CHOMBEZO; STORI TAMU YA KUSISIMUA SITA KWA SITA 03 4 hours ago SEHEMU YA TATU MTUNZI : ABDUL JUMA INSTAGRAM: @ABBYKAMCHORO WHATSAPP: 0766025554  "Nyie acheni tu , mmemwona huyo kaka mrefu  aliyepita hapa ? " aliuliza Fifi "Huyo Osward ndo anakutoa kwenye mambo yenu unamwangalia yeye " aliongea Juliana huku akibetua midomo yake "Unamjua !? " Fifi aliuliza "Mm Naachaje kumjua anajiita Handsome wa chuo kizima " aliongea Juliana "Kumbe ni mwanafunzi ! , Siku ile ya sherehe nipo na kinywaji changu ile nguo iliyokuwa imechafuka ndo alinipamia Mimi nikajua mwalikwa " aliongea Fifi "Hahahahahahha kuna mtu asiyemjua Osward ndo kwanza mwaka wake wa kwanza ila karibia chuo kizima kinamjua , ile sherehe angekosa nadhani angekufa anayopenda kuzamia usione kapendeza uliza uambiwe shoga angu " aliongea Juliana "Hahahahha Makubwa " aliongea Nana na kuangua kicheko Siku iliyofuata Osward akiwa amekaa na rafiki zake anawaonesha picha za kadada kamoja aliko kuwa amelala nako na kukapiga picha za utupu, kuna gari ikaingia na kupaki pembeni kidogo na kuteremka msichana Fifi mkononi akiwa amebebelea mkoba wake akipiga hatua kuelekea upande yalipo mabweni ya wasichana Osward akiwa anaendelea kuwaonesha picha rafiki zake "Mwanangu izi rangi zako Osward , we mtu mbaya watoto wakali wanakuelewa ile mbaya huyu nigei namba zake kanitia hamsha hamsha " aliongea Phili huku Osward akaperuzi namba ya huyo bishosti na kumpatia Phili "Akiuliza umetoa wapi namba yake tusitajane we pambana na hali yako" aliongea Osward alipoangalia pembeni akaweza kumwona Fifi anaishilizia "Enheee! Wanangu yule Malaika yule kulee anaishilizia , yule lazima nimpate , wazee lazima aingie kingi " aliongea Osward huku akiwasonteshea "Duuuh! Yule Demu Mimi namjua kaka gusa kote pale acha kabisa yule demu kwao wanapesa chafu hatari utaozea ndani yule namjua mpaka kwao anaitwa Fifi mzee wake Don Ostarbay nzima" aliongea Jenes "Pesa zake mimi hazinishindishi na kiu pale lazima nilambe kaka hizo ndo type zangu sitembei na midosho Mimi , Demu asiye na pesa Mimi wa kazi gani, Jenes halafu nimekusoma we mwoga mwoga sana ngojeni akitoka niwaonesheni " aliongea Osward wakakaa wakimchora pindi tu atakapo toka anyayuke na kumwibukia Baada ya muda mchache Fifi akawa anarudi Osward alipomwona tu akanyanyuka na kuanza kumfuata kule alipokuwa anatokea Fifi , alipomkaribia akajifanya kujipitilizisha yani Osward mjanja Fifi si akamwona kwanini asimpapatikie "Kaka ! We kaka " aliita Fifi "Unaniita Mimi Dada ! "Osward  alijisimamisha na kujiulizisha "Ndiyo , Mambo ! " sauti nyororo ya Fifi ikapenya kwenye masikio ya Osward "Safi vipi " akarudishia Osward "Samahani , sijui unanikumbuka ?" Aliuliza Fifi "Mmmm! Hapana labda unikumbushe, sikumbuki tumewahi kuonana wapi " aliongea Osward "OK, mmm ile siku ya sherehe ulinipush Kwa bahati mbaya na kunimwagia wine yangu " aliongea Fifi "Oooh! Sawaa , Daaah! Pole Sana Dada nilikuwa naongea na simu ivo sikuweza kukuona nisamehe tena kwa Mara nyingine " "Wala usijali , nimefurahi kuonana na wewe Kwa Mara nyingine , Naitwa Fifi sijui mwenzangu nani ? " aliongea Fifi na kumwuuliza Osward Jina lake "Woww! Una jina zuri sana Kama jinsi ulivyo , mmm Mimi naitwa Osward " "Ahsante, hata jina lako pia ni zuri , Aamm sijui ningeweza kupata namba yako ya simu maana kuna mahali naenda muda huu kuna mengi nahitaji tuongee zaidi Kama hutojali lakini " aliongea Fifi "Wala usijali " Fifi akatoa simu yake na kumpatia Osward akaandika namba yake ya simu na kumrudishia Bidada simu Huku rafiki zake wanaangalia tukio zima lilivyokuwa likiendelea maskini Fifi angeijua Tabia ya Osward angeliachana nae tu maana siyo mtu wa mchezomchezo halafu mawindoni kajiingiza mwenyewe bila ya kujua namna Osward alivokuwa na hamu ya kuwa nae Majira ya usiku Osward akiwa amejilaza Ghetto na  jamaa zake hakuweza kuruhusu usingizi umpite alikuwa akiitazama simu yake huku akiwatizama jamaa zake wakiwa hoi wanakoroma tu Kipindi iko bidada Fifi ndo anatoka bafuni kuoga huku kajifunga na kitaulo chake kimoja akijifutafuta maji usoni na kusogea kitandani alipokuwa ameibwaga simu yake na kuichukua kisha akaketi kitandani na kuitoa loki na kuzama kwenye phonebook akilitafuta jina la Osward na baada ya kulipata na kuipigia Osward alipoona simu yake inaita namba ngeni akajua tayari akairekebisha sauti yake na kuipokea "Hallo ! Mambo Osward " . . . Itaendelea

at 6:17 AM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top