MAPENZI YA FACEBOOK-09 Kwanini mapenzi yaendelee kunitesa, kwanini niendelee kuishi maisha ya kuwa kama mkimbizi katika dunia hii ya mapenzi. Mapenzi yaliyowaacha watu wengi katika maumivu makali sana. Kila mtu analia na maumivu yake, wengine wanayachukia mapenzi huku wengine wakitamani kujiua sababu kubwa ikiwa ni mapenzi. Kuna muda huwa najiuliza hivi ni nini kipya katika mapenzi lakini sipati jibu kabisa. Kwa kweli sikutaka kuendelea kuwa katika yale maumivu niliyokuwa nikiyapata kwa wakati ule, ni ukweli usiopingika kuwa nilimpenda sana mke wangu wala hakukuwa na mwanamke mwingine niliyekuwa nikimpenda zaidi yake, naweza kusema ukiotoa upendo niliyokuwa nao kwa mama yangu mzazi, mwanamke aliyekuwa akifuatia ni yeye. Nilimpenda sana katika maisha yangu, nilimpa nafasi kubwa sana katika moyo wangu wa mapenzi. Aliishi kwa kujiachia sana nadhani hii ndiyo sababu iliyopelekea kuanza kunichanganya. Tukio la kushuhudia namba ngeni zikiingia katika simu ya mke wangu pamoja na meseji mbalimbali halikuwa la kwanza kutokea, nakumbuka mara ya kwanza nilipolishuhudia niliweza kumkanya na alikiri kutorudia tena, ni kweli ilikuwa ni kama alivyokuwa ameniahidi lakini haikuwa katika maana ya kile alichokuwa akikizungumza. Bado aliendelea na tabia yake ya kisirisiri mpaka pale nilipobahatika kumfumania. Kwa kweli sikutaka moyo wangu uendelee kupitia katika yale maumivu uliyokuwa ukiyapitia, niliamua kuachana na mke wangu. Niliamua kuachana naye ni kutokana na vituko alivyokuwa akinifanyia. Mapenzi aliyokuwa nayo kwangu yote aliyahamishia katika mtandao wa facebook, aliipenda sana Facebook na ndiyo sababu ambayo naweza kusema iliyosababisha mimi na yeye kutengana. Yalikuwa ni maamuzi magumu sana ambayo yaliugharimu moyo wangu lakini nilijikaza kiume, sikutaka kuwa mdhaifu katika hilo hasa katika harakati za kupigania amani ya moyo wangu. “Kwanini umeamua kufanya maamuzi hayo?” lilikuwa ni swali la kwanza kabisa la Juma kuniuliza mara baada ya kukutana naye na kumsimulia kila kitu kilichokuwa kimetokea. “Juma sikuwa na njia nyingine ya kufanya,” nilimjibu huku nikimtazama, alionekana kuchukizwa sana. “Phidelis rafiki yangu hivi unajua haupo sawa?” “Kivipi?” “Hivi utawezaje kumuacha mke wako kisa facebook.” “Juma unazungumza kwa kuwa hujaoa, ingia katika ndoa utafahamu ni kwa jinsi gani mke anauma, asikwambie mtu ndoa ni ngumu mno imejaa kila aina ya matatizo.” “Una maanisha nini?” “Unaniuliza tena?” “Ila haukuwa sahihi kuachana na mke wako.” “Kama kuvumilia nimevumilia mengi tu, acha aende zake,” nilimwambia Juma huku akiendelea kunishangaa. **** Baada ya kupita mwezi mmoja nilipata habari kuwa Ester anaolea tena, kiukweli sikutaka kuamini habari hizo japo kwa wakati ule nilikuwa nimeachana naye lakini kwa upande mwingine iliniuma hasa baada ya kusikia mke wangu niliyeachana naye alikuwa akiolewa na mwanaume mwingine, hilo lilizidi kunichanganya sana. Nayakumbuka maumivu niliyowahi kuyapata kipindi kile alipokuwa akinifanyia visa lakini haya yalikuwa ni maumivu mengine kabisa, niliumia kwasababu ya wivu. Wivu wa kumshuhudia mke wangu niliyeachana naye akiolewa na mwanaume mwingine. Niliamua kuchunguza ukweli wa habari zile na hatimaye nikaweza kufahamu. Ester mke wangu alikuwa akiolewa na yule mwanaume aliyejulikana kwa jina la Osmon ambaye mapenzi yao yalianzia Facebook. Kwa kweli sikutaka kuamini kabisa kwa kile nilichokuwa nakishuhudia kwa macho yangu. Sijui ni kwanini nilikuwa katika maumivu makali kiasi hicho, niliamua kulipa kisasi, kisasi cha kumtafuta mwanamke facebook ambaye ningeweza kumuoa. Ama kwa hakika facebook imeficha siri nyingi sana, kama lilivyo jina lake nilikwenda kupenda kitabu nisichokifahamu kabisa. Je, nini kitaendelea? Usikose sehemu ijayo... #Share kwa wingi.

at 12:46 PM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top