SUBIRA YAGU SEHEMU YA 01
.
.
Ilikuwa asubuhi tulivu kabisa na hali ya hewa ikiwa mwanana na tena yenye kuvutia siku hiyo…nilikua najiandaa kwenda shule lakini sikuweza kwenda shule bila kumpitia rafiki yangu kipenz Joshua kwani nilikuwa nimeshajenga mazoea ya kupita kwao au yeye kupita kwetu…
Mimi na Joshua ni marafiki wa siku nyingi sana tulipendana na kuheshimiana kama kaka na dada, hata familia zetu zilikua na ule ukaribu sana. kwenye familia yetu tumezaliwa wawli mimi pamoja na kaka yang utu, mimi nilikua mtoto wa mwisho katika familia ya mzee Bernad, kaka yangu alikua ulaya kimasomo yeye alisoma chuo na mimi nilikua A-level kwani yeye alipata nafasi ya kwenda nje kusoma hivyo alituata takiribani miaka mingi sana……!
Kwa upande wa rafiki yangu Joshua yeye alizaliwa peke yake tu huku akilelewa malezi mazuri na wazazi wake na pindi awapo shule huwa na tabia ambayo wengi wao walishindwa kumzoea hivyo tulikuwa tunelewana sana mimi naye. tulishirikiana kimasomo kwani tulisoma darasa moja, nakumbuka siku moja nikiwa peke yangu darasani najisomea huku nikiwa mpweke walitokea wakaka wawili wakaanza kuniletea fujo mahali nilipokuwa nimekaaa….! jambo ambalo sikupenda huku wakilazimisha sana nami uvumilivu ulinishinda na kufumbua kinywa changu…
”jaman naombeni muondoke sipendi usumbufu” nilijikuta naongea kwa hasira.
“hatuwezi kuondoka tukakuacha mtoto mzuri kama wewe ukae peke yako wakati huu”..aliongea mkaka mmoja huku akishika nywele zangu, niliinuka kwa hasira nikitaka kuondoka mahali hapo lakini wakanizuia kwa nguvu zao huku wakiwa kama wanataka kunifanya jambo baya na pia nyuso zao zilibadilika na kuwa tofauti na mwanzo, nilipiga kelele kuomba msaada kwani walinibanisha ukutani na mmoja wao akijaribu kunifungua shati langu huku nikiwa mapigo ya moyo yalikuwa yakienda mbio…! gafla alitokea Joshua na kunikuta kwenye hali ile
“mnafanya nn hapo nyie wajinga” Joshua aliongea kwa hasira hadi mm niliogopa kwan sikuwahi kumuona amekasirika kiasi hicho tangu tunajuana, gafla aliwavamia na kuanza kupambana nao,, kitendo kile kilinipa kiwewe na kukimbilia ofisini kutoa taarifa, lakini sikukuta mwalim hata mmoja wakati huo kwani ulikuwa mda wa kuondoka kurudi nyumbani, nikaamua kurudi niweze kupambana namimi ili kutoa msaada kwa Joshua.. nilishangaa kuona wale wakaka wakikimbia mithili wameona nyoka mkali pindi walipokuwa wakipambana, ,nkaingia darasani na kukuta Joshua akijiweka sawa huku akiwa amefanya jambo la kuniokoa, Joshua alikuja haraka upande wangu na kuniuliza kama nimeumia
“vipi love wamekuumiza mama?”.
”hapana jo” nilijibu kinyonge..gafla Joshua alinivuta kwake na kunikumbatia na kunambia”sipendi kukuona unaonewa au kupata shida na mimi rafiki yako nipo”.
”ahsante jo kwa kujali hakikia we ni rafiki bora” nilijibu huku nikitabasamu huku nikimuangalia usoni..
” usijali love, twende nyumbani mda umeshaenda sana” alinijibu huku akinishika mkono na kurudi nyumbani wote tukiwa na furaha ya kushinda vita vile……
Alinifikisha hadi nyumbani.”mbona unaishia mlangoni leo?” nilimuuliza Joshua
“aah love mda ushaenda wacha mimi niwahi nyumbani” Joshua alijibu huku akitaka kuondoka lkn mimi nikamvuta mkono na kumwabia”noo bana basi njoo umsalimie mama yuko ndani” Joshua akakubali kuingia ndani na kumkuta mama sebleni..
”shikamoo mama” Joshua alisalimia
“marhaba mwanangu vipi za shule?”mama aliitikia huku akienda kwenye friji na kutoa juice na kutuandalia ”aah mama mi nimeshiba ngoja niwahi nyumbani” Joshua aliongea huku akionekana ana haraka ya kuondoka, maama alimbembeleza abaki Joshua alikaza basi ikabidi nimsindikize na mimi nkarudi zangu home, nilipitiliza hadi chumbani nikalala kwan nilichoka sana siku hiyo kwani waliniumiza kiasi chake................!
No comments:
Post a Comment