Home → simulizi
→ JAMANI BABA!
SEHEMU YA 17
ILIPOISHIA
“Sawa kipenzi . ”
Wakabusiana na mzee kupata kiburudisho chake
kwa saa moja na kisha kurudi nyumbani huku
akiwa mwepesiii, hakuacha kumtembelea Mwaija
nyumbani hapo , kazi ikawa ni kujilia tunda kila
siku.
SASA KANYAGA MWENYEWE .. .
Mwezi mmoja ulikatika tangu Mwaija aondoke
nyumbani hapo . Siku hiyo mama kama mama,
uchungu wa mwana ulimwingia , akaamua
kumpigia Mwaija japo amjulie hali . ..
“Ni mtoto wangu wa kumzaa , siwezi kumtupa
hivi. Mwenye makosa ni baba yake, kwani si
anajua yule ni mwanangu ?
“Sidhani kama Mwaija ndiye aliyemtongoza baba
yake wa kambo . Lakini mwanangu yule naye
amezidi uzuri . We mtoto mdogo wowowo vile ,
kiuno kiuno kweli . Mguu wanasema wa bia,
halafu yale macho mwanangu yale ndiyo
yanayomponza kabisa, ” alisema mama Mwaija
simu ikiwa sikioni tayari. ..
“Shikamoo mama,” Mwaija alimsalimia baada ya
kupokea.. .
“Marhaba , hujambo ?”
“Mi sijambo.”
“Hajambo shangazi yako ?”
“Hajambo .”
“Maisha yanaendaje?”
“Kawaida tu mama. ”
Mama Mwaija alishtuka kusikia kelele za wapiga
debe wakisema ...
“Msasani Posta... Msasani Posta.”
“Mwaija ,” aliita. ...
“Uko Dar ?”
“Hapana mama , niko Tanga.. .”
“Unanidanganya mimi wewe?”
“Hapana mama , kwa nini ?”
“Mbona nasikia watu wa daladala wakisema
Msasani Posta?”
“Siyo Msasani mama , unasikia vibaya .
Wanasema Mkwakwani Posta. Siku hizi Tanga
kuna daladala za Mkwakwani Posta, ” alisema
Mwaija huku akitetemeka.
“Kweli ?”
“Kweli mama , kwani we hujui kuna daladala za
Mkwakwani Posta?”
“Mi nimesikia Msasani Posta.”
“Hapana mama bwana. ”
“Haya , shangazi yako anaendeleaje ?”
“Anaendelea vizuri . Nipe niongee naye .”
“Mimi nipo mtaani , nimemwacha nyumbani.”
“Ukirudi tu, nipe niongee naye. ”
“Sawa mama .”
Mwaija alipomaliza kuzungumza na simu na
mama yake , akampigia Masilinde.. .
“Baby uko wapi ?”
“Kazini, vipi ?”
“Kimenuka. Njoo haraka sana.”
“Nini?”
“Ungekuja baby bwana .”
“Oke, nakuja sasa hivi . ”
Mwaija alizidi kutetemeka, hasa alipoambiwa
akifika nyumbani ampe simu shangazi yake ili
mama yake aongee naye .
Ndani ya nusu saa , Masilinde akawa amefika
nyumbani kwa Mwaija huku akiwa na sura yenye
mshangao.. .
“Vipi Mwaija , kuna nini ?”
“Inabidi niende Tanga haraka sana , hata
nikiondoka leo hii .”
“Kuna nini ?”
“Mama. ”
“Mama gani?”
“Mkeo .”
“Kafanyaje?”
“Kanipigia simu .”
“Enhe , kasema anakwenda Tanga kesho? Maana
kama anasafiri kesho tatizo liko wapi, mi si
nitamzuia tu?”
“Siyo hivyo baby. Mama kasema nimpe simu
shangazi aongee naye, nikamwambia nipo
mtaani, shangazi nilimwacha nyumbani. ”
“Sasa ikawaje?”
“Akasema nikirudi atataka aongee naye . Na
mimi najua lazima baadaye jioni mama atapiga
tena. Halafu akaniuliza Mwaija upo Dar ?
Nikamwambia hapana mama, akasema mbona
nimesikia sauti za daladala zikisema Msasani
Posta? Nikamdanganya siyo Msasani Posta ni
Mkwakwani Posta. Ndiyo akatulia.”
“Kha! Kwani we leo ulifika Msasani ?”
“Si ulinikubalia niende kwa yule rafiki yangu .”
“Oo ! Sasa sikia , sidhani kama ni ishu.. .”
Kabla Masilinde hajamaliza , mama yake alipiga
tena...
“Huyo , anapiga ,” alisema Mwaija ...
“Usipokee kwanza. ..nataka kujua , kwani
shangazi kule Tanga ana simu ?”
“Hapana, alikuwa akitumia ya kwangu. ”
“Oke. Sasa itabidi tumkodishe mwanamke,
tumwambie ajifanye shangazi yako , aiige sauti ,
wewe utamwambia sauti ya shangazi ilivyo. ”
“Shangazi ana sauti ndogo sana , utadhani
mtoto.”
“Ah! Kumbe ni hivyo , hata mimi naweza kuigiza
sauti ya kitoto . Hebu pokea mwambie ongea na
shangazi, ” alisema Masilinde.
Mwaija aliogopa lakini mama yake aliendelea
kupiga, ikabidi apokee . ..
“Haloo mama .”
“Umesharudi nyumbani?”
“Ndiyo.”
“Nipe shangazi yako. ”
“Huyu hapa , ongea naye. ”
Masilinde alijibana sawasawa , akavuta pumzi
inavyotakiwa ili atoe sauti ya kitoto .. .
“Halo. ”
“Ee, wifi za leo?”
“Njema, za huko Dar ?”
“Huku kwema wifi , unaendeleaje na huyo binti
yako?”
“Tunaendelea vizuri , ila mi mwenyewe kifua
kidogo si kizuri sana .”
“Oo ! Pole, ndiyo maana sauti inatoka kama
inataka kukatika. ”
“Ee. Umeona ee?”
“Ee. Pole sana. haya, nilitaka kukusalimia tu wifi
maana huyo aliniambia alitoka, nikamwambia
akirudi niongee na wewe .”
“Asante sana wifi yangu. Msalimie sana
Masilinde.”
“Haya zimefika wifi .”
Baada ya kumaliza kuongea na mke wake
akijifanya ni shangazi mtu, Mwaija na Masilinde
walicheka kiasi cha kushindwa kuhimili na
kujishika matumbo yao lakini kumbe simu
ilikuwa haijakatwa upande wa pili.. . itaendeleaaa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: