Sitaki tena – 08 Ilipoishia.. ....uku mwili wangu ukiwa hautamaniki.. Endelea.. "...Ingia kwenye gari mpumbavu wee..!" Aliendelea kunikaripia yule polisi ambaye sikumfahamu kwa jina lakini lafudhi aliyokuwa akiongea ilinifanya niamini kabisa atakuwa ni muhaya tena yule wa kule Bukoba ndani ndani (Vijijini),Tukiwa ndani ya ile gari aina ya 'One Ten' huku nikiwa nyuma na askari mmoja na yule mwingine akiwa anaendesha gari, Ujasiri wangu feki niliuweka pembeni hivyo nikawa ni mtu wa kutoa machozi na kujiuguza sehemu zilizoonesha kuumizwa katika mwili wangu,njia nzima mpaka tunaingia Kibaha nilikuwa mtulivu bila kusemeshwa kitu chochote na yule polisi,Tulipofika maeneo 'Mbezi' yule polisi akafungua kinywa chake na kuniuliza, "Unasikia njaa..?" "Kimya..!" "Dereva embu pitia pale 'Mnama Restaurant' tupate chochote..." Maswali aliyoniuliza na maongezi aliyokuwa akiongea na dereva ndo kati ya vitu vilivyoanza kuuchanganya ubongo wangu.. "Mbona kabadilika tena huyu polisi..? Asije kuwa wananifanyia njama kama Baba Ali..? Kwanini wameniagizia chakula kama kweli nina hatia?..sijui nimuulize kosa langu ni lipi hapa hapa..?" Nikiwa bado nimekaa katika kiti cha mgawaha mmoja pale mbezi nikiwa mimi na polisi wawili mmojawapo ndo yule aliyekuwa akinishikia bunduki na ndo aliyenifunga pingu, "Wewe muuaji unakula nini? "Hapana..., Sili chochot..." kabla sijamalizia kusema nilishtukia napigwa na kitako cha bunduki na yule yule polisi.. "Usitufanye siye wapumbavu, kuua uue..! Tunakuonea huruma japo na wewe upate chochote unatuletea 'usenge' au umeshazoea maharage ya Gerezani nini...?" Nilijikuta nanywea na kuwa mdogo na kukubali kula chakula kama walichoagizia wao ambapo walikuwa wakila wali nyama.. Ndani ya nusu saa nikarudishwa tena kwenye lile gari lakini safari hii nilishangaa hawakunifunga tena pingu mikononi hivyo nikabaki na maswali mengi sana kichwani.. * * * * Mawasiliano ya mimi na wale askari bado hayakuwa mazuri kwani hadi tunapita kimara hakuna hata mmoja aliyenisemesha zaidi ya yule mmoja kukaa karibu na mini nisiweze kutoroka huku mwingne akiwa dereva ndani ya ile gari... Mawazo yalitawala sana kichwa changu huku nikijiona si mtu tena wa kuonana na mama yangu wala Gervas..,nikiwa bado niko kwenye dimbwi la mawazo huku tukiingia kwenye foleni ya mataa pale ubungo ghafla macho yangu yakaamia kwenye gari la pembeni yetu aina ya 'suzuki' hasira nilizoshikwa nazo ghafla ziliwafanya hata abiria waliokuwa ndani ya daladala ambayo ilikuwa nyuma ya ile gari niliokuwa nimeikodolea macho waweze kunishangaa,hilo sikulijari kabisa maishani mwangu kwani Levina mi aibu ilishanitokaga siku nyingi ukianzia pale shuleni kwa kina Gervas waliponigalagaza wale wanafunzi,pia katika basi nililokuwa nimeshushwa hvyo ukinishangaa mi ntakuona mtu wa ajabu sana., Akili na mawazo yakiwa bado ndani ya kale ka suzuki ambapo macho yangu yalikutana uso kwa uso na mama ambaye sitakuja nimsahau hata nife, hakuwa mwingine bali ni yule mama aliyenipeleka polisi kwa mara ya kwanza na ndiyo aliyefanya maisha yangu yapo hivi mpaka sasa.., "lazima nife mimi au wewe" Nilijisemea kimoyomoyo huku nikimtolea macho yalioambatana na mchozi ulioanza kuniteremka kwa ghadhabu niliyokuwanayo, kilichofuata ni kuhema haraka haraka huku pua zangu zikianza kujaa makamasi kama mtu aliyepatwa na mafua ya ghafla..kama kawaida yangu sikutaka kuchelewesha mda.. "Bunduki kitu gani wacha anifyatue tu lakini kwa huyu adui yangu siwezi kamwe kumuacha.." Nikatoka spidi katika lile gari nililokuwa huku nikimwacha yule askari akinilenga huku akinikimbilia lakini hilo sikulijari ndani ya sekunde chache nikawa nshafungua na kuingia kwenye ile suzuki na ku loki milango yote tayari kwa kumvagaa yule mama aliyekuwa akiendesha peke yake ndani ya kale kagari.., Nilitumia kucha zangu na meno kama filamu zile za kutisha 'VAMPIRE' kuisambaratisha kwanza sura ya yule mama kisha nikachukuwa mtandio wake aliokuwa nao amejifunga mabegani na kuuvingirisha shingoni mwake tayari kwa kumnyonga,akiwa bado anakurupuka na kutapatapa pale gari zilikuwa tayari zimeruhusiwa na trafiki na wale polisi niliokuwa nao tayari niliweza kuwaona wakiwa nje wanataka kuingia ndani nilipokuamo,sikujua hata siku moja kuendesha gari lakini nilisikia kwa wenzangu tu kuwa kunakitu kinaitwa gia kipo kama rungu pia kingine kinaitwa krachi kipo miguuni, sikulielewa hilo lakini nilijikuta nimekanyaga chini bila kujua kama ndo breki au ndo hiyo krachi kisha nikalishikilia rungu na kulisogeza kisha nikashangaa kuona gari ikitoka tena kwa mwendo wa kasi pale,nikiwa huku nimekaza ule mtandio shingoni mwa yule mama huku upande mmoja nikishikilia msteringi nilijikuta nimevamia gari za watu wengine waliokuwa mbele yangu na kusababisha ajali mbaya pale huku umati wa watu ukifurika katika lile eneo kushuhudia ile ajari., Watu walikuwa ni wengi sana mpaka nikachanganyikiwa japokuwa nilijihisi mwili wote haufai kwa maumivu, ile gari niliokuwa nayo ilikuwa imeharibika vibaya baada ya mda mchache nilihisi kuna watu nje wanavunja vioo vya gari wanataka kuingia ndani katika kuangalia vizuri macho yakamwona yule polisi alionifikisha hapa nilipo.., "Levina...! Levina...!Jisalimishe mwenyewe unajitafutia matatizo" Yale maneno ya yule polisi aliyokuwa akiniambia, hayakuniingia akilini mwangu kabisa niliona kama anampigia mbuzi gitaa ili acheze.,yule mama sikujua kama alikuwa amekufa ila nilimwacha pale akiwa anahema kwa kasi ya juu huku akiwa hajitambui wala hajiwezi hata kunyanyuka,haraka haraka nikafungua mlango upande wa nyuma kisha nikatoka spidi huku nikiuacha umati wa watu ukiwa haujui nini kinaendelea kutokana na lile tukio.. Spidi niliyotoka nayo pale huku watu wachache wakinishangaa si kwasababu nimeponea chupuchupu kwenye ile ajali bali pia waliniona kama mtu aliyechanganyikiwa kwa jinsi nguo zangu zilivyokuwa hazitamaniki kwa uchafu tena ule uliokolea damu katika ile suruali aina ya trakisuti ilivyobadilika rangi nyekundu iliyokuwa imetapakaa damu na kuwa kama nyeusi nyeusi, Sikumuogopa hata mtu nilizidisha mbio huku nikielekea barabara ya kwenda mwenge, kelele za wapiga debe pale ubungo ziliongeza hisia zaidi ndani ya kichwa changu kwani kitendo cha kugeuka nyuma ilikuwa kosa kubwa sana kwangu kwani niliamini na kujua tu lazima umati mkubwa wa watu uwe unanikimbiza nyuma yangu huku, nikiwa nasonga mbele haijapita hata hatua ishirini mara kundi la watu wengine wakawa tayari wametanda mbele ya macho yangu... * * * * Baada ya yule polisi kunishika ndani ya basi akanifunga pingu baada ya pale akatikisa kichwa chake kuashiria kuwa ananifahamu akaniita na jina "Levina...!" "kwanini umeua tena?" "Au unapenda kwenda gerezani tena" Hayo ni kati ya maneno ninayoweza kuyakumbuka kwani yalinifanya niishiwe nguvu na kudondoka mpaka nikapoteza fahamu,ninachokumbuka nilishtuka na kushuhudia nikipepelewa na yule polisi huku nikiwa kwenye gari ambayo sikuitambua vizuri kwa nje kwani alikuwa amenilaza ndani ya lile gari na mikononi mwangu bado nilikuwa na pingu hivyo nilipopata usingizi akaendesha gari mpaka nakuja kushtuka tumeshafika Dar na nilikuwa nikiota ndoto tena matukio ya ajabu ajabu kama lile la kumuua yule Mama na kuharibu vibaya lile gari lake pia kufukuzwa na umati mkubwa wa watu pale ubungo.. "Mungu wangu kumbe yote yale ilikuwa ni kama ndoto..!" Nilijikuta nausemea moyo huku nikishusha pumzi kubwa.. "Uuhh...! uuhh...!" Taaratibu nikiendelea kuhema kwa nguvu na hasira kali., "Hapa ni wapi?" Nilijikuta nikimuuliza swali yule polisi aliyenitoa kule Chalinze na ndiye alikuwa amenipakia baada ya kuzimia pale Chalinze.. "Hupaswi kujua..unapaona pale?" "Nikakaa kimya.." Huku nikiona kibao kimeandikwa mbele yangu.., 'CENTRAL POLICE' Nilitamani kutoroka pale lakini nisingeweza kwani mda wote nilikuwa na pingu mikononi. "Levina...! Embu niambie ukweli hizo damu katika hyo suruali ilikuwaje?" Nikawa najiuma uma nashindwa nimpe jibu gani kwani ni kweli nimeua lakini nikisema ajue itanigharimu sana maishani mwangu.. "Afande hizi ni damu za kawaida tu ambazo nilipitia buchani kuchukuwa nyama na kupeleka nyumbani nilipokuwa kule Morogoro..!" Nilijikuta namdanganya lakini kiukweli alionesha kuchekeshwa na mimi sana mpaka nikamshangaa.. "Levina acha kunichekesha we mtoto..., Mbona kule nilipokushusha kwenye basi nilikuuliza swali kama hili na ukaniambia kweli umeua ila kwa bahati mbaya..?" "Mi mi...? Labda utakuwa ulisikia vibaya afande...." Nilijitahidi sana kujikaza na kubadilika lakini yule askari hakuridhika na majibu yangu,na kwa safari hii hakuwa mkali wa kunipiga bali nilimshangaa pia kwa kuongea na mimi ndipo akataka kuniambia ukweli sababu kubwa ya kunichukuwa na kunileta mpaka maeneo haya kituo cha polisi endapo tu nitamjibu maswali yake kikamilifu, huku tukiwa tumeliangalia lango la kuingia polisi... "Sitapenda nikuingize tena pale polisi najua utateseka sana mpaka uje kutoka tena mdogo wangu..,Ila kitu kimoja ninachotaka kuongea na wewe ni unipe jibu moja tu ili niweze kukusaidia.. "Huko ulipotoka umeua?" "Sijaua na naogopa sana kuua maishani mwangu..!" Nilimjibu mara ya pili lakini kwa sasa nilianza kuonesha kauoga,kwani nilianza kuingiwa na hofu huku nikitoka jasho jembamba mwilini mwangu na niliamini kabisa ntakuwa nategwa.. "Mimi nataka kukusaidia Levina lakini unakuwa mbishi si ndio..?" Alianza kubadilika yule afande huku akinikodolea mijicho na kunionesha ufunguo wa zile pingu kuwa kama nitakuwa mkweli atanifungua pingu kisha nitakuwa huru na salama,kitendo kile kikanifanya uzalendo uanze kunishinda na kujikuta namjibu anavyotaka.. "Ni kweli nimeua lakini si kwa kukusudia.." "Umeua..? ..Nani uliyemuua Levina?" "B...aa..a..a..b..a.. A...l..i.." Nilitaja jina kwa kujiuma uma pale pale yule afande akabadilika ghafla na kugeuza ile gari kisha safari ikaanza lakini sikuweza kujua ni wapi nilipokuwa napelekwa zaidi ya kushuhudia akitoka kwa mwendo wa kasi huku nikiwemo ndani ya lile gari lake... *************** * * * Levina anapelekwa wapi? * * * Je., ukweli gani aliokuwa nao yule afande...?

at 8:57 PM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top