MAPENZI YA FACEBOOK-04 Baada ya kupita siku kadhaa niliyaona mabadiliko makubwa sana kwa mke wangu, hakuwa mtu wa kusumbuliwa tena na namba ngeni. Kwa kweli hali hiyo ilinifurahisha sana, niliona maneno yangu yalisaidia sana hasa kwa kumbadilisha mke wangu. Sikuacha kumsifia katika hilo, alionyesha kunipenda sana na kila kitu kilichokuwa kikitokea ilikuwa ni lazima aniambie. Ni katika tukio hili nilizidi kumuamini sana kupita kawaida. “Mume wangu,” aliniita siku moja nilipokuwa nyumbani, ilikuwa ni siku ya jumapili, siku hiyo sikwenda kabisa katika mihangaiko yangu ya kila siku. “Naam,” niliitika huku nikimtazama, alionekana kuwa na kitu alichokuwa akitaka kuniambia ila alisita kuniambia akawa anatazama chini. “Kuna nini?” nilimuuliza. “Hakuna kitu,”alijibu huku akiwa ameinamisha kichwa chake chini. “Mbona sasa upo hivyo,” nilimwambia huku nikijaribu kumuinua, alizidi kuona aibu kunitazama. “Kuna kitu nataka kukuambia.” “Kitu gani?” “Kuna mtu ananisumbua.” “Nani?” “Mimi simjui ila ni wa facebook ila ananisumbua sana,” aliniambia huku akionekana kuchukizwa sana na kitendo hicho cha watu wanaomsumbua. Nilichomuambia ni kuacha mawasiliano na mtu huyo ambaye alikuwa akimsumbua. “Usimjibu chochote,” nilimuambia. “Sawa mume wangu,” alinijibu. Nilizidi kumuamini sana mke wangu, kwa jinsi alivyokuwa akinieleza ukweli wa kile kilichokuwa kikindelea katika maisha yake pamoja na watu waliokuwa wanamsumbua hakika kiliniweka katika wakati wa kujiamini sana. Sasa kwanini nisimuamini wakati alikuwa akinieleza ukweli. **** Siku moja niliamua kuingia facebook na kuanza kuipitia akaunti ya mke wangu. Nilikuwa mwenye furaha sana kwani mpaka kufikia hapo sikuwa na wasiwasi wowote kabisa kwa mke wangu, Ester wangu, Uaridi la maisha yangu. Ghafla! nilishangazwa na kile nilichokuwa nikikiona katika akaunti ya mke wangu. Picha za nusu uchi alizokuwa amezipost huku nyingine akiwa amekaa mikao ya ajabu, zilizidi kunishangaza sana. Niliendelea kuipekuwa akaunti yake ambayo iliongoza kwa kufuatiliwa na wanaume wengi. Niliziangalia zile like elfu moja pamoja na komenti mia saba alizokuwa akikomentiwa katika picha zake. “Mambo dada.” “Poa Aidan.” “Umetokelezea sana miss.” “Asante sana.” “Uko pande zipi mrembo.” “Dar.” “Nimekupenda ghafla!” “Huhuhuhu! Asante jomoni.” “Njoo inbox.” “Nakuja.” Ilikuwa ni moja kati ya komenti alizokuwa akijibu mke wangu, nilikuwa nikizisoma huku nikiwa siamini kabisa. Kwa kweli sikutaka kuamini kile nilichokuwa nikikiona kwa macho yangu, nilihisi wenda nilikuwa katika ndoto na muda wowote ningeweza kuamka lakini haikuwa hivyo, nilikuwa katika ukweli mtupu, ukweli wa kuishuhudia akaunti ya mke wangu. Je, nini kitaendelea? Usikose sehemu ijayo…..

at 7:26 PM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top