Sitaki tena – 03 BAADA YA MIAKA 5 Vurugu zilizokuwa zinaendelea katika Gereza la kufungwa watoto watukutu lililopo mbeya, Ndizo zilizosababisha watoto wengi kupoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa maisha kutokana na mgomo waliokuwa wameuanzisha kutokana nakupewa chakula kidogo sana tena kichafu,milipuko ya magonjwa kama kipindupindu,msongamano wa wafungwa kiasi cha wengine kufariki kwa kukosa hewa wakati wa kulala usiku.. Namba CG.016/007369, ndiyo namba iliyokuwa inasomeka katika sare yangu ya Gerezani ., Tayari maisha nlikuwa nimeshayazoea mule gerezani,taarifa kutoka nyumbani nilikuwa nikiletewa na afande mmoja ambaye tayari nilimzoea na hata kuanzia siku ile nilipo hukumiwa pale mahakaman hali ya baba yangu kiafya haikuwa nzuri na hakukaa mda mrefu akawa amepoteza maisha, Mwenyezi mungu amlaze pahala pema peponi.. Na sasa mama ndio mzazi wangu pekee aliyebaki hata kama nitatoka gerezani... ucheshi, ufanyaji kazi kwa nguvu,bidii na kujituma zaidi ndicho kitu kilichokuwa kikiwavutia maaskari wengi pale kiasi kwamba nikapendwa sana na kuaminika.. "Levinaaa... Levinaaa.. ...Wewe Levina Christian?.. Aliniita askari wa zamu lakini sikuweza kumsikia vizuri kwa sababu ya makelele ya wenzangu waliokuwa wakipigana mule ndani.. "Abeee afande..nilimuitikia" "Embu fanya haraka kuna mgeni wako kaja kukutembelea fanya ukamuone.." "Sawa afande..." Mapigo ya moyo yalikuwa yakinienda mbio,lakini halmashauri ya kichwa changu iliweza kupambanua haraka haraka na kujua atakuwa ni mama tu... "Lakiiini...mbona afande hakuniambia kama ni mama au la! Maana mama yangu anamjua angeniambia tu?" ndio maswali niliokuwa najiuliza nikiwa njiani kuelekea chumba cha wageni.. Ghafla... "Sasa mbona simuoni mgeni wangu?.." nilijikuta namgeukia yule afande aliyekuja kuniita na kuniambia kuwa nina mgeni.. "Umeanza kisilani chako enhee..? Au unataka ukalime heka tatu peke yako sa hivi...? " enhee..! Nikabaki kimya huku nikiendelea kumtolea macho ya ukali yule askari ambaye alikuwa anajulikana 'Jesca Tester' kutokana na kuwa mkorofi kwa wafungwa wabishi hata kipindi kingine huwa anakorofishana na maaskari wenzake.. "Si naongea na wewe kinyamkera...? Haya na huyu hapa ni mgeni wa nani sasa..?" Nikajinyamazia kimya huku nikikaa katika kajidirisha cha kuongea na wageni..nikimuacha yule askari akiendelea kubwabwaja pale.. "Na Nakupa dakika kumi tu uwe umeshamalizana naye na upotee hapa,sawa..?" "Sawa mkuu nimekuelewa..!" nilimjibu kwa heshima huku nikianza mazungumzo na yule mgeni wangu pale.. GERVAS; Sijui umeshanikumbuka..?" LEVINA; Hapana.. GERVAS; "Naitwa Gervas Phota..Tumeishi wote kurasini na kuchez..." kabla hajamalizia kuongea tayari akili yangu ilishaweza kuchambua fasta na kumjua.. LEVINA; we si mtoto wa mzee Phota pale jirani na nyumbani kwetu.? GERVAS; Haswaaa..! Ndiye mimi kumbuka tulikuwa wadogo sana lakini kwa bahati mbaya sikuweza kuwepo kuanzia siku ya tukio,kipindi cha kesi yako mpaka leo kwa sababu nilipelekwa shule mapema mno.. LEVINA; Usijali Gervas yote hayo nimaisha namshukuru mwenyez mungu mpaka nilipofikia hapa kwani nimebakiza miaka sita tu niwe huru.. "Mda umekwisha..haya we Levina inuke uwafate wenzako shambani..inuka" aliongea yule askari Jesca ambaye mda wote alikuwa akitusimamia.. Haraka haraka nilimuona Gervas akitoa kijimfuko kilichoashiria kina nguo.,kisha akatoa noti ya shilingi elfu kumi akanipatia kisha yule askari akampa shilingi elfu tatu kisha akaniaga na kuniahidi kuwa atakuwa akinitembelea mara kwa mara... Siku hiyo sikuweza kupata hata lepe la usingizi kwani nilijihisi tayari nipo nyumbani kwa zile nguo nilizoletewa na Gervas nilijikuta machozi yakinitoka japokuwa yalikuwa ni machozi ya furaha, Ikawa haipiti mwezi lazima Gervas aje kunitembelea na kuniachia japo chochote, hivyo nikaamini kuwa mtetezi wa maisha yangu ni Gervas na mama yangu pekee japo tangu nilipoletwa huku gerezan hajawah kuniona,moyo wa upendo taaratibu ulianza kunijia kwani hakukuwa na mtu aliyejionesha kunijali kama Gervas.. BAADA YA MIAKA 2 Nakumbuka siku hiyo Gervas alikuja kunitembelea lakini safari hii alionekana kuwa tofauti na siku nyingine kwani alikuja na furaha ambayo sikuitegemea na hakuweza kukaa sana ila akachukuwa mkono wake wakati ananiaga alipoachia nilihisi itakuwa kama kawaida yake ya kuniachia pesa lakini haikuwa pesa ila ilikuwa ni kijikaratasi kilichokuwa na ujumbe.. Niliagana na Gervas kisha nikaenda kutafuta eneo lililokuwa tulivu,taaratibu nikaanza kufungua ile karatasi ghafla moyo ukanilipuka, "Mpendwa Levina,natumai u mzima afya kwani mara nyingi huwa tunaonana., Nashukuru mwenyezi mungu mpaka hapa tulipofikia kwani umenifanya nijue mengi yanayotendeka humu ndani kwa kifupi nimejuana na kuzooena na maaskari wengi hapa, Levina mim na wew tumetoka mbali na sitapenda nikuache uendelee kuteseka hapo gerezani, Mwezi huu Rais atatoa msamaha ikiwa ni pamoja na gereza lenu lakini msamaha wenyewe utalenga wale wenye ulemavu nilichokifanya ni.. Kabla sijamalizia kusoma alitokea afande Jesca Tester na kunifokea.. "Hivi wewe Levina mda wote umekaa hapo umewakimbia wenzako kule,unafanya nini?" "Nika kaa kimya".. aliendelea kuongea afande kwa sauti ya ukali.. "Na kwanini umekuja kujitenga peke yako huku?" "Nisamehe afande sitarudia tena..wakati namjibu ghafla kile kikaratasi kikadondoka chini.. "Haya lete hicho ulichoangusha..Letee..! Inaendelea...

at 8:54 PM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top