MINE.ONLY MINE
Part one
Maya alikuwa akishuka ngazi haraka haraka huku akifungua pochi na kuingiza mkono lengo likiwa ni kuitafuta simu yake ya mkono.
Aliipata na kuitoa na kisha akaenda hadi kwenye orodha ya majina ya watu aliohifadhi namba zao kwenye simu na kutafuta namba aliyokuwa akiitafuta.
Ni wakati akiwa anatafuta namba hiyo na alikuwa amefika kwenye mlango wa Kuingilia kwenye hoteli hiyo alijikuta alipigana kikumbo na mtu aliyekuwa akiingia hotelini hapo.
" ooh ooh! ", alijikuta akisema kwani kikumbo kile lilipelekea simu yake kuanguka.
" samahani...! ", alijikuta akisema Maya kwani ni yeye aliyekuwa na makosa ya kutembea pasipo kuangalia mbele tena kwa mwendo kasi kama ule.
Aliinama kuokota simu ile na hapo akajikuta akiangusha kitu mfano wa kadi lakini kabla hajaifikia simu ile mtu yule aliyekuwa amempiga kikumbo alikuwa tayari ameshaiokota simu ile simu ile.
" ahsante...! ", alisema Maya huku akipokea simu ile pasipo kumtazama mtu yule aliyemuokotea simu yake.
Akitafuta tena namba ile aliyokuwa akiihitaji na kuipata kisha akapiga na kuweka simu sikioni iliitwa mara ya kwanza pasipo kupokelewa.
Ikaotaara ya pili pasipo kupokelewa na mara ya tatu ndipo iliyopokelewa.
"Hallooo...., Jimmy nakuomba uje unishikie kwa mda... tafadhali nimepata dharula nimekukosea ofisini kwako... natika nyumbani kuna dharula tafadhali nisaidie haitazidi saa moja nitakuwa nimerejea..., nitashukuru mpenzi ubarikiwe... ", alisema kisha simu ikakatwa.
Alienda nje ya geti la hoteli hiyo na kuingia kwenye moja ya Tax ambazo huitumia akiwa na dharula.
" Nipeleke kwangu... harakisha tafadhali", alisema Maya huku akitafuta jina jingine kwenye simu ile na kuipiga.
" eeeh mpenzi nakuomba mara moja nyumbani...tafadhali naomba uje", alisema Maya kisha akakata simu na kutafuta tena namba nyingine.
" nakuomba baba yangu nivumilie baba yangu natika hapo dakika kumi na tano tu", alisema Maya kwa kusihi kisha akakata simu.
************
Alimkuta baba mwenye nyumba wake akiwa amesimama pale nje ya geti upande wa nyumba yake.
Alimlipa dereva Tax pesa yake naye akashuka na kumuelekea baba yule ambaye alionekana amechoka kusubiri.
" shikamoo baba! ", alisalimia kwa heshima Maya huku akimpatia mkono mzee yule aliyekula chumvi nyingi kwenye hii dunia.
" Marhaba mama! ", aliitikia mzee yule.
" pole nimekutoa ofisini kwako haraka haraka ", alisema mzee yule.
" usijali nisingekusumbua uje hadi kule na kwa hali yako hiyo...!" alisema kisha akashusha pumzi kwa nguvu.
" kwahiyo baba unataka kuniambia mwenyewe kishafika na kasema anahitaji nyumba yake? " aliuliza Maya kwa sauti usiyotaka kuamini swali lile aliloliuliza yeye mwenyewe.
"ndio hivyo mama yangu kasema ana haraka sana ..anataka afanye ujenzi kabla hajasafiri tena... ", alijibu mzee yule.
"dah!, na nilijisahau kabisa kutafuta nyumba huwezi hata kunisaidia kwa watu Unaowafahamu wenye nyumba kama hii yako... Yaani nyumba ilikuwa nzuri hii.", alilalamika Maya.
" ninao ndugu zangu wanazo lakini mama utakaa wewe Tabata halafu uende Kazini Mbezi kweli...? ", aliuliza mzee huyo.
" tena zile za kule ni kubwa na nzuri kuzidi hii yangu na hata bei ni rahisi", alijibu mzee yule.
" mmmh Tabata mbali baba yangu na nimekuambia nyumbani Buguruni nikaja huku Kijitonyama kufuata ukaribu... Sasa kuvuka tena Buguruni na kurudi nyuma si ndio yaleyale tena nakuwa nimezidi kurudi nyuma", alijikuta akijibu kishingo upande.
"pole mwanangu... sina namna ya kukusaidia... Hata ingekuwa wewe mtu anakupa pesa ya kuzidi thamani ya nyumba yako mara mbili wala usingekataa... Hapa kama ningekuwa kwa mwananchi wa kawaida ningeuza kwa milioni mia hamsini hadi mia mbili lakini mtu anakupa milioni mia tatu... Unakataaje...", alisema mzee yule na Maya kujikuta alijiunga mkono mzee yule kwa uamuzi wake aliochukua.
Sio kuwa taarifa zile zilikuja ghafla hapana..., alikuwa amepewa taarifa miezi minne kabla kuwa nyumba imepata mfanyabiashara anayetaka kuinunua na atawapa miezi mitatu kutafuta nyumba nyingine na kwakuwa ndio ilikuwa miezi yake mitano ya kumaliza mkataba wa kodi ya mwaka mzima aliyolipia hivyo angekuwa kwa mwezi mmoja tu uliobakia.
Kutokana na kuwa na mabadiliko makubwa ofisini kwake alipokuwa akifanya kazi alijikuta akikosa muda wa kutafuta nyumba na hata akalisahau suala hilo la kufuatilia nyumba nyingine.
Ni simu aliyoipokea mchana huo toka kwa baba mwenye nyumba yake kuwa mnunuzi ameshafika na anahitaji kuichukua nyumba hiyo kwani miezi minne inakaribia kuisha hivyo wajiandae.
Na pia alihitaji kumuona kumrudisha kodi yake ya mwezi mmoja iliyobakia ndipo alipochanganyikiwa na kutoka ofisini kwake kwenda kuonana na mzee huyo.
" pesa yako iliyobakia ni hii hapa... ila ningekushauri utafute yule dalali aliyekutafutia hii anaweza kukusaidia ", alisema mzee yule akimkabidhi Maya bahasha iliyokuwa na pesa yake....ITAENDELEA
MINE... ONLY MINE
part 2
Maya aliipokea bahasha ile kishingo upande kisha akafungua pochi yake na kusumbuliwa bahasha ile kisha akaifunga vema.
"sasa mama mimi naomba nikuache siku utakayohitaji kuhama utanipiga simu nifuate funguo... ", alisema mzee yule.
" sawa baba ahsante... Na msalimie mama", alijibu Maya na mzee yule akashika njia na kupotea mbele yake na muda huohuo aliona gari la Jackson liliingia eneo.
Hakuwa hata na nguvu za kumfuata taarifa ile ilichanganya akili... Kupata nyumba kwa haraka na zile pilikapilika za kazini kwake Kutokana na ujio wa bosi mpya ofisini kwao.
" vipi babe umenikimbiza harakaharaka kuna usalama kweli... Na huu si muda wako wa kazi mbona upo nyumbani? ", alijibu Jackson akimjongea Maya kisha akambusu shavuni.
" mbona mnyonge hivyo... nini tatizo mpenzi? ", aliuliza Jackson mara baada ya kumuona Maya akiwa amepooza.
Babe unakumbuka kipindi kile nilikuambia kuhusu hii nyumba kununuliwa?, aliuliza Maya.
" sasa leo mwenye nyumba kanipigia simu na kasema mnunuaji ameshafika na anaitaka nyumba yake muda wowote kuanzia sasa! ", alisema Maya.
" aaah kwani sasa hilo nalo ni la kukufanya uanze kuwaza mpenzi wangu..., kwani we nilikuambiaje kuhusiana na swala hilo? ", aliuliza Jackson.
" nilikuambia kwangu nyumba ipo kubwa tu... Na hilo unaijua na wajua naishi peke yangu na wala usije kuleta suala la ndugu sijui wamefanya nini..., wajua kwetu tupo watatu na mimi ndio kitinda mimba na wajua dada zangu wanamuziki uwezo na hawapo nchini.... Hivyo sina hata mzigo wa kutaka kuja kunitegemea!", alijibu Jackson kitendo kilichomfanya Maya asikitike.
" kwahiyo unaamini hilo ndio suluhisho pekee? ", alijibu Maya.
" nilishakueleza wazi kuwa siko tayari kuishi kinyumba na wewe bila ndoa... na hata hiyo ndoa yenyewe bado kidogo kusema nimekubali kuolewa nawe Jackson! ", alijibu Maya.
" hivi we binti una matatizo gani lakini wenzako kibao wananililia miwale lakini wewe unaringa utafikiri sijui nini! ", alisema Jackson kwa dharau.
" unataka kujua kwanini siko tayari kuolewa na sio tu siko tayari kuolewa ila ni kuwa siko tayari kuolewa na wewe! ", alisema Maya akimsogelea Jackson pale aliposimama.
" ni kwasababu kuu mbili..., moja ndio kwanza tuna miezi saba tangu tufahamiane... Pili ni hii tabia yako ya kuwaleta wanawake zako wengine kwenye mazungumzo yetu! ", alisema Maya akimsonta kidole cha kifuani Jackson kisha akampita na kuanza kushika njia kuelekea barabarani.
" sasa unaenda wapi? ", aliuliza kwa mshangao Jackson.
" narudi kazini!", alijibu Maya pasipo kusimama wala kugeuka.
" si ungoje nikupe lifti! ", alisema Jackson mara baada ya kumuona Mama akilivuka gari lake na kuendelea kwenda mbele.
" save it fir your other girls!", alijibu kwa nyodo Maya na kuzidi kusonga mbele na ni hiki ndicho kimojawapo ambacho kilifanya Jackson azidi kumpenda Maya... Hakuwa mrahisi...hakuwa akibabaika na pesa wala ushawishi wowote kutoka kwake kwani pindi akisimama jambo lake basi hilo ndilo huwa siku zote.
Akihangaika kumbembeleza kwani alimjua kuwa amekasirika na maneno yake na sio kwa muda tena ambao anaishi kazini angeweza kumueleza wakaelewana....
Alikiendea gari lake na kuingia kisha akaliwasha na kuliongoza barabarani ambapo alikiona Maya akiingia kwenye Tax iliyokuwepo kituoni na kujikuta akitabasamu mwenyewe huku akitokea kichwa chake.
" binti ana jeuri huyu... ", alisema Jackson.
" ila ndio ninachompendea hikohiko" , alijikuta akisema kisha akakunja kulia na kutokomea anapokujua yeye.
**********
Michael ambaye ndio alikuwa akitoka hitelini hapo badala ya kimakosa wote aliokuwa alihitaji kuwaona alishangaa kuona kitu chenye mng'ao kwenye majani.
" alikiendea na kukiokota na hapo aligundua kilikuwa ni tembo card toka CRDB na alipoigeuza nyuma aliona picha ya msichana na alikumbuka msichana yule kuwa alikuwa ni yule waliyegongana mlangoni wakati akiingia hotelini hapo.
" maskini sijui hata alikuwa anaishi wapi! ", alijikuta akisema huku akichukua tembo card ile na kuifanya ndani ya Wallet yake.
Alitembea kuelekea sehemu zilipo Tax na kuingia kisha akamuelekeza dereva mahali anapoelekea.
Tax ile ilipaki mbele ya jengo kubwa la ghorofa tatu lenye vioo vya rangi ya bluu bahari maeneo ya Oysterbay kisha akamlipa dereva ujira wake na kushuka.
" Unknown furniture company limited ndivyo lilivyokuwa limeandikwa jengo hilo na Michael alishika njia kuelekea ndani ya mjengo huo na hii ilikuwa ni moja ya miradi yake mingi sana ambayo alikuwa nayo jijini Dar es salaam....ITAENDELEAMINE... ONLY MINE
part 3
Martha alikuwa ndio anatoka kupata chakula cha mchana muda huo wakati alipopita karibu na jengo hilo lenye vioo vya blue na kujikuta akisimama ili kujitazama.
Kwakuwa palikuwa ni sehemu tulivu alijikuta akitumia muda mrefu kidogo kujitazama.
Aliiangalia nywele zake na kujirekebisha kidogo kabla hajajitazama midomo yake na hajafungua pochi yake kuubwa na kutoa lipstick kisha akajiongezea.
Aliichezesha midomo yake mithili ya mtoto mdogo anayejufunza kusema mama au baba kisha akawa kama anailamba na yote hiyo ni kutaka kuiweka lipstick yake ikae vyema kwenye midomo yake.
Kisha akajitazama blauzi yake kama imekaa vizuri na akafungua kifungo kimoja cha shati lake la rangi nyeupe na kusababisha matiti yake makubwa yaliyonona vema kwenye sidiria ile ya push up kuweza kuonekana sehemu ya katikati pale yanapokutania.
Alijitazama namna sketi yake ya rangi nyekundu ilivyomkaa kisha kisha akauvuta juu kidogo japo ilikuwa ipo juu ya magoti tayari lakini aliamua kuuongezea upande juu zaidi.
Aligeuka na kujitazama nyuma kwenye makalio yake na akajikuta akitabasamu kwani alijaliwa kiasi chake na hakuwa amepigwa pasi kama walivyo wanawake wengine.
Mguu wake wa bia ulimfanya azidi kujifaharisha mbele ya kioo kile kisha akajikuta akikunja uso mara baada ya kuona soli yake ya kiatu chake kile kirefu imechafuka.
Alifungua pochi akatoa tishu na kuinama kujifuta viatu vyake vya rangi nyeusi miguu yote miwili na ni muda huu ndio Michael alikuwa akiingia ndani ya ofisi yake na kushangaa kuona alikutana na mapaja manene na makalio ya haja akiwa amesusiwa na binti yule aliyekuwa katingwa na usafishaji ule wa viatu.
Alijikuta akitabasamu huku akisiikitika kisha akavuta kiti na kukaa na laiti isingekuwa sura ya binti yule kumfanya ahisi ameshawahi kumuona mahala fulani basi pasi na shaka asingeendelea kumtazama tena.
Ila alikiona akifanania na mtu aliyetoka kumuona muda si mrefu lakini hakukumbuka ni wapi alipouona binti huyo na wakati akailazimisha kumkumbuka kwa kuvuta kumbukumbu zake binti yule aliondoka mbele ya kioo kile.
Alifungua diary yake kisha akaenda hadi sehemu aliyoandika KING'S PALACE HOTEL na kuandika alama ya X kisha akafunga kitabu chake hicho.
Alichukua simu yake ya mkononi kisha akaenda hadi kwenye majina kisha akatafuta jina Mzee Abdul kisha akapiga namba hiyo.
************
Maya alifika ofisini kwake akiwa bado na hali ileile alikotoka nayo nyumbani kwake...hali ya kutokujua afanyae ili kuweza kupata nyumba yenye viwango kama vile vilivyokuwepo kwenye nyumba anayoishi sasa.
Alitamani kama angekuwa na uwezo wa kuhamisha nyumba ile na kwenda kuhamia nayo huko kwingine ambapo angeenda kupanga.
" We Maya! ", sauti ya Mhasibu... mama mtu mzima ilimshtua kutoka katika lindi la tafakari lile.
Akiwa palepale mlangoni mwa ofisi yake ambapo alikuwa amesimama tangu afike pasipo kufungua mlango aligeuka na kumtazama mhasibu huyo ambaye alikuwa amesimama mlangoni pake akiwa amefura kwa hasira.
"mbona umeondoka bila kuaga! ", aliuliza mama yule na kumfanya Maya ashangae iweke swali kama hilo.
" umeshika kazi enhee!", aliuliza Mama yule na kumfanya Maya avunje uso kwa dharau kisha pasipo kumjibu alifungua mlango wa ofisi yake na kuingia ndani.
Aliketi na kuanza kushughulikia kiporo ambacho alikiona kabla hajanyanyuka na kwenda kuonana na baba mwenye nyumba.
" hivi wewe kinqchokupa jeuri haswa ni nini? ", alihoji mama huyo na kumfanya Maya aache kufanya kazi na kumtazama.
"samahani mhasibu... Huenda wewe umeshamaliza kazi zako hivyo uko hurubkufanya utakalo muda huu wa kazi... Ila mimi bado akamaliza kazi zangu... Hivyo nipishe niendelee na kazi! ", alijibu kwa sauti ya utaratibu na kugeukia tena kompyuta yake ya mezani na kuendelea na kile alichokuwa akikifanya mwanzo.
" mshzxxxzxz!", alitoa msonyo mrefu sana mama yule kisha akatoka ofisini hapo.
" we si unajidai jeuri nitakuonyesha sasa nani zaidi mimi au wewe! ", alisema mama yule akiwa nje ya korido na sauti ilimfikia vyema Maya pale kwenye meza yake alipokuwa.
"MshxZxzxs!", alijikuta naye alirudisha msonyobule kisha akabetua midomo yake juu na kuendelea na kazi punde kidogo akaingia Jimmy akiangua kicheko bila shaka alikuwa amekishikilia akingojea mhasibu afike mbali.
" vipi nawe mbona hivyo na hilo kicheko! ", aliuliza Maya naye akicheka bila shaka vitendo vya mwanamke huyu vilianza kuchekesha badala ya kumhuzunisha kama ilivyokuwa awali.
"si huyo mama yako wa kambo... ", alisema Jumla huku bado kicheko kimemshika.
" nilivyofika tu kuja kukushikia nafasi yako akaja mbiombio bila shaka alijua wewe ndio umerudi ila aliponiona ni mimi aligwaya.
" huyu cha kuringa yupo wapi? " aliniiuliza.
' nikamjibu Ametoka mara moja... ", alisema Jimmy.
"loh!, wacha aanze kufunguka mwanamke... Huyu anafanya ofisi kama ya baba yake... Anatoka anavyojisikia na ngja dawa yake iko jikoni inachemka", alisema Jimmy.
" sasa kilichonichekesha ni vile alivyotaka kurudi ofisini kwake na alivyo mfupi halafu kibonge dah!, ni kama ksmgambo lako depo bado hawajajua mafunzo vizuri!", alisimulia Jimmy na hapo Maya akajikuta akiungana kucheka.
" yaani kako hivi kashingo kakakaza....", alisema Jumla akimuigizia mhasibu namna alivyokuwa akitembea.
" we champlin hebu itokee hapa..., unanichekesha nashindwa kumalizia kazi zangu.. toka vyama! ", alisema Maya akichukua kipande cha karatasi nyeupe Akaikunja kunja na kumpiga nayo Jimmy ambaye alitoka mbio huku akiendelea kucheka.... ITAENDELEA
MINE...ONLY MINE
part 4
Jioni ile alivyotaka ofisini alipita moja kwa moja kwenye ofisi ya dalali wa mwanzo ambaye alimtafutia nyumba ya kwanza.
Kwa bahati alimkuta ndio anafunga ofisi yake kwani ilikuwa ni majira ya saa moja kasoro.
" dah!, bora nimekuwahi ndugu kaka yangu!", alisema Maya alijongea pale ofisini kwake.
" na imeniwakia kweli maana hapa nilikuwa natoka na simu imeniishia charge nimeshindwa natembea watu siku nzima kuangalia vyumba.
" mmmh niambie dada yangu... Naona unazidi kupendeza tu! ", alisema dalali yule.
." mmmh asante ikiwa machoni pako naonekana kupendeza...,, alisema Maya kisha akanieleza hitaji lake alilokuwa nalo.
Mmmh tena bahati ni yako kuna nyumba ipo maeneo ya kawe na Nyingine Drive inn ila zina bei kidogo dada yangu ni tofauti na hiyo unayokaa.
Ya Drive inn ni laki tatu kwa mwezi na ya kawe laki mbili na nusu ", alijibu na hapo Maya akajikuta nguvu zikimuishia.
" kutoka laki moja na nusu hadi laki mbili na nusu ni parefu sana jamani.. Hakuna ya pungufu na hapo basi hata laki mbili! ",.aliuliza Maya.
"dada zipo hadi za laki moja ila tofauti na mazingira hayo inayotawala wewe... Zipo Kinondoni... Buguruni ila choo cha kushea yaani unakuta nyumba ina vyumba sita na ni chumba na sebule hivyo wapangaji watatu na choo cha ndani Mnashea", alisema dalali yule.
" mmmh hayo ndio siyatakagi hata. maswala ya kukuta mtu kuacha mzigo wake hajaflash halafu nimekuzwa na kutumia choo changu mwenyewe hivyo maparago tabu nikiwatembelea rafiki zangu wwnapoishi", alisema Maya.
" ila vipo Kimara bunju Pugu tena vikubwana vizurinkuzidi pale unapokaatatizo huwezi kuishi sehemu hizo", alisema dalali.
" aaah majina chumvi tena na kutwa kuamka saa kumi kuwahi.usafiri na kurudi nyumbani saa nne ya nini yote hayo!", alijikuta akisema Maya kuonesha hawezi kuishi sehemu hizo
" dah!, ngoja nikajisachi nione Kama itawezekana kupata hilo cha kawe kitakuwa kizuri sana maana ni karibu na kazini kwangu", alisema Maya kisha akaagana na dalali yule.
************
Babe bwana mie hii simu nimeichoka nataka nyingine.. Nataka IPhone 6 plus alisema Martha kwenye simu kumwambia mpenzi wake Brown mara baada ya kumpigia.
Uso wake alikuwa amepata mask ya parachichi hivyo pale kwenye kochi alipokuwa ameketi alikuwa ni kama kizuka fulani hivi.
" jamani hii Iphone S si ya tangu mwaka jana mpenzi... Mie nimechoka bwana! ", alijibu Maraha kwa kudeka.
" huu ni mwezi wa tano!", alijibu Martha.
" mmmh sijui ilikua awa kumi na mbili vile... Ilikuwa zawadi ya christmass nakumbuka ndio ulimiminika hii simu!", alijibu Martha.
" aaah mpenzi jamani sa miezi mitano midogo kukaa na simu hiyohiyo tu. Mi nataka simu nyingine bhana... ", alisema Martha huku jazba ikianza kumpanda.
" asa hiyo flat screen ya LG
Imeingialianaje na simu? ", aliuliza huku kabinua midomo kana kwamba huyo anayezungumzia naye anamuona.
" aaah sasa si nilikuambia mie nimechoka kuchungulia TV... nataka kuangalia Tv... we umeniletea mie ka-TV ka inch 32 hadi nifumbe jicho ndio nione.
Nataka ya 45 inch hadi raha unajikuta unamuona beyonce, Ciara, Jlo kwa ukaribu kabisa", alisema Martha.
" aaah we nawe sasa milioni moja na laki tano ikijumuisha na hiyo nyingine huzidi hata milioni tatu...
Na we si umeenea kupeleka mzigo hilo ukarudi una pesa zaidi ya milioni kumi sasa kupunguza milioni unaona hasara!", alijibu Martha.
"sio upige mahesabu we nijibu kuwa utaniletea kurudi navyo tena huko bei yake ni rahisi sana tu", alisema Martha.
" ok babe i love you... Mwaa! ", alijibu Maraha kisha akakata simu na kuitupia simu pembeni.
" mwanaume mbariki huyu yaani milionintatu anajilalamikisha... Oohh nitawapa wenzie wamsaidie kutunza mzigo", alisema kisha akachukua vipande viwili vya tango kisha akamlaza kwenye kochi lile na kufumba macho akaviweka juu ya macho yake...ITAENDELEA
MINE...ONLY MINE
part 5
" laki nane! !", alijikuta akisema kwa mshangao Maya mara baada ya kuuliza salio la akaunti yake ya bank punde tu alipofika nyumbani kwake.
Sasa laki nane mimi nitaifanyia nini?', aljikuta alijiuliza Maya huku usingizi wote aliokuwa nao ukiwa umempa.
Dah!, ningekumbuka kuwa natakiwa kuhama hapa basi pasi na shaka nisingenunua ile mashine ya kufulia! ", alijikuta akisemaambapo alitumia karibia nusu ya mshahara kununua mashine ile na kilichobakia alikihifadhi kwenye kwenye akaunti yake ya bank.
" sasa natoa wapi pesa nyingine na ndio kwanza tarehe kumi na saba leo na muda wowote huyu mwenye nyumba anakuja kuchukua nyumba yake! ", alijikuta akisema Maya.
Alitafakari kwa dakika kadhaa ndipo akafanikiwa kupata wazo la wapi anaweza kupata pesa hiyo anayohitaji.
Hapo sasa hata hamu ya kula iliweza kumjia na kujikuta akinyanyuka na kwenda kubandika maziwa ambapo alichukua mayai mawili na kuyakaanga pamoja na kesi nne za mkate.
Aliridhika na mlo huo ambapo aliingia bafuni kuoga kisha akajitupa kitandani na kutokana na kutingwa kwa siku nzima alikokuwa nako alijikuta ikimchukua dakika chache kupotelea usingizini.
Kulipokucha aliwahi kuamka kama kawaida yake na kujiandaa kwenda kazini zake.
Alifika na kumsalimu Rose msichana wa mapokezi ambaye aliitikia salamu yake na kujikuta akitabasamu huku akisikitika.
Rose alikuwa ni mpenzi wa Jimmy ila ukaribu wake na Jimmy ulimkwaza Rose na kujikuta akianza kumfanyia vituko.
Maya hakuwa na chuki na Rose licha ya vituko vyote alivyokuwa amefanyiwa alielewa ni kutokujiamini kwa Rose na wivu tu ndio uliomsumbua.
"Jimmy mambo! ", alisalimia Maya kumsalimia Jimmy aliyekuwa akishusha ngazi bila shaka alikuwa akimfuata Rose.
" vipi mhasibu yupo? ", aliuliza Maya.
"naam yupo kajaa tele",alijibu Jimmy.
" mmmh unataka uende ukayatibue ya jana? ", aliuliza Jimmy.
" hamna nina shida naye tu... ", alijibu Maya.
Alipandisha ngazi hadi ghorofa ya pili na kushika njia kuelekea ilipokuwa ofisi ya mhasibu huyo.
Aligonga mlango lakini hakuitikiwa... Aligonga tena lakini hakutokea akajikuta akichukua maamuzi ya kushika kitasa na kukifungua.
" lahaula alimkuta mhasibu akiwa amelazwa juu ya meza na mwanaume akiwa juu yake na kuwashtua ambapo wote walishtuka na kusimama na hapo alimgundua yule mwanaume aliyekuwa juu ya kifua cha mhasibu alikuwa ni meneja uajiri mwanaume ambaye alikuwa kumkosesha raha kila siku kwa kumtaka kimapenzi.
" mnatia aibu yaani mnafanya kazi hotelini halafu bado mnafanya uchafu ofisini... Si mmeona tu hata chumba kimoja.. Looo ptuuu!!", alijikuta akisema Maya kwa dharau kisha akatoka hata hamu ya kufanya kile kilichompeleka ofisini humo alikighairi kwa muda huo.
Ni wakati anaingia ofisini kwake ndipo Michael aliyekuwa ametulia pasipo kupandisha wala kushusha ngazi zile alipojitokeza toka kwenye kificho kile.
Alikuwa amesikia maneno ya Maya na kujikuta akitabasamu huku akisikitika na aliamua kubaki kwenye ngazi kuepuka kuhusishwa na fumanizi ambalo hakuwa amepanga kulifumania.
Alisubiri hadi meneja uajiri alipotoka ofisini kwa mhasibu ndipo naye alipoamua kupiga hatua na kujongea ofisi hiyo.
Aligonga mlango japo ulikuwa wazi ambapo aliweza kumuona mhasibu akiwa amekufa kwa aibu na hasira kutokana na fumanizi like..
" ingia! ", alijibu kwa jazba na Michael kwa ustaarabu wa hali ya juu aliingia ofisini mule.
" Shikamoo mama! ", alisalimia kwani kiumri mwanamke yule Alikuwa na uwezo wa kumzaa lakini alipokelewa na jicho la imekuwaje umri wangu hadi uniamke.. Usinizeeshe kijana.
" nikusaidieje! ", alijibu mhasibu hukubakijitahidi kuifuta gauni yake ya mpira impate vizuri.
" nilitumwa proposal ya fanicha za chumbani na ikakubaliwa... Sasa akapokea malipo ya awali ili kudeliva hizo fenicha", alisema Michael.
" ooh kumbe wewe ndio bwana Michel! ", alijikuta akisema mhasibu na hapo akamtazama Michael vizuri na kuuona muonekano mzuri aliokuwa nao kisha akaanza kujichekeshachekesha.
" aaah nilikuwa nimeshaandika cheki... Ila sijui nimeiweka wapi... ", alisema huku akijidai kufungua droo za kabati kuitafuta ilhali hakuwa ameandika chochote na hata mahesabu yenyewe hakuwa ameyaandaa zaidi ya kuisoma proposal basi.
" aaah sokoni jamani samahani naomba uende halafu kesho tutakuletea mwenyewe ofisini kwako... Samahani kwa usumbufu", alisema mhasibu na kisha Michael hakuwa na chochote zaidi ya kumuaga mwanamana yule.... ITAENDELEAMINE...ONLY MINE
part 6
" nahitaji mkopo wa milioni tatu... ", alisema Maya mara baada ya kuingia ofisini kwa Mhasibu mara baada ya kufungua kinywa.
" umesema! ", alisema kwa mshangao mhasibu.
" nimesema nahitaji mkopo wa milioni tatu tena nahitaji kwa haraka ndani ya wiki hii na mtanikata nusu ya mshahara wangu hadi utakapoisha ambapo ni miezi mitatu", alisema Maya kwa kujiamini kwakuwa alijua wazi kwamba uwezekano wa kupewa mkopo huo upo bila kizuizi.
" siwezi kukupatia mkopo huo", alijibu kwa nyodo mama yule.
" kwa vigezo vipi!", alihoji Maya.
" ulitakiwa ulete proposal ya kuwa unahitaji mkopo wiki kabla ili nikuandalie ", alijibu mama yule.
" hiyo ni kwa mkopo mkubwa lakini wangu ninmdogo na ni wa haraka na kanuni inaruhusu ikiwa sina mkopo ninaodaiwa nyuma na nina mkataba wa zaidi ya miezi sita kazini", alijitetea Maya.
" nimesema kanandile proposal ulete tena nilifikiri! ", alijibu kwa nyodo Mama yule.
"ila hii sio sawa kabisa yaani umeanza kuiendesha ofisi kama yako....", alilalamika Maya huku akinyanyuka na hakuweza kufanya chochote kwani mtu pekee wa kumpatia mkopo ni yule mhasibu na sehemu pekee ya kwenda kutoa malalamiko ni kwa meneja muajiri ambaye alikuwa ndio hawara yake.
Watu wawili Hawa waliigeuza hotel Hii kama yao wakifanya chochote walichotaka kwa wafanyakazi wenzao bila kujali kanuni za kazi zinasemaje na hili liliweza kushika hatamu zaidi kwani meneja uajiri alikuwa ni ndugu wa mkurugenzi mtendaji wa hoteli Hiyo na alimuchia majukumu yote ya hoteli hiyo.
Alirudi ofisini kwake akiwa amenyong'onyea akiwaza namna nyingine ya kupata pesa hiyo.
Meneja uajiri alikuwa ni wale waajiri ambao wana tabia za kuwa hayuko tayari kukupa kazi hadi ahidiana kimapenzi na muajiriwa.
Na hiki ndicho kilichokuwa kimtokea hotelini hapa ambapo wasichana wengi walikuwa wakipitiwa kwanza kabla hawajapewa mkataba wa kufanya kazi hotelini hapo.
Ni wasichana wachache ambao walikuwa wakijielewa ambao hawakuwahi kupitiwa na meneja uajiri huyo na miongoni mwao alikuwa ni Maya na Rose.
Hawa walikuwa ni wasichana wqliojitambua na waliothamini utu wao na ni mara nyingi sana walifuatwa na meneja muajiri huyo lakini hakukubali jambo lililowafanya wasumbuliwe na kupata usumbufu wa hapa na pale toka kwa meneja uajiri huyo
Isingekuwa ni mshahara mnono na marupurupu ambayo Maya alikuwa akipata hotelini hapo basi pasi na shaka angekuwa ameshaacha kazi hiyo kitambo sana.
Lakini kwa mshahara ule wa milioni moja na laki sita pamoja na marupurupu ya karibia laki kila wiki alijikuta akiyafumbia macho matatizo hayo na kuwekeza nguvu zake kwenye kazi yake.
Alichukua simu yake na kutafuta namba ya Jackson na kumpigia na walikuwa waliwasilisha tangu jana mchana walipoachana.
" hey babe...! ", alisema Maya mara baada ya Jackson kupiokea pinde tu alipopiga simu hiyo.
" babe nina shida ya milioni tatu it possible niazime nitakurudishia", alijieleza Maya.
" hakuna neno mpenzi njoo nyumbani uchukue au nikuletee kazini kwako ",.alijibu Jackson.
" mmmh hamna haja ya kukuambia nitapiga mwenyewe jioni nilitoka kazini", alijibu Maya na kumuaga mpenzi wake huyo.
" hivi huyu pesa zake huwa anatoa wapi... Naweza hata nikamuomba milioni kumi akanipa sio mchoyo sana ila sasa tatizo lake ni hilo anaamini anaweza akanibadili mawazo yangu na pesa zake... ", alijikuta akisema Maya.
Katika kipindi chote alichofahamiana na Jackson hakuwahi kujua anafanya kazi gani kuingiza kipato kikubwa vile.
" mi ni mfanyabiashara...", ndivyo alivyojitambulisha mara ya kwanza lakini hakuwahi kuziona biashara zake aliyodai anafanya.
Hakuwahi kuona duka genge wala soko ambalo mwanaume huyo alidai anafanya biashara ila aliweza kuona pesa na zawadi na mitoki ya gharama toka kwa mwanaume huyo.
" jamani kwahiyo wewe unataka uone duka langu la biashara! ", alijibu siku moja mara baada ya Maya kumhoji sana kuhusiana na biashara anazidi anafanya.
" usijali siku moja nitakutambukisha kwenye biashara yangu! ",alijibu Jackson lakini hiyo siku moja haikutimia. ... ITAENDELA
Jina langu ni Penny Hope tunatoa kiwango cha maslahi ya mkopo ni 1%. Je! Unahitaji
ReplyDeletemkopo? ikiwa ndiyo, wasiliana nasi na barua pepe hii: pennyhope01@gmail.com
kwa zaidi au wasiliana nami kupitia whatsapp {+2348105849778} habari, jina kamili:
Kiwango cha Mikopo: Muda: Nchi: Anwani: Nambari ya Simu Mungu akubariki.
Penny Hope