Sitaki tena –04 Nilijikuta nachukua kile kikaratasi na kumpatia afande Jesca nikiamini kuwa hajui kusoma kwani huwa mara nyingi akitumiwa ujumbe kwenye simu yake huwa ananitafuta nimsomee.. Alikichukuwa kile kikaratasi akakigeuza geuza kisha akanirudishia.. "Acha upuuzi wako nenda kwa wenzako sawa?" "Sawa" nilimuitikia lakini kishingo upande huku akili yangu ikinituma nielekee chooni nikakimalizie kukisoma,taratibu nikaongoza hadi chooni nikakifungua kwenye gauni kilipokuwa na kumalizia kukisoma, enhe ikawaje vilee., "lakini msamaha wenyewe utalenga wale wenye ulemavu nilichokifanya ni kutoa ada yangu yote niliyotumiwa shilingi laki mbili na kuwaonga polisi kisha wakalipitisha jina lako kwenye orodha ya watakao kuwa huru" Hapohapo nikakichukuwa Kile kijikaratasi na kukichana chana kisha nikakitupia katika tundu la choo,nikitoka na furaha ya hali ya juu huku nikijiona mshindi, BAADA YA WIKI MOJA Ikiwa ni asubuhi na mapema tukiwa tumejipanga mstari halmashauri ya kichwa changu kikawa kimeshafanya kazi nakutambua ni kitu gani kilituleta katika eneo lile., Kama kawaida ya afande kimbele mbele afande Jesca alikuwa tayar akiwanyosha watu mistari huku akiwapiga na kuwafokea wale waliojifanya ni wabishi, Tayari maafande takribani nane walikuwa mbele yetu huku mkuu wa gereza akiwa kashikilia karatasi bila kuchelewesha mda akaongea kilichotuleta eneo lile na kuanza kutuita majina naweza kusema sikuamini kilichotokea kuwa kama ndoto kwani ni kweli na mimi nilikuwa katika ile orodha ya walioachwa huru, "nashndwa kujua nimfanyie nini huyu kaka 'Gervas'.. Gervas...! Gervas...! Nakupenda na Nitazidi kupenda daima" nilijisemea kimoyomoyo huku nikipiga ishara ya msalaba na kukusanyika na wenzangu huku tukitokea lango kuu, **** Gari aina ya Land Rover yenye namba T643 ABK iliyokuwa imebeba magunia ya mpunga kutoka Tunduma kuelekea Dar es salaam huku ikiwa imepakiza abiria wa nne tu,wawili wa kiume na wawili wa kike.. nikiwamo katika hilo gari kwa mwendo wa taratibu huku nikiwa na mawazo mengi yalionijaa akilini mwangu ikiwa ni pamoja na hofu juu ya safari kama tutafika salama, mda huo ilikuwa imeshatimia saa 2 usiku,tulikuwa tunakaribia kufika Iringa., mawazo gongana yaliniandama ndani ya kichwa changu hasa kwa kuzingatia kuwa bado nilikuwa sijajiamini kwa kile kilichonitokea kama kweli niko huru ama la.! Huku nikiendelea kuwa katika dimbwi la mawazo usingizi ukanipitia. "Lete Jeki fasta...waambie na hao wadada washuke huko..!" sauti ya dereva wa ile gari akiongea na mwenzake ndiyo ilinishtua sana kwani gari lilikuwa limeharibika kilomita chache kabla hatujaingia Iringa.. Baridi lilikuwa kali sana,nilihisi kama mwili umeganda sikuwa na nguo yoyote ya kubadilisha,hivyo sikuwa na jinsi zaidi ya kujilaza pembeni ya lile gari huku nikitetemeka mdomo na meno yakiumana kama nimepigwa ganzi.. Nikiwa pale chini natafuta tena usingizi huku dereva akiendelea kutengeneza lile gari., kwa mbaaali niliona mwanga mkubwa ukitumulika huku unasogea taaratibu, akili yangu na wale wenzangu haikuwa mbali kwani lilikuwa ni gari lakini ilipofika karibu yetu dereva wetu akawa ameipungia mkono isimame kwa ajili ya kuomba spana.. ilisimama kisha wakashuka wanaume watano waliokuwa wamevalia makoti meusi huku mikononi wameshika panga na bunduki wakitufuata eneo tulilokuwa.. "Wote mikono juu" Na ole wake mtu asimame au aongee hata neno moja.." aliongea mmoja wa wale wanaume aliekuwa anasura ya kikomavu iliyojikunja kunja mithili ya mchekeshaji wanaomwita 'King'wendu', huku kavalia miwani meusi na mdomoni akivuta sigara na kutupulizia moshi..tukiwa bado tupo pale chini tukitetemeka na kuogopa pia tulikuwa kama tumeshajitolea kwa lolote litakalotupata.. Ghafla milio ya risasi ikaanza kurindima kuelekea kwenye matairi ya lile gari letu yakapasuka yote manne kisha wakamchukuwa dereva na wenzake wakawachinja mbele ya macho yangu kisha wakaondoka na kuniacha na mwenzangu niliyetokanaye gerezan, Roho ya Ujasiri,ukatili na ukakamavu niliokuwa nayo toka nipo kifungoni ilinisaidia sana kwani sikuogopa hata kidogo kilichonitokea mda mfupi uliopita nilimchukuwa mwenzangu na kutokomea naye msituni.. Nikiwa nimemshika mkono mwenzangu Pendo tulikuwa tayari tumeingia msitu wa Ruaha ambao kiukweli ulikuwa ni mkubwa sana na uliojaa na miti mirefu,hatukuweza kuogopa kitu kwani maisha ya gerezani yalikuwa tosha kwa mimi na Pendo kuwa wajasiri,wakatili na wakakamavu mda wote, "Nimechoka.,nimechoka siwezi kuendelea tena Pendo..tupumzike hapa.." Nilimwambia pendo huku nahema nikitokwa jasho usoni kwa mwendo tuliokuwa tunatembea haraka haraka hakika ulikuwa ni mwendo mrefu sana., "Sasa ukiendelea kudeka deka mi nakuacha, au unapenda kubakia hapa porini?" alisema Pendo kwa ukali kudhihirisha kuwa alikua amechoshwa na kitendo cha mimi kupumzika.,Nilijikaza na kuinuka tayari kwa kuendelea na safari lakini.. "Pendo.! Pendo.! Mama yangu wee mguu wangu..! Nilijikuta namuita Pendo asiondoke kwani mguu wangu kwa upande wa nyuma ulikuwa umeshachanika na damu nyingi zilikuwa zikinitiririka., Pendo hakuwa na jinsi kwani aliona kubaki na mimi katika ule msitu kungemchelewesha kufika kwao kwani safari yake ilikuwa inaishia Dodoma., "Pendo..! pendo..! Usiniache pendo..! ntabaki na nani tena Pendo..!" aliniacha nikiwa katika hali mbaya huku machozi yakinitoka,na kukata tamaa,nakuona bora ningemsubiri Gervas aje kunichukuwa.,ulikuwa tayari ni usiku sana nahisi ilikuwa imetimia kwenye saa nane au tisa kwani giza tororo ndilo lilitawala sana, Nikiwa bado katika dimbwi la mawazo na hasira nyingi pale chini huku milio ya wanyama wakali ikipaza huku na kule, Ghafla nikaanza kusikia mshindo wa kitu kama kinakuja tena kwa kasi ya ajabu, kadri mlio ulivyokuwa unazidi kuwa mkubwa mapigo yangu ya moyo yalizidi kunipelekesha.nilihema mpaka nikajihisi nimeishiwa pumzi sikuwa na lakufanya zaidi ya kujitoa kwa lolote litakalonipata kutokana na mguu kuumia vibaya kutokana na kujiumiza na kipande cha bati kwenye gari wakati tunakimbia kujiepusha na yale majambazi waliotuteka kulee.. Hatimaye nikaanza kutambua kitu kilichokuwa kinakuja kwani mwanzoni nilijua labda atakuwa Pendo amerudi kuja kunichukuwa lakini haikuwa hivyo kwani alikuwa mnyama mkubwa mweusi aliyefanania na nyati ila alikuwa akija kwa mwendo wa taratibu huku akinifuata katika eneo nililokuwa nimekaa..mwili ulinitetemeka sana hofu kubwa ilitanda ndan ya kichwa changu,nilitetemeka sana huku mchozi ukiwa unanitoka ukiambatana na mkojo kwa kasi,maumivu ya ule mguu yakatoweka kutokana na kile kilichokuwa mbele yangu.. "jamani..! jamani..! jamani..! Nisaidieni nakufaa..! nakufaa..!" Nikiwa bado nalia pale ghafla.. INAENDELEA...

at 8:54 PM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top