SIMULIZI: JINA LA URITHI SEHEMU YA NNE(04) ⚪⚪⚪ILIPOISHIA⚪⚪⚪ hatimae baba Laula akazaliwa,,,lakini aliishi na kufanikiwa kuoa Lakini akaanza kuota magome ya miti katika mwili wake akapelekwa hospitali lakini haikufahamika anaumwa ugonjwa gani,,,ndugu zake wakaamua kumpeleka kwenye tiba mbadala wakampeleka kwa mganga wa kienyeji....mganga akasema,,mkitaka mtu huyu apone,,ni lazima akafukue kaburi la muanzilishi wa ukoo wake,,achukue jino la mbele katika fuvu la muanzilishi wa ukoo wake...ikalazimika afanye hivyo! siku hiyo akadamka usiku wa saa sita akaelekea makaburini! alipolikaribia kaburi hilo mara ghafla!!!!! ⚪⚪⚪ENDELEA⚪⚪⚪ akahisi miguu yake imekuwa mizito kupiga hatua,,lakini akajipa moyo,,akalisogelea kaburi hilo,,punde si punde kaburi likafunguka akafanikiwa kuona mabaki ya mifupa ya muanzilishi wa ukoo wake,,akatumbukia ndani ya kaburi hilo,akachukua jino moja la upande wa mbele katika fuvu la muanzilishi wa ukoo wake! akatoka ndani ya kaburi hilo,,,ghafla akahisi mwili wake umekuwa mwepesi akapapasa mwili wake akafurahi kuona yale magome ya miti yametoweka katika mwili wake,,akaweka jino hilo katika mifuko ya suruali aliyokuwa kaivaa kisha akaondoka zake... akajisemea moyoni,,"mtoto wangu wa kiume nitamuita Laula,,hii ni kama shukrani yangu kwa muanzilishi wa ukoo wetu,,mtoto wangu nitamrithisha jina lake. baada ya miezi kadhaa kupita,,mkewe akashika ujauzito,,akazaliwa Laula. hiyo ni historia fupi ya chimbuko la jina Laula. ************** kule nyumbani Njile,,maisha yaliendelea,lakini mtoto Laula aliendelea kufanya matukio ya ajabu,,,habari zikazagaa kila kona ya kijiji,,kuwa Laula si binadamu wa kawaida.... mkuu wa kijiji hicho,akaamuru Njile pamoja na mtoto wake wafukuzwe,,wasiendelee kuishi katika kijiji hicho.. Njile hakuwa na namna,,akalazimika kuuza kila kitu kilichokuwa ndani ya nyumba,,pamoja na nyumba yenyewe ,,,lakini hakuna mtu aliyejitokeza kununua hata kitu kimoja,,hakuna aliyetamani hata kupewa kitu bure..Njile akaamuaa kuondoka na mwanae Laula,, akaelekea mjini,,ni mbali na kijiji hicho! Maisha ya Njile yakawa magumu kupita kiasi,,wakati mwingine hakuweza kupata mlo siku nzima,, Laula akashindwa kuendelea na masomo,,Njile akafanya jitihada za kutafuta vibarua ilimradi apate pesa ya kumpatia mlo mwanae Laula,, siku zilizidi kusonga,,wakiwa wanalala nje,,kitendo hicho kilimuumiza sana Laula. lakini hakuna namna. siku moja nyakati za usiku,,Njile aliugua ghafla,,homa ilikuwa kali na hakupata msaada wa matibabu,,Laula akatimua mbio kutafuta msaada lakini hapakuwa na mtu yeyote kuonekana kupita maeneo hayo,,zaidi ya magari pekee,,Laula akakata tamaa akaamua kurudi kule alipokuwepo mama yake,,akakuta tayari ameshakata roho! Asubuhi palipokucha ,,,Maiti ya Njile ikachukuliwa na maaskari,,na kuzikwa kwa sababu hakuwa na ndugu... siku zilizidi kusonga,,Laula akawa chokoraa,,akaishi kwa tabu na misukosuko ya kila namna,,, baada ya mwezi mmoja kupita,,wazo likajia Laula,,akaamua kurudi katika kile kijiji chao,,angalau akavhukue nguo za marehemu baba yake,pamoja na vitu vinavyobebeka, huenda akaviuza na kupata pesa ya kununua nguo za kuvaa yeye.. siku hiyohiyo safari ikaanza,,akatembea kwa miguu kuifuata njia ya kuelekea kijijini kwao,,hatimae,, akafika salama,,,akaifuata nyumba yao,,alipoingia upande wa ndani,,akastaaajabu kuona,,kila kitu kipo vilevile kama walivyoacha siku alipoondoka yeye na mama yake...akakifuata chumba alichokuwa analala mama yake,,,akafungua sanduku kubwa la mbao,,lililokuwa na nguo za baba yake,,akaanza kutoa nguo mojamoja...akafanikiwa kuchukua mashati kadhaa,,lakini akaona suruali moja ikamvutia,,,akaichukua suruali hiyo na kuivaa,ingawa ilikuwa kubwa lakini hakujali,,akaikunja upande wa chini kisha akafunga kamba kwenye sehemu ya kiuno,,,akachukua redio ndogo iliyokuwa chumbani humo pamoja na picha za mama yake zikiwemo pamoja na picha za babq yake akazishikilia mkononi,,kisha akatoka nje,,,kabla hajafika mbali,,akaamua kuziweka picha hizo katika mfuko wa suruari hiyo. akashtuka! akahisi kama kunakitu ndani ya mfuko wa suruali hiyo,,akaingiza mkono wake ili aone ni kitu gani hicho! TAHARUKI!!!! ↔↔↔↔↔ITAENDEA↔↔↔↔↔ Kila msomaji hakikisha una LIKE hadithi hii kuipa nguvu..niirushe kila siku. Ungana nami katika sehemu ya 5. wingi wa Like zenu ndizo zitafanya nilete muendelezo kwa wakati.s

at 3:47 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top