya kutoka nje ya nyumba hiyo , walipofika kwenye mlango wa kutokea muuza maziwa alimbusu lisa kwa mara ya mwisho , alipomaliza kufanya hivyo alitoka ndani ya chumba hicho na kutokeza koridoni ili atoke nje kabisa ya nyumba hiyo lakini kabla ya kufanya hivyo alisikia muungurumo wa gari, halikuwa gari lingine bali gari la Jerry mume wa Lisa. Hofu iliwaingia kwa ghafla na haraka haraaka walirudi tena chumbani kwa penina , ambapo kama kawaida alimfungia muuza maziwa kabatini, hawakuwa na njia nyingine tena bali hile waliyoipanga awali, muuza maziwa asubiri mpaka usiku wa manane Penina atakapo lala ndipo atoke kwani Lisa atauacha mlango wa kutokea wazi. Lisa alipomaliza kumfungia muuza maziwa katika kabati alitoka nje ya chumba hicho,akiwa koridoni aligongana ana kwa ana macho na mumewe. Wote wawili waliinamisha vichwa vyao chini. Kwani kila mmoja aliona aibu kwa kumsaliti mwenzake. Lisa kwa muuza maziwa na Jerry kwa sekritari wake. “Ah, mmh, wifi amekuja , kakaribu!” Aliongea Lisa kwa kujiumauma huku akiwa na wasi wasi. “ asante amekuja saa ngapi?” “sio muda mrefu” “aah yuko wapi sasa nimsalimie?” “yuko bafuni anaoga” “Okey” [sawa] Aliitikia na kisha kuelekea chumbani kwake. Lisa nae alimfuata mumewe nyuma hukubado akiwa na hofu juu ya kugundulika kwa uwepo wa muuza maziwa ndani ya nyumba hiyo. “Pole na kazi dear” Aliongea Lisa huku akijibaraguza kwa kumvua tai mume wake, macho yake bado yalikuwa na aibu sababu bado alikuwa na wasi wasi kwamba labda mumewe amegundua chochote. “ah, asante mpenzi” Aliitikia Jerry huku akitabasamu, lakina nae pia tabasamu lake liliishia mdomoni tu moyoni nafsi ilimsuta . Maovu aliyoyafanya na sikritari wake ofisini kwake yalikuwa bado yakionekana katika kichwa chake. Akavua nguo na kuingia bafuni kuoga lisa nae alimfuata na kujumuika nae kuoga . Alifanya hivyo ili Jerry hasihisi chochote. Walioga huku kila mmoja akiwa hana habari na mwenzake. Kwani wote wawili walikuwa wamechoka, walipomaliza kuoga wakavaa na kasha kwenda sebuleni. Huko wakamkuta Penina akianga lia tv. “mdogo wangu huyo!” Jerry aliongea kwa furaha huku wakicheka. “kaka!” Penina aliitikia na kisha kumkimbilia kaka yake. “waoo!!!” Waliongea kwa pamoja na kisha kukumbatiana kwa furaha. “habari za masomo!?” ITAENDELEA.. ... Read More
*MUUZA MAZIW EP 08* “nzuri tu kaka, shikamoo!” Aliitikia Penina na kasha kumwamkia kaka yake “marhaba mdogo wangu>“ Aliitikia salamu. “Penine kanenepa kweli safari hii, shule imempenda kweli.” Aliongea Lisa. “hapana wifi!?” Penina aliongea na kasha kucheka, ukweli ni kwamba kweli alikuwa amenenepa na kujengeka shepu kwa mahipsi na makalio yaliyo fungashika kiinye plus gwedegwede. Waliongea mengi wakiwa na furaha ya kuwa pamoja tena. Upande wa Lisa moyoni hakuwa na furaha hata kidogo, muda wote alifikiria jinsi ya kumtoa muuza maziwa ndani ya nyumba hiyo. Alifahamu fika jinsi swala hilo lilivyokuwa gumu kwani chumba alichomficha ndicho chumba atakacholala penina , hakuelewa angeweza vipi kumtoa muuza maziwa katika chumba hicho bila ya Penina kugundua. “sijui nitafanya nini mungu wangu?” Aliwaza bila kupata jawabu, hakuona aibu kumshikilikisha Mungu katika uovu wake. “atalala tu lakini , na hivi alivyochoka, na huo ndio utakuwa muda muafaka” Alizidi kuwaza, Hiyo ndio ilikuwa njia pekee aliyoitegemea alitumaini Penina atakapolala ndio uwe muda muafaka. “wifi vipi mbona utafikiri uko mbali sana!?” Penina aliuliza baada ya kugundua kwamba Lisa hayupo pamoja nao katika maongezi. “hapana nipo , mbona tupo pamoja!.“ Aliitikia Lisa haraka haraka baada ya kuzinduka toka kwenye mawazo mazito aliyokuwa nayo. “kweli Lisa upo tofauti sana leo” Jerry nae alikazi “hapana jamani mbona nipo sawa!” Lisa alizidi kujitetea kwa nguvu zake zote kwani hakutaka mtu yoyote ahisi chochote kuhusiana na swala hilo la muuza maziwa, alichokifanya baada ya hapo ni kujaribu kujichekesha na kuonyesha kuwa ana furaha ili kupoteza kabisa hisia za mumewe pamoja na wifi yake. Waliongea kutwa nzima mpaka usiku ukaingia , baada ya chakula cha usiku kila mmoja alielekea chumbani kulala Jerry na mkewe chumbani kwao na Penina pia alielekea chumbani kwake. Wakiwa kitandani kwao si Jerry wala mkewe aliyeonekana kumjali mwenzake, kila mmoja aligeukia upande wake , kila mmoja alirizika na usaliti alioufanya mchana wa siku hiyo. Jerry alipotembea na Sekritari wake wakati Lisa alipotembea na muuza maziwa. Hakuna aliyejua maovu ya mwenzie kila mmoja alimuona mwenzake karanga bao na kumlalia mzungu wa nne. xxxxx- – – – xxxxxx—- – — xxxxxxxx Saa sita na nusu usiku Penina alishtuka toka usingizini , hii ni baada ya kusikia mlio wa kabati likifunguliwa , haraka alisogeza mkono wake kwenye swich ya taa na kuiwasha. Mwanga ulitanda chumba kizima . Penina hakuamini alipomuona mtu akiwa amesimama karibu kabisa na kabati huku kabati likiwa wazi. “kaka! , kaka!, mwizi! Mwizi!1” Penina alipiga yowe kwa hofu huku akimwangalia muuza maziwa vizuri. Muuza maziwa alikuwa akitetemeka mwili mzima, sauti ilikwisha fika chumbani mwa akina Jerry, Jerry alikurupuka na kumwamsha mkewe . Lisa alichanganyikiwa kusikia taarifa hizo alijua kwa vyovyote vile huyo atakuwa ni muuza maziwa. “mungu wangu, sijui nifanyeje mie!!” Aliongea Lisa kwa mshituko CHANZO: /“utafanyeje nini?, twende au umesahau kwamba tuna Bastora!?” Jerry aliongea akiwa ameishikilia bastora yake kwa kujiamini. Hakujua kwamba mkewe hakuwa anaogopa mwizi bali alimhurumia muuza maziwa. Muuza maziwa alizidi kutetemeka hakujua afanye nini miguu yote iliishiwa nguvu alishindwa kusimama wima akaegamia kabati. “da– da—mi-mi si-o mwi-zi!-zi-zi” Aliongea muuza maziwa huku akitetemeka kupita kiasi. ITAENDELEAMUUZA MAZIW EP 09 ILIPOISHIA….. “kaka! , kaka!, mwizi! Mwizi!1” Penina alipiga yowe kwa hofu huku akimwangalia muuza maziwa vizuri. Muuza maziwa alikuwa akitetemeka mwili mzima, sauti ilikwisha fika chumbani mwa akina Jerry, Jerry alikurupuka na kumwamsha mkewe . Lisa alichanganyikiwa kusikia taarifa hizo alijua kwa vyovyote vile huyo atakuwa ni muuza maziwa. “mungu wangu, sijui nifanyeje mie!!” Aliongea Lisa kwa mshituko “utafanyeje nini?, twende au umesahau kwamba tuna Bastora!?” Jerry aliongea akiwa ameishikilia bastora yake kwa kujiamini. Hakujua kwamba mkewe hakuwa anaogopa mwizi bali alimhurumia muuza maziwa. Muuza maziwa alizidi kutetemeka hakujua afanye nini miguu yote iliishiwa nguvu alishindwa kusimama wima akaegamia kabati. “da– da—mi-mi si-o mwi-zi!-zi-zi” Aliongea muuza maziwa huku akitetemeka kupita kiasi. MUENDELEZO WAKE : “kumbe wewe nan……….?” Penina alijikuta anakatisha kauli yake baada ya kumuangalia vizuri muuza maziwa, hakuamini alichokiona alihisi kama vile yuko ndotoni. “Karani!!!!” Aliita Penina kwa mshangao huku akiwa ameduwaaa. “Penina!!!” Muuza maziwa nae aliita mara baada ya kumuangalia vizuri penina. Wote walibaki wakishangaa huku wakiangaliana usoni, kumbukumbu zao zilirudi nyuma miaka miwili iliyopita. Suji sekondari katika bweni la wasichana chumba namba ishirini na moja. Penina akiwa amelala kwenye kitanda cha dabodeka, ikiwa ni mara yake ya kwanza kulala ndani ya chumba hicho. Sababu hiyo ilikuwa ni siku yake ya kwanza toka ahamie bwenini , mwanzo alikuwa akikaa kwenye nyumba ya mkuu wa shule. Akiwa kitandani hapo alisikia mlio wa mluzi ukisikika kwa mbali karibu kabisa na dirishani sehemu ambapo alikuwa amelala. “it ndizi time!” [ni muda wa ndizi] Mwanafunzi mmoja aliongea kwa sauti ya kunon’gona kasha wenzake walicheka kwa sauti za chinichini. Penina hakuelewa chochote kilichoendelea. Mwanafunzi mmoja aliamka na kwenda kufungua mlango. Watu wane wakiwa wamejitanda khanga waliingia ndani, Penina alizani watu hao ni wasichana. Aliduwaa pale walipotoa Khanga zao. Wote walikuwa ni wanaume. Kila mmoja alienda kwenye kitanda chake waliongea lakini sauti zao zilikuwa za kunon’gona. Penina alibaki ameduwaa tu asijue nini cha kufanya , katika chumba hicho ni yeye peke yake ndio alikuwa amelala peke yake. Alijaribu kuutafuta usingizi lakini alishindwa , vilio vya mahaba alivyokuwa akivisikia usiku huo vilimtesa kupita kiasi, alitamani na yeye lakini hakukuwa na mwanaume kwa ajili yake. Alibaki akijigaragazagaragaza tu kitandani kwake. Mpaka kufikia saa kumi na nusu alfajiri wanaume walipoondoka bado yeye alikuwa hoi. Mchna alimfuata maria na kumweleza shida yake. “na wewe unataka ndizi?” “mmh, mwenzangu manaake hali mbaya!” “usihofu , nitamwelza Bakari akufanyie mpango”. “nitafurahi kweli maanake we acha tu!” Ahadi ya maria ilikuwa kweli , Penina aliteseka kwa siku moja tu , siku iliyofuata nae aliletewa ndizi yake. Ni hapo ndipo alipokutana naKarani mchunga n’gombe wa akina Bakari, ambae sas ndio muuza maziwa. Karani alikuwa akimfikisha Penina mpaka basi jambo lililomfanya Penina ampende kupita kiasi, alimuahidi kwamba atakuwa nae milele lakini ajabu ghafla alitoweka. Alipomuuliza Bakari kuhusu swala hilo alimwambia hajui alikoelekea. “nyumbani katoroka alafu ameiba baadhi ya nguo zangu , hafai kabisa yule jamaa.” BakaRi aliongea kauli hiyo iliyomaliza kabisa nguvu za Penina. Alimpenda sana Karani na alitaka kuwa nae siku zote za maisha yake. Hakuelewa ataishi vipi bila kuwa nae. “lakini usihofu Penina nimekuletea mwingine” Bakari aliongea akiwa ametabasamu huku akishika bega la kijana mpya aliyekuja nae siku hiyo. Penina alimwangalia kijana huyo kuanzia chini mpaka juu lakini hakuona hakuona cha kumlinganisha na Karani. “Siitaji tena kama Karani hayupo basi “ Penina alijibu kwa dharau. “Penina hata huyu yuko bomba tena mkali kuliko hata Kara….” “Nimesema sitaki husikii” Penina alifoka tena kwa sauti kubwa jambo ambalo liliwaogopesha wote, sababu lilikuwa ni jambo la hatari, hawakutaka kuendelea kumsemesha waliogopa angewasababishia msala kwa mlinzi endapo ataisikia sauti yake. Siku iliyofuata Penina aliamua kuhama chumba hicho kwani hakuona raha tena ya kuwa ndani ya chumba hicho wakati Karani hayupo. Rafiki zake walimbembeleza asahau habari ya Karani na akubali kuwa na yule kijana mpya ili arudi kwenye kile chumba lakini yeye aliwakatalia katakata , hakuona mwanaume wa kumfananisha na Karani wake. Wiki moja baada ya Penina kuhama ndani ya chumba hicho mlinzi alishtukia mlinzi alishtukia kila kitu . Aliwakamata wanaume wote wakiwa ndani ya kile chumba cha kina Maria na kasha wanafunzi wote waliokutwa ndani ya chumba hicho walifukuzwa shule. Penina alikuwa ameponea chupuchupu, kama isingekuwa Karani kutoroka nyumbani kwa kina Bakari basi leo hata yeye angelikuwa miongoni mwao na Karani wake. Wiki moja baada ya Penina kuhama ndani ya chumba hicho mlinzi alishtukia mlinzi alishtukia kila kitu . Aliwakamata wanaume wote wakiwa ndani ya kile chumba cha kina Maria na kasha wanafunzi wote waliokutwa ndani ya chumba hicho walifukuzwa shule. Penina alikuwa ameponea chupuchupu, kama isingekuwa Karani kutoroka nyumbani kwa kina Bakari basi leo hata yeye angelikuw miongoni mwao na Karani wake. Jambo hilo lilimfanya azidi kumpenda Karani na kujipa ahadi kwamba lazima siku moja atamtafute mahali popote duniani.. Ajabu leo anamkuta ndani ya chumba chake cha kulala. Hakutaka kumuuliza amefikaje , iwe kweli amekuja kuiba au vyovyote alichofikiria sasa ni kumuokoa ili kaka yake asijue kwamba yumo humo. “Ngo, ngo ngo” Mlango uligongwa , Penina pamoja na Muuza maziwa walichanganyikiwa. “Penina!, Penina! Fungua mlango usihofu nina Bastora!” Kauli hiyo toka kwa Jerry ndio ilizidi kuwachanganya akili. “Tafadhari niokoe Penina sitaki kufa leo!” “Usihofu Karani nitafanya kila njia!” Penina aliongea. ITAENDELEA..*MUUZ MAZIW EP 10* MWISHOOOOOOOOO Wazo la kuingia kabatini lilikuja tena kichwani kwa muuza maziwa, na Penina bila kuchelewa akaufunga mlango wakabati hilo. “Penina fungua mlango” alijua labda mwizi huyo amemteka mdogo wake. Upande wa lisa alizidi kuchanganyikiwa. Sauti ya Jerry ilisikika tena huku akizidi kuugonga gonga mlango kwa nguvu, akilini mwake “Fungua Penin…..” Jerry alikatiza kauli hiyo baada ya Penina kufungua mlango. “yuko wapi, yuko wapi huyo mwizi?’” Jerry aliuliza huku akiwa ameishika Bastora yake sawia , tayari kwa kufyatua risasi. “hapana kaka!” “hapana nini kakimbia eeh au kaificha?” “sio mwizi kaka!’ “sio mwizi!? ,nani? Na yuko wapi?” Aliuliza kwa mshangao. “Ni ndoto nilikuwa naota “ “Ndoto!!?” “ndio kaka!” “ooh! Jamani penina umetushtua wenzako , uuh!” Aliongea Lisa na kuvuta pumzi , kwani wasi wasi ulimtoka baada ya kusikia kama ni ndoto. “Penina unauhakika kama ni ndoto!” Jerry aliuliza huku akiliangalia kabati, kasha akaanza kulisogelea taratibu. “ndio ! Ndio! Kaka” Penina aliitikia kwa hofu , alihisi kwamba pengine Jerry amegundua kitu, hali ilikuwa mbaya zaidi kwa Lisa ambae alichanganyikiwa kabisa. “hapana siwezi kurihusu jambo hili hata kidogo” Aliwaza Lisa pale Jerry aliponyoosha mkono ili kushika kitasa cha kabati hilo., alimkimbilia haraka. “Honey umekwisha elezwa kwamba ni ndoto kwanini unapoteza muda , twende tukalale mpenzi mwenzako nimechoka>“ Lisa aliongea kwa sauti laini. “Hapana nataka kufunga vizuri hili kabati”. Aliongea Jerry huku akilisukumiza kabati, hakujua kwamba halijajifunga vizuri kwa sababu kuna mtu ndani. Alilisukumiza huku muuza maziwa akisikilizia maumivu ya kuminywa na kabati hilo, alijuzuia kupiga kelele huku mwili mzima akitetemeka kwa woga. “Achana nalo hilo Dear kwanza kabati lenyewe hilo bovu.” “bovu!!!” “eeh bovu hata mimi wifi alinieleza’ Penina alidakia “sasa kwanini hamjamuita Fundi?” “usijali mpenzi nitamuita kesho, twende basi tukalale.” Lisa aliongea kwa sauti nyororor ambayo ilimshawishi Jerry moja kwa moja. “Lala salama Penina “ Aliaga “sawa kaka “ Walitoka na kwenda chumbani kwao wakiwa wamekumbatiana.. Penina aliufunga mlango kwa furaha na kisha kwenda kulifungua kabati. Alikuwa na hamu kweli ya kuwa na Karani wake. Karani ambae hadi wakati huo alikuwa akitetemeka kwa hofu, hakuamini kabisa kwamba ndani ya chumba hicho yumo yeye na Penina pekeyeo. “kabla ya yote nikumbatie mpenzi!.“ Penina aliongea akiwa na tabasamu zito usoni kwake . Muuza maziwa hakusita kumkumbatia. “siamini kabisa mpenzi!” “hata mimi penina!” “hivi umejuaje kwamba ninaishi hapa?” Aliuliza penina akiamini kwamba kilichomleta muuza maziwa humo ni yeye. “Nilikuona ulipokuwa unaingia” Muuza maziwa alijibu, hakutaka kumweleza kwamba aliyemleta humo ni wifi yake. “ndio maana nakupenda Karani!” “hata mimi nakupenda!” Karani nae akaitikia Alimsogelea zaidi na kumbusu ‘mwaaaa!!!’ ‘Mwaaa!!!’ Penina nae aliitikia busu hilo. Muuza maziwa kama kawaida yake akaanza manjonjo yake, Penina alikwisha jua nini kinachofuata akaanza kujichekesha kwa kicheko cha kugunaguna. “unajua nafanya kazi gani sasa?” Muuza maziwa aliuliza “sijui!” Penina aliitikia “Nauza maziwa!” “aah kwa hiyo nikuite Muuza maziwa sio.” “sawa sawa watu wote wananiita hivyohivyo.” “haya basi muuza maziwa nataka unipe mambo” “hapa ndio mahala pake, utapata ondoa hofu!” Muuza maziwa aliitikia na kuanza kumtekenya Penina kwa ulimi wake. Penina alicheka kwa kicheko cha chinichini, mambo ya muuza maziwa yalimfanya akumbuke kipindi walipokuwa wote kule shule kipindi Karani ni mchunga ng’ombe lakini sasa yuko mjini na ni MUUZA MAZIWA. END OF SEASON ONE. ... Read More
Story........ NI WEWE TU PENINA Sehemu ya kumi na mbili (12) By GIVAN IVAN Phone & whatsapp.... 0769673145 Ilipoishia.......... Penina na Frank walishangazwa Sana na maamuzi ya Nolan lakini hata hivyo Nolan hakutaka wamuulize swali lolote, alimwamuru dereva wa tax ile awashe gari na kuondoka. Kisha Nolan naye akaingia kwenye gari yake na kugeuza kuwafuata vijana wale wa the killer na wakati huo walikuwa tayari wameshaungana wote kwa maana ya kikosi kile cha kwanza kilichokuwa kikimtafuta Nolan na kile cha pili kilichokuwa kikimtafuta Frank. *********Endelea ********* Vikosi vile viwili ambavyo vilikuwa kwenye magari mawili viliweza kumuona Nolan akiwa anarudi kule alikotoka. Vikosi vile navyo haraka haraka vikageuza magari yao na kuanza kumfuata Nolan. Nolan aliweza kuwaona wakimfuatilia na ndio kitu ambacho Nolan alikitaka, lakini kilichomshangaza Nolan ni kwamba Sasa anafuatiliwa na magari mawili tofauti na mwanzo walipokuwa wakimfuatiliwa na gari moja. Lakini Nolan hakujali hilo, akaacha barabara na kukataa kushoto na kuingia kwenye njia moja ya vumbi ambayo haikuwa ikipita watu Mara kwa Mara. Nolan baada ya kuingia kwenye barabara ile akasimamisha gari na kushuka ndani ya gari lile. Na sekunde hiyo hiyo magari mawili ya vijana wale wa the killer wakawasili pale alipo Nolan na kusimamisha magari yao Kisha wote wakashuka kwenye magari yao ambao kwa pamoja walikuwa Nane. Vijana wale wa the killer walishaangaa baada ya kufika na kumkuta Nolan peke yake badala ya kuwakuta wote Nolan pamoja na Frank. Nolan alikuwa amesimama pembeni ya gari yake huku akiwatazama vijana wale waliokuwa wakimsogelea taratibu. "mwenzako yuko wapi?" kijana mmoja wa the killer akamuuliza Nolan huku akijaribu kumkamata Nolan kwenye shingo. Kijana yule alijikuta akipokea ngumi Nzito ya tumbo kutoka kwa Nolan ambayo ilimfanya adondoke chini kwa magoti. Wale vijana wengine walishtuka kuona mwenzao alivyotandikwa ngumi ya tumbo. Lakini hata hivyo bado vijana wale waliamini Nolan hawawezi kwasababu wako wengi na wote wana silaha. Vijana wale kwa pamoja wakaanza kumfuata Nolan, Nolan naye akapiga hatua kadhaa na kurudi nyuma na kuwasubiri. Vijana wale walipomkaribia Nolan kwa pamoja wakaanza kurusha ngumi na mateke kumvamia Nolan. Lakini Nolan alikuwa akiwakwepa tu bila kumgusa mtu yoyote, ndani ya dakika tano Nolan alikuwa akiwakwepa vijana wale waliokuwa wakimshambulia bila mafanikio. Lakini Nolan alizubaa kidogo na kujikuta akipokea ngumi Nzito ya uso kutoka kwa mmoja wa vijana wale. Lakini hata hivyo kijana yule aliyembahatisha Nolan ngumi ya uso ikawa ndio mwisho wake wa kuishi duniani, kwani Nolan alimkamata na kuanza kumshambulia kwa ngumi za haraka haraka na kummaliza kwa kumvunja shingo. Wale vijana wengine ndio walishtuka vibaya mno na kuona huyu mtu sio wa kawaida, wakaamua wamshambulie kwa silaha zao baada ya kuona hawatamuweza kwa mkono. Vijana wale walichomoa bunduki zao na kuziweka tayari kummaliza Nolan. Lakini Nolan alikuwa tayari ameshaingia kwenye gari na kuondoka kwa spidi kali na kuwaachia vumbi kali Vijana wale. Nolan aliamua kukimbia baada ya kuona vijana wale wakitoa bunduki zao, hivyo asingewaweza kwa sababu yeye hakuwa na silaha yoyote. Vijana wale nao hawakumuacha waliingia kwenye gari na kuanza kumfuatilia Nolan. Lakini mpaka pale Nolan alikuwa tayari ameshawapoteza vijana wale na yeye Sasa alikuwa ameshika njia ya kuelekea nyumbani. * Mzee Joel akiwa ameketi sebuleni kwake akisubiri majibu ya kuuwawa kwa Frank na Nolan simu yake ilianza kuita na alipoangalia mpigaji ni nani alikutana na Jina la Dickson, kijana ambaye mzee Joel ndio anataka amuoe mtoto wake Penina. Mara moja mzee Joel akaipokea simu ile. "mzee Joel habari yako?" akauliza Dick baada ya simu yake kupokelewa na mzee Joel. "salama kijana wangu habari ya huko"? Akajibu mzee Joel na kuuliza. " huku Safi tu, Sasa mimi nilikuwa nataka nije kumchukua Penina moja kwa moja nahitaji kuwa na familia Sasa. " akaongea Dick kumwambia mzee Joel. " kijana wangu usiwe na haraka tunaweka mambo Sawa na Muda wowote tutakuita uje umchukue mke wako. " akaongea mzee Joel kumpa moyo Dick. " unaweka mambo Sawa unaweka mpaka lini kama ni pesa nikekupa za kutosha mbona unanizungusha zungusha tu au nikuongezee pesa zingine? " akaongea Dick huku akionesha kuchoshwa na namna mzee Joel anavyomzungusha. "kijana wangu tafadhali naomba utulie Penina ni wako usiogope." mzee Joel akamwambia Dick. "nitulie nitulie mpaka lini nakuja Tanzania kujua Kwanini unanichelewesha kumuoa Penina na wakati nimeshakupa pesa nyingi Sana." akaongea Dick na kukataa simu. Mzee Joel alihisi kuchanganyikiwa hakujua afanye nini ili aweze kumuunganisha Penina na Dick. Na wakati huo huo mlango ulifunguliwa na akaingia Nolan huku akiwa amechafuka kwa vumbi. "Wewe mbwa mbona unaingia ndani kwangu bila hodi?" mzee Joel akamuuliza Nolan huku akiwa amevimba kwa hasira. "mzee tulia huu mchezo umeutaka mwenyewe lazima Frank amuoe Penina." akaongea Nolan maneno hayo ambayo yalizidi kumpandisha hasira mzee Joel na kujikuta akimrushia Nolan glass ya maji iliyokuwa kwenye Meza. Nolan aliigonga ngumi glass ile na kuipasua pasua. "ukiniletea upuuzi na wewe nitakupasua pasua kama hiyo glass." Nolan akamwambia baba yake mzee Joel na kuelekea chumbani kwake. * Frank na Penina baada ya kufika uwanja wa ndege walifuata taratibu zote na hatimaye wakafanikiwa kuingia ndani ya ndege na dakika chache baadae walikuwa angani wakielekea South Africa. "kama tukifanikiwa kufunga ndoa nitafurahi Sana yaani furaha nitakayokuwa nayo sidhani kama itaelezeka." aliongea Penina huku akiwa amejiegemeza kwenye kifua cha Frank. "usijali mpenzi kila kitu ambacho kinatokea kimepangwa na Mungu na vitakavyotokea mbele ni Mungu pia anajua, hakuna mwanadamu asiyependa furaha." akaongea Frank kwa upole kumuambia Penina. "ni kweli mpenzi wangu." akajibu Penina na safari ikaendelea kwa masaa kadhaa na hatimaye wakawasili South Africa Katika jiji la Johannesburg na kuchukua chumba Katika hoteli moja ya kifahari. Baada ya kupumzika kwa dakika kadhaa Penina na Frank waliwasiliana na Nolan na kumjulisha jinsi safari yao ilivyokuwa. Nolan aliwataka wakae kwa amani na wasiwe na hofu yoyote yeye anaweka mambo Sawa na yakiwa tayari bas atawajulisha. * Vijana wa the killer bado walikuwa wakimtafuta Nolan na Sasa waliwasili nyumbani kwa kina Nolan na kukutana na mzee Joel ambaye aliweza kuwaambia Nolan yupo ndani na akawaelekeza chumba chake wakammalizie huko. Vijana wale taratibu walianza kuelekea Katika chumba cha Nolan, lakini kwa bahati mbaya ama nzuri Nolan aliwaona. "mmeamua kunifuata mpaka nyumbani nyie mmeisha." akajisemea Nolan Kisha akatoka chumbani kwake akiwa kifua wazi na kukutana na vijana wale sebuleni. Kilikuwa kitendo cha kushtukiza vijana wale hawakutarajia kukutana na Nolan sehemu Ile. Kitambo waseme waweke silaha zao tayari Nolan alianza kuwashambulia, na baada ya dakika chache Nolan aliwaweka vijana wale wote chini kwa kuwavunja vunja sehemu za miili yao. Mzee Joel ndio hakuamini baada ya kuingia ndani na kukuta vijana wote wamelazwa chini alafu kidogo hivi akatokeza Nolan akiwa amepigilia suti nyeusi Kisha akamwambia baba yake ambaye ni mzee Joel, "naenda kwenye kikao cha harusi ya Penina na Frank na kama utahitaji kadi unijulishe nikuletee ya kwako." ....... Itaendelea. ... Read More
Story........ NI WEWE TU PENINA Sehemu ya Tano (5) By GIVAN IVAN PHONE & WHATSAPP_____0769673145 Ilipoishia........... Na wakati huo huo taratibu Frank alianza kurudiwa na fahamu Zake. Milango ya gari Ile aliyowekwa Frank ilifungwa, na Kisha gari likaanza kuondoka kwenda kumtupa Frank sehemu ambayo kamwe hatoweza kuonana tena na Penina. ********Endelea ******* Zaza pamoja na wenzake walipongezana kwa kazi waliyoifanya na kuamini tayari wameshampoteza Frank. Zaza alitoa simu yake na kumpigia mzee Joel na kumpa taarifa Ile. Mzee Joel alifurahi Sana na akaamini sasa tayari anakaribia kutimiza lengo Lake kumtenganisha Penina na Frank. "hahahaaaa ninachokitaka mimi lazima nikitimize mtoto ni wangu lazima aolewe na mtu ninayemtaka mimi." alisikika mzee Joel akijitambaa mwenyewe. * Masaa manne yamepita Sasa bila mafanikio yoyote ya kumpata Frank. Baba yake Frank, mama yake Frank pamoja na Angel wakiwa na Penina walishindwa kuelewa Frank amepatwa na nini ghafla hivyo. Penina ndio alihuzunika Sana hakujua afanye nini kwa wakati ule. "mama ngoja mimi nirudi nyumbani tu maana nahisi kuchanganyikiwa." aliongea Penina kumuambia mama yake Frank. Kisha akaingia kwenye gari yake na kuondoka huku akiwa hana furaha kabisa. Wazazi wake Frank walihisi kuchanganyikiwa kwa mtoto wao kupotea ghafla, lakini walijipa moyo na kuamua kusuburi labda pengine atarejea baada ya Muda. Penina alifika nyumbani na kuanza kupiga honi kwa fujo afunguliwe geti. Hii ilikuwa sio kawaida ya Penina kufanya hivyo, ikabidi Wazazi wake pamoja na Nolan pamoja na Irene watoke nje ili kujua kwa nini Penina amefanya vile. Geti lilifungjliwa Penina akaingiza gari ndani kwa kasi na kulipaki sehemu yake, Kisha akashuka huku akiwa amenuna na kuingia ndani bila kumsemesha mtu yoyote. "kulikoni tena huyu mbona haeleweki?" akauliza mama yake Penina kwa mshangao. "Nenda kamuulize unatuuliza sisi kwani tulikuwa naye." mzee Joel akamjibu mama Penina. Mama yake Penina aliondoka na kumfuata Penina chumbani kwake. Nolan naye akaungana na mama yake kwenda chumbani kwa Penina ili kujua tatizo ni nini. Mzee Joel alibaki akiwa anatabasamu tu kwasababu yeye alijua kila kitu kuhusu Penina. "Penina ni nini tena mwanangu?" akahoji mama yake Penina baada ya kufika chumbani kwa Penina na kumkuta akiwa analia. "Frank mama." akasema Penina huku akizidi kulia, na wakati huo huo Nolan naye aliwasili chumbani kwa Penina. "Frank kafanya nini tena mwanangu hebu nyamaza unieleze vizuri." akaongea mama yake huku akimbebeleza. Penina alimwelezea mama yake pamoja na Nolan mkasa mzima wa jinsi Frank alivyotoweka kimaajabu. Mama yake Penina pamoja na Nolan kaka yake Penina, walipigwa na butwaa kwa maelezo ya Penina. Lakini hata hivyo Nolan akamwambia Penina, "usijali mdogo wangu kwa Sasa wewe tulia mimi nitalifuatilia hili swala hapa nahisi kuna kitu." "kaka mimi naumia Sana sikutegemea kitu hichi tena ghafla hivi." akaongea Penina huku akizidi kulia. "najua unaumia ila nipe Muda nilifuatilie hili swala, naomba uwe mvumilivu." akaongea Nolan kumtuliza Penina. "nyamaza mwanangu usilie tena, mwachie kaka yako hii kazi atakusaidia." akaongea mama yake pia kumtuliza Penina. * Frank taratibu alianza kurudiwa na fahamu akiwa Katika gari Ile aliyowekwa, Frank alianza kujikagua na kugundua kuwa amefungwa miguu mikono pamoja na usoni, hivyo hakuweza kuona chochote zaidi alihisi yupo kwenye gari ambalo lipo kwenye mwendo wa kasi sana. Frank alipiga kelele lakini alitulizwa kwa kupigwa na kitu kizito cha uso na kuzimia tena. Baada ya safari ya masaa ishirini na nne, hatimaye Frank alifikishwa Katika misitu fulani inayopatikana huko tabora. Mida ya usiku usiku Frank alitolewa kwenye gari na kutupwa pembeni ya misitu Ile Kisha wao wakaingia kwenye gari na kuondoka kwa kasi sehemu ile na moja kwa moja wakaanza safari ya kurudi dar es salam na kumuacha Frank akiwa Katika hali mbaya Katika misitu Ile. Baada ya masaa kadhaa mbele Frank alizinduka na kujihisi yupo sehemu ambayo hakuweza kuilamba. Frank alipojaribu kunyanyuka aligundua kuwa amefungwa miguu, mikono pamoja na usoni hivyo hakuweza kufanya lolote. Frank aliamua kupiga kelele ili aweze kupata msaada lakini hakuweza kufanikiwa kupata msaada. Baada ya kupiga kelele kwa Muda mrefu bila kupata msaada, Frank aliamua kutulia na kusubiri chochote kitakachotokea huku akimuomba Mungu amsaidie.* Wazazi wake Frank walihangaika usiku na mchana bila mafanikio yoyote ya kumpata Frank. Ilifika sehemu Sasa wakaamua kumuachia Mungu kwasababu wao wameshachoka kumtafuta bila mafanikio yoyote. * Kaka yake Penina aitwaye Nolan yeye hakuamini kama Frank amepotea bali aliamini kuna mchezo unafanyika, Nolan alianza kuchunguza juu ya upoteaji wa Frank. Kwanza Nolan alianza kumchunguza baba yake ambaye Muda wote alikuwa pamoja na Irene mdogo wake Penina. "Baba wewe unalichukuliaje hili swala la kupotea kwa Frank mpenzi wake Penina?" akauliza Nolan. "hahahaaaa! wewe nani amekwambia Frank amepotea? Frank hajapotea kashapata mwanamke mwingine akatoroka naye wewe unasema amepotea, acha kujisumbua mwanangu." akaongea mzee Joel baba yake Penina kumuambia Nolan. "Kaka sikia nikuambie, mimi Nina uhakika Frank yupo na mwanamke mwingine nyie mnahangaika tu tena mwambie Penina aache kuhangaika na mwanaume ambaye hajatulia." akaongea Irene mdogo wake Penina kuunga mkono maneno ya baba yake. "Irene mdogo wangu huko unakoelekea unapotea, wewe una uhakika gani na maneno unayoongea?" akauliza Nolan kwa upole. "ana uhakika na anachokiongea wewe unafikiri yupo kwenye ndoto?" akadakia baba yake Penina kumtetea Irene. "Mbona mnateteana kama kuna kitu ndani yenu mbona siwaelewi?" akaongea Nolan kwa mshangao. "huwezi kutuelewa kwasababu upo nyuma Sana kama mkia wa ngombe." akaongea mzee Joel maneno hayo ambayo kidogo yalimfanya Nolan apandwe na hasira, lakini akajitahidi kuzishusha. "ok nashukuru kwa maneno yenu lakini nawaahidi lazima ukweli utajulikana." akaongea Nolan Kisha akanyanyuka na kuondoka. Penina Sasa alikuwa mtu wa kushinda ndani tu huku akiwa hana furaha kabisa kutokana na kutoweka kwa mpenzi wake Frank. Mzee Joel naye Sasa kumbe alikuwa tayari ameshamtafutia Penina mwanaume mwingine wa kutoka Norway na ndio alitaka amuoe mtoto wake Penina. * Hatimaye kulipambazuka Katika misitu ile aliyotupwa Frank. Frank alizidi kuhangaika bila kupata msaada wowote. Njaa pamoja na kiu vilimtesa Sana Frank pale msituni, alipiga kelele mpaka sauti ikaisha bila kupata msaada wowote. "Eeh Mungu Kwanini unaniacha niteseke hivi? Kama huu ndio mwisho wa maisha yangu bas naomba unichukue haraka usiniache nife Katika mateso makali kiasi hiki." akajisemea Frank kwa sauti ya chini akimuomba Mungu wake. Lakini hata hivyo baada ya masaa mawili mbele, aliweza kupita mzee mmoja aliyekuwa akichunga ngombe, karibu na sehemu Ile aliyotupwa Frank na pia akaweza kumuona Frank akiwa amelala pale chini akiwa hajiwezi kwa lolote. ....... Itaendelea Tukutane JUMATATU ... Read More
Story...... NI WEWE TU PENINA Sehemu ya kumi na tatu (13) Ilipoishia....... Mzee Joel ndio hakuamini baada ya kuingia ndani na kukuta vijana wote wamelazwa chini alafu kidogo hivi akatokeza Nolan akiwa amepigilia suti nyeusi Kisha akamwambia baba yake ambaye ni mzee Joel, "naenda kwenye kikao cha harusi ya Penina na Frank na kama utahitaji kadi unijulishe nikuletee ya kwako." ***********Endelea ********* Nolan baada ya kumuambia baba yake maneno hayo aliingia kwenye gari na kuondoka. Nolan alifikia sehemu ambayo ilikuwa maalumu kwa ajili ya kutengeneza kadi za harusi. Nolan alitengeneza kadi za harusi zisizopungua Mia moja hamsini kwa ajili ya harusi ya Penina na Frank. Kadi hizo hazikuwa za kuchangia harusi ya Frank na Penina bali kadi za mualiko. Nolan alijipanga kusimamia kila kitu Katika harusi ya Penina na Frank hivyo yeye alitengeneza kadi ambazo ni kama kiingilio cha kuhudhuria harusi hiyo bila kuchangia chochote. Nolan baada ya kukamilisha zoezi la kutengeneza kadi zile akaanza kutafuta ukumbi Mkubwa wenye hadhi ya kufanyia sherehe ya harusi ya Frank na Penina. Nolan alifanikiwa kuupata ukumbii ambao aliuhitaji na baada ya hapo Nolan akaanza kuzigawa kadi zile kwa watu mbali mbali ikiwemo na marafiki pia. Nolan moja kwa moja aliwasili nyumbani kwa kina Frank na kuwakuta Wazazi wake Frank ambao walimpokea kwa furaha Sana. "kikubwa kilichonileta hapa ni kuhusu harusi ya mtoto wenu Frank pamoja na mdogo wangu Penina, napenda kuwaafahamisha kuwa taratibu za harusi ya ndugu zetu hawa inaendelea vizuri na hapa nimewaletea kadi za mualiko." alianza kuongea Nolan baada ya kukaribishwa ndani na Wazazi wake Frank huku akiwakabidhi kadi zile Wazazi wake Frank. "Asante Sana kijana wetu na hongera Sana kwa hapa ulipofikia Mungu azidi kukusimamia zaidi na zaidi." wakaongea Wazazi wake Frank huku wakimshukuru Sana Nolan. "msijali Sana hii kazi ilikuwa lazima niifanye na lazima nitaitimiza, na kingine ninachotaka kukifanya kwa Sasa nataka niwahamishe hapa nyumbani kwenu niwapelekee sehemu mkakae hapo kwa siku kadhaa mpaka pale harusi ya mtoto wenu itakapokamilika, nafanya hivi kwa sababu ya usalama wenu kwasababu kuna vita kubwa inaendelea. " akaongea Nolan na kutoa maelezo hayo ambayo Wazazi wake Frank walikubaliana nayo bila wasi wasi wowote. Wazazi wake Frank pamoja na Mdogo wake Frank walijiandaa na kuondoka na Nolan ambaye aliwapeleka Katika hotel moja iliyopo nje kidogo ya jiji la dar es salam na kuwataka wakae hapo kwa wiki tatu kabla ya harusi ya Frank na Penina na gharama zote atazisimamia yeye Nolan. Nolan baada ya hapo alishika njia ya kurudi nyumbani kwa ajili ya kwenda kupumzika kidogo. * Dickson aliwasili Tanzania kwa Mara nyingine tena Ila awamu hii alikuwa na vijana wake wanne alioongozana nao. Baada ya kuwasili uwanja wa ndege moja kwa moja Dickson pamoja na vijana wake walichukua gari ndogo na kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwa mzee Joel.* Mzee Joel alizidi kuchanganyikiwa baada ya kumaliza siku ya pili Sasa bila kumuona Penina na wala hajui ni wapi Penina alipo. Jambo hilo lilimvuruga Sana mzee Joel na kumfanya ashindwe hata kula chakula anachopikiwa na mkewe. Mzee Joel pia aliweza kuwasiliana na mkuu wa kikosi cha the killer na kumueleza jinsi vijana wake walivyoshindwa kuifanya kazi waliyoagizwa na kujikuta wakipokea kichapo kikali kutoka kwa Nolan. Mkuu yule wa kikosi cha the killer aliyejulikana kwa Jina la buffalo alipigwa na butwaa baada ya kupewa taarifa zile na mzee Joel. buffalo hajawahi kuamini kama kuna mtu yoyote anayeweza kupambana na vijana wake na akawaweza, hivyo taarifa zile zilimshangaza Sana. Buffalo akaamua ni lazima amjue huyo kijana ni nani aliyeweza kuwatandika vijana wake. "mzee hiyo kazi niachie mimi nitapambana nae mwanzo mwisho." akaongea buffalo kumwambia mzee Joel. Mzee Joel aliweza kumuelewa buffalo na kukataa simu na kumsubiri buffalo aingie kazini mwenyewe kwasababu yeye ndio mtu pekee Sasa aliyebaki wa kumtegemea. Dakika chache baada ya mzee Joel kuongea na buffalo, mzee Joel alipata taarifa kuwa kuna wageni nje wanahitaji kuonana na yeye. Mzee Joel alitoa ruhusa wageni hao wakaribishwe ndani. Kitendo bila kuchelewa wageni wale walifunguliwa geti na kukaribishwa mpaka ndani. Mzee Joel alishtuka baada ya kuona ugeni wenyewe ni wa Dickson pamoja na vijana wake wanne. "karibuni karibuni Sana." akaongea mzee Joel huku akijaribu kujichekesha japo hakuwa na amani hata kidogo. "hatuna haja ya kukaa mzee Joel, tumekuja kumchukua Penina nataka kujua kama inawezekana au haiwezekani?" akauliza Dick huku akionesha dhahiri kupandwa na hasira. "inawezekana kijana wangu tafadhali kaeni kidogo bas." akaongea mzee Joel kwa upole. "nimeshakuambia hatuna haja ya kukaa sisi tumekuja kumchukia Penina tu." akaongea Dick kwa msisitizo. "kijana wangu Dick naomba nipe muda wa siku mbili tu nitakuwa tayari nimeshakamilisha hili swala." akaongea mzee Joel kuwaambia wakina Dick. "Mzee umenipotezea Muda na umekula pesa zangu nyingi Sana, Sasa naondoka na kesho nitarudi unikabidhi Penina la sivyo pesa zangu utarudisha na utalipa Muda wangu nilioupoteza kwa ajili yako." akaongea Dick kwa jazba na kuondoka pamoja na vijana wake na kumuacha mzee Joel akitokwa na jasho jembamba. Baada ya dakika chache wakina Dick kuondoka Nolan naye aliwasili nyumbani na kumkuta baba yake akiwa na mawazo tele huku pembeni akiwa chupa ya pombe kali. "Baba shikamoo" akasilimia Nolan lakini alijua baba yake hataitikia salamu yake. Mzee Joel kweli hakuitikia salamu ya Nolan alibaki akimtizama tu kwa hasira. Nolan naye hakujali alitoa kadi tano za harusi ya Penina na Frank na kumwekea baba yake kwenye Meza iliyokuwa mbele yake. "karibu Sana Katika harusi ya Penina na mpenzi wake wa Muda mrefu Frank, wewe pamoja na rafiki Zako mnakaribishwa. " Nolan ndio alimwambia baba yake mzee Joel baada ya kumuwekea kadi zile kwenye Meza iliyokuwa mbele yake, Kisha akaondoka na kuelekea chumbani kwake. ............ Itaendelea ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: