Monday, November 20, 2017

SUBIRA YANGU SEHEMU YA 02 Niliamka asubuhi na mapema sana kwani siku hiyo ilikua jimamosi nikaanza na udobi siku hiyo basi nilikuwa naendelea na kazi ya kufua mara geti liligongwa na mlinzi akaenda kufungua geti na hakua mwingine bali ni Joshua nilitabasam kumuona Joshua “bora umekuja unisaidie kufua” nilimtania Joshua akanijibu.. ”leo nimekuja tushinde wote hadi jioni” nilifurahi sana bila kuchelewa Joshua akaanza kunisaidia kufua na kukinga maji yaani tukajikuta tunaanza mchezo wa kumwagiana maji huku tunakimbizana, kwa bahati mbaya Joshua akateleza akadondoka chini na mimi nilijikuta nikimuangukia juu yake, tulibaki tumetoleana macho tu huku tukiwa tumeganda kama mishumaa takiribani dakika chache, nguvu zikaja gafla na kuinuka haraka na kuanza kumvuta Joshua asimame.. ”pole Joshua” nilimpa pole kwa aibu naye akajibu “asante” Tulivomaliza kufua nguo tukaingia kwenye mapishi Joshua akanambia “mim leo napika wali we pika mboga sawa?”. nikatabasam na kumwambia “sawa ila usipike vibichi”.. “haha haa love mimi kiboko sana kwenye mapishi na ni hodari kwenye sekata hiii” Joshua alijigamba huku akichambua mchele huku mimi nikikata vitunguu na nyanya, bahati mbaya nikajikata nikapiga kelele ya maumivu, Joshua akaja haraka kunisaidia “pole mama kua makini” Joshua alinambia huku akitafuta huduma ya kwanza. “Joshua nimeumia jamani kidole change kinauma” niliongea kwa kudeka “subiri nkuletee dawa na plasta sasa” Joshua alijibu huku akienda kuleta dawa.. baada ya mda akaja na dawa na plasta navyo akaniwekea dawa niliumia huku nikitoa miguno ya maumivu “shiii pole mtoto mzuri” Joshua alisema huku akinifunga pasta sio siri kitendo kile cha Joshua kunishika shika mikono yangu nilihisi kusisimka mwili sana mpaka nikawa najishangaa kwani inakua hivi nilibaki nikimuangalia Joshua tu bila kusema neon lolote kutoka kinywani mwangu “sasa wewe pumzika mimi ntapika vyakula vyote sawa malkia?”alisema Joshua huku akinipeleka sebleni…. baada ya muda aliandaa chakula mezani na kuja kunifata sebleni “chakula tayari mama twende mezani”alisema Joshua huku akinishika mkino kuelekea mezani “mmmh chakula kinanukia we ni mpishi haswaa” nilimsifu Joshua kabla sijaonja nikaanza kuchukua sahani nipakue akaema “noo wewe tulia mimi naandaa kila kitu we mgonjwa tulia” nilitabasamu tu bila kujibu kitu akaniandalia na kuanza kula “vipi utaweza kula au nikulishe?” Joshua aliniuliza nkamjibu “ntakula bwana usijali” tulikula zetu tukamaliza na kumuita dada wa kazi aje kutoa vyombo.. ‘’asante sana Joshua kwa msosi mzurii we kiboko” “usijali ni wajibu wangu….. sasa mimi ngoja nkuache niende zangu mjini kidogo” Joshua aliaga ila moyo wangu haukutaka Joshua aondoke kabisa.. “jaman mbona mapema sana?” “kuna ishu nafatilia so natakiwa niende mama” nilikubali kishingo upande na kumkumbatia Joshua kwa hisia zote na kumshukuru gafla mama akafungua mlango na kutukuta tumekumbatiana….moyo wangu ulistuka sana “P a a a a a a a a a…………….. SUBIRA YANGU SEHEMU YA 03 . Nilijitoa kwa Joshua na kukaa pembeni huku nikiangalia chini mama akaniuliza “vipi kuna nini?” "aah nilikua namuaga Joshua anaenda kwao” mama akamgeukia na kumuuliza “Baba unaondoka?” “ndiyo mama kuna mahali nawahi kidogo” “haya mwanangu wasalimie” Joshua akaondoka na kutuacha mimi na mama….mama akawa ananiangalia tu kama mtu mwenye maswali basi nikawa naelekea chumbani mama akaniita “love mwanangu” nikageuka na kuitikia “abee mama” mama akasema “kama kuna mchezo unaendelea kati yako wewe na Joshua naomba uuache mara moja maana nadhani baba ako unamjua alivyo” nilijikuta nikipata kigugumizi “hamna kitu mama” basi naye mama alibaki akinyamaza na kuniacha nikiwa nimejishika huku nikiwa mpole…… usiku nilichat sana na Joshua hadi nikawa nasinzia mda si mrefu akanipigia na kunambia “kuna msichana nimetokea kumpenda sana sijui nifanyeje iliniweze kua nae please love nisaidie kwa hilo” moyo ulifanya paaaa! Na kuanza kujiuliza moyoni ni nani uyo, nikamuuliza “msichana yupi Joshua?”…’ “mmh utamjua tu soon usijali naimani utanisaidia kumpata..usiku mwema tulale sasa maana tumeongea sana”. Basi alikata simu yake na kuniacha huku nikifikria sana juuu ya msichana huyo, usiku kucha sikulala zaidi ya kufikiria maneno ya Joshua, maneno yake yalikua yanajirudia sana akilini mwangu huku ndotoni yakiwa yametawala na kuhisi labda ni mimi Joshua ananipenda na anataka kua muwazi kwangu..! mmmh nilijikuta natabasamu tu mwenyewe huku nikijishika shika mwili wangu akili yangu yote ikiwa kwa Joshua, muda si mrefu nikapitiwa na usingizi name kulala fofofo…..! niliamka asubuhi kama kawaida nikamsaidia dada kazi chache na nilivomaliza nikaenda zangu kanisani mida ya mchana nikarudi home na kukuta baba na mama wametoka alibaki dada tu…nikiwa naandaa chakula mezani gafla Joshua aliingia ndani akiwa na furaha sana nikawa na mshangaa tu huku nikiwaza kuwa uwenda kaja kunipa jina la mschana yule aliye mtaja usiku ule, akanikumbatia na kunibusu shavuni huku akifurahi mmh nilisisimka sana ila nilitaka nijue kwanini ana furaha utadhani kaokota fedha “we Joshua una nn kwan leo” nilimuuliza kwa shauku kubwa nijue “love we acha tu yani am so happy” alisema na kunibeba juu juu “khaa wewe hebu nambie basi tufurahi wote” “gues what?”.. “what jo tell me” “Finally ombi langu limekubaliwa” alinijibu lakin sikuelewa ana maanisha “ombi gani tena kwani uliomba kazi sehemu?” “ Hapana kuhusu jana nilivyokwambia jana nimeongea nae amekubali so nimekubaliwa ombi langu ni yule rafiki yako glory asee nilikua natamani sana awe mpenzi wangu tangu zamani nikawa na shindwa jinsi ya kumuanza sasa jana nikampa mistari amekubali kwa roho moja yani”… moyo wangu ulilipuka kwa mshituko kidogo ambao sikuelewa umetokea wapi huku masikioni mwangu sauti na maneno yalijirudia huku na kule basi kupelekea nizimie, gafla nilijikuta nimenywea tabasamu hakuna na machozi yakaanza nilenga nikajikuta nakaa chini mwenyewe bila hata kuambiwa na mtu yoyote. SUBIRA YANGU SEHEMU YA O4 “Vip love unatatizo kwani mbona umebadilika gafla?’’aliniuliiza Joshua huku akinishangaa nilibaki kimya nikiwa nimejiinamiia kichwa chini huku machozi yakinichuruzika mashavuni taratibu,Joshua alichuchumaa chini hku akiinua uso wangu alinishika kidevu kwa sura ya upole kabisa akaniuliza “ love una nini mama mbona sikuelewi?’’ nilijikuta sina cha kuongea mdomo ukawa mzito nlibaki nikimtazama tu Joshua huku machozi yakiendelea kunitoka “love talk to me plz au umekasirika kwa sababu sijakushirikisha kweny jambo hili?’’ Joshua alizidi kuniuliza maswali mengi bila majibu ‘’Joshua najisikia vibaya kichwa kinauma so plz naomba nikapumzike kidogo”nilijikuta namjibu Joshua huku nikisimama na kuelekea chumbani huku nikimwamwacha Joshua njia panda asijue nini cha kufanya…nilijitupa kitandani na kuanza kulia kwa uchungu sana utadhani labda nilipata msiba sikutegemea kama Joshua angeongea maneno yale… ‘’ina maana Joshua akuwahi kuwa na hisia na mm,hakuwahi kunipenda hata kuniwaza?”nilijikuta najisemea mwenyewe tu, ‘’ kwaiyo kumbe rafiki yangu glory ndo alikua anampenda na kumuwaza kila siku?!..kwan mm nina kasoro gani labda mbona mimi ni mrembo kuliko glory,mbn nasumbuliwa na wakaka wengi kwann Joshua asinipende?”nilijigeuza geuza kitandani huku bado nikiwa nafikiria mara sms ikaingia alikua Joshua “love naomba umeze dawa sawa mama ntakuja kukuona badae upumzike” sikujibu chochote nikaweka simu pembeni na kuchapa usingizi…. Nilikuja kustuka saa2 usiku mlango ulikua unagongwa… ‘’hodi dada” niliinuka kiuchovu hku macho yakiwa yamenivimba kwa kulia ‘’ nakuja subiri’’ nikafungua mlango na kukuta dada wa kaz amesimama mlangoni ‘’ vipi dada leo unaumwa nn maana siku nzima umeshinda ndani ‘’aliuliza dada chausiku “nahisi uchovu tu” mama na mzee wako sebleni wanakuulizia…nikaenda had sebleni nilistuka kwan sikutegemea kumuona Joshua mda ule nyumbani “ shikamoo baba na mama”nilisalimia na kukaa wakaitikia huku mama akianza ‘’vipi wewe macho yamekuvimba una nn mwanangu?’’ “ amna mama kichwa kinauma sana leo?” “dawa umemeza?”baba aliuliza “ nishameza dady” Joshua alivunja ukimya na kuniuliza unaendeleaje saiv love? Naendelea vizuri basi joshua aliaga na kuondoka zake na sis tukaingia chumbani kulala ila kwa upande wangu sikupata usingizi kabisa niliwaza sana had nikaona ntakua chizi ndipo usingiz ukanipitia……asubuhi na mapema nilijiandaa kwenda shule kama kawaida yang niliwah lkn siku hiyo sikumpitia Joshua kama navofanyaga siku zote kwan baba alinipeleka na gari yake hadi shuleni,nilifika class glory alinipokea kwa furaha na kunikumbatia kwa furaha huku akinambia “ love leo nina furaha ya ajabu yani my dear” nilimuuliza furaha gani japo nilijua anachotaka kunambia..me na Joshua ni wa penzi alisema huku akitarajia furaha toka kwangu lkn mm sikuonesha kufurahia wala kuchangamka nilimwambia tu “hongera” na kwenda kuketi..glory alistuka na kushangaa hali ya mm kua mnyonge na aliamua kunifata “vip love kuna tatizo..una nn kwan mbona naona uko tofauti?”glory aliniuliza kwa mshangao “ hamna niko sawa tu” nilimjibu na kuendelea na kaz nyingine za class bas glory alirud kinyonge kwenye siti yake , mda si mrefu aliingia Joshua moja kwa moja alienda kwa glory na kwenda kumsalimia na kuongea kidogo japo sikujua walikua wana ongea nn alivomaliza akaja kwangu na kunisalimia “mambo love?” nikamjibu “poa” “mbona leo hukunipitia my dear na unaendeleaje kwanza maaana niliku txt hukunijib”alinijib Joshua huku akitaka kujua sababu “leo nilitoka na baba”nilijib huku nikiendelea kuandika Joshua alishangaa kuniona katika hali ile lakini akaamua kwenda kwenye siti yake….. Muda wa mapumziko na kwenda kupata kifungua kinywa siku hiyo nikaenda mgahawani mwenyew bila kuongozana na Joshua kama kawaida yetu nilivomaliza nikaondoka zangu lakini kabla sijafika mbali Joshua alinivuta mkono na kuniuliza love ina maana navokuita hunisikii?”Joshua aliniuliza huku akinisogelea nikageuza macho pembeni na kumwabia “sijasikia unasemaje kwani?” “ kwann leo umeenda kunywa chai peke yako?”aliniuliza ila “ah nilikua na kaz darasani ndomana” nilimjib “ mmh haya mama bas badae” nbiliondoka zangu bila kugeuka nyuma nilipanga kuwa mbali na Joshua na glory kwan ningeendelea kua nao karibu ndo ningezid kuumia moyo wangu jambo ambalo ckupanga litokee,,siku zilizid kwenda na kujikuta niko mbali na Joshua ule urafiki kama zaman ulipungua jambo ambalo Joshua alishangaa kwann nimebadilika hivi,,simu zake nilikua sipokei hata sms nilikua sijibu ilifika kpnd Joshua alizoea hali ile, huku mapenz yao yakizid kushamiri siku had siku Ilibaki wiki moja tumalize mtihani wa fom six ndipo glory siku moja alihitaj kuongea namm,baada ya break tulitoka na kukaa chini ya mti nikawa tyr kusikia nn glory anataka nambia love leo nimekuita nahitaj kuongea naww kama rafiki yangu wa mda mrefu sana “,nakusikiliza glory”nilimjibu “ unajua love kipindi kama cha mwez umebadilika sana siyo love niliemzoea kama zamn mm kama rafiki yako naona kabisa hauko sawa tafadhali nambie una nn nikusaidie hata kimawazo” nilishusha pumzi ndefu na kumjibu “ glory niko sawa tu sina tatizo” “ hapana love nakujua ukiwa na tatizo pia nakujua ukiwa sawa so usinidanganye’’glory aliendelea kunilazimisha nimweleze nn tatizo ilifika kipindi nikawa nimecghoshwa na maswali yake nikanyanyuka na kutaka kuondoka lkn glory alinizuia kitendo kile kiliniuzi sana “ glory nishakwambia sina tatizo kwann unalazimisha nikwambie matatizo ambayo sina bwana” no love ww n best yangu nakufahamu nilijikuta naropoka kwa hasira yes nina tatizo tatzo langu n Joshua I LOVE HIM SO MUCH kwa mda mrefu sana nampenda…haya sema are you happy now umejua ukweli?”nilongea kwa kupanic had machozi yalikua yananitoka glory alipatwa na bumbuwazi nae alibaki kimya huku machozi yakimtoka pia kwan hakutegemea majibu kama yale

No comments:

Post a Comment