Riwaya: SARAI SEHEMU YA KUMI(10) ***ilipoishia*** upande mwingine alionekana baba sarai akizipiga hatua za taratibu mpaka akafika nyumbani kwake alipoingia chimbani alistahajabu kulikuta begi lake akafungua zipu harakaharaka akatazama upande wa mdani ya begi aliziona pesa zake...""mmh!! inamaana jana sikuangalia vizuri au nilikuwa nimechanganyikiwa!!!!!?? baba sarai hakujali akafunga zipu ya begi nakuliweka uvunguni mwa kitanda mara ghafla alisikia mtu akigonga hodi.. ***Endelea*** alipofungua mlango alistahajabu kumuona mtu ambae hajawahi kumuona machoni mwake...mtu yule aliomba msaada wa chakula baba sarai alisema" inamaana umetoka huko ulipotoka ukazipitiliza nyumba zote ukaona hapa hotelini au?? aliongea maneno hayo ya kejeri kisha akamfukuza mtu yule"" nasema toka na usirudi hapa tena fukala wewe.... mtu yule aliondoka zake...baada ya dakika kadhaa kupita mtu yule aliyeomba msaada alionekana akitembea na kuingia porini kisha akabadilika...kumbe alikuwa ni sarai kule nymbani kwa baba sarai alionekana akiwa bafuni anaoga..alipomaliza alirudi chumbani kwake akavaa nguo na kuondoka zake...alikwenda mpaka MID HOTEL kilosa mjini alipofika aliagiza nyama ya mbuzi wa kuchoma na ugali....baada ya dakika tano kupita chakula kililetwa akala... alipomaliza akaagiza bia akaanza kunywa. alikunywa sana ilipofika majira ya saa mbili za usiku alihisi amelewa akakodi taxi impeleke nyumbani kwake...... *******BAADA YA MWEZI MMOJA KUPITA***** Pesa zilianza kuisha kwa sababu alikuwa akizitumia bila kuzifanyia mzunguko wa kuzizalisha.....hatimae aliamua kuuza yale mashamba aliyoyanunua..kabla hata hajaanza kulima.......alipopata pesa hizo alizitumia kwenye starehe....siku moja aliamua kuzihesabu pesa zilizobaki alistuka zilikuwa ni milioni moja pekee...baba sarai akaanza kuhisi kuchanganyikiwa......baada ya wiki moja kupita alikata tamaa ya kuendelea kuishi kilosa akaamua kuuza vitu vyake vyote akarudi jijini Dar es salaamu....mpaka anafika jijini alikuwa na shilingi milioni tatu......akaamua kupanga nyumba mbagala.......siku moja akiwa katika matembezi alikutana na mwanamke mmoja alipomtazama kwa makini alikuwa anafanan na marehemu mke wake......mwanamke yule alikuwa akifanya bihashara ya kutembeza mboga za majani kwenye beseni alilolibeba kichwani huku kabeba mtoto mdogo mgongoni....baba sarai aliamua kumfuata mama yule kisha akasema"" nahisi kama nakufahamu...yule mama alitabasamu kisha akasema""yawezekana kwa sababu mimi huwa natembeza mboga maeneo mbalimbali ..... baba sarai akauliza"mbona unatembea na mtoto mchanga kwenye jua kali kama hili???? yule mama alisita kwa sekunde kadhaa kisha akasema ni stori ndefu lakini kama hautojali nitakusimulia kwa kifupi. baba sarai alisema hakuna shida naomba unisimulie japo kidogo.... yile mama akaanza kusimulia. ******************* """"nilikuwa naishi na mume wangu kwa amani na furaha siku zote lakini baada ya kujifungua mtoto huyu unaemuona....mume wangu alinitelekeza mimi pamoja na mtoto huyu mchanga kwa sababu mtoto huyu ni mlemavu...nilimzaa akiwa hana mikono yote miwili.....tangu mume wangu kanitelekeza maisha yangu yakawa magumu sana ikabidi nianzishe bihashara ya kuuza matunda pamoja na karang...nilifanikiwa kupata pesa kiasi nikafungua duka...lakini wafanya bihashara wenzangu walinionea wivu wakaichoma nyumba yangu....hivi unavyoniona sina mbele wala nyuma nalala popote pale giza litakaponikutia....aaah lakini kama baba wa mtoto wangu akikumbuka na kulitambua kosa alilolifanya basi atubu kwa Mungu muumba atasamehewa...kisha mama yule akaanza kuzipiga hatua.. baba sarai alibaki mdo wazi...kumbukumbu ikamjia na yeye alishawahi kumtelekeza mama sarai miaka mingi iliyopita alafu matukio yaliyompata mama huyu mpaka lile tukio la kuchomewa nyumba lilifanana natukio la mama sarai...wakati baba sarai anataamaki alipoinua uso wake ili ampe pole mama yule hakumuona alipojarubu kuangazaangaza macho hakufanikiwa kuona mama yule kapitia njia gani wakati anajiuliza mara ghafla...aliguswa begani alipogeuka kumtazama aliyemgusa!!!baba sarai alistuka sana kumuona mtu huyo..alikuwa ni yule bosi wake aliyemfukuza kazi baada ya sarai kuiba kimiujiza zile myaraka ofisini kwa baba sarai.. ITAENDELEA....... Usikose kufatilia simulizi hii nzuri ya kusisimua ASANTENI.

at 1:19 PM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top