Home → simulizi
→ SIMULIZI: JINA LA URITHI
SEHEMU YA SABA(07)
⚪⚪⚪ILIPOISHIA⚪⚪⚪
alipojaribu kutafakari hapo ni wapi? ghafla akahisi mkono wake umeshikiliwa kwa nguvu, tofauti na mwanzo! akaanza kuhisi maumivu katika mkono wake! akasema kwa sauti kavu,,"babu unaniumiza mkono wangu.
lakini mzee huyo hakuachilia mkono wa Laula,,akaendelea kumuongoza mpaka ktikati ya makaburi,,mbele ya kaburi moja wakasimama,,Laula akashindwa kuvumilia maumivu hayo,,akaanza kulia huku akinyanyua uso wake kumtazama babu yake! Laula akashtuka kumuona babu yake amebadilika na kuwa mifupa mitupu,,aliweza kuona hivyo kwa sababu mifupa hiyo ilikuwa inaang'ara kama saruji! akaingiwa na hofu! punde si punde lile kaburi lililokuwa mbele yao likapasuka na shimo likabaki wazi! Laula akapiga kelele!
mara ghafla ukimya ukatawala!!!!!!!!!!
⚪⚪⚪ENDELEA⚪⚪⚪
Laula akashtuka usingizini ,,,akaangaza angaza macho yake huku na kule,,mapigo yake ya moyo yakaanza kupiga kwa kasi ya ajabu! akatimua mbio kutoka eneo hilo,,baada ya dakika kadhaa kupita akajikuta katooezea mtaa wa pili,,kulikuwa na maduka mengi yamefungwa.....akalifuata duka moja na kuketi kwenye kibaraza,,,baridi lilikuwa kali,,kutokana na upepo uliovuma mfululizo.. akajikunyata na uanza kuutafuta usingizi,,
Asubuhi palipokucha,,akadamka mapema kabla maduka hayajafunguliwa,,akazipiga hatua pasipokujua ni wapi anakwenda!
baada ya masaa kadhaa kupita,,akahisi njaa kali! akaamua kulifuata soko lililokuwa kando ya barabara...akaona ndizi mbivu.akazitamani ndizi hizo,,,akazipiga hatua mpaka katika meza hiyo...akachukua ndizi na kuanza kula.
alifanya vivyo hivyo kwa mara kadhaa hatimae akala ndizi tano! alipohisi kashiba akazipiga hatua kuondoka zake! punde si punde ikasikika sauti ya mama muuza ndizi,,akisema,,"wewe mtoto mbona unaondoka pasipo kulipa pesa ya ndizi ulizokula.
aliongea maneno hayo huku akizipiga hatua kumfuata Laula akamkamata mkono!
Laula akamtazama mama huyo kwa sura ya huruma! kisha akasema,,"naomba unisamehe sina hata shilingi....nilikuwa na njaa kali...nihurumie tafadhali.
mwanamke huyo akaingiwa na roho ya huruma akaamua kumuacha Laula aondoke zake.
upande mwingine kule kijijini,,hofu ilizidi kutanda ndani ya kijiji hicho! Nyumba ziliungua moto pasipokujulikana chanzo cha moto huo,,,ni zile Nyumba za watu walioshiriki kuichoma Nyumba ya Njile!
mkuu wa kijiji akaitisha mkutano,,,wanakijiji wote wakakusanyika kujadili nini suluhisho la mambo hayo yanayotokea.......wakakubaliana aletwe mganga mchawi kutazama ni kitu gani kinachoendelea ndani ya kijiji hicho,,
upande mwingine alionekana Laula akiendelea kurandaranda mitaani,,,alitembea umbali mrefu pasipokujua ni wapi anakoelekea! akajikuta anatoka katikati ya mji...baada ya kutembea masaa kadhaa mfululizo,akahisi uchovu,,akaangaza macho yake huku na kule kutafuta mti wenye kivuli,angalau ajipumzishe,,,
akafanikiwa kuona mti mkubwa akaamua kuufuata mti huo,,akajipumzisha....Laula akajikuta anazama kwenye dimbwi la mawazo mazito akanyanyua uso wake kutazama kando,,,akashtuka kuona eneo hilo kama alishawahi kuliona,,na sio mara ya kwanza,,alipojaribu kuvuta kumbukumbu,,,akastaajabu sehemu hiyo ni eneo la makaburi aliyoyaona ndotoni usiku wa jana! akanyanyuka harakaharaka....akazipiga hatua kuelekea katikati ya makaburi...huenda akaliona lile kaburi laliloliona kwenye ndoto...punde si punde akasikia sauti ya vishindo vya mtu akitembea nyuma yake!!!!
TAHARUKI!!!!!
↔↔↔↔↔ITAENDEA↔↔↔↔↔
Kila msomaji hakikisha una LIKE hadithi hii kuipa nguvu..niirushe kila siku
NAAM..je? ukimya huo unaashiria jambo gani?
je? hiyo ni ndoto au ni kweli,,yamemtokea LAULA?
Ungana nami katika sehemu ya 8.
wingi wa Like zenu ndizo zitafanya nilete muendelezo kwa wakati.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: