Home → simulizi
→ JAMANI BABA!
SEHEMU YA 18
ILIPOISHIAA
“Sidhani kama nitakuwa na uhusiano mzuri na
mama,” alisema moyoni Mwaija. ..
ENDELEA KIVYAKO SASA .. .
“Hivi nitarudi vipi nyumbani leo ? Hii si aibu
kubwa! Yaani mke wangu amejua kila kitu
kuhusu mtoto wake . Niliomba samahani siku zile
yakaisha, kaenda Tanga nikamleta tena mjini
sasa faida yake ndiyo haya yanayonitokea .
“Mbaya zaidi kuna wakati Mwaija alinishukuru
kwa kumpangia chumba, sasa pale mama yake
si amesikia kila kitu !” alitafakari Masilinde,
akaishiwa nguvu na kuanguka chini kisha
akapoteza fahamu .
Mwaija alifanya kazi ya ziada kumzindua mpenzi
wake huyo lakini alipozinduka na kutulia kidogo
wote wakawa na swali moja ni kwa nini mama
Mwaija baada ya kukatiwa simu muda huo
hakupiga tena?!
Wakiwa wanafikiria kuhusu hilo , simu ya Mwaija
ikaita ikiwa kwenye meza ndogo...
“Hebu angalia ni yeye?” alisema Masilinde...
“Mimi naogopa, angalia wewe, ” alisema Mwaija .
Simu iliendelea kuita na kila mmoja akiwa hataki
kuangalia nani aliyepiga .. .
“Angalia Mwaija .. .”
“Angalia wewe bwana mimi naogopa .”
Mwishowe, Masilinde alijitoa fahamu , akaenda
kuangalia...
“Mh ! Yeye bwana ,” alisema akiwa ameishika
simu.. .
“Mimi sipokei hata iweje! Mama anaweza kuniua
hata kwenye simu,” alisema Mwaija huku
akitetemeka.
Chumba kilizizima , kila mmoja alikosa amani,
alikosa raha! Ilifika mahali wote walikaa
kitandani wakiwa wamejiinamia kwa mawazo.
Kila mmoja aliwaza la kwake , lakini hakuna
aliyemwambia mwenzake alichokuwa
akikiwaza...
“Mwaija , mimi nadhani kuanzia leo tuamue moja ,
tuwe mke na mume au tujiue , kwa kuwa najua
mimi na mama yako kurudiana hakupo hata
iweje?”
Kabla Mwaija hajajibu, meseji kwenye simu yake
iliingia, ikaingia pia kwenye simu ya Masilinde...
“Mh ! Hizo meseji atakuwa yeye, ” alisema
Mwaija. Sasa alianza kujijua kumbe yeye ni
bogasi kupita wasichana wote duniani . Kuna akili
ilikuwa ikimwambia
“Hivi kweli wewe na akili zako unaweza kumpa
penzi mume wa mama yako? Ona sasa,
umejiingiza kwenye matatizo maishani mwako .. .
mume wa mama yako hata kama hajakuzaa , ni
baba yako tu. ”
Masilinde ndiye aliyekuwa wa kwanza kuifungua
meseji hiyo na kuisoma tena kwa sauti .. .
“Nimeamua kujiua ili kuepuka aibu na fedheha
hii.”
Mwaija naye akaisoma meseji yake kwa sauti ...
“Mwaija , endelea kufaidi penzi la baba yako
maana uliona mimi nafaidi peke yangu , tukutane
ahera.”
Masilinde alikurupuka, akaondoka mbio kwenda
kwake. Mwaija naye hakutaka kusubiri, alifuata
nyuma. Walimkuta mama Mwaija ameshakata
roho kwa kujinyonga kwa kamba .
Kilio kilianzia hapo, majirani walipofika , Masilinde
alikiri kusababisha kifo cha mkewe , Mwaija
naye alikiri kuchangia mama yake kujinyonga .
Wakaahidi kutoendelea na uhusiano tena, Mwaija
alirudi Tanga kwa shangazi yake ambako mpaka
sasa anataabika na maisha akiwa kama
mwendawazimu.
MWISHO.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: