Sitaki Tena - 02 (season 1) Usiku ule tangu nirudishwe tena rumande kwangu haukuwa mzuri,akili na viungo vya mwili wangu vilikuwa vimechoka sana, yote hiyo ni kutokana na kulia na kupigwa pigwa,sikuweza kupata hata chembe usingizi kila nilipofikiria kilichonikuta. . "Hivi kweki nimeua..? Mimi nimeua.? Miiiimi..? Hilo ndo swali nililojikuta najiuliza usiku kutwa bila kupata majibu,nilitamani nishuhudie Jeni akizikwa pengine labda ndo ningeshawishika na kuamini kama kweli nimeua lakini hiyo haikuwezekana, hakika usiku ulikuwa mrefu sana kwangu,mawazo mengi yalikuwa tayari yameshatawala kichwa changu pengine hata umri wangu haukuniruhusu kufikiri sana lakini tayar nikawa na fikra tena za kikubwa zaidi kwa mda mfupi tu tangu niwekwe rumande.. Sauti za bundi,popo na mbwa ndizo zilikuwa zinapaa sana kuzunguka huku na kule katika lile eneo la kituoni, wenzangu walikuwa wamelala fofo hawajielewi hiyo yote ni kutokana na shuruba shuruba za humu ndani, Mpaka ilipotimia saa 9 za usiku usingizi ukawa Tayari umeshanipitia lakini kimoja kilichokuja kunishtua ni kaubaridi kalikokuwa kakipenyeza ndani ya gauni nililokuwa nimevaa, huku miköno yangu miwili ndio ilikuwa mto,mwili wote ulikuwa ukinitetemeka mithili kifaranga cha kuku kikinyeshewa na mvua,kifupi palikuwa na baridi sana nadhani ni kwasababu sakafu ndo ilikuwa kitanda changu.. Taaratibu nilianza kujihisi kama kuna kitu kinanipapasa kupitia mapajani mwangu..lakini sikuwa na wasiwasi kwani nilijiamini sana kuwa tupo wanawake tu na kama askari ndo walikuwa mchanganyiko wakiume kwa wakike..kila mda ulivyokuwa unasogea ndivyo hisia zikawa zinabadilika ndani ya kichwa changu kwani niliweza kulifungua jicho langu La upande wa kushoto kuangaza huku na huku kujua kitu gani kinachonipapasa ghafla.. "Shhh... nyamaza...! Na ole wako ufungua domo lako.?" ilikuwa ni sauti ya askari wa kike niliyekuwa nikimfahamu kwa sura,alikuwa kanishika mapaja yangu kwa nguvu huku akiwaambia askar wenzake ambao walikuwa wakiume wafanye haraka haraka., Moyo ulinipasuka,nguvu ziliniisha,hasira zilinikaa ghafla huku nikikosa pumzi kutokana na kuzibwa mdomo kwa mda mrefu.. hatimaye wale askari waliokuwa takribani watatu walifanikiwa kuniingilia tena kwa nguvu kwa takriban nusu saa pale huku wakiniacha damu nyingi zikinitiririka.. BAADA YA MWEZI Hatimaye upelelezi ukawa umeshakamilika na nilikuwa tayari niko kizimbani..nywele zilikuwa hazitamaniki,miguuni sikuwa hata nandala,mavazi nayo yakawa yameshachoka na kuchafuka kwani toka mwezi ule nibakwe Levina mimi ckuwa hata na nguo nyingine ya kubadilisha,nao mwili ulikuwa tayari umeshadhohofika kutokana na msosi mbaya tuliokuwa tunapewa hakika yalikuwa ni mateso makubwa na si jambo dogo akilini kwangu.. Kama kawaida ya kesi nyingine nadhani hii ni kutokana na shauku iliowataka watu wajue ni nini kitakachofuatia katika kesi yangu kwani umati mkubwa sana wa watu ulikuwepo ukishuhudia kiasi cha kunifanya moyo wangu ulipuke kwa huzuni.. Huku macho yangu yakiangaza huku na kule ghafla nilifanikiwa kumuona baba na safari hii hakuwa na mawakili kama ambavyo ningetegemea bali alikuwa kakalia kibaiskeli cha kupakia wagonjwa walemavu wa miguu huku akikokotwa na dada aliyekuwa amevalia mavazi meupe wazo lilinijie paleple na kugundua kuwa ni lazima atakuwa ni nesi.. "lakini kwanini amekuwa vile..? Au atakuwa amepooza nin?..." nilijiuliza mengi kichwani bila kupata majibu.. Mda wa kuanza kusoma kesi yangu ulifika,pande zote mbili zilikutana ikiwa ni pamoja na mashahidi wa pande zote mbili.. "wewe ndio binti Levina..? Ndio mimi.. Unakumbuka mnamo tarehe 1 mwezi wa 2 mwaka 2009 ulifanya kosa... Nakumbuka.. Uliweza kuua tena kwa kukusudia..? Ndio.." hayo ndiyo maswali niliokuwa naulizwa na kuyajibu.. Hatimaye yalikusanywa maswali na majibu yote kuashiria kesi imeeleweka na kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani.., "Mwanangu...! mwanangu..! Kweli unafungwa mwananguu..?" hayo yalikuwa maneno ya mwisho kwa mama yaliyofanya na watu wengine waachie vilio pale pale huku nikibakiwa na roho ya kishujaa na kijasiri bila hata kutoka mchozi.. BAADA YA MIAKA 5 Vurugu zilizokuwa zinaendelea katika Gereza la kufungwa watoto watukutu lililopo mbeya, Ndizo zilizosababisha watoto wengi kupoteza maisha na wengine kupata ulemavu wa maisha kutokana na mgomo waliokuwa wameuanzisha kutokana nakupewa chakula kidogo sana tena kichafu,milipuko ya magonjwa kama kipindupindu,msongamano wa wafungwa kiasi cha wengine kufariki kwa kukosa hewa wakati wa kulala usiku.. Namba CG.016/007369, ndiyo namba iliyokuwa inasomeka katika sare yangu ya Gerezani ., Tayari maisha nlikuwa nimeshayazoea mule gerezani,taarifa kutoka nyumbani nilikuwa nikiletewa na afande mmoja ambaye tayari nilimzoea na hata kuanzia siku ile nilipo hukumiwa pale mahakaman hali ya baba yangu kiafya haikuwa nzuri na hakukaa mda mrefu akawa amepoteza maisha, Mwenyezi mungu amlaze pahala pema peponi.. Na sasa mama ndio mzazi wangu pekee aliyebaki hata kama nitatoka gerezani... ucheshi, ufanyaji kazi kwa nguvu,bidii na kujituma zaidi ndicho kitu kilichokuwa kikiwavutia maaskari wengi pale kiasi kwamba nikapendwa sana na kuaminika.. "Levinaaa... Levinaaa.. ...Wewe Levina Christian?.. Aliniita askari wa zamu lakini sikuweza kumsikia vizuri kwa sababu ya makelele ya wenzangu waliokuwa wakipigana mule ndani.. "Abeee afande..nilimuitikia" "Embu fanya haraka kuna mgeni wako kaja kukutembelea fanya ukamuone.." "Sawa afande..." Mapigo ya moyo yalikuwa yakinienda mbio,lakini halmashauri ya kichwa changu iliweza kupambanua haraka haraka na kujua atakuwa ni mama tu... "Lakiiini...mbona afande hakuniambia kama ni mama au la! Maana mama yangu anamjua angeniambia tu?" ndio maswali niliokuwa najiuliza nikiwa njiani kuelekea chumba cha wageni.. Ghafla... INAENDELEA..

at 8:53 PM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top