Home → simulizi
→ JAMANI BABA
Sehemu 16
ILIPOISHIA
Asante ila mimi nataka talaka yangu tu kama
amekwambia kuhusu kumfumania na
mwanangu. ”
“Ameniambia lakini unakumbuka mwaka huu ,
mwezi wa pili na wewe ulifumaniwa kule kwa
mzee Bakari na yule mzee wa genge la
Mwembeni, ulimwambia mumeo ?”
TEMBEA NAYO MDOGOMDOGO. ...
Kitendo cha kusema maneno hayo tu, Masilinde
akaona afadhali kwamba naye alipata pa
kujitetea kwani hata mke wake aliwahi
kufumaniwa.
“Kumbe alishawahi kufumaniwa?”
“Ndiyo.”
“Na nani?”
“Kwa mzee Bakari, yule mzee muuza genge
mtaa wa pili ” alisema mzee Kimanama .
“Mama Mwaija umesikia hayo? Unanishia bango
wakati hata wewe umewahi kufumaniwa ?”
Masilinde alimwambia mkewe .
“Wala sijawahi kufumaniwa, halafu we mzee
acha uchuro wako hapa. Nataka talaka yangu ... ”
“Talaka sikupi, kama umenifumania, na wewe
ushawahi kufumaniwa, kwa hiyo ngoma droo,
kama umefunga na mimi nimefunga. ..”“ Nasema
hivi nataka talaka yangu. ”
“Mimi si ndiye muandikaji wa talaka , siwezi
kutoa ...halafu niliweka nadhiri kwamba katika
maisha yangu sitakuja kutoa talaka mpaka
naingia kaburini... ”
Kwa hasira, mama Mwaija akamgeukia Mwaija .
“Halafu na wewe ni lazima uondoke hapa
nyumbani, nikipewa talaka na wewe safari kwani
siwezi kuendelea kuishi na mtoto mwenye tabia
chafu kama yako ... ”
“Nisamehe mama, sitorudia tena ... ”
“Hakuna cha msamaha, ungekuwa umefanya
kosa lingine ningekusamehe lakini siyo kufanya
mapenzi na baba yako, kwa mwanamke yeyote
ni aibu kubwa sana .”
Hapohapo akamgeukia mzee Kimanama .“ Na
wewe mzee mbeya , umesema kwamba
nimefumaniwa, lini nimefumaniwa?”
“Unajifanya hukumbuki ?”
“Na nani?”
“Si yule mzee muuza genge, alijifanya
kukuongezea vimbogamboga kumbe alikutaka na
ukaingia mkenge, tena mzee nuksi sana kwa
wake za watu yule. ..” Mama Mwaija akakasirika,
alijua kwamba hakuwahi kufumaniwa ila mzee
huyo alikuwa akidanganya, alichokisema ni
kwamba waende kwa mzee huyo, kweli
wakaenda na kumkuta akiwa amesimama nje .
“Karibuni. ..”
“Asante , wewe mzee , hujawahi kufumaniwa na
huyu mwanamke ?” aliuliza mzee Kimanama .
“Mwanamke gani ?”“Usijifanye hujui, kwani hapa
wanawake wapo wangapi?”
“Namuona mmoja tu. .”
“Sasa kama unamuona mmoja kwa nini unauliza
jibu? Aya tujibu .”
“Sijawahi kufumaniwa naye , kwanza hata mapaja
yake tu sijawahi kuyaona .”
“Wewe mzee muogope Mungu , leo unaruka na
wakati siku ile ulipigwa mpaka picha !’
“Nimekumbuka sasa , kweli nilishawahi
kufumaniwa, ila si na huyu mwanamke, yule
alikuwa mama Mwajabu , yule wa mtaa wa tatu,
mwanamke mweupe wa Kitanga aliyefanana na
mkeo ,” alisema mzee huyo , alionekana
kukasirika na hivyo kumzingua mzee Kimanama.
“Huo sasa utani .. .”
“Kama ni utani basi jua wewe ndiye umeanza
kunitania, kwanza naomba muondoke nyumbani
kwangu kabla sijawaitia polisi . ”Hawakuendelea
kusubiri, tayari Masilinde akaonekana
kushindwa, alichokifanya mara baada ya kufika
nyumbani ni kuanza kuomba msamaha kwa
mkewe kwa kilichotokea .
“Mke wangu naomba unisamehe ni shetani
alinipitia nakuahidi sitarudia tena kosa hilo ,
nisamehe mama na nipo chini ya miguu yako,”
Masilinde alimwangukia mkewe .
“Ukitaka tuelewane kuna sharti moja .”
“Lipi ?”
“Huyu malaya sitaki akae hapa nyumbani. ”
“Eeeh ! Amekuwa malaya tena, huyu si mtoto
wako wa kumzaa!”
“Hata kama , umekubaliana na mimi?”
“Sawa . Kwa hiyo nikampangie chumba ili atoke
hapa?”
“Umpangie chumba! Nani kasema hivyo , unataka
uwe unajiachia kila siku, haiwezekani, huyu arudi
Tanga.”
“Arudi Tanga?”
“Ndiyo.”
“Mbona unamtupa hivyo ?”
“Mimi si ndiye mama yake ! Arudi Tanga .”
Kwa sababu mke wake aliamua hivyo na
hakutaka kumpoteza kwa kuendelea kudai
talaka, akakubaliana naye.
Alichokifanya mzee huyo ni kumsisitizia Mwaija
kwamba waendelee kuwasiliana hata kama
angekuwa wapi kwani bado moyo wake
ulimpenda sana na hakutaka kumuacha.
“Kwa hiyo ndiyo hivyo baby, tuwe tunawasiliana,
usimuogope mama yako, kutembea nje ya ndoa
ni faulo za kawaida tu, kama kuchezewa rafu
uwanjani, ” alisema mzee huyo .Siku iliyofuata
mama Mwaija aliamua kumrudisha Mwaija
Tanga. Mawasiliano na msichana huyo
yaliendelea kisiri na baada ya wiki moja, mzee
huyo akamtumia binti huyo nauli na kumvuta
tena Dar , kipindi hiki akampangia chumba
kabisa, mtaa wa Tandale karibu na Kwa Mtogole.
“Utakuwa ukiishi hapa mpenzi , hapa sasa kwa
raha zetu , mama akipiga simu, mwambie upo
Tanga, siku nyingine akisumbua sana, kata simu
kisha baadaye utamwambie network inazingua, ”
alisema mzee huyo .
“Sawa kipenzi .”
Wakabusiana na mzee kupata kiburudisho chake
kwa saa moja na kisha kurudi nyumbani huku
akiwa mwepesiii, hakuacha kumtembelea Mwaija
nyumbani hapo , kazi ikawa ni kujilia tunda kila
siku. Itaendeleaaa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: