SIMULIZI: JINA LA URITHI SEHEMU YA KWANZA(01) Njile alimlea mwanae kwa upendo wa hali ya juu,,japo hakuwa na uwezo mkubwa kifedha....mumewe alifariki, siku ambayo alizaliwa mwanae wa pekee,,siku hiyo Mume wa Njile,,alidamka mapema na kumuaga mkewe kuwa anakwenda katika shughuli zake za kila siku kama ilivyo kawaida yake,,lakini Njile alishangazwa sana na kitendo hicho cha mumewe kudamka alfajiri, na sio kawaida yake! Njile hakuwa na kipingamizi,, mumewe akachukua kibuyu kilichokuwa na maziwa ya ng'ombe kabla hajatoka ndani ya nyumba akasema,,"nakupenda sana mke wangu,,mtoto utakayemzaa, kama ni wa kiume jina lake ataitwa Laula,,na kama ni wa kiume ataitwa Minze....aliongea maneno hayo kwa msisitizo,,, Njile,,akaonekana kuyazoea maneno hayo,,haikuwa mara ya kwanza mumewe kumwambia maneno hayo,,tena huwa anaongea kwa msisitizo,,,Njile akaitikia kwa kutikisa kichwa,,kisha akavuta shuka na kuendelea kuuchapa usingizi. Mumewe akatoka nje ya nyumba akafunga mlango na safari ya ikaanza kuelekea kusikojulikana,, maisha yake yote alikuwa anajishughulisha na ukulima,,alikuwa analima mashamba ya watu na kulipwa pesa baada ya kumaliza kulima mashamba hayo! baada ya masaa mengi kupita, kule nyumbani,hali ya Njile ikaanza kubadilika,,akaanza kuhisi maumivu makali,,chini ya kitovu,,maumivu hayo yalizidi,,kumbe siku za kujifungua zilikuwa zimetimia,,,Njile akajikaza akajikongoja kutoka nje ya nyumba huku akitambaa kama mtoto mdogo! wakati huohuo alionekana,,mumewe akiwa njiani kuruei nyumbani,,alipokaribia maeneo ya nyumbani kwake,,akastaajabu kumuona mkewe,akiwa anatambaa pale nje ya mlango,,..akaamua kutimua mbio na kumfuata mkewe,,akambeba na kumkimbiza kwanye kituo cha Afya, palikuwa na umbali kama kilomita tisa hivi.. alijitahidi kumbeba mkewe pasipokuchoka,,lakininkila dakika zilivyozidi kusonga,,hali ya Njeli ilizidi kuwa mbaya zaidi,,uchungu ulimuuma kupita kiasi....mtoto akazidi kuteremka na njia ya uzazi ikawa tayari imefunguka,,,akasema nilaze chini,,najifungua muda si mrefu,,hatutaweza kufika hospitali..mumewe akaamua kufanya kama alivyoambiwa na mkewe,,akamlaza chini,,Njile akaanza kusukuma mtoto kwa nguvu zake zote! hatimae mtoto akatoka tumboni,,,mara ghafla akastaajabu kumuona mumewe anajishika shingoni,,huku akikoroma,,kama kabanwa na kitu ndani ya koo...macho yakamtoka!!! mumewe akaongea kwa sauti ya chini,,akisema,,mtoto huyu aitwe LAULA, punde si punde akadondoka chini na kutulia tuli! mkewe akabaki na mshangao! akashtushwa na sauti ya mtoto wake,,ni baada ya kulia sauti kali,,,akajinyanyua akang'ata kitovu kilichokuwa bado kimeungana na kitovu cha mtoto,,kisha akakifunga fundo! alipomaliza akamtunika mtoto wake kwa khanga aliyokuwa amejifunga! khanga hiyo ilionekana kutapakaa damu! ghafla zikasikika sauti za ngurumo zilizoambatana na upepo mkali! kiza likazidi kutanda! Njile akaingiwa na hofu kupita kiasi,, ghafla wakajitokeza watu wawili kimiujiza,,watu hao walionekana kuwa wazee kupita kiasi,,ni mwanamke na mwanaume! wakati njile anatahamaki,,,ikasikika sauti ikisema...hakika wewe ni MKOMBI(mwanaume),,umetimiza kile kilichokusudiwa,, ni sauti ya mwanaume mzee kati ya watu hao wawili waliojitokeza kimiujiza,,kisha akaisogelea maiti hiyo akachomoa kisu na kukata kipande cha nyama katika mwili wa maiti hiyo. Njile akatamani kutimua mbio,,lakini alishindwa kwa sababu mwili wake haukuwa na nguvu hata za kumuwezesha kutembea,,akastaajabu kumuona mzee huyo,,akimfuata,,na kumnyang'anya mtoto kwa nguvu! pumde si punde yule bibi akazioiga hatua kumsogelea mzee huyo aliyekuwa kamshikilia mtoto mchanga,,Njile alipowatazama kwa makini wazee hao akashtuka kuona ni baba na mama wa mumewe,,kilichomshangaza zaidi wazee hao walikufa na wakazikwa miaka mingi iliyopita....wakati anatafakari nini cha kufanya mara ghafla!!!! TAHARUKI!!!!!! ↔↔↔↔↔ITAENDEA↔↔↔↔↔ Usikose kufatilia SIMULIZI hii ya kusisimua yenye maajabu ya kutisha,,iliyojaa mafunzo katika jamii zinazotuzunguka. Ungana nami katika sehemu ya 2. wingi wa Like zenu ndizo zitafanya nilete muendelezo kwa wakati.

at 3:47 AM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top