Sitaki tena – 05 Ilipoishia., "jamani..! jamani..! jamani..! Nisaidieni nakufaa..! nakufaa..!" Nikiwa bado nalia pale ghafla.. Endelea., Ghafla nikamulikwa mwanga mkubwa nikaangaza huku na huku nikaweza kuwaona watu wakiwa wamenizunguka.. "Wewe ni nani.? Na unafanya nini hapa?" aliongea mmoja wa watu wale waliokuja pale nilipokuwa baada ya kupiga makelele kwa kuona mnyama akinifuata kumbe hakuwa mnyama wa kunidhulu bali alikuwa ni ng'ombe aliyechelewa kuingizwa bandani na katika lile eneo walikuwapo wanaishi watu., "Naitwa Levina nimetokea mbeya ila gari yetu ilipata ajali tukawa tumevamiwa na majambazi hivyo nikaamua nikimbilie huku msituni..kwani hapa ni wapi?" niliwajibu hapo hapo huku nikishusha pumzi na kuwauliza swali bila hata ya kuonyesha woga wa aina yoyote, "Hapa ni kijiji cha LIAMKENA tupo katikati na hili pori la msitu wa Ruaha., Haya mbebeni tumpeleke nyumbani na wewe John swaga huyo ng'ombe turudini nyumbani" aliamrisha mmoja wao kwa sauti ya juu., Safari ya kutoka katika ule msitu mpaka kuingia katika kijiji cha 'Liamkena' usiku wa manane ilifanikiwa kwani nilipofika tu wakaanza kunitibia kidonda changu kwa kutumia dawa za kienyeji huku wanakijiji wengine kutoka katika kijiji kile wakija kunishangaa si kwakuwa nilikuwa natisha bali walistaajabu kuokotwa usiku wa manane kwenye ule msitu ulioaminika kuwa na wanyama wakali tena wengi, Ndani ya siku mbili nikawa tayari nimeshazoea mazingira uku akili yangu nashauku kubwa nikiielekezea nyumbani na jinsi gani ntampata Gervas na kumshukuru kwa yote aliyonitendea., Hali ya kidonda changu haikuwa mbaya kwani kilianza kufunga taratibu, ila wanakijiji walipenda niendelee kubaki mpaka nipone kabisa jambo ambalo lilipingana na halmashauri ya kichwa changu, Ilipofika saa tano usiku huku kijiji chote kikiwa kimerindima kwa giza nene,sikuwa na hata chembe ya usingizi, jicho langu liliweza kupenyeza kupitia katundu kadogo kadirisha kalichokuwa kametengenezwa kwa kutumia miti, niliweza kujua mara moja sehemu ya kutokea hivyo nikachana kipande cha gauni langu na kukifunga katika eneo lakidonda changu kisha nikachukuwa mishale na upinde huku upande wa kulia kwangu nikashikilia panga tayari kwa kuingia tena msituni huku nikitafuta barabara ya kutokea,nilifanikiwa kutoroka na kuingia msituni,akili yangu na mwili wangu vikawa kama vimeshapigwa ganzi kwani sikuwa muoga hata kidogo,nilitembea taratibu lakini nikaona kama nachelewa hivyo nikaanza kukimbia wakati nakimbia niliweza kusikia kama kuna watu wananikimbiza nyuma yangu kama sivyo basi ntakuwa nimeingia katika ulimwengu wa wanyama pori tena wale wakali nikasimama na kujificha nyuma ya mti kisha taratibu nikachomoa mshale japo nilikuwa sijui kuutumia lakini niliweza kuuelekezea upande wa ile sehemu niliyotoka na kuhisi kile kitu kitakuwa kinatokea upande huo, Niliunyosha na kufanikiwa kuuachia,nikasikia sauti ya kike.. "Nakufaa mama niokoe.. Ooh.! Uuh.! Uuh.!" ghafla ikafuatia mshindo kuashiria kile kitu kimeanguka chini baada ya kuachia mshale wangu wenye sumu kali, bila kuwa na woga kwa kunyemelea nikaanza kufata lile eneo kumtambua yule mtu, huku nikikaribia pale nimeshika panga langu akatokea fisi maeneo ya karibu nikamfyeka akawa amekufa,nikaendelea na zoezi langu la kutambua ni kitu gani kitakuwa mbele yangu, sikuwa na tochi,ila nilipoukaribia ule mwili niliupapasa lakini bado haikusaidia kumjua ni nani lakini ulikuwa ni mwili wa mtu pale chini ambao kwa namna moja au nyingine sikuweza kuutambua mara moja, kwa ushupavu wa halmashauri ya kichwa changu ikanituma nichukuwe panga na ku Nichukuwe panga na kuchana kipande cha nguo yake,nikafanya hvyo kisha kile kitambaa nikakificha katika pindo la nguo yangu ya ndani halafu safari ikaendelea,nilikatiza msituni bila kuogopa kitu chochote na wala kumuogopa yeyote hatimaye baada ya kukimbia mda refu nikahisi kama kitu kigumu nakanyaga chini,furaha na amani vikaanza kutawala ndani ya moyo wangu kwani nilikuwa tayari nipo katika barabara ya lami,akili ikawa katika kukisia ni upande gani ndo utakuwa unaelekea Dar na upande gani utakuwa unarudi Mbeya,nikiwa bado natafakari likapita basi la kwanza,nikashindwa kulisimamisha nikaamua kusubiri gari nyingine,kwani sikuwa hata na nauli hvyo nikaamua nijifiche niweze kudandia gari lolote litakalopita kwa mwendo mdogo., Baada ya kukaa pale takribani lisaa moja na nusu bila ya kuona gari lolote hatimaye nikaliona gari kubwa likiwa linakuja kwa kujikongoja., "Kama kufa wacha nife tu.,lakini hili gari siliachi.." nilijisemea kimoyomoyo huku nikijiweka tayari kwa kurukia lile gari aina ya roli,huku mikuki na mishale pamoja na lile panga nikilitupia msituni,kitendo cha lile gari kufika karibu yangu kikawa kosa kubwa sana kwangu kwani ndani ya mda mchache nikawa tayari nipo nyuma ya lile lori lililokuwa limebeba mbao., Kwa ujasiri niliokuwa nao nikaingia mpaka mule ndani ya lile lori kwa nyuma ambapo sikumuona mtu yeyote kisha nikarudishia mlango na kujilaza kwenye zile mbao huku nikiwa sina uhakika na ninapoenda, "Sijui ndo litaishia morogoro au ndo la Iringa hili gari?" hayo ni kati ya maswali yaliyokuwa yameandama ndani ya kichwa changu,huku safari ikiendelea taratibu baada ya mwendo mrefu kidogo, ghafla gari likasimama kwa mbali nikahisi sauti ya watu wanajibizana kwa nje., "Hapana mkubwa mzigo wetu hauwezi kuzidi kiasi hicho" hapohapo jibu likanijia kuwa tutakuwa tumefika maeneo ya mizani, "Embu fungua nyuma tuhakikishe maana tani zimezidi na kama hutaki paki pale gari yako uandikiwe faini" Wakiwa bado wanabishana pale tayari kwenye gari nikawa natetemeka mwili mzima huku nywele zikinisimama na akili ikinituma nifungue mlango, nikisema nijifiche nyuma ya mbao siwezi kwani ni kweli kulikuwa na mbao nyingi kiasi kwamba nilipata kanafasi kadogo sana ka kujificha, "Mungu saidia.! Mungu saidia.! Saidia jamani.!" Ndio maneno niliyokuwa naomba nisiweze kukamatwa kwani nia yangu nikufika Dar, Mda si mrefu nikaskia mungurumo wa gari kuwashwa kuashiria safari inaendelea moyo wangu ukawa na furaha upya nikajihisi ni mtu tofauti sana duniani tena aliye na bahati mbaya kupelekwa gerezani lakini aliyejawa na bahati nzuri uraiani, Nikiwa sina hata lepe la usingizi huku safari ikiendelea niliweza kushuhudia tena kwa mara nyingine kuki kuchwa kwani mwanga ulikuwa umeshatoka kuashiria kuwa ni alfajiri,gari nalo likatembea ka mwendo kidogo kisha likasimama, sauti na makelele ya watu ndio yalichochea hisia zangu,niliweza kutoa jicho langu kupenyeza kwenye kauwazi ka mlango nikaweza kushuhudia watu mbali mbali,moja kwa moja nikapata wazo la kuangalia kile kipande cha nguo nilichokikata kule kwa yule mtu msituni alikuwa ni nani, Taaratibu mkono wangu ukaanza kupenyeza mpaka kwenye upindo wa nguo yangu ya ndani nikakichukuwa kile kitambaa na kukiangalia., "Mamaa..! mamaa..! nimeuwa tena mungu wangu..! Nisamehe Pendo..! Sijakusudia mimi..! Maaaaa aaaaaaah..!" Kumbe kile kilikuwa nikipande cha nguo cha rafiki yangu niliotokanaye gerezani 'Pendo'.. wakati nikiendelea kutoa sauti kali nikahisi kunawatu wamezisikia kelele zangu hivyo nikasikia mlango unafungulia eneo nililokuwa.., "Sauti inatokea humu ndani bwana, tena ni sauti ya kike." aliongea mmoja ya watu waliokuwa wanazungumza nje ya lile lori nililokuamo ndani., "Mtoeni.!, mtoeni.! Tena anasema ameua,embu mkamateni tumpeleke polisi.." Nilibaki nimezubaa huku nikiwa sijitambui kipi cha kufanya,nikawa natetemeka sana huku nikiishiwa na pumzi,nahisi mapigo ya moyo yalizidiwa kasi kwani nilijihisi napata joto ghafla huku kijasho chembamba kikiambatana na mchozi uliokuwa unanitoka mithili ya maji yakifata mkondo wake, sikuwa na jinsi tena kwani niliamini ndoto zangu za kuwa uraiani zimekwisha na sijui ntawaambia nini Gervas na mama yangu endapo watasikia nipo tena gerezani, Huku kojo likiwa linanimwagika, ukakamavu na ujasiri wote ukinitoka nilijikuta natoa tena sauti ya ukali., "Sio mimi..! Sio mimi..! Jamani msinikamate.." Huku nikinyosha mikono yangu miwili kuelekea ile sehemu niliyoamini ni mlango,taratibu nikaanza kufungua ili nijisalimishe ile namalizia kufungua tu.. Itaendelea

at 8:55 PM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top