JAMANI BABA! SEHEMU YA 18 ILIPOISHIAA “Sidhani kama nitakuwa na uhusiano mzuri na mama,” alisema moyoni Mwaija. .. ENDELEA KIVYAKO SASA .. . “Hivi nitarudi vipi nyumbani leo ? Hii si aibu kubwa! Yaani mke wangu amejua kila kitu kuhusu mtoto wake . Niliomba samahani siku zile yakaisha, kaenda Tanga nikamleta tena mjini sasa faida yake ndiyo haya yanayonitokea . “Mbaya zaidi kuna wakati Mwaija alinishukuru kwa kumpangia chumba, sasa pale mama yake si amesikia kila kitu !” alitafakari Masilinde, akaishiwa nguvu na kuanguka chini kisha akapoteza fahamu . Mwaija alifanya kazi ya ziada kumzindua mpenzi wake huyo lakini alipozinduka na kutulia kidogo wote wakawa na swali moja ni kwa nini mama Mwaija baada ya kukatiwa simu muda huo hakupiga tena?! Wakiwa wanafikiria kuhusu hilo , simu ya Mwaija ikaita ikiwa kwenye meza ndogo... “Hebu angalia ni yeye?” alisema Masilinde... “Mimi naogopa, angalia wewe, ” alisema Mwaija . Simu iliendelea kuita na kila mmoja akiwa hataki kuangalia nani aliyepiga .. . “Angalia Mwaija .. .” “Angalia wewe bwana mimi naogopa .” Mwishowe, Masilinde alijitoa fahamu , akaenda kuangalia... “Mh ! Yeye bwana ,” alisema akiwa ameishika simu.. . “Mimi sipokei hata iweje! Mama anaweza kuniua hata kwenye simu,” alisema Mwaija huku akitetemeka. Chumba kilizizima , kila mmoja alikosa amani, alikosa raha! Ilifika mahali wote walikaa kitandani wakiwa wamejiinamia kwa mawazo. Kila mmoja aliwaza la kwake , lakini hakuna aliyemwambia mwenzake alichokuwa akikiwaza... “Mwaija , mimi nadhani kuanzia leo tuamue moja , tuwe mke na mume au tujiue , kwa kuwa najua mimi na mama yako kurudiana hakupo hata iweje?” Kabla Mwaija hajajibu, meseji kwenye simu yake iliingia, ikaingia pia kwenye simu ya Masilinde... “Mh ! Hizo meseji atakuwa yeye, ” alisema Mwaija. Sasa alianza kujijua kumbe yeye ni bogasi kupita wasichana wote duniani . Kuna akili ilikuwa ikimwambia “Hivi kweli wewe na akili zako unaweza kumpa penzi mume wa mama yako? Ona sasa, umejiingiza kwenye matatizo maishani mwako .. . mume wa mama yako hata kama hajakuzaa , ni baba yako tu. ” Masilinde ndiye aliyekuwa wa kwanza kuifungua meseji hiyo na kuisoma tena kwa sauti .. . “Nimeamua kujiua ili kuepuka aibu na fedheha hii.” Mwaija naye akaisoma meseji yake kwa sauti ... “Mwaija , endelea kufaidi penzi la baba yako maana uliona mimi nafaidi peke yangu , tukutane ahera.” Masilinde alikurupuka, akaondoka mbio kwenda kwake. Mwaija naye hakutaka kusubiri, alifuata nyuma. Walimkuta mama Mwaija ameshakata roho kwa kujinyonga kwa kamba . Kilio kilianzia hapo, majirani walipofika , Masilinde alikiri kusababisha kifo cha mkewe , Mwaija naye alikiri kuchangia mama yake kujinyonga . Wakaahidi kutoendelea na uhusiano tena, Mwaija alirudi Tanga kwa shangazi yake ambako mpaka sasa anataabika na maisha akiwa kama mwendawazimu. MWISHO.

at 12:35 AM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top