Home → simulizi
→ SIMULIZI: JINA LA URITHI
SEHEMU YA SITA(06)
⚪⚪⚪ILIPOISHIA⚪⚪⚪
ikasikika sauti ya mmoja wa vijana hao akisema,,"MAMAAAA NAKUFAAA!
ghafla ikasikika tena sauti ya kijana mwingine akisema,,"tafadhali usiniuwe, kabla hajaongea neno lingine akastaajabu anavutwa juu qngani na kuachiliwa akadondoka chini,,na kupasuka kichwa..
punde si punde lile giza likatoweka kimiujiza! pakawa na mwanga!
baadhi ya vijana waliobaki hai,,wakashtuka kuona wenzao wamekufa vifo vya kutatanisha! walipotazama ile nyumba iliyokuwa imeteketa kwa moto,, macho yakawatoka! hofu ikazidi kutanda hawakuamini walichokiona mbele yao!!!!!!!
KIZAA ZAA
⚪⚪⚪ENDELEA⚪⚪⚪
Wakamuona Laula akiwa kasimama mbele yao,,mikono yake ikiwa imetapakaa damu! kila aliyejaribu kunyanyua mguu wake atimue mbio alishindwa,miguu yao ilikuwa mizito hakuna aliyeweza kunyanyua mguu,utadhani wamewekewa gundi kali!
hofu ikatanda juu yao....
Laula akazipiga hatua kuondoka eneo hilo! kabla hajafika mbali akaanza kubadilika taratibu,,kutoka katika umbile la mtoto Laula,,na kuwa mzee kikongwe! kisha mzee huyo akatoweka kimiujiza,,na nyumba ikaonekana kama haijachomwa moto,,ikawa vilevile,,kama inavyo onekana miaka yote! punde si punde wale vijana watatu walioonekana wamekufa,,wakafufuka na kurudi katika uhai wao!!!
wale vijana wengine wakahisi kama miili yao imeachiliwa hata wakaweza kunyanyua miguu yao,,wakatimua mbio! kila mmoja alipita njia yake!
na kutokomea kusikojulikana!
baada ya dakika kadhaa habari zikaenea kijiji kizima kuwa imeonekana miujiza,kule katika nyumba ya Njile,! mashuhuda ambao ni wale vijana wakasimulia matukio yote waliyoyaona! kijiji kikazizima wanakijiji wote wakaingiwa na hofu kutokana na uvumi huo,,kilichowashangaza zaidi,Nyumba imechomwa moto na ikateketea kabisa,,lakini Nyumba hiyo ikarudi upya na kuonekana kama haijachomwa moto!
Upande mwingine,,alionekana Laula akiwa anazipiga hatua,,alitembea pasipokujua ni wapi anaelekea! kwa mbali akaona watoto wa lika lake,,wanacheza mpira wa miguu! Laula akatabasamu,,akaonekana kuvutiwa na mchezo huo,,akaamua kuwafuata watoto hao na kujumuika nao katika mchezo huo.
Laula akaonekana kujua kusakata kabumbu zaidi ya wale watoto wote,,,wakiwa mchezoni,kwa bahatimbaya mtoto mmoja akamkanyaga Laula akadondoka chini na kuvunjika mkono!
watoto wote wakaogopa kumuona mwenzao kavunjika mkono!
watoto wengine wakatimua mbio kurudi majumbani kwao..
lakini cha kushangaza Laula hakuonyesha kupata maumivu katika mkono wake! akanyanyuka na mkono wake ukajiunga na kurudi katika hali yake ya kawaida kama vile haujavunjika!
kitendo hicho kiliwafanya wale watoto waliobaki wakimshangaa Laula,waogope,,bila kuchelewa wakaanza kutimua mbio!
kwa mbali akaonekana yule mzee kikonge akimtazama Laula kisha mzee huyo akazipiga hatua na kutokomea katika kichochoro!
Laula akamuona mzee huyo,,akashtuka! akajisemea moyoni,,"huyu aliniambia kuwa ni babu yangu,,huwa ananifuata nyakati za usiku na kunipeleka kuleeee!
Laula alijisemea maneno hayo huku akitimua mbio kwenda kumfuata babu yake! angalau ajue ni wapi anapoishi! kwa sababu huwa anamuona nyakati za usiku tu,,na sehemu anayopelekwa huwa hakuna nyumba hata moja,,hivyo hakuwahi kubahatika kumuona nyakati za mchana.
Laula alipofika katika kichochoro hicho,,hakumuona tena mzee huyo! akaangaza angaza macho yake huku na kule lakini hakufanikiwa kumuona! Laula akabaki akijiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu! akaamua kuondoka eneo hilo na kuelekea katikati ya mji!
masaa yalizidi kusonga! na giza likaanza kutanda,,Laula akaamua kuketi nje ya kibaraza cha duka moja lililokuwa limefungwa,,,akajilaza hapo,,baada ya dakika kadhaa akapitiwa usingizi! akalala usingizi mzito,kutokana na uchovu aliokuwanao! baada ya masaa kadhaa kupita akaijiwa na ndoto katika usingizi!
akahisi kunamtu anagusa mkono wake,,akafumbua macho yake!
akamuona babu yake ndiye amemshika mkono!,, Laula akanyanyuka na kuongozana na mzee huyo! wakatoweka kimiujiza! na kujitokeza kando ya makaburi! Laula akastaajabu kuona makaburi mengi ,,,alioojaribu kutafakari hapo ni wapi? ghafla akahisi mkono wake umeshikiliwa kwa nguvu, tofauti na mwanzo! akaanza kuhisi maumivu katika mkono wake! akasema kwa sauti kavu,,"babu unaniumiza mkono wangu.
lakini mzee huyo hakuachilia mkono wa Laula,,akaendelea kumuongoza mpaka ktikati ya makaburi,,mbele ya kaburi moja wakasimama,,Laula akashindwa kuvumilia maumivu hayo,,akaanza kulia huku akinyanyua uso wake kumtazama babu yake! Laula akashtuka kumuona babu yake amebadilika na kuwa mifupa mitupu,,aliweza kuona hivyo kwa sababu mifupa hiyo ilikuwa inaang'ara kama saruji! akaingiwa na hofu! punde si punde lile kaburi lililokuwa mbele yao likapasuka na shimo likabaki wazi! Laula akapiga kelele!
mara ghafla ukimya ukatawala!!!!!!!!!!
↔↔↔↔↔ITAENDEA↔↔↔↔↔
Kila msomaji hakikisha una LIKE hadithi hii kuipa nguvu..niirushe kila siku
NAAM..je? ukimya huo unaashiria jambo gani?
je? hiyo ni ndoto au ni kweli,,yamemtokea LAULA?
Ungana nami katika sehemu ya 7.
wingi wa Like zenu ndizo zitafanya nilete muendelezo kwa wakati.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: