Home → ushauri
→ Hivi Mungu Aliweka Nini Kwenye Ubongo wa Mwanamke?
Am just thinking loudly.
siku mbili zilizopita nilisafiri kwa shughuli za kiofisi. Kama mjuavyo mambo ya serikali yetu hii, unajaza imprest, hela ya safari inachelewa kutoka, au unaweza kulipwa hata baada ya wiki au mwezi tangu urudi toka safari. Sasa mimi ndo yakanikuta. Ikabidi nijiongeze tu ili kuokoa ratiba zangu. Na kumbuka ni tarehe za karibia na mishahara. Nikaacha hela ya mahitaji, nikasisitiza kuwa tusifanye manunuzi yasiyo ya lazima kwa sababu tuko kwenye ujenzi na mafundi hivi wanatudai, hivyo mshahara ukitoka tu tuwalipe. Leo ndo nimerudi kutoka safarini na leo ndo mshahara umetoka. Nilikuwa nimechoka sana leo. Asubuhi nilikunywa kikombe cha maziwa na maandazi mawili, nikashinda nayo njia nzima mpaka nimefika home mida ya saa kumi na nusu. Tangu asubuhi nilijihisi siko vizuri kichwa kinaniuma, najisikia kuchoka. Nikiwa nimekaribia home nikampigia wife kuwa nakaribia kufika. Nashukuru nilifika salama. Njiani nikanunua vitu mbalimbali kama matunda na mboga.
Sasa kilichonifanya niwaze sana kuhusu hawa viumbe wanawake, nilipofika nilisalimia walio nje, then nikaingia ndani. Nikamkuta yuko chumbani amelala. Baada ya salamu, nikarudi nje binti wa kazi alikuwa anaosha vyombo. Nikakaa sebuleni kama dakika 10 nikaona hakuna anayekuja siyo yeye wala msichana. Nikachukua glasi nikanywa maji, nikarudi kukaa kwenye sofa. Nikaona watu wako bize na ratiba zao, Nikatoka nje binti bado anaosha vyombo. Nikarudi ndani chumbani. Nilipoingia nilikutana na swali, "mshahara wako umetoka?"Nikajibu ndiyo. Akasema "hata mimi wa kwangu umetoka, sasa naomba niongezee laki mbili niende mjini sasa hivi kuna nguo nataka nikanunue".
Niliwaza tuu haraka hata sijapewa maji ya kunywa, wala sijaoga niko na jasho la safari, hata sijapumzika, kichwa kinaniuma, njaa inaniuma (maana huwa sipendi sana kula hovyo hovyo njiani), hata hajaniuliza safari ilikuwaje; Nilijisikia kizunguzungu flani cha ghafla, nikatoka nikafunga mlango, nikaondoka zangu nikawasha gari kwenda mjini kutafuta sehemu ya kupumzika walau nipate hata uji au supu nipashe tumbo.
Mpaka sasa sijarudi nyumbani, nasubiria muda uende nikifika naoga nalala tuu. Inaniuma sana, hivi vitendo siyo mara ya kwanza. Mpaka sasa ana masanduku matatu makubwa yote yamejaa nguo zake bado anaona hana nguo, eee Mungu uwarehemu hawa viumbe. Mimi nawaza tumalizie ujenzi tuachane na nyumba ya kupanga, yeye wala haoni kama kuna shida. Alafu sisi wanaume tukichepuka tunalaumiwa sana na hawa wanawake kuwa tunatelekeza familia. Anyway, nafikiria kitakachotokea nikirudi nyumbani
Hivi Mungu Aliweka Nini Kwenye Ubongo wa Mwanamke? Am just thinking loudly. siku mbili zilizopita nilisafiri kwa shughuli za kiofisi. Kama mjuavyo mambo ya serikali yetu hii, unajaza imprest, hela ya safari inachelewa kutoka, au unaweza kulipwa hata baada ya wiki au mwezi tangu urudi toka safari. Sasa mimi ndo yakanikuta. Ikabidi nijiongeze tu ili kuokoa ratiba zangu. Na kumbuka ni tarehe za karibia na mishahara. Nikaacha hela ya mahitaji, nikasisitiza kuwa tusifanye manunuzi yasiyo ya lazima kwa sababu tuko kwenye ujenzi na mafundi hivi wanatudai, hivyo mshahara ukitoka tu tuwalipe. Leo ndo nimerudi kutoka safarini na leo ndo mshahara umetoka. Nilikuwa nimechoka sana leo. Asubuhi nilikunywa kikombe cha maziwa na maandazi mawili, nikashinda nayo njia nzima mpaka nimefika home mida ya saa kumi na nusu. Tangu asubuhi nilijihisi siko vizuri kichwa kinaniuma, najisikia kuchoka. Nikiwa nimekaribia home nikampigia wife kuwa nakaribia kufika. Nashukuru nilifika salama. Njiani nikanunua vitu mbalimbali kama matunda na mboga. Sasa kilichonifanya niwaze sana kuhusu hawa viumbe wanawake, nilipofika nilisalimia walio nje, then nikaingia ndani. Nikamkuta yuko chumbani amelala. Baada ya salamu, nikarudi nje binti wa kazi alikuwa anaosha vyombo. Nikakaa sebuleni kama dakika 10 nikaona hakuna anayekuja siyo yeye wala msichana. Nikachukua glasi nikanywa maji, nikarudi kukaa kwenye sofa. Nikaona watu wako bize na ratiba zao, Nikatoka nje binti bado anaosha vyombo. Nikarudi ndani chumbani. Nilipoingia nilikutana na swali, "mshahara wako umetoka?"Nikajibu ndiyo. Akasema "hata mimi wa kwangu umetoka, sasa naomba niongezee laki mbili niende mjini sasa hivi kuna nguo nataka nikanunue". Niliwaza tuu haraka hata sijapewa maji ya kunywa, wala sijaoga niko na jasho la safari, hata sijapumzika, kichwa kinaniuma, njaa inaniuma (maana huwa sipendi sana kula hovyo hovyo njiani), hata hajaniuliza safari ilikuwaje; Nilijisikia kizunguzungu flani cha ghafla, nikatoka nikafunga mlango, nikaondoka zangu nikawasha gari kwenda mjini kutafuta sehemu ya kupumzika walau nipate hata uji au supu nipashe tumbo. Mpaka sasa sijarudi nyumbani, nasubiria muda uende nikifika naoga nalala tuu. Inaniuma sana, hivi vitendo siyo mara ya kwanza. Mpaka sasa ana masanduku matatu makubwa yote yamejaa nguo zake bado anaona hana nguo, eee Mungu uwarehemu hawa viumbe. Mimi nawaza tumalizie ujenzi tuachane na nyumba ya kupanga, yeye wala haoni kama kuna shida. Alafu sisi wanaume tukichepuka tunalaumiwa sana na hawa wanawake kuwa tunatelekeza familia. Anyway, nafikiria kitakachotokea nikirudi nyumbani
Artikel Terkait
Kwa Wanawake tu..Fahamu Mbinu Kuntu za Kummaliza Mumeo Ndani ya Sita kwa Sita Hadi Akapagawa   Weekend hii nimeona ni vyema tuzungumzie kidogo kuhusu masualaya mahusiano pia kutokana na sekta hiyo kuwa na umuhimu wake pia katika maisha ya mwanadamu. Katika masuala haya ya mapenzi nimeona ni vyema niaanze kuongea na wanawake kuhusu namna ya kuweza kufanikisha kummaliza mwanaume katika sita kwa sita. Jambo la kwanza wanamke unapaswa kuwa jasari na mwenye kuamini katika kile unachofanya katika mapenzi, ambapo wewe mwanamke unatakiwa mkishafika katika uwanja wenu wa zoezi husika katika sikiu hiyo, Hakikisha unajitahidi wewe kuanza kumvua nguo mwanaume, huku ukimshika baadhi ya sehemu mbalimbali za mwili wake ambazo unaamini zitamsababishia msisimko mkubwa. Baada ya zoezi hilo nawe pia (mwanamke)unaweza kutoa nguo zako kisha mkumbatie mmeo , huku mkigusanisha ngozi za miili yenu. Tambua ya kwamba ngozi huwa na mishipa midogo midogo yenye ufahamu ambayo hutoa taarifa mbalimbali za mwili kwenye ubongo, hivyo kitendo cha miili yenu kugusana huchangia kuibua hisia za kimapenzi zaidi. Unapoona tayari mwanaume yupo tayari katika hali ya hisia kali za kimapenzi kabla ya kumruhusu akuingilie unaweza kuendelea kumshika baadhi ya sehemu za mwili mfano ndevu, sehemu zake za siri na mkune kwenye viganja vyake na mapaja na nk. Fahamu ya kwamba mapaja ya mwanaume huwa na hisia kali, hivyo unaweza kuyashika zaidi kwa ustadi mkubwa, huku ukitumia vidole vyako na utaona akisisimka zaidi. Sehemu nyingine ambayo itakusaidia wewe mwanamke kuweza kumsisimua vizuri mwanaume ni kwa kumshika maeneo ya kifuani kuelekea tumboni maeneo hayo huwa na msisimko mkubwa kwa wanaume walio wengi. Eneo jingine lenye hazina kubwa na ya msisimko wa mapenzi kwa wanaume ni sehemu ya uume ambapo mwanamke huweza kushika ile sehemu ya mbele (kichwa cha uume) ambapo humfanya mwanaume kupata msisimko wa kimapenzi kwa haraka zaidi. Uwapo katikati ya tendo hakikisha unkuwa serious na zoezi hilo, huku ukijitahidi kuepuka kucheka kwa jambo lolote lile hata pale mwenzi wako anapotoa sauti za kufurahisha wakati wa katikati ya tendo. Pamoja na hayo, mwanamke uwapo katikati tendo hilo na mwenzi wako jitahii sana kujiachia maungo yako kwa mmeo, kwani kwenye tendo hilo la ndoa huwa hakuna uheshimiwa hivyo ni vyema ukajiachia. Katika tendo la ndoa pia sauti na maneno ya kimahaba ni muhimu sana wakati wa tendo la ndoa kwani huongeza hamasa katika tendo hilo. Baada ya kumaliza tendo hilo kumbuka kusema asante na mpe pole mwenzi wako kwa kazi pevu, kisha chukuwa kitambaa na mkaushe kijasho cha utamu wa penzi kwa taulo uliloandaa maalum. ... Read More
UMESOMA HADITHI NYINGI ZA MAPENZI, LAKINI HII ITAKUSISIMUA KULIKO ZOTE, UTATUMIA DAKIKA 2 KUSOMA LAKINI...  1st year nikiwa nimekaa leacture room nikimuangalia msichana aliyekaribu yangu,niliyekuwa nikimuita "Bestfriend"nilikuwa nikimuangalia nywele zake nzuri na sura yake ya upole huku nikitamani awe wangu,lakini yeye hakuwa akitamani hilo na nilikuwa nikilitambua hilo. Baada ya leacture,alikuja kwangu na kuniomba notes za siku ya nyuma kwa sababu hakuweza kuingia darasani hiyo siku iliyopita.baada ya kumpa akasema "asante" na kushikana mikono na mimi.I wanted to tell her,i want her to know that i don't want us to be just friends,i love her but i'm just to shy,and i don't know why 2nd year Simu yangu iliita,kupokea alikuwa yeye alikuwa akilia akinielezea jinsi gani boyfriend wake broke her heart,she asked me to come over because she didn't want to be alone,kwa kuwa ni rafiki yangu kipenzi ilinibidi kwenda kumfariji,as i sat next to her on the sofa,nilikuwa nikimuangalia Machoni nikitamani awe wangu.Baada ya masaa mawili baada ya kuangalia nae movie mbili tatu na kula nae chakula pamoja akarudi katika hali yake ya kawaida,hivyo akaamua kwenda kulala,before akaniangalia na kuniambia "asante" na kunipa tabasamu tamu,i want to tell her to know that i don't us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why. 3rd year Siku moja kabla ya Tamasha la muziki chuoni alikuja kwenye meza yangu leacture room na kuniambia "Boyfriend wangu amepata udhuru hivyo naomba unipe campan katika tamasha la muziki leo usiku" kwa kuwa tuliwekeana promice kwamba ikitokea kila mmoja wetu amekosa mtu wa ku-date nae basi tutaenda pamoja just as "bestfriends".hivyo tukaenda. katika tamasha baada ya kila kitu kuisha na muziki kufungwa,nilikuwa nimekaa nje ya ukumbi nikimuangalia jinsi alivyokuwa akicheka na rafiki zake,she saw me looking to her she smiled at me,i want her to be mine lakini yeye alikuwa hafikirii hilo kabisa na nilikuwa nikilitambua hilo,then she said to me "nimekuwa na muda mzuri na wewe asante sana" and she gave me a sweet smile.I want to tell her to know that i don't us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why. Graduation Day siku,wiki kisha mwezi ukapita ilikuwa ni mahafali yetu tukimaliza masomo ya chuo,akiinuka kwenda kutunukiwa shahada yake ya uchumi nilikuwa nikimuangalia akiwa amependeza sana siku ile,i wanted her to be mine,but she didn't notice me like that,and i knew it. kabla watu hawajatawanyika kwenda makwao,alikuja kwangu akiwa na vazi lake la mahafali,na kulia pale nilipomkumbatia akainua kichwa chake na kuniambia "you are my bestfriend asante sana" i want to tell her to know that i don't us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why. Miaka michache baadae Nikiwa kanisani Yule Msichana akiwa anaolewa sasa,nilimuangalia akisema "ndiyo nakubali " and drive off to new life,kaolewa na mwanaume mwingine,i wanted her to be mine,but she didn't see me like that,and i knew it. but before she drove away,alikuja kwangu na kusema "asante sana" and kissed me on the cheek.I want to tell her to know that i dont us to be just friends,i love her but i'm just too shy,and i dont know why. Kwenye Mazishi Miaka ilipita i looked down katika jeneza lilokuwa na msichna ambaye alikuwa ni "bestfriend" wangu,Katika Service ya mazishi wakasoma diary ya Bestfriend ambayo alikuwa akiiandika enzi za maisha ya chuo' Diary yake ilikuwa Ilikuwa ikisomeka hivi I stare at him napenda awe wangu,but he doesn't notice me like that,and i know it,i want to tell him,i want him to know that i dont want us to be just friends,i love him but i'm just to shy,and i dont know why.I wish he would tell me he loved me! Nilipiga magoti huku nikilia nikijisemea moyoni i wish ningemwambia tu ukweli,nimeshachelewa sipo nae tena katangulia mbele za haki i cried!! Vunja ukimya ... Read More
AINA 10 ZA WANAUME AMBAO WANAWAKE HUJUTIA WAKIWA NAO  1. Wanaojiona Kama Wafalme (King Husband). HIi ni aina ya wanaume ambao hutaka kusujudiwa kama wafalme na hupenda kuwafanya wake zao kuwa kama watumwa. Hawafanyi chochote ndani ya nyumba kazi yao ni kutumatuma hata kama mke anaumwa atapaswa kuamka na kupika, wanataka waheshimiwe wao tu na mwanamke akikosea kidogo ni maneno au kipigo. Mwanamke hana kauli ndani na mume akiingia nyumbani ni kama bosi anavyoingia ofisini, wote kimya hakuna hata kuongea. 2. Wanaume Wanaojihisi Bado Hawajaoa (Bachelor Husband). Hii ni aina ya wanaume ambao hawawashirikishi wake zao kwa chochote. Hufanya mambo kama vile bado hawajaoa, hutumia muda wao mwingi na marafiki zao wakifanya mambo ambayo mke hata hayajui mke anaweza kustukizia tu mume kanunua gari bila kumshirikisha na mume haonyeshi hata kujali kuweza kumshirikisha. Hajali kama ana mke na mda mwingi huutumia akiwa na marafiki kufanya mambo yasiyo na msingi ambayo hayana mnanufaa yoyote katika ndoa yake. 3. Wanaume Wenye Gubu (Acidic Husband). Hawa hukasirika kila mara tena bila kua na sababu ya misngi, mambo hayaishi, kosa la mwaka juzi anaweza kukukasirikia leo. Wamemuudhi kazini hataki kusemeshwa na mnanuniwa nyinyi, mwanamke akiomba hela ya chakula ni shida ni kununa kutwa nzima, wanahasira na nirahisi kumpiga mke. 4. Mume Wa Kila Mtu (Genarel Husband). Hawa wanajifanya wasamaria wema, wanajali kila mwanamke, wanajali marafiki wakike wa mke na wakwao kuliko wanavyowajali wake zao. Mke anaweza kuwa na shida akasema hana hela lakini rafiki akampa. Wana marafiki wengi wakike na mara nyingi huwa hawaachani kabisa na ma X wao, wakiwalalamikia wanawasaidia kuliko hata wanavyowasidia wake zao wakati wakiwa na shida. 5. Wanaume Wanaojifanya Wagumu (Dry Husband). Hawa wanajifanya wagumu sana, hawana yale mambo ya kimahaba na wao hujua kuwa ndoa ni kuleta chakula tu na kushughulika kitandani. Hakuna kuongea na hawajali hata hisia za mke, mke akiongea kwao wala hawajali wanajifanya ni vidume sana na wanaona mambo kama vizawadi, kupiga simu, kutuma sms, kusema nakupenda, kununua maua ni mambo ya kike, yaani hawaonyeshi juhudi yoyote kuwafurahisha wekea zao. 6. Wanaume Wanaopenda Kutumia Wake Zao (Panadol Husband). Hawa huwa wanaume pale tu wanapokuwa na shida, wanakuwa na wake wazuri wanaowajali lakini wao wala hawajali. Wanapomhitaji mwanamke, wanapotaka mwanamke awafanyie kitu flani basi huja na maneno mazuri na hata kuleta vizawadi, wanajua udhauifu wa wake zao na huutumia kuwalaghai kuwatimizia mahitaji yao lakini wanapotimiziwa tu basi husahau hata kama wanawake, hawajali tena. 7. Wanaume Ambao Hawataki Kukua (Baby Husband). Bado wanatabia za kitoto, hawawezi kufanya maamuzi yao wenyewe mpaka kuuliza kwa ndugu zao, mtu kaoa lakini kila siku humpigia simu Mama yake kuuliza hiki na kile. Yaani wakiongea kitu na mke nilazima aulize ndugu kwanza ndiyo kipitishwa na mke akifanya kosaa kidogo kazi nikulinganisha mke na ndugu zake, mbona flani alifanya hivi, flani anaweza fanya zaidi na mambo kama hayo. Kwakifupi hawawezi kufanya maamuzi na mkewe, ndugu zake hasa Mama yake anakuwa kama shemeu ya ndoa. 8. Mume Mtalii (Visiting Husband). Hawa wanakuja nyumbani kama wageni vile, mume ataihudumia familia yake kwa kila kitu lakini hawezi kuipa muda wake. Akirudi mke na watoto wamelala ni kugonga na hana sababu za msingi za kuchelewa, hata mwisho wawiki hupenda kutumia na marafiki au ndugu lakini si na mke. Hakuna kitu cha pamoja ambacho anafanya na mkewe au watoto wake, kila akiingia tu anakua na safari ya kutoka yaani hata atoke akakae nnje tu lakini si kukaa na mke au watoto. 9. Wanaume Wanaofuatilia Kila Kitu (Stalking Husband). Hii ni aina ya wanaume ambao hufuatilia kila kitu, huchunguza kila kitu mwanamke anachofanya na hawampi pumzi. Akienda sehemu atachunguza anaenda na nani na alikutana na nani, huwa na wivu wa ajabu ajabu na kila saa huhisi wake zao ni wasaliti. Kila mtu mwanamke anayeongea naye wa jinsia tofauti huhisi ni mchepuko na hata marafiki wa mke wakike pia huhisi wanamkuwadia, kwakifupi hampi pumzi mwanamke. 10. Mwanaume Mbahili (Miserly Husband). Huyu anaweza kuwa na hela lakini mbahili ajabu. Akimpa mwanamke hela atafuatilia matumizi yake mpaka senti ya mwisho, anafuatilia mpaka mambo ya jikoni. Sukari ikiisha naataka ajue iliisha ishaje na kila mara huhisi mke anamuibia hela labda akajenge kwao, huwa msumbufu sana na mgumu kutoa hela. Mwanamke akifikiria mchakato wa kuomba hela kwa mume hukata tamaa na wakati mwingine kuamua tu kukaa kimya na matatizo yake. ... Read More
NI JINSI GANI UNAMWOMBA MPENZIO MSAMAHA, JE NI KWA KUMPA ZAWADI? Msamaha una nafasi kubwa sana katika mapenzi. Hamna mtu aliyemkamilifu ndiyo maana neno samahani lipo. Ila neno hili linaweza kutumika sahihi au isiwe sahihi. Hivyo ni vizuri ukawa makini katika matumizi ya neno hili. Kuna baadhi ya watu hawawezi kabisa kutamka hilo neno na badala yake hutumia maneno yafuatayo (mbadala) kama ; yaishe,basi samahani,umeshinda,sorry(kama njia yakupunguza makali na wakati lugha iliyokua ikitumika ni kiswahili). Jinsi yakutumia samahani kiusahihi Unapotoa samahani kutoka katika kilindi cha moyo wako ina maana sana zaidi ya chochote. Samahani itumike tu pale unapotenda kosa moja kwa mara ya kwanza, hapo ni rahisi kusamehewa na kuaminiwa zaidi.Heshima, pendo na mapenzi yatakuwa kama awali na utaheshimika nakuonekana unajali. Hakikisha hauombi samahani zaidi ya mara moja kwa kosa moja ndo mana wanasema, “kosa sio kosa ila ukirudia kosa ndio kosa’’. Kama ulikua haufahamu ni vizuri ujifunze na ikiwezekana rudisha kumbukumbu zako katika matukio yanayohitaji msamaha kwenda kwa mpenzi wako na ulinganishe na hatua ulizozifanya. Kiri kosa ndiyo msamaha wako uweze kukubalika.Usiombe msamaha huku unasema lakinii…… ila……. Siamini kama haya yangetoa……… aina hizi za midokezo inapotumika katika kuomba msamaha ujue unataka kuonesha ulichokifanya sio kosa… Its simple, admit your mistake for the heartest forgiviness .Utapelekea upande wa pili (uliokosewa kukuamini tena na ni rahisi kusamehe na kusahau) tofauti na kuwa na maneno meeengi yakujitetea ilihali umetenda kosa. Sasa nije kwenye suala la zawadi, Jamani zawadi isiwe ndiyo silaha ya kudai msamaha. Zawadi inatumika wakati wowote kuimarisha mapenzi kwa kuonesha unamjali mwenzi wako nakumfanya ahisi faraja wakati wote na uwepo wake katika maisha yako. Epuka tabia ya kutoa sana zawadi wakati unamplease mpenzi wako.Kwa wakati mwingine utamjengea fikra za kosa pindi tu unapomletea zawadi. Hivyo asiifurahie ile zawadi na badala yake atakua na shauku kufahamu msamaha wa siku hiyo ni wa kitu gani au umetenda kosa gani tena. Wakati mwingine zawadi inapotumika katika kuomba msamaha itakua ni kama KUMBUKUMBU YA KOSA ulilomfanyia mwenzi wako, hivyo kumfanya akumbuke mara kwa mara kosa ulilolifanya. Kuwa makini sana katika njia za kuomba msamaha. Njia nzuri ya kuomba msamaha na ukubaliwe kwa upesi Kubali kosa pale ambapo umetenda,(note; Usikiri kosa kwa sababu tu unampenda na hutaki kumpoteza ,au hutaki malumbano. Ukifanya hivo ndo unaweza haribu uhusiano wako kabisa) Badili mazingira ya maongezi yaani tofauti na eneo la nyumbani/mlilozoea kukaa Omba msamaha wakati hasira zimepungua na ukiwa sio mlevi (hasa kwa wale wenye hasira au wanywaji wa pombe) Usilazimishe kusamehewa ,yaani mwenzako anapokua haridhii tumia njia nyingine mfano kumshirikisha mtu wenu wa karibu saana (kwa wote wawili) ila hapa uwe makini kwa sababu sio wote wanapenda siri zao za uhusiano kujulikana na wengine.Hapa itategemea na jinsi mlivyo Anayeomba msamaha ahakikishe sio mtu wa kukumbuka makosa ya mwenzie yaliyofanyika kipindi cha nyuma.Hapa na maanisha wale wenye tabia yakusamehe wenzao ila niwakukumbuka, endapo atakosewa kwa kitu kingine hata kwa bahati mbaya.Mfano akikosewa huwa ni mtu wakusema; ''hiyo ni kawaida yako'' that means anashikilia vitu moyoni.Itamuwia vigumu mwenzako kukubalia msamaha kwa urahisi, kutokana na tabia yakumshikilia bango kwa kumkumbusha yaliyopita endapo yeye atakukosea. Ni vizuri kujitahidi katika kufanya mambo mazuri kwenye uhusiano wako.Usitegemee zawadi kuwa ni kitu kizuri katika kuomba msamaha. Timiza malengo yako,jiheshimu,kuwa mwaminifu na kumthamini mwenzio na kumpenda kwa dhati. Bila kusahau kusikilizana na kufanya maamuzi kwa pamoja. ... Read More
JIFUNZE KUMTAMBUA MTU MWENYE MAPENZI YA DHATI NA WEWE: Unajua unaweza kuwa na mahusiano na mtu unayempenda sana ila yeye hakupendi kama vile umpendavyo lakini anashindwa kukwambia kuwa "sikupendi". Unawakati mzuri sana wa kumtambua mtu ambaye hakupendi na pia kumtambua anayekupenda. Vilevile kukubaliana na hali halisi. Watu wengi hawapendi kutambua kwamba mtu anayempenda yeye hampendi, kwasababu ni maumivu makubwa sana moyoni. Unapokuwa kwenye mahusiano na mtu huyo nae inamuwia vigumu kukwambia "sikupendi" hufanya hivi katika kuzihurumia hisia zako juu yake. MTU AMBAYE HAKUPENDI KWA DHATI: ==> Anapokuwa nawe inamuwia vigumu sana kukwambia neno NAKUPENDA mara kwa mara, utajikuta wewe ndio unakuwa mtumwa kwake kwa kumwambia nakupenda kila mara. Majibu yake baada ya neno hilo, mara nyingi atakwambia asante kwa kunipenda basi, na akikuhurumia sana atakwambia nakupenda pia ili kukuridhisha wewe na moyo wako. ==> Utajikuta una mawazo sana juu yake na kujiuliza "hivi kweli mtu huyu ananipenda?" Utajaribu kumuuliza, "je unanipenda?" Jibu lake kwanza litafikiriwa sana, sababu ya kufanya hivyo ni kwa vile anatambua kwamba hakupendi sasa kukwambia ukweli wa swali lako anahisi utaumia, kwahiyo baada ya swali hilo anaweza kukuuliza swali na wewe "kwani unaonaje?" kwavile unampenda sana utamjibu, "naona kuwa unanipenda" naye atakwambia "basi ndio hivyo". Mara nyingine baada ya wewe kumuuliza swali kuwa je anakupenda kweli, atakujibu "ukweli unaujua ila kwanini unapenda kuniuliza swali hilo kila mara?" kama umeshaingiza dosari juu ya upendo wake utajikuta unamuuliza "ukweli upi?" naye atakujibu "kuwa nakupenda", hapo utajikuta umepata furaha kugundua kuwa anakupenda kumbe mwenzio amekuhurumia tu. ==> Huwa hajali mambo yako unayomwambia, ukimueleza muda huu badae anajifanya kusahau ili tu akupotezee mueleleo. ==> Unapopanga kukutana nae huwa ni mtu asiyeishiwa na sababu za kushindwa kufika, huwa na aibu ya kukutambulisha kwa watu. Unaweza kufika nae mahali akakwambia kuwa "kuna watu wanafahamiana na mama/baba mahali hapa kwahiyo tusiongozane karibu", hapo anaweza yeye akatangulia mbele au kukuacha wewe utangulie. ==> Hufanya tabasamu la kuigiza au kicheko cha kejeli ili wewe uridhike kwamba anafurahishwa na uwepo wako kwake. ===> Wakati mwingine inampasa mtu kujitambua na kumpa uhuru huyo umpendaye aweze kuamua mwenyewe labda kuendelea na wewe au kumfata anayempenda yeye. Cha muhimu ni kuwa using'ang'anie mahusiano ambayo yanayoumiza moyo kwani yanaweza pasua moyo wako kwa mawazo. MTU ANAYEKUPENDA KWA DHATI: ==> Hachoki kukwambia NAKUPENDA, kwani anajisikia raha sana pale atamkapo neno hilo juu yako kwahiyo unaweza ukawa kama wimbo wake kwako. ==> Anajivunia kuwa na wewe na atapenda kukupa sifa nzuri kila mara, yani Hachoki kukusifia. Atakushauri pale unapokosea ili uwe katika njia nzuri. Unaponuna atajua cha kufanya ili wewe ufurahi na kurudi kwenye hali ya kawaida. ==> Hachoki kukuombea mema na kukutakia mafanikio. ==> Atapenda kukueleza ukweli kila mara ili uweze kujenga uaminifu na imani juu yake. ==> Wewe utakuwa ni mtu muhimu sana katika maisha yake, atakuthamini na kukujali. Tatizo lako litakuwa sawa na tatizo lake, atakupa ushauri bila kuchoka. ==> Kabla ya kumuuliza swali kuwa "je unanipenda?" atakuwa ameshakujibu tena kwa hisia nzito kuwa "nakupenda sana mpenzi wangu". ==> Hatokuonea aibu kukutambulisha kwa watu kuwa wewe ndiye mpenzi wake, kwakuwa wewe ndiye furaha yake. ====> Thamani yako ni kubwa sana kwake, anakuona mpya kila siku na hachoki kuvutiwa na wewe. Anakupenda kwa kumaanisha na si kukupenda kimazoea tu. Neno NAKUPENDA litamtoka moyoni na ataridhihirisha kwa kinywa chake. Mtambue mtu huyu kuwa anakupenda kwa dhati. NB: Hakuna aliyekamilika, kila mtu ana kasoro na mapungufu yake. Si vyema kutumia mapungufu ya mwenzio kama fimbo katika mapenzi, cha muhimu ni kumuelimisha na kumuelekeza ili muweze kwenda sambamba. Nadhani baadhi ya maswali ya wadau yatakuwa yamejibiwa na hiyo mada. Kama kuna nyongeza au swali lolote kuhusiana na hiyo mada tuambiane hapa na kupatiana majibu hapa hapa wadau. ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: