CHOMBEZO; STORI TAMU YA KUSISIMUA SITA KWA SITA 02 1 day ago SEHEMU YA PILI MTUNZI : ABDUL JUMA INSTAGRAM: @ABBYKAMCHORO WHATSAPP: 0766025554  Osward alinyanyua uso na kumtazama yule Dada, uso kwa uso na mwanadada mrembo aliyejulikana kwa jina la Fifi mtoto wa kigogo mmoja naye alikuwa ni mmoja wa watu wanaosherekea kuingia mwaka wa mwisho  kimasomo "Ai ! Dada samahani sana Dada angu sikukuona kabisaa naomba unisamehe " aliongea Osward huku akilitia simu lake mfukoni na kutoka na kitambaa akataka kumfuta Fifi "Usijali kaka , Unaweza kwenda nitajisafisha " Fifi aliuzuia mkono wa kijana Osward na kumwomba amwache Ila kitu cha kusangaza Fifi hakuonekana kuchukia,  Osward aliondoka na kuweza kumwacha Fifi akiwa amepigwa na butwaa wakati huo Osward anaenda huku akigeuka na kumtazama Jinsi alivyokuwa ameumbika kuanzia sula mpaka umbo lake zuri lililokuwa limekaa vizuri ndani ya gauni alokuwa amelivaa Fifi akaamua kwenda washroom kwaajili ya kujisafisha "Eee! Vipi tena yamekukuta yapi ?! " aliuliza rafiki yake Nana baada ya kutoka msalani na kumkuta Fifi akijisafisha "Mwenzangu acha tu yalonikuta nilitoka kuongea na simu ile narudi kukaa sinimekutana na kimbwanga nimepamiwa wine yote imeishia kwenye nguo " aliongea Fifi "Mmm! Shoga angu pole haya huyo mtu alokufanya ivi umemwachaje ?" Aliuliza Nana "We acha tu , nimeacha aende sijamfanya chochote kile " alingea Fifi "Mmmm! Nasikia hasira ivi Fifi mtu anakuchafua kiasi hiki halafu unamwacha tu ki rahisi rahisi unadhani hiyo wine itatoka Leo hapo umezidi uzungu Fifi, Ashukuru Mungu wake sikuepo hii sherehe ingegeuka kigoma ningemchamba hatari " aliongea Nana "Sikutaka tu ugomvi Nana ivi tu kweli kuna haja ya kugombana na mtu kwa kisa Kama hiki !" Aliongea Fifi "We unaona madogo hayo kunukishana mipombe "aliongea Nana "Tuachane na hayo ,Juliana umemwacha kule maana mkoba wangu nimeuacha pale tulipokuwa tumekaa " aliongea Fifi "Ndiyo , kila kitu anacho " Waliamua kutoka msalani na kurudi kwenye sherehe Baada ya siku ile kupita Osward akiwa amekaa na rafiki zake Jenes , Petro pamoja na philimon wanajisomea Osward alikuwa bize akichezea simu huku akijiachilia na vicheko "Oya ! Mwanangu unazingua , ungeenda basi hata mbali na hapa we huoni kama wenzio tunasoma mzazi " aliongea Jenes "Aaaa ! Msinizingue wakusoma itakuwa nyinyi ... Halafu sikieni jana kuna jambo nilisahau kuwaambia Aisee ! Kuna Malaika mmoja nimeonana nae jana Chaaa! Wallahy hiki chuo kizima sijao .. Sijaona , Mtoto mkali balaa Daaah! Sijui yule demu anasomea nini ila najua ntampata ivi nimemwelewa kichizi lazima nimdumange , halafu Jana nimewachezeshea Kama nane ivi yule Suzan anajifanyaga ana lembalemba kumbe hamna kitu nimemchezeshea Jana hoi sijamwona kabisa tangu asubuhi nikimwona ntamcheka ,omba asionane namimi mshezi yule, nimezoa zoa vihela vyao " Aliongea Osward huku akijimwagia sifa na idadi ya aliolala nao Jana "Nikwambie kitu Osward , hayo mambo ungeachana nayo kabisa ndo kwanza mwaka wako wa kwanza hapa chuoni , ungedili na masomo kwanza wasichana wapo kibao tu mbona , unajiuza kisa pesa" aliongea Petro "Huyu anaongea nini , Unajua Petro Unazingua Mimi najua hizi mambo we huwezi ndo maana unaongea , huu ndo mwanzo anae jilengesha simwachi Mimi mwanaume wewe sijiuzi nauzika Kama Dada yako anasoma hapa mwambie kabisa la sivyo Mimi ntapita nae hata bure Mamaee " aliongea Osward "Hahahahahhaha , We jamaa bhana Osward Mimi nakuaminia we jembe cheza nao ila kusoma pia kuna umuhimu " aliongea Philimon "Mimi Phili nakuelewaa we mtu wangu nigeie tano kwanza .... Sasa Kama vipi baadae kuna kibinti kimejileta inbobo chenyewe ngoja nika meet nacho tutaonana jioni niwape mkanda mzima " Osward alinyanyuka na kuondoka Wiki moja baadae Fifi akiwa na rafiki zake Nana pamoja na Juliana wanakula chakula maeneo ya Samaki Samaki huku wakiongea na kufurahi kipindi icho icho wakiwa wanaendelea kuongea Fifi aliweza kumwona Osward akipita na kuelekea Kwenye Mall macho yote yakamkodoka na kujikuta akimsindikiza kwa macho Namna Osward alivokuwa amevalia nguo zake na kumkaa vizuri Fifi alibaki amezubalia upande ule ule alokwisha pita Osward na kuingia ndani ya Mall "Fifi ! Fifi !" Aliita Juliana na kumshtua Fifi kutoka alipokuwa amezubalia "Jully umenishtua ! " aliongea Fifi "Fifi usitake kuniambia huko kuzubaa kote tunaongea hapa kumbe mwenzetu mawazo yako yapo kwingine " aliongea Nana . . . Itaendelea .....

at 6:17 AM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top