Home → ushauri
→ Wanawake Tunakuwa na Thamani Pale Tunapokuwa Nguo
Napenda kuzungumzia thamani ya mwanamke mbele ya mwanaume.
Nimejifunza mengi kupitia kwa marafiki zangu na hata dada zangu na ndugu wa Karibu. Thamani ya mwanamke mbele ya mwanaume ni pala anapokuwa amevaa nguo na si vinginevyo.
Mwanaume akishakuvua nguo haoni thamani yako tena huendelea kumuwazia yule ambae bado hajamvulia.
Nimeshudia wanawake wengi wakiishia kuumizwa kwasababu ya kukubali kuwavulia nguo wanaume kirahisi.
Binafsi baada ya kuushuhudia waliofanyiwa wanawake wenzangu nimeamua kutomvulia nguo mwanaume asiye mume wangu, na hii imenipa thamani kubwa sana.
Wanawake tusijirahisishe kwa hawa viumbe tutaendelea kuumizwa daima.
Wanawake Tunakuwa na Thamani Pale Tunapokuwa Nguo Napenda kuzungumzia thamani ya mwanamke mbele ya mwanaume. Nimejifunza mengi kupitia kwa marafiki zangu na hata dada zangu na ndugu wa Karibu. Thamani ya mwanamke mbele ya mwanaume ni pala anapokuwa amevaa nguo na si vinginevyo. Mwanaume akishakuvua nguo haoni thamani yako tena huendelea kumuwazia yule ambae bado hajamvulia. Nimeshudia wanawake wengi wakiishia kuumizwa kwasababu ya kukubali kuwavulia nguo wanaume kirahisi. Binafsi baada ya kuushuhudia waliofanyiwa wanawake wenzangu nimeamua kutomvulia nguo mwanaume asiye mume wangu, na hii imenipa thamani kubwa sana. Wanawake tusijirahisishe kwa hawa viumbe tutaendelea kuumizwa daima.
Artikel Terkait
UNAJUA KUMWONYESHA MPENZI WAKO KAMA UNAMPENDA????  Kwa upendo wao wote, kwa nguvu zao zote, na uzuri , mahusiano ni kama mmea ambao unahitaji kumwagilia maji na kuwekewa mbolea na kupata jua la kutosha ili uweze kunawiri vizuri Sababu kubwa ambayo watu hukosa kujua kama wanapendwa ni kutohisi upendo. Kwa nini? Kwa sababu hata kama wanasema I love you mwisho wa kuongea kwenye simu au kabla ya kwenda kazini, hayo maneno hayana miujiza bila ya kuwa na mengine yalio rahisi . Kuna vitu vidogo vidogo sana vinavyoonyesha upendo na kumfanya mtu ajisikie kupendwa. 1.Usisahau kumkumbatia kabla ya kusema kwa heri. Uelewa wa kimwili ni wa muhimu kuliko maneno 2.Mwambie jinsi alivyo muhimu kwako. Hii huenda zaidi ya neno i love you. 3.Express understanding panapohitajika kusema. Nimeelewa unachokisema. Kama hujaelewa elezea, kwa kusema hivi , Niambie jinsi unavyojisikia ili nikuelewe. 4.Sema mara nyingi jinsi unavyomkubali anapokuwa amefanya jambo kwako. Husband and wife in park 5.Mwambie jinsi gani unafurahia vipengele vya upekee wake. Kwa mfano , napenda uchangamfu wako, mpongeze. 6.Toka nae siku nzima bila ya kusema kitu chochote zaidi ya kumsifia. 7.Mnunulie chakula anachokipenda bila yeye kusema. 8.Msaidie kupika 9.Kama mna watoto wapeleke kutembea, ili kufurahia michezo ya watoto ili kumwacha awe peke yake kwa utulivu. 10.Tuma ujumbe wa kimapenzi kwa mwenza wako bila sababu . 11.Mtumie email wakati yuko kazini ili kujua anajisikiaje. 12.Mpigie wakati akiwa break kusema tu hujambo 13.Karibia gari, meza, au kochi na umshike mikono yake japo kwa muda kidogo. 14.Mvutie kiti anapotaka kukaa au mfungulie mlango anapotaka kutoka au kuingia. 15.Kumbuka kumpa tabasamu, sio fake, lile ambalo umetunza kwa ajili yake . 16.Badala ya kumweleza jinsi ulivyokuwa na siku mbaya kazini, mwambie kuwa siku hio ulihitaji kuwa na yeye kwa sababu…au nimekuwa na siku mbaya nahitaji unikumbatie. 17.Fanya utani na ucheke nae 18.Nendeni kulala kwa wakati mmoja, ongeeni pamoja au kama kusoma msome pamoja au kama kutulia kwa muda fanyeni pamoja. 19.Kama una watoto mpongeze mwenza wako mbele yao. Watoto watafurahi pia. 20.Mkumbatie mbele za watu, ingawa ataona aibu lakini atafurahia. 21.Tafuta njia nzuri za kuambiana badala ya I love you 22.Muwe na tabia ya kutoka japo mara moja kwa wiki kama mkiweza 23.Mpe zawadi 24.Mpeleke movie 25.mpe massage bila sababu au kwa ajili ya kazi nyingi 26.Mwambie kuwa yeye ni rafiki yako 27.Usiogope kumshirikisha hisia zako, Ni vizuri kufahamu kama una furaha au huna furaha wakati huo na kwa nini 28.Sikiliza anapokuambia jinsi anavyojisikia 29.Kumbuka kila mara unapoweza nunua kitu kidogo kwa ajili yake. 30.Andika ujumbe mdogo wa kimapenzi na kuacha sehemu ambapo atafika 31.Mshike mikono yake mbele za watu 32.Mpate fundisho pamoja, halijalishi ni aina gani 33.Omba msamaha unapokosea 34.Wakati mwingine yeye awe sahihi 35.Mcheze game pamoja 36.Mpe nafasi anapohitaji hivyo.lakini afahamu kuwa upo kama atakuhitaji 37.Mchemshie maji ya kuoga anapokuwa na stress 38.Mwoshee gari yake 39.Jaribu kufanya kitu cha wema kila siku kwa ajili yake 40.Jaribuni kufanya kitu kipya pamoja. Changamoto moja ni bora 41.Mwache alale miguu pako 42.Mtengenezee breakfast, kama inawezekana mpelekee kitandani 43.Mkumbushe kuwa yeye yuko hot au sexy 44.Mkatembee kwenye hewa nzuri pamoja 45.Mnaweza kuvaa nguo za kufanana mnapotoka kupunga upepo 46.Mjitolee pamoja 47.Mtengeneze nywele zake 48.Muweke lengo kama wanandoa, kwa ajili ya fitness, finance, na personal growth 49.Kusafiri pamoja 50.Mpe compani anapoenda mpirani, kwenye game na uwe mmoja wao 51.Chukua muda wa kuwajua rafiki wa mwenza wako 52.Mwache atoke peke yake wakati mwingine 53.Mwekee nyimbo anazozipenda na mcheze pamoja 54.Usiwe serious sana, uwe mcheshi wakati mwingine 55.Mwimbie nyimbo anazopenda 56.Mwambie unampenda zaidi ya jana 57.Kama una siku mbaya , sikiliza kila unachotaka kusema 58.Mwambie kuwa anavutia kuliko wakati mliokutana mara ya kwanza 59.Mwambie unamfikiria kila mara 60.Mwambie kuwa unamsaidia kwa kuwa umemwelewa 61.Mwambie unapenda mwili na akili yake 62.Mwambie unachokifurahia siku hio. Na jinsi gani kinakukumbusha kuhusu yeye. 63.Siku yako imeendaje leo Kila ukiamka mwambie habari za asubuhi kila siku 65.Kila siku ukitaka kulala mwambie usiku mwema 66.Hakikisha anafahamu kuwa yeye ni namba moja kwako 67.Mwonyeshe kuwa unamuheshimu kwa kusikiliza mawazo yake kwenye maamuzi muhimu 68.Onyesha kukubali alichokifikiria na kukiamua hata kama unaona kabisa hukubaliani nacho. 69.Mwambie akuchagulie nguo za kuvaa kazini 70.Nendeni gym pamoja 71.Mnunulie kadi bila sababu , hata kama hakuna sikuku 72.Tamani kumkiss kila mara 73.Mwambie kuwa umepata bahati ya kuwa na yeye na kuwa umebadilika tangu ukiwa nae 74.Kuwa mkweli . mfahamishe makosa uliyoyafanya 75.Kuwa mpole kwake kwa sababu mwanamke ni laini 76.Mwonyeshe kuwa unamwamini ili nae awe wazi kwako 77.Pigeni picha pamoja 78.Fanyeni mambo ya kijinga pamoja 79.Alika familia yake kwenye chakula cha jioni 80.Mwombe mwenza wako mshirikishane ndoto zenu 81.Cheka anapotania,hata kama utani huo hauchekeshi 82.Uwe rahisi ili aweze kukupenda. Utagundua kuwa kumbe ni mkarimu na ana wema. ... Read More
Wanawake: Mumeo akikukera usilale mpaka pakuche hamjasameheana  Usiku kama mumeo kakukera usilale mpaka pakuche hamjasameheana, hata malaika baraka hawawezi shuka kwenu. Huyo ulionae amezaliwa kwao kaja na tabia zake na wewe umezaliwa kwenu una tabia zako. Sasa ukitaka kila kitu kiwe wewe unavyotaka atakuwa mwanao tena huyo sio mumeo samehaneni kwa kila mnalofanyiana. Usiweke vinyongo tena ukajua unamkomoa mana unavyonuna ndo mchepuko unavopata chance ya kuwasiliana na si kila mwanaume anamchepuko wengine washkaji tu sasa ukijitia umenuna kisa umemuona kachat, sijui umekuta meseji sijui nini utakonda uzikwe na presha na unavyotiwa kaburini tu huku wenzio wanamtext pole kazi ya Mungu mpenzi. Gangamala mtoto wa kike sio kidogo kununa kama unga wa ngano ulokosa amira. Tabasamu njia nzuri na sahihi ya kumuua mtu akikosea ukatabasamu ataanza kutafuta mchawi kumbe mchawi mwenyewe, ataanza kutoka kujua kwanini hujakasirika atatulia tu akiamini anakuvizia kumbe anajivizia. ... Read More
MWANAUME ANAPOSEMA HATAKI KUKUOA: MWAMINI  Naandika hii makala kwa sababu nimekutana na maswali mengi ambayo yanaumiza wanawake wengi. Swali linakuwa hivi. Nimekuwa na huyu mwanaume kwa muda mrefu na tumekuwa tukishirikiana mambo mengi. Sijawahi kuwa na hisia kama nilizo nazo kwa mwanaume huyu kwa mtu yeyote. Na nilijua tutakuwa pamoja maisha yetu yote. Tatizo ni kwamba anasema hataki kunioa? Nitafanyaje ili aweze kujua kuwa nampenda na tunaendana vizuri pamoja na tunatakiwa tuoane? Wanaume wengi huwa wanaogopa kuweka ahadi kama hawana uhakika na upendo walio nao kwa mwanamke. Semeni ukweli wanaume. Je ameongelea kuhusu maisha ya baadae? Kuna mpango gani? Ni rahisi kubadilisha mwanaume? Unawezaje kumlazimisha akuoe? Kitu gani cha kufanya kama amesema hawezi kukuoa? Kama amesema hatakuoa, Mwamini . Elewa. Najua tayari jibu umepata kwenye maandiko yangu ya juu, lakini napenda kurudia, huwezi kumlazimisha mwanaume akuoe kama amesema hataki kukuoa. Hataweza. Sasa basi sisemi kama haiwezekani kweli. Kuna wanaume ambao husema hawatakuoa na hubadili mawazo yao na kuamua kuoa mwanamke ambaye alikuwa hapendi kumuoa. Lipo hilo. Mwanaume anayesema hatakuoa na wakati anaishi na wewe, mara nyingi anakupotezea muda na atakwenda kuoa mtu mwingine anayempenda kuliko wewe. Tuangalie kwa nini iko hivyo. Ina maana gani anapokuwa anaongea kuhusu kuchukia ndoa Aina ya mwanaume ambaye atakuambia hatakuoa ni yule ambaye anachukizwa na taasisi ya ndoa au sheria yake. Mwanaume huyo hafikirii kama wazo la kuoa ni zuri kwa kila mtu- anaona hata wanandoa ambao wako pamoja hawaonyeshi kama wana upendo wa kutosha, hawana upendo wa kweli ( anaweza kuwa haamini hata kama kuna upendo) Anafikiria hata kama ataona, mbona ndoa nyingi hazifiki mwisho, au mbona ugomvi ndani ya ndoa hauishi. Vyovyote vile , kwa sababu zozote zile, lakini mwanaume huyu anaonyesha kuchukia taasisi ya ndoa, na hataki kuingia huko, ndio maana hataki kuoa. Kama utasikia akisema hivyo mwamini. Haonyeshi kama atatafuta mwingine ambaye ataweza kubadili mawazo yake kuhusu kuoa.hata kama mnakaa pamoja na mnapendana sana , lakini hatafunga ndoa. Ina Maana Gani Anaposema Muda Wa kuoa Bado. Huyu ni aina nyingine tena.Anasema muda bado, anakuwa na sababu nyingi.Kama hali yake ya maisha haijakaa sawa, hajajenga nyumba, hana gari, na sababu kibao. Mwanaume huyu hana tatizo katika kuoa , Ila wakati bado , hataweza kuoa wakati unaotaka wewe, hata kwa sababu zipi hataweza. Unachotakiwa kufanya ni kumwamini anachokisema. Sababu zake hazina msingi. Kitu cha msingi ni Ukweli anaokuambia.Inaumiza lakini ndio ukweli.Inavunja moyo lakini ndio ukweli, Amini hilo na itaokoa muda wa kwako kusubiri.Na wakati huo huo utakuwa unafanya maamuzi ya kusubiri, kukubali jinsi ilivyo. Lakini kumbuka kuwa ndoa ni kitu cha muhimu sana. Wanaume wanaosema hawataoa huongea ukweli.Kama anakuambia hatakuoa Amini tu. Wanaume wanajua ni mwanamke wa aina gani atakayeishi nae maisha yake yote, uwe makini asije akawa anakutumia huku ana mipango yake .Yapo mambo wanaume huyapenda kwa mwanamke, vile vile yapo mambo ambayo wanawake wanapenda kwa mwanaume. Kama unaona unamlazimisha jambo fulani hataki , kuwa makini. ... Read More
NIFANYE NINI ILI MUME WANGU AWE NA HAMU NAMI?  Mume wangu anasema ananipenda sana, nami nampenda sana. Tuna watoto wawili wa kiume. Nimejaribu kila kitu cha kumfurahisha, kama vile kuvaa vizuri, kuandaa chakula kizuri akipendacho na kinywaji lakini Lakini mwenzangu haonekani kuridhishwa na jitihada zangu. Baada ya chakula cha usiku huwa tunakaa na kuangalia Luninga huku tukiwa na vinywaji. Lakini cha ajabu nikimsogelea na kutaka niwe karibu naye ananiepuka. Yaani HATAKI hata nimguse ni kama NINANUKA au ninamsumbua vile. Je, tatizo ni nini hasa, Je nanuka? Najiuliza na jibu sipati….Alimalizia kusema huyu mama huko chozi likimdondoka…...... Naam mara nyingi hivyo ndivyo inavyokuwa kwa sisi wanawake pale tukutanapo, si jambo geni sana kwa sisi wanawake kushirikiana kihisia. Ni jambo la kawaida kabisa kukuta mwanamke akimsimulia shoga yake anayemuamini juu ya madhila yake. Yote hiyo ni katika kutafuta nafuu na kuondokana na msongo wa mawazo. Mara nyingi simulizi nyingi zinazowakutanisha wanawake ni zile zinazohusiana na mambo ya Ndoa, mahusiano, watoto au mambo ya kifamilia kwa ujumla, mara nyingi tunatamani kupata mahali pa kulinganishia, ili kutaka kujua kama tatizo nililo nalo lina ukubwa kiasi gani. Ni hivi majuzi nikiwa kazini na mfanyakazi mwenzangu ndipo aliponieleza kile kinachomsibu kwa muda mrefu sasa, inavyoonekana, ni jambo ambalo alikaa nalo muda mrefu akijaribu kupambana nalo kimya kimya huku likiendelea kumtafuna, dada huyu wa Kiswidish. Ili kujiridhisha na kutaka kujua ukweli halisi nikamuuliza kama amemuuliza mume wake jambo hili akajibu amefanya hivyo na jawabu alilolipata ni kwamba, mume wake huwa anachoka. Yaani kazi zake ni nyingi pia malezi ya watoto yanamchosha. Nikamuuliza kama hawawezi wakati wa wikiendi watoke ili kuwa peke yao? Hapo nikapata jibu ambalo sikutegemea. Alidai kwamba akisema hivyo mume wake anaona kama yeye anaamua nini wafanye. Huyu mama akaendelea kusema, mimi ni binadamu Yasinta.,,,,,,,,,, Na nahitaji tendo la ndoa na sitaki kutoka nje kwani nampenda sana mume wangu. Nami sikuachia hapo kama mnavyonifahamu na u-Kapulya wangu nikamuuliza kama tatizo hilo lina muda gani au limeanza siku za karibuni? Mama yule akashusha pumzi, akaniangalia kwa jicho la huzuni, kisha akajibu kuwa inatokea wanafanya tendo la ndoa mara moja kwa mwezi na hapo ni ile ya haraka haraka na halafu baada ya hapo mume wake anampa mgongo na kulala . Hapo….akasita kidogo …nikamuuliza ulitaka kusema nini? Akaendelea unajua Yasinta mwanamke anahitaji kuandaliwa kwanza, mimi huwa siandaliwi kabisa........ Mweh! Nikaona makubwa haya ......nilikosa Jawabu la kumpa kwa kweli, nikabaki kuguna tu. Hata hivyo nilijaribu kumshauri aende kwa washauri nasaha wa masuala ya Ndoa na mahusiano, lakini akadai kuwa mumewe ni mkaidi na hawezi kukubali. Mwenzenu swala hili limenishinda maana sijui nimsaidieje! Je Wewe kama msomaji unaweza kunisaidia ni ushauri gani nimpe mama huyu, ili awe na furaha katika Maisha ya ndoa yake? Ushauri tafadhali........... ... Read More
SABABU YA KWELI WANAWAKE KUENDELEA KUTEMBEA NA WANAUME WALIO OA  Jane ni mwanamke mwenye mafanikio, anamiliki kampuni ya kutengeneza mifuko ya plastic, ana studio. Ana akili , anavutia na ni mwenye ujasiri. Pia anatembea na mume wa mtu. Amekuwa akiwauliza rafiki , familia yake ambao wanafahamu kuwa kitu gani kinamfanya mwanamke mwenye mafanikio, akili na ujasiri kutembea na mume wa mtu kwa miaka zaidi ya mitatu? Hamu ndio Inayoanza Mwanaume ambaye ameoa anapomkaribia mwanamke , anakuwa na hatari— hatari ambayo inaonyesha kumuhitaji zaidi. Kuwa na muda naye. Huenda kwa meseji au kupata chakula pamoja kwa siri, au kulala nae kwa siri. Huonyesha kuwa na majukumu kama mwanaume single. Lakini mwanaume single huandaa date. Huwa na sababu nyingi za kufanya hivyo, na ukiri wao huwa ni wa makini na huonyesha kuwa hawako interested. Hujikuta wameingia kwenye majukumu ambayo hakuwa amejiandaa. Kwa ushindani, kazi ya mwanaume aliyeoa Inamlinda kutokana na nia yake kwa mwanamke single ili kuonyesha hamu yake. Kama hataweza kuonyesha hisia zake kwa kumtazama macho yake, sauti yake, kumsugua mwanamke mgongo wake, kumfanyia massage kwenye mabega, mwanamke atajuaje kama anamtaka? Na ataendeleaje kubaki nae kama hamtimizii haja zake? Kwa kufanya hayo anaweza kumuwekea ulinzi, mahusiano yao kukomaa na kuwa mazuri na kuwa ya kawaida. Lakini akili Itakuja. Marafiki aliowaambia watamkumbusha.Ni mume wa mtu. Familia watamuuliza , bado yuko na mke wake? Wakati anapoanza kujiuliza ndani yake , mume alienae, Ataanza kuwa na njia mbili. Kwa wanawake wengi, hio imepitwa na wakati. Kwa wengine mchezo utaendelea—kwa kufahamu maamuzi haya…tuangalie sasa 1.Wakati mwanaume anapotoka nje, uwezekano mkubwa hana furaha ndani ya nyumba yake. 2Talaka zinaongezeka . ndoa zinafikia mwisho, na wanaume wanaoa tena. 3.Uzinzi unaongezeka kwa wanaume. Huenda kuishi muda mrefu peke yao sio mpango mzuri. Kwa mtu kama Jane kuishi maisha kama hayo, huenda ni katika kumpata mtu sahihi na kumuondoa kwa mke wake hata kama kutakuwepo hatari katika hisia zake. Mwanamke kama Jane ni wepesi wa kujifunza zaidi kuhusu tabia za wanaume ambao wanacheat kabla ya kuamua kuingia kwenye mahusiano ya kudumu. Wengi wa wanaume wanasema , sababu kubwa ya kucheat ni kukosa sex Ni kiasi kidogo sana cha wanaume ambao hupotea katika mapenzi ya nje Baadhi ya wanaume wanaocheat walitoa taarifa kuwa wanafanya hivyo kwa wenza wengi karibu miaka yote Kwa kulinganisha wanawake na wanaume. Wanawake wao huingia kwenye mahusiano kwa mwanaume aliyeoa kwa sababu ya kuwapenda. Lakini sio nzuri kama mtu ameoa ni bora kujiheshimu na kumuheshimu mke wake , Na kama kuna tatizo ni vizuri kurekebisha kuliko kwenda kutafuta majibu ya tatizo lako nje.Kwa nini nasema hivi , ni kwa sababu ipo siku mwanamke huyo atahitaji kuwekwa wazi , utafanyaje na wewe ulikuwa ni mwizi. kwa upande wa mwanamke Utavunjika moyo, inapofika wakati kama huo.Maumivu ya kuachwa na mwanaume aliyeoa ni makubwa kuliko ya kuachwa na mwenza ambaye ni wako kabisa. Black woman hugging her knees 1.Utajisikia kama mkosaji mara mbili. Kwamba hukuweza kumpata mtu ambaye tayari kwanza alikuwa ameoa na amekuacha baada ya kuridhika kwake. 2.Wasaliti wanaokatiza mahusiano huwa wanaonyesha kabisa kuwa hawana hisiana za kutosha kwako. Wanakuchukulia kama wewe ni msichana mkubwa, na unaelewa kitu gani unachokifanya. 4.Mfumo unaompa support unaweza ukawa upo gizani. HUenda ni aibu au hamu ya kumlinda msaliti au vyote. Hakuna mtu ambaye anafahamu. Kama wapo basi ni wa katibu sana. Kwa hio watu kama Jane wataepuka vipi hatari inayotokana na aina hii ya mahusiano? Ukweli ni kwamba, ufahamu una nguvu.Kama msomaji unahusika na mume wa mtu, rudia tena kusoma makala hii kwa makini kabla hujaendelea zaidi. Maisha ni mafupi.Muda wa kumsaidia mume wa mtu ambaye amekosa kitu fulani kwa mwenza wake umekwisha. Mwache akatengeneze kwa mwenza wake. Wanaume Single wako wengi wanakusubiri na hawana hatari kama hizo. Hata kama atakuonyesha kuwa wako cool mwanzoni usidanganyike. ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: