Sitaki tena – 06 Ilipoishia.., bado haikusaidia kumjua ni nani lakini ulikuwa ni mwili wa mtu pale chini ambao kwa namna moja au nyingine sikuweza kuutambua mara moja, kwa ushupavu wa halmashauri ya kichwa changu ikanituma nichukuwe panga na ku.. Endelea., Nichukuwe panga na kuchana kipande cha nguo yake,nikafanya hvyo kisha kile kitambaa nikakificha katika pindo la nguo yangu ya ndani halafu safari ikaendelea,nilikatiza msituni bila kuogopa kitu chochote na wala kumuogopa yeyote hatimaye baada ya kukimbia mda refu nikahisi kama kitu kigumu nakanyaga chini,furaha na amani vikaanza kutawala ndani ya moyo wangu kwani nilikuwa tayari nipo katika barabara ya lami,akili ikawa katika kukisia ni upande gani ndo utakuwa unaelekea Dar na upande gani utakuwa unarudi Mbeya,nikiwa bado natafakari likapita basi la kwanza,nikashindwa kulisimamisha nikaamua kusubiri gari nyingine,kwani sikuwa hata na nauli hvyo nikaamua nijifiche niweze kudandia gari lolote litakalopita kwa mwendo mdogo., Baada ya kukaa pale takribani lisaa moja na nusu bila ya kuona gari lolote hatimaye nikaliona gari kubwa likiwa linakuja kwa kujikongoja., "Kama kufa wacha nife tu.,lakini hili gari siliachi.." nilijisemea kimoyomoyo huku nikijiweka tayari kwa kurukia lile gari aina ya roli,huku mikuki na mishale pamoja na lile panga nikilitupia msituni,kitendo cha lile gari kufika karibu yangu kikawa kosa kubwa sana kwangu kwani ndani ya mda mchache nikawa tayari nipo nyuma ya lile lori lililokuwa limebeba mbao., Kwa ujasiri niliokuwa nao nikaingia mpaka mule ndani ya lile lori kwa nyuma ambapo sikumuona mtu yeyote kisha nikarudishia mlango na kujilaza kwenye zile mbao huku nikiwa sina uhakika na ninapoenda, "Sijui ndo litaishia morogoro au ndo la Iringa hili gari?" hayo ni kati ya maswali yaliyokuwa yameandama ndani ya kichwa changu,huku safari ikiendelea taratibu baada ya mwendo mrefu kidogo, ghafla gari likasimama kwa mbali nikahisi sauti ya watu wanajibizana kwa nje., "Hapana mkubwa mzigo wetu hauwezi kuzidi kiasi hicho" hapohapo jibu likanijia kuwa tutakuwa tumefika maeneo ya mizani, "Embu fungua nyuma tuhakikishe maana tani zimezidi na kama hutaki paki pale gari yako uandikiwe faini" Wakiwa bado wanabishana pale tayari kwenye gari nikawa natetemeka mwili mzima huku nywele zikinisimama na akili ikinituma nifungue mlango, nikisema nijifiche nyuma ya mbao siwezi kwani ni kweli kulikuwa na mbao nyingi kiasi kwamba nilipata kanafasi kadogo sana ka kujificha, "Mungu saidia.! Mungu saidia.! Saidia jamani.!" Ndio maneno niliyokuwa naomba nisiweze kukamatwa kwani nia yangu nikufika Dar, Mda si mrefu nikaskia mungurumo wa gari kuwashwa kuashiria safari inaendelea moyo wangu ukawa na furaha upya nikajihisi ni mtu tofauti sana duniani tena aliye na bahati mbaya kupelekwa gerezani lakini aliyejawa na bahati nzuri uraiani, Nikiwa sina hata lepe la usingizi huku safari ikiendelea niliweza kushuhudia tena kwa mara nyingine kuki kuchwa kwani mwanga ulikuwa umeshatoka kuashiria kuwa ni alfajiri,gari nalo likatembea ka mwendo kidogo kisha likasimama, sauti na makelele ya watu ndio yalichochea hisia zangu,niliweza kutoa jicho langu kupenyeza kwenye kauwazi ka mlango nikaweza kushuhudia watu mbali mbali,moja kwa moja nikapata wazo la kuangalia kile kipande cha nguo nilichokikata kule kwa yule mtu msituni alikuwa ni nani, Taaratibu mkono wangu ukaanza kupenyeza mpaka kwenye upindo wa nguo yangu ya ndani nikakichukuwa kile kitambaa na kukiangalia., "Mamaa..! mamaa..! nimeuwa tena mungu wangu..! Nisamehe Pendo..! Sijakusudia mimi..! Maaaaa aaaaaaah..!" Kumbe kile kilikuwa nikipande cha nguo cha rafiki yangu niliotokanaye gerezani 'Pendo'.. wakati nikiendelea kutoa sauti kali nikahisi kunawatu wamezisikia kelele zangu hivyo nikasikia mlango unafungulia eneo nililokuwa.., "Sauti inatokea humu ndani bwana, tena ni sauti ya kike." aliongea mmoja ya watu waliokuwa wanazungumza nje ya lile lori nililokuamo ndani., "Mtoeni.!, mtoeni.! Tena anasema ameua,embu mkamateni tumpeleke polisi.." Nilibaki nimezubaa huku nikiwa sijitambui kipi cha kufanya,nikawa natetemeka sana huku nikiishiwa na pumzi,nahisi mapigo ya moyo yalizidiwa kasi kwani nilijihisi napata joto ghafla huku kijasho chembamba kikiambatana na mchozi uliokuwa unanitoka mithili ya maji yakifata mkondo wake, sikuwa na jinsi tena kwani niliamini ndoto zangu za kuwa uraiani zimekwisha na sijui ntawaambia nini Gervas na mama yangu endapo watasikia nipo tena gerezani, Huku kojo likiwa linanimwagika, ukakamavu na ujasiri wote ukinitoka nilijikuta natoa tena sauti ya ukali., "Sio mimi..! Sio mimi..! Jamani msinikamate.." Huku nikinyosha mikono yangu miwili kuelekea ile sehemu niliyoamini ni mlango,taratibu nikaanza kufungua ili nijisalimishe ile namalizia kufungua tu tu nikawa tayari nipo mikononi mwa raia nisiowafahamu lakini walikuwa ni wanaume wamevalia sare ambazo sikuweza kuzitambua mara moja huku juu wakiwa na mashati meupe na wengine masweta mekundu kutokana na hali ya baridi kali lililokuwa limezunguka maeneo haya, Ilikuwa ni mchana tulivu kwani jua lilikuwa si kali sana kutokana na kaubaridi katika huu mji,wale wenye hasira wakaanza kunishambulia kwa kunipiga makofi huku wengine wakinishambulia kwa matusi makubwa ya nguoni huku wakiniburuza mithili ya mzoga aliyeoza anayeenda kutupwa,nilipiga kelele lakini haikusaidia nilivutwa sana na wale vijana.. "Wauaji kama nyinyi ndo tunaowatafuta" aliongea mmoja wa wale watu huku wakiwa wamenichania vipande vya nguo yangu, nilikuwa sina tena ujanja na pia kulikuwa hakuna tena muujiza utakaotendeka kwangu ili niweze kujikomboa katika mikono ya wale watu nisiowafahamu walioonekana makatili wasio na huruma hata kidogo., Waliniburuta kwa mwendo mrefu sana,huku umati wa watu ukifurika kunishuhudia, walipokezana kunishika na kunivuta,huku nikiwa bado nalia na kung'ang'ania nisiweze kupelekwa kituoni, Nikiwa naendelea kulia huku nguvu zikiniishia na kuacha wafanye wanachokitaka,nikahisi pumzi zimeniisha kwani kwa sasa nilikuwa nahema juu juu huku damu zikinimwagika pembezoni mwa mdomo wangu, maji machafu pamoja na matope vilitawala mwilini mwangu huku sura ikiwa imenivimba sana, niliamini hata nikiendelea kulia haitasaidia chochote,na pale malengo yangu yalikuwa yamefikia tamati kwani nilikuwa nikipelekwa polisi, Tukiwa njiani mwa safari huku kipigo kikinizidia katika mwili wangu huku macho yangu yakiangaza huku na kule kupata japo msaada wowote ndipo yakakutana uso kwa uso na kibao kilichoandikwa, 'TOSAMAGANGA HIGH SCHOOL' Halmashauri ya kichwa changu ikafanya kazi fasta hapo hapo nakugundua kuwa wale si raia wakawaida kama nilivyodhani bali walikuwa ni wanafunzi katika kile kijiji tena katika shule anayosoma Gervas japokuwa sikumuona katika wale watu waliokuwa wakinipiga lakini niliamini lazima alikuwa akisoma katika shule ile kama alivyonielezea hapo awali kwamba anasoma shule ya wavulana tupu iliopo Iringa na inaitwa 'Tosamaganga' hayo yote aliniambia kipindi kile nipo gerezani, "kabla hamjanifikisha huko kituoni naomba mniitie Gervas Phota nimuage" Niliposema hivyo tu wale jamaa waliokuwa wamenishikilia wakaniacha ghafla kwa mshangao huku wengine wakiamini huenda nilikuwa nimejifanyisha nimeua ili niweze kuonana na Gervas na wengine wakijiuliza nimemjuaje Gervas? Wakanikazia macho, "Gervas.? Mbona sisi hatumjui" Walinijibu huku wengine wakinicheka na kunisonya kwa dharau, "We dada una mashetani au kichaa enhh.. Unamuitaji nani?" jibu alilonipa mmoja wa wale watu lilinifanya niingiwe na woga huku meno yakiumana nakuhisi labda Gervas alinidanganya anasoma shule hii lakini haiwezekani., Hasira zilizidi kunipanda kwani kipigo kiliongezeka mara mbili ya pale huku damu nyingi zikiendelea kunimwagika, ghafla nikasikia kama mlio wakengele ukipigwa pembeni ya shule huku watu waliokuwa wamevalia kofia wakiwa wako na virungu mikononi wakinifuata pale nilipokuwa nimeburuzwa na wale wanafunzi,hofu ilizidi kutanda kwenye ubongo wangu,mwili ulininyong'onyea kuona wale watu wamevalia sare kama polisi, kila walipokaribia lile eneo ndipo nilitamani nife hapohapo,nikiwa nagala gala pale chini huku wale wanafunzi wakianza kutawanyika kwa kuwaogopa wale watu huku wakiniacha peke yangu nilianza kujisogeza kwa mwendo wa taratibu huku nikitumia magoti na makalio yangu kujisogeza mpaka nikaona chupa ya soda,nikaivunja ili niweze kujiua kabla ya wale askari hawajanifikia, nikiwa nataka kuanza zoezi la kujiua mara yule askari akawa ameshanikaribia na kunipokonya ile chupa., "niache nife..,niacheni jamani..! Nikiwa nimeshakata tamaa tena ya kuishi,kwa haraka nikaweza kuyakodoa macho yangu na kumuangalia mtu aliyenipora ile chupa niliyokuwa nimeivunja vunja na kuacha ncha kali nikitaka kujiua,nikaangalia mara mbili mbili nikagundua kuwa yule hakuwa askari polisi kama nilivyodhani bali alikuwa ni mmoja kati ya wale walinzi wa ile shule waliokuja kutawanya na kuwakamata wanafunzi sugu waliokuwa nje ya shule mda wa masomo, "Pole sana binti angalia sana siku nyingine watakuja kukubaka wale wanafunzi wavuta bangi wale...!" nilishangaa sana yule mlinzi kunipora kisha akaniacha na kuendelea kuwafukuza wanafunzi wengine,nilijawa na nguvu na furaha ya ajabu nakujiona ni mtu wa bahati tena ya mtende, watu wengi walinishangaa sana hilo sikujali kwani maisha ya kupigwa kama yale nilishayazoea tangu kipindi kile nipo Gerezani. Huku nikiwa nimelowa damu na kuchanika karibu nguo yote nliokuwa nimeivaa, nliweza kujikokota chini chini mpaka eneo la nyuma na ile shule kisha nikaegemea chini ya mti mkubwa, kwa uchovu na maumivu niliyoyapata yalinifanya nianze kunyemelewa na kausingizi japokuwa kulikuwa na baridi kali sikuwa na jinsi yoyote yakukabiliana nalo, "Twende bwana au unapenda kubaki hapa porini..? Mi nakuacha...Hapana., Pendo usiniache..! Pendo usiniache...! Usiniache..! Usiniache...! Usiniache..! Peeeendooooooooo.......!" Ghafla nikashtuka nakuanza kuhema kwa kasi huku nikitetemeka Levina mimi kumbe ilikuwa ni ndoto tena nilikuwa nikiota nipo na marehem pendo kule msituni,usingizi ukanikata nakuanza kuangaza kila upande nakuona giza limeanza kutanda lakini upande wa mbele yangu kulikuwa na taa kali zilizomulika ile shule, nikaanza kusogelea taratibu kwa kuzunguka yale majengo yaliokuwa yamewekewa uzio huku nikitafuta lango la kuingilia, hatimaye nikagundua geti lilipo,walinzi takriban watatu walikuwa wametanda pale lango la kuingilia hivyo nikatafuta eneo la choo kwani niliamini kukijua choo itakuwa ni njia nyepesi ya kuingia ndani ya ile shule, haraka haraka macho yangu yakaweza kuona wanafunzi wakiongozana wakiingia kwenye jengo lingine lililoonekana si kubwa sana kama majengo mengine huku wakiingia na kutoka, haraka haraka kwa ujasiri na kwa shauku niliokuwa nayo ya kutaka kupambana mpaka nimuone Gervas nikawa na nguvu ya ajabu yakuweza kuruka ukuta japokuwa haukuwa mrefu sana ndani ya dakika chache nilikuwa tayari nipo kwenye kale kajengo kalichokuwa na vyoo vingi vyote vikiwa na milango nikaingia choo kimojawapo na kujifungia huku nikishuhudia hamna mtu ndani, harufu kali ya kinyesi na mikojo katika vile vyoo nilipokuwamo ndani havikunizuia hata kidogo kuondoka mule ndani,niliweza kutulia kimya huku nikiombea aje kati ya Gervas au mwanafunzi yeyote nimuulizie Gervas, mpaka nikajishangaa kwa jinsi nilivyokuwa sina woga wowote, Ghafla nikasikia sauti ya kama mtu anakuja,nikazidi kukaa kimya ndani ya choo huku nikijiuliza ntaanzaje mara ile sauti ya mtu akiingia na kuanza kukojoa mlango wa pembeni yangu, nikafungua mlango wangu taratibu na kuanza kunyata kuelekea mlango aliokuwepo huku akili ikinituma nimuwahi na kumnyamazisha kabla hajashtuka na kuanza kupiga kelele, " Shhh..usiniogope wala usikimbie..Naitwa Levina natokea..." Kabla sijamaliza kujitambulisha yule mwanafunzi akawa ameshanitambua.. " We si yule dada ambaye nimetoka kuskia stori yako sa hivi kwa wenzangu kuwa umepigwa na kukuburuzwa mchana kutwa pale nje na umeokolewa na walinzi..?" "Ndio mimi ila nipo hapa kwa msaada mmoja tu, unamfahamu Gervas Phota..?" "Namfahamu na ninasoma naye lakini yupo Chumbani anaumwa leo siku ya pili yupo kitandani.." "Tafadhali nisaidie kwa hili nenda kaniitie mwambie Levina, nipo hapa hapa chooni kwenye mlango huu nawasubiria mtanikuta.." Ndani ya mda mfupi nikawa tayari nimeshayazoea mazingira ya kile choo ikiwa ni pamoja na harufu kali ya mule ndani, niliweza kujifungia mlango mmojawapo kwa mda mrefu tangu nimefika bila ya hata mtu yoyote kujua, mara nikasikia sauti ya watu wanaongea kwa nje huku sauti kama niliyokuwa naifahamu nilianza kuingiwa na furaha na amani isiyokuwa na kifani kwani niliamini Gervas ndiye mkombozi wangu na anayepajua mpaka nyumbani kwetu kwani nilikuwa nimeshapasahau hadi jina la mtaa,sikutaka kujitokeza hvyo nikavuta subira huku nikiisikia ile sauti kwa umakini taaratibu nikaweza kuitambua kuwa haikuwa sauti ninayoifahamu hata kidogo na hata maongezi waliokuwa wanaongelea hayakuwa yakiunafunzi hivyo halmashauri ya kichwa changu ikapambanua fasta na kujua kuwa wale watakuwa ni walinzi kwani walikuwa wanaongelea mambo ya kifamilia na kikazi tena kazi ya ulinzi, moyo ulianza kuniripuka kwani walikaa mda mrefu huku wakipiga story na hata wanafunzi walipokuja nilisikia wakiwaamkia na kujisaidia na kuondoka zao,kwa ujumla nililegea sana na akili ilishaanza kuchoka,nikiwa bado nipo nao wale walinzi chooni huku wakinogewa na stori ila mlango nilikuwa nao tofauti bila ya wao kujua ghafla nikasikia sauti kali iliyotokea upande wa nje huku ikilitaja jina langu., "LEVINAAAA...! LEVINAAA...! LEVINAAA...! " YUPO MLANGU UPI UMESEMA..?" Nilitamani niweze kutoka lakini haikuwezekana kutokana na wale walinzi kukaa mda mrefu wakipiga stori, hakika ile sauti ilikuwa ni ya Gervas akiongea na mwenzake huku nikihisi ameshakaribia kuingia mule chooni,ghafla nikasikia ukimya umetanda halafu yakafuatia maswali kutoka kwa wale walinzi wakimuuliza Gervas, "Levina..! Levina ndo nani? Na mbona mwenzako amenyoosha kidole mlango huo ambao umefungwa..? Kuna nani...?" ************************* *** Je? Ndoto za Levina kumpata Gervas zitatimia? *** Itakuwaje akikamatwa wakati ile ni shule ya Wavulana tupu? Inaendelea

at 8:56 PM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top