SUBIRA YANGU SEHEMU YA O5
Glory alikaa chini gafla huku akiwa hamini alichosikia namm nikajikuta nakaa chini huku nikimshika began a kumwambia huku bado machozi yakiendelea kunitoka “glory usijali kwani Joshua amekuchagua wewe na anakupenda sana naomba mpende mpe furaha and plz usimuumize ata sku moja…nawatakia maisha mema”niliongea kwa uchungu huku wote tukiwa tualia taratibu niliinuka na kutaka kuondoka lkn glory alinizuia na kuja kunikumbatia kwa uchungu huku sote tukilia kwa uchungu sana,tulikumbatiana kama dakika mbili hku kila mtu akilowesha shati la mwenzie kwa machozi ndipo glory alipovunja ukimya na kunambia am so sory love kwa yote nisamee kwa kukuumiza moyo wako msikujua akma unampenda Joshua nipo radhi niachane na Joshua uwe nae ww kwan ndiyo furaha yako’’.. ‘’no glory usifanye ivo Joshua anakupenda sana ukijaribu kumwacha ataumia sana..plz take care of him okey ..joshua ananipenda kama rafki tu ila ww anakupenda kweli”nilimjibu love huku nikiwa nimemshika mikono yake plz “ glory naomba Joshua asijue ukweli huu tafadhali” baada ya maongezi tulirud class kujisomea kujiandaa na mtihani kwan siku zilibaki chache sana
Jioni nilirudi home nikawasha simu na kukuta ujumbe kutoka kwa Joshua nilistuka nikawaza labda glory kashamwambia ukweli kwan si kawaida yake kuni txt tangu nilivo mchunia uliandikwa hivi ‘’love my friend nimekumiss sana sijui nilikukosea nn had ukakata urafiki namm..nimemis love Yule tuliekua tunapika wote,tunasoma wote,tunataniana,tunafua wote na mengine mengi sijui love Yule wa zaman atarudi lin..nimemmis sana’’…nilimalizia ujumbe ule hkuu machozi tayari yalikua yamelowesha mashavu yangu yote,,kiukweli ule ujumbe uliniumiza sana lakini sikujibu chochote…kesho asubuh na mapema tulikua na mtihan wa kwanza tulifanya vizur na kumaliza salama..nilijisogeza chin ya mti na kuendelea kupitia somo la pili..kugeuza shingo nkamuona Joshua anakuja upande wangu nilistuka…vipi love mtihani ukoje mgumu au mwepesi?’’ aliniuliza kwa bashasha ‘’ah wastani tu”nilimjibu huku nikiendelea kusoma bas naomba tusome wote if u don’t mind nikamjibu sawa karibu,,tulisoma wote had mtihan wa pili ulipowadia tukafanya na kumaliza vzr tu..ikafika mida ya kurud nyumbani nikawa na ondoka zangu mdogomdogo glory alinikimbilia na kutaka twende wote home bas tukafika home ile naingia ndani sikuamin macho yangu ‘’brother kim?!’’! Niliita jina la kaka huku nikienda mbio kumkumbatia kwa furaha… ‘’jamani kaka umerudi sangapi mbona hujanambia?’’ ‘’mdogo wangu nilitaka iwe surprise’’ kaka alinijibu huku akitabasamu asee nilifuarah saana kwan sijaonana na kaka kwamda mrefu sana ‘’ glory kutana na bro angu alikua nje kimasomo” nilimtambulisha glory kwa kaka… ‘’wakashikana mikono nafurah kukufaham karibu tanzania’’ ‘’ ahsate sana naitwa kim” naitwa glory basi baada ya salam aliaga na kuondoka zake…tukaingia mezani kula hkuu tukipiga story na bro tuliongea mengi sana siku iyo had nikasahau kama nina mitihani…mama akaniambia nenda kasome kaka yupo tu utaongea nae had bas ndipo nliingia chumbani na kujisomea….tulimaliza mtihani salama na kuandaa graduation kaka aliniandalia keki kubwa sana tulisherekea kwa pamoja familia ya kina glory na kin Joshua ilijiunga nas tukala na kunywa pamoja mzee aliwaalika kina glory na joshua nyumbani kwan baba aliandaa tafrija ya kunipongeza…jioni ilifika nilijiandaa,kiukweli nilipendeza sana siku iyo wageni walifika na shereh ilianza watu walikula kunywa na kupata burudani..tulichezac sana siku hiyo nikaamua nipumzike akaja Joshua na ‘’ kuniuliza naomba tucheze wote love” alinishika mkono na kwenda kucheza taratibu nilihis faraja sana moyoni siku hiyo..tulicheza huku tukiongea mengi sana na kujikuta nimechangamka kwan nilipooza sana..nilipata hisia kali nakujikuta nikimsogelea Joshua kama mtu anae taka kukis lakini Joshua alizuga kama haelewi vile japo nilijitahd kumweka karibu gafla glory akaja na kunifanya nistuke ‘’bby nilikua nakutafuta kumbe upo huku” glory aliongea na kumvuta jo na wakaondoka zao..niliumia sana kwa kweli
Nikarud kwenye kiti na kuendelea kunywa kinywaji nikawa na pepesa macho labda Joshua anawza kurudi lkn sikumuona kwa mbali nilimuona kaka anaongea na glory ah nkaamua kuachana nao kwan sikuwatilia maanani nlivogeuka tena sikuwaona pale waliposimama nikawa najiuliza watakua wapi??...joshua akaja na kuniuliza kama nimemwona glory nikamjibu hapana sijamuona..nikaamua nianze kuwatafuta watakua wapi nilistuka baada ya kumuona glory na kaka wakipeana mabusu moto moto huku wakikumbatiana…”bro kim”niliwastua wote wakageuka kunitazama
SUBIRA YANGU SEHEMU YA 06
Niliona aibu kwa kile nilichokiona kwa sikutegemea bro kua kimapenzi na glory,niliondoka pale haraka bila kuwasemesha na kurud nilipokaa mwanzo huku nikitafakari kitu nilichokiona,nikiwa bado kwenye bumbuwazi lile mara Joshua akawa anakuja upande wangu na kuniuliza “vip love umeshamuona glory maana simu hapokei”..nilibak na kigugumizi tu huku nikimwangalia Joshua usoni, Joshua akaniita tena “love inamaana hunisikii nacho kuuliza ama ndo umelewa?”…nilimjibu kwa shida huku nikibabaika “ha..pa..na bado cjamwona sijui kaenda au labda ameenda kwao” nilidanganya kwani sikutaka kabisa kuumiza moyo wa Joshua maana alimpenda glory sana.. “sawa nawewe unaonekana umechoka twende ukapumzike ndani” niliinuka na Joshua kunisindikiza ndani kupumzika tukaagana na Joshua aliondoka zake…. Nilipata uchungu sana moyoni nikamuonea huruma sana Joshua nikawaza sana hadi nikapitiwa na usingizi….
Niliamka asubuhi na kufanya shuhuli ndogo ndogo hku kichwani nikipanga kaka akiamka niongee nae kirefu zaidi kuhusu jana..had natenga chai mezani kaka alikua hajaamka ikanibid nikamgongee ndani, aliamka na kuonekana mchovu sana… “vipi love daah bora umeniamsha maana leo ningelala sana” “chai tayari”nilimwambia bro na kwenda zangu kunywa chai….bro alipomaliza kazi zake nikamuita “bro nataka kuongea naww” “ haya nambie dogo langu”.. “hivi bro una mahusiano na glory si ndio?”nilimuuliza “yes ni mpenzi wangu na nina mpenda sana” alijibu kwa ujasiri nilishangaa sana hayo mapenzi wameanza lini “ amekwambia hana mpenzi?”nilimuuliza bro.. ‘’ ndiyo kasema hana kwan vipi au hupendi mimi kutoka na rafiki yako?bro alinambia nkamjib “ siyo hivyo bro tatizo unakurupuka bro bila kumjua mtu vizuri’’ “mmh una maanisha nn kusema ivo love?”bro alihamaki huku akinitolea macho, nilipata kigugumizi maana sikutaka bro ajue ukweli kuhusu glory na joshua “yani unatakiwa ukae nae mda umchunguze tabia zake umjue kiundani ” nilimjibu kaka “sasa wewe unamuonaje glory anafaa kua wifi yako and ashawahi kukwambia ana mtu labda.. ww ni rafiki yako najua huwez nidanganya”.. ‘’ mh mi sijui bwana ila kama nilivokwambia bro fanyia kazi jambo langu” nilimaliza na kuinuka zangu na kuingia chumbani kupanga nguo kabatini mara kidogo nikasikia hodi ..nani? “ mimi glory” nkajibu “ ingia”.. glory akaingia kabla hajakaa nikamvamia na kumzaba kofi jambo ambalo lili mshangaza sana nkamsogelea huku nikiwa na hasira “glory ndo nini sasa umefanya?” glory huku akiendelea kusikilizia maumivu mkono bado ukiwa shavuni “ mbona sielewi love unamanisha nn”…hunielewi?...”jana ndo ukafanya nini pale hivi wewe ni Malaya au?”nilijikuta naropoka tu “ love mimi sio mhuni”aliongea huku machozi yakimlenga “unawezaje kutembea na wanaume wawili, kwann unapenda kuumiza hisia za watu wewe, nilikwambia nin kuhusu Joshua?” glory alikaa kimya kichwa akiinamisha chini huku machozi yakimtoka hivi ushasahau niliyokwambia glory hujui kua Joshua anakupenda na sipendi umuumize moyo wake kwann sasa unafanya hivi?..”niliongea kwa kuumia kiasi kwamba namm machozi yakaanza nitoka nikaendelea kumsema “Joshua amekukosea nini hadi kumtenda kiasi hiki hebu fikiria akija kujua itakuaje glory na unafaham jins anavokupenda” bado glory aliendelea kulia tu bila kuongea kitu “naomba uachane na kaka angu mapema kabla Joshua hajagundua glory plz sitaki umuumize Joshua” glory akainua sura yake na kusema “ NO! siwezi kumwacha kaka ako nampenda sna kutoka moyoni” hee! We glory una wazimu wewe unasemaje wewe?...what about Joshua?..hujui kua ndo mwanaume akupendaye na mlikua na mahusiano” nilimuuliza kwa mshangao maana alizidi kunivuruga na majibu yake……
SUBIRA YANGU SEHEMU YA 07
“Najua love kwamba tuna mahusiano lakini”….. “lakini nini glory mbona umebadilika hivyo una nini kwani?”nilizidi kumpa maswali “love najua unampenda Joshua kwa mda mrefu sana japo mimi nlikua nae lakin tambua nimefanya haya yote kwa ajli yako nataka nawewe uwe na furaha, na joshua ndo furaha yako love sitaki kukudhulumu furaha yako..”glory aliongea kwa kumaanisha “mmh glory mi sikuelewi ujue” “wewe ndo unaweza kumpa Joshua furaha ya kweli na mapenzi ya kweli coz mmejuana kwa mda mrefu sana so nimekuachia Joshua kwa roho moja tu”glory aliongea kwa huzuni huku machozi nae yakiomtoka mimi ndo nilibaki kimya tu machozi kibao usoni mwangu kwani maneno yale yale yalinigusa sana “ lakini Joshua hakuwahi kunipenda mimi alinichukulia kama rafiki,mtu aliye mpenda kwa dhati ni wewe tu sasa unadhani ukimwacha inakuaje?” najua lakini sina jinsi love” “sasa ushamwambia kuhusu hili jambo?”nilimuuliza hapana nashindwa jinsi ya kumwambia
Basi tulimaliza maongezi ambayo hayana muafaka m nika baki chumbani na glory akaenda kwa kaka kuongea nae maana mapenz yalinoga sna baada ya muda nikajiunga nao sebleni huku glory akipakatwa na kaka na kupigana mabusu mengi mengi, kwa aibu nikatoka na kwenda kuandaa chakula mezani mara gafla akaingia Joshua na kukuta kaka kim na glory wakiwa kwenye ma love love…moyo ulifanya paaa kwa kuogopa kwan sikutegemea Joshua kama angekuja mda ule,Joshua macho yalimtoka huku akivima kwa hasira, gafla alimvamia bro kim na kumkaba “unafanya nn na mpenzi wangu” Joshua akliongea kwa jazba had nikatoka mbio kwenda kumtoa Joshua “ plz stop Joshua acha bwana”.. “wewe glory naomba umwambie uyo mm ni nani yako maana naona anashobokea wanawake za watu”joshu alipanik na kutaka glory aseme kila kitu kwa kaka maana kaka alibaki njia panda cha ajabu glory hakujibu kitu alikaa kimya ndipo kaka akamwambia glory naomba unambie whats happen hapa” kka nae alitaka kujua kinachoendelea.. mmh hali ilikua tete mule ndani maana sikutegemea kama mambo yangefikia huku niliogopa sana siku hiyo ndipo glory akainua uso wake na kuongea “nampenda sna kim sipo tayari kumwacha …am so sory Joshua”glory aliongea kwa machozi ….what?..unasemaje glory? Joshua aliongea huku macho tayari yakiwa mekundu, nilizidi kuogopa sana…..Joshua hakuamini ilichokisikia alibaki akiwa amesimama tu huu akimkazia macho glory hadi glory alianza kuogopa, mim nilibaki nikiwa nimejiinamia nisijue cha kufanya… ‘’glory wewe ndo wa kunitenda mim hivi?..ahsante nashukuru’’ aliongea Joshua huku akifuta machozi na kuondoka, nilimkimbilia Joshua kabla hajafungua geti nakumwita “ Joshua ningoje” lakini Joshua aligeuka na kuniangalia huku macho yake yakionesha kunilaumu… ‘’love yani yote haya yanatokea hata kuniambia ukaamua kunificha si ndiyo?...au kisa ni kaka ako ndo mana ukaamua nificha?..anyway ahsanteni’’ Joshua alimalizia na kuondoka, nilitamani nimfate lakini nilijikuta siwezi na kubaki nikiwa nimesimama mlangoni huku machozi yakinitiririka mashavuni mwangu, nikarudi ndani na kukuta glory bado kajiinamia asijue nini cha kufanya illa bro sikumkuta, nikamfata glory alipo ‘’love kaka ako amenikasirikia hataki ata kuniongelesha’’ kidogo nikamuona bro ameshika funguo ya gari kama anataka kuondoka mahali glory akainuka na kumfata kaka lakin bado kaka alionekana ana hasira ‘’glory please don’t touch me’’ kaka aliongea na kumsukumiza glory akafungua mlango na kuondoka, nilibaki nikiwa sijui nifanye nini ‘’love niombee msamaha kwa kaka ako nampenda sana kim’’glory alizidi kulia kwa machozi… ‘’usijali ntaongea nae na atakubali tu hata yeye anakupenda ‘’nilimpa moyo na kuendelea kumbembeleza had alipo tulia na kurudi kwao
Ilipotimu saa mbili usiku mama na bab walirudi na niliwasalimia vizuri ila baba akauliza ‘’kaka yako yuko wapi?’’ nilikosa cha kujibu maana sikujua kaka ameenda wapi kwan simu zangu hazikupokelewa ‘’katoka na rafiki zake’’ niliamua kudanganya ‘’katoka mda gani?’’baba alihoji “ jioni hii baba’’ ok akirudi niambie baba alisema na kuingia chumbani mimi na dada wa kazi tuliandaa chakula mezani na kuzid kuangalia saa nikaamua kumpigia tena kaka lakini hakupokea hadi wasi wasi ukaanza nijia sikuweza kula kabisa had wazee wakawa wananishangaa kwanini sili…ilifika mida ya saa4 baba akauliza ‘’huyu kim hajarudi tu?’’ ‘’ bado baba ila nahisi yuko njiani anakuja” ‘’ kahaanza uhuni huyu’’ baba aliongea hku akielekea chumbani kulala lakini mimi sikwenda lala niliamua kumsubiri kaka joakim, nilikaa sebleni hadi nikapitiwa na usingizi…nilikuja kuamka saa12 asbh nikaanza kujiuliza imekuaje hadi nimelala sebleni wazo la kaka likanijia nikaenda kumwangalia chumbani kama alirudi nikafungua mlango na kumkuta amelala fofofoo mmh moyo wangu ulifarijika maana niliwaza sana nikarudi jikoni kumsaidia dada kazi,hadi kufika mida ya saa tatu asubuhi nikamuona kaka ameshaamka huku akionekana mchovu sana ‘’vipi bro jana ulikua wapi napiga simu hupokei wala simu za baba hupokei” nilianza kwa maswali ‘’aah nilenda kulewa jana kupunguza stress’’alijibu na kukaa mezani akingoja chain a mm nika kaa ‘’ lakini kaka ujue glory anakupenda sna ?’’nilianza kumpigia debe glory ‘’ wee sitaki kusikia hilo jina masikioni kwangu’’kaka alioneasha bado mekereka “sasa bro kwani glory amekosa nini sasa wakat amekuchagua wewe” nilimuuliza kwani love we huoni kosa apo yani kumbe alikua na mpenzi wake mm alikua ana nichora tu we hujui mapenzi yanauma kiasi gani ndo maana unasema tu’’bro alionekana aliumia sana kile kitendo kilichotokea jana….kabla sijamjibu iliingia sms kutoka kwa Joshua ilisomeka hivi ‘’ love naomba uje nyumbani please sasa hivi” mmh niliguna
SUBIRA YANGU SEHEMU YA 08
“Nilimjibu sawa nakuja saivi’’ nilivomjibu Joshua nikamtizama kaka na kumwambia ‘’kaka kua na moyo wa huruma mtoto wa watu anakupenda samehe yaishe muanze upya kwani hakuna mkamilifu!..glory amekuchagua wewe badala ya Joshua we huoni amejitoa kiasi gani kwaajili yako?’’nilijitahid kumpa somo ‘’ mmh siyo rahisi kama ufikiriavyo”alijibu bro huku akiendelea kunywa chai, gafla mlango ukagingwa na kuingia alikua glory bro kumuona tu glory akasimama na kuelekea chumbani lakini gliry akamkimbilia na kumzuia ‘’ noo! kim usinitese kiasi hiki..kama ni adhabu unayo nipa basi naomba unipunguzie siwezi bila wewe nakupenda kim plz nisamehee”glory alizid kuomba msamaha lakin bro hakujibu chochote zaid ya kuangalia pembeni tu.. ‘’kim wewe ndo kila kitu kwangu wewe ndo mwanaume nikupendae kwa dhati naomba niurumie naumia kwaajili yako”glory alipiga magoti hadi mm nikaanza kumuonea huruma kaka alimuinua na kumkumbatia ‘’oky nimekusamehe nakupenda pia glory” hatimae wakapatana tena nilifurahi sana kuona furaha imerudi upya nikawaambia ‘’am happy for you guys” nilimaliza na kwenda kujiandaa niende kwa kina Joshua aliponiita, sikua najua ananitia nini lakini nilienda tu na kumsikiliza….nilifika hadi ndani na kukuta nyumba ipo kimya sana niligonga mlango akaja msichana wa kazi kufungua tulisalimiana na kumuulizia Joshua na kunambia yuko chumbani kwake nilikuta amejifunika shuka ‘’vipi Joshua unaumwa?’’nilimuuliza maana si kawaida yake ‘’ ndiyo nahisi homa kichwa kinauma sna”alijibu kwa sautii ya chini sana lakini chumba kilijaa pombe kali chupa nyingine zionekana zishatumika mmh nilishituka ‘’Joshua umekunywa mapombe?’’nilimuuliza na kuketi kitandani kwake ‘’ndiyo love nimekunywa’’alijibu huku akianza kulia ‘’hapana usiwe hivyo kwani pombe haitamaliza matatizo yako Joshua ‘’ nilimwambia huku nikimuonea huruma nikainuka na kwenda kuchukua kitambaa na maji ili nimkande kichwa homa ishuke, sikuweza kumpa dawa kwani bado pombe ilikua kichwani ‘’love kwani mimi nimemkosea nin glory?’’joshua aliniuliza huku nikiendelea mkanda ‘’hapana hujamkosea kitu ila inabidi ukubaliane na matokeo wasichana wako wengi utapata mwingine”nilimjibu baada ya kumkanda nikamwacha apumzike kidogo nikainuka na kutaka kutoka lakini Joshua akanishika mkono na kunambia ‘’love please don’t liv me naomba ukae na mm’’ mmh hapa sasa ikawa mtihani kwani nilihisi Napata majaribu ‘’sawa nipo siondoki ‘’ nilimjibu na kurudi kitandani nikawa nasubiri alale namm niweze kurudi nyumbani kwani mda ulishaenda nikambembeleza hadi akapitiwa usingizi nikamkiss shavuni na kuondoka zangu nyumbani…nilirudi nyumbani na kukuta glory bado yupo na kaka nikapitiliza had chumbani na kujilaza huku bado nikimuwaza Joshua jinsi alivyonishika mkono na kunambia nibaki nae…mmmh nilizidi kupagawa na kutamani hata anibusu mdomoni roho yangu itulie , niliwaza sana hdi nikapitiwa na usingizi, nilkuja kustuka simu yangu inaita nikatazama alkua Joshua mmh niliguna kwanza na kuanza kufikiria anataka nini saizi huyu
No comments:
Post a Comment