Home → simulizi
→ SIMULIZI: JINA LA URITHI
SEHEMU YA TANO(05)
⚪⚪⚪ILIPOISHIA⚪⚪⚪
akafungua sanduku kubwa la mbao,,lililokuwa na nguo za baba yake,,akaanza kutoa nguo mojamoja...akafanikiwa kuchukua mashati kadhaa,,lakini akaona suruali moja ikamvutia,,,akaichukua suruali hiyo na kuivaa,ingawa ilikuwa kubwa lakini hakujali,,akaikunja upande wa chini kisha akafunga kamba kwenye sehemu ya kiuno,,,akachukua redio ndogo iliyokuwa chumbani humo pamoja na picha za mama yake zikiwemo pamoja na picha za babq yake akazishikilia mkononi,,kisha akatoka nje,,,kabla hajafika mbali,,akaamua kuziweka picha hizo katika mfuko wa suruari hiyo.
akashtuka! akahisi kama kunakitu ndani ya mfuko wa suruali hiyo,,akaingiza mkono wake ili aone ni kitu gani hicho!
TAHARUKI!!!!
⚪⚪⚪ENDELEA⚪⚪⚪
Akastaajabu kuona jino la binadamu! akalishikilia juu ya kiganja chake kisha akatabasamu,,,akajisemea moyo,,"bila shaka lilikuwa jino la baba yangu,,
lakini sijui yuko wapi! mama alisema baba kasafiri mmh! inamaana hatorudi tena! au atakuwa amepata mke mwingine!?
mpaka sasa Laula hajui ukweli kuhusu kifo cha baba yake!
akaendelea kuzipiga hatua na kuondoka zake.
Uoande mwingine,,alionekana mwanamke mmoja,,akitimua mbio na kuingia kwa pupa kwa mkuu wa kijiji! kisha akasema,,"wale watu waliofukuzwa hapa kijijini,,wamerudi tena! nimemuona mtoto wa Njile akitokea ndani ya nyumba yao!
Mkuu wa kijiji akaingiwa na hasira akasema,,"hii ni dharau! Nyumba hiyo ichomwe moto haraka iwezekanavyo....
akaamuru jinana wakachome moto nyumba hiyo.
Wakati huo huo,,upande mwingine, alionekana Laula akiendelea kuzipiga hatua kurudi mjini,,
baada ya masaa kadhaa kupita,,akahisi kuchoka na pia njaa ilimuandama! akapiga moyo konde na kuendelea kuzipiga hatua.
Kule Kijijini,,walionekana wale vijana walioamrishwa waichome moto nyumba ya Njile,,,wakiwa wamesimama kando wakisubiri nyumba hiyo iteketee kabisa ndipo waondoke eneo hilo.
Upande mwingine alionekana Laula akiendelea kuzipiga hatua,,hatimae akafika mjini,,,angalau akanza kupata matumaini ya kupata chakula, kwa mbali akaona genge dogo la kuuza samaki,,akaamua kulifuata genge hilo,,,alipofika akachukua samaki mmoja mkubwa kisha akaanza kula samaki huyo.
muuzaji hakuwa na wasiwasi kwa sababu,,baadhi ya wateja wake wengine hununua samaki na kula hapohapo...Laula akaendelea kumtafuna samaki huyo kwa pupa,,kisha akachukua samaki mwingine,,akaanza kula.....alipomaliza kula samaki huyo akazipiga hatua kuondoka zake,,pasipo kulipia pesa!
mama muuza samaki akapaza sauti,,"wewe mtoto.
lakini Laula hakugeuka,,akaendelea kuzipiga hatua!
yule mama muuza samaki,,akakasirika, akapaza sauti kwa hasira,,"wewe mtoto rudi hapa! Laula akasita kutembea akasimama,,akageuza shingo yake,akakutanisha macho na mama muuza samaki,wakatazamana nyuso zao! mara ghafla yule mama muuza samaki akatimua mbio huku akipiga mayowe.
Laula akaendele kuzipiga hatua na kutokomea kusikojulikana!
Wakati huo huo,,kule kijijini,walionekana wale vijana wengi wakishuhudia nyumba ya Njile ikiendelea kuwaka moto,,vijana hao walikuwa wamesimama kando huku wakiimba kwa kilugha chao nyimbo za matusi,,wakiitukana familia ya Njile...
Nyumba iliendelea kuwaka moto hatimae ikateketea,,na moto ukaanza kupungua,,,,ghafla likatanda wingu kubwa!
winngu hilo lilisababisha taharuki,,giza totoro likatanda...
kwa mbali akajitokeza mtu kisha akatoweka kimiujiza! baadhi ya vijana hao walimuona mtu huyo lakini hawakutambua ni nani! hofu ikatanda juu yao,,giza lilizidi kutanda,,hakuna aliyeweza kumuona mwenzake! punde si punde ikasikika sauti ya mmoja wa vijana hao akisema,,"MAMAAAA NAKUFAAA!
ghafla ikasikika tena sauti ya kijana mwingine akisema,,"tafadhali usiniuwe, kabla hajaongea neno lingine akastaajabu anavutwa juu qngani na kuachiliwa akadondoka chini,,na kupasuka kichwa..
punde si punde lile giza likatoweka kimiujiza! pakawa na mwanga!
baadhi ya vijana waliobaki hai,,wakashtuka kuona wenzao wamekufa vifo vya kutatanisha! walipotazama ile nyumba iliyokuwa imeteketa kwa moto,, macho yakawatoka! hofu ikazidi kutanda hawakuamini walichokiona mbele yao!!!!!!!
KIZAA ZAA
↔↔↔↔↔ITAENDEA↔↔↔↔↔
Kila msomaji hakikisha una LIKE hadithi hii kuipa nguvu..niirushe kila siku
je? vijana hao wameona nini mbele yao?
je? ni nani aliyefanya mauwaji hayo?
Ungana nami katika sehemu ya 6.
wingi wa Like zenu ndizo zitafanya nilete muendelezo kwa wakati.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: