VIDONDA VYA TUMBO Ugonjwa wa vidonda vya tumbo hutokea iwapo kidonda cha ukubwa wa angalau wa nusu sentimita kitatokea kwenye sehemu yeyote ya ukuta wa tumbo au utumbo wa binadamu. Kwa kawaida tatizo hili huleta maumivu makali sana ya tumbo ingawa si lazima kila maumivu ayapatayo mgonjwa husababishwa na vidonda vya tumbo. Tafiti zimeonesha kwamba karibu asilimia 70 mpaka 90 ya vidonda vya tumbo husababishwa na aina ya vimelea vya bakteria wajulikanao kama . Aidha matumizi ya baadhi ya dawa za kutuliza maumivu za jamii ya kama au huweza kusababisha au kuongeza uwezekano wa kupata ugonjwa huu. Kuna dhana iliyozoeleka kuwa vidonda vya tumbo huathiri zaidi mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo ( ). Dhana hii si kweli kwani sehemu inayoadhiriwa zaidi na tatizo hili ni sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo ijulikanayo kama Makundi ya PUD Kuna makundi makuu yafuatayo ya ugonjwa huu 1. Vidonda vinavyotokea kwenye mfuko wa kuhifadhia chakula yaani tumbo 2. Vidonda vinavyotokea kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo 3. Vidonda vinavyotokea kwenye koo 4. Vidonda vijulikanavyo kama Visababishi vya PUD Vidonda vya tumbo husababishwa na Maambukizi ya bakteria aina ya Imeonekana kuwa zaidi ya asilimia 50 ya watu duniani wana vimelea hivi katika utumbo. Aidha, miongoni mwao, karibu asilimia 80 huwa hawaoneshi dalili yeyote ya kuugua ugonjwa wa vidonda vya tumbo. Aina hii ya vimelea vya bacteria husababisha karibu asilimia 60 ya vidonda vinavyotokea kwenye tumbo ( ) na zaidi ya asilimia 90 ya Hali hii husababishwa zaidi na kushindwa kwa mfumo wa kinga mwilini kuwaua na kuwaondoa kabisa vimelea hawa ndani ya mwili. Matokeo ya kushindwa huku husababisha kuwepo kwa uambukizi wa kudumu katika kuta za tumbo ( ), uambukizi ambao huharibu mfumo na uwezo wa kuta za tumbo kutunza homoni ya ambayo ni muhimu katika kuhakikisha mazingira ya tumbo yanakuwa na kiwango salama cha tindikali. Kwa kawaida, kazi ya ni kuchochea utolewaji wa tindikali ( ) kutoka kwenye seli za ukuta wa tumbo zijulikanazo kama Iwapo bacteria hawa watashambulia na kuharibu ukuta wa tumbo, mfumo wa pia uharibika, na hivyo kusababisha kuzalishwa kwa wingi hali ambayo pia huchochea uzalishaji wa kwa wingi. Matokeo ya kuzalishwa kwa wingi kwa tindikali hii hupelekea kuchubuka kwa ukuta wa tumbo na hivyo kusababisha vidonda vya tumbo. Matumizi ya muda mrefu ya dawa za kuondoa maumivu za kundi la NSAIDs: Ukuta wa utumbo hujilinda na madhara yatokanayo na tindikali ya utumbo ( ) kwa kuwa na utando laini ( ) ambao hutolewa na vichocheo vijulikavyo kama Dawa hizi za kundi la huharibu mfumo wa kutengeza vichocheo hivi yaani na hivyo kufanya kuta za tumbo kukosa utando wa kuzilinda na mashambulizi ya tindikali hali ambayo hupelekea kutokea kwa vidonda vya tumbo. Uvutaji wa sigara: Uvutaji sigara sambamba na maambukizi ya bakteria aina ya huongeza madhara ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo. Ifahamike tu kuwa uvutaji sigara pekee hausababishi vidonda vya tumbo. Vyakula au viungo vya chakula vyenye uchachu: Kinyume na dhana iliyozoeleka miongoni mwa watu wengi, baadhi ya vyakula vyenye uchachu na upilipili kama vile pilipili, ndimu, limao na masala havina uhusiano na uwezekano wa kupata vidonda vya tumbo. Watu walio katika kundi la damu la O: Imeonekana pia kwamba kundi la damu lijulikanalo kama , halina uhusiano wa kusababisha vidonda vya tumbo. Unywaji wa pombe: Unywaji wa pombe pekee hausababishi vidonda vya tumbo. Hata hivyo, unywaji wa pombe sambamba na maambukizi ya vimelea vya huongeza madhara ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo. Vitu vingine: Vitu vinavyohusishwa na uongezaji wa madhara ya vidonda vya tumbo ni pamoja na upasuaji wa tumbo ), kuungua kwa moto ( ), ugonjwa wa figo; na kubadilishwa kwa viungo vya mwili kama figo au ini. Dalili au viashiria vya PUD Maumivu makali au kiungulia maeneo ya chembe moyo ( ): Maumivu juu kidogo ya tumbo mara nyingi huendana na muda wa kula chakula. Mtu mwenye vidonda kwenye tumbo ( ) hupata maumivu makali sana kipindi anapokula au mara tu baada ya kumaliza kula wakati aliye na vidonda kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo ( ) hupata maumivu makali anapokuwa na njaa na hupata nafuu pindi anapokula. Kuvimbiwa au tumbo kujaa gesi. Hali hii pia yaweza kuendana na kubeua au kujamba mara kwa mara. Kucheua na kuongezeka kwa mate yanayoshuka tumboni baada ya kucheua. Kichefuchefu na kutapika Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito Kutapika damu Kupata haja kubwa cha rangi nyeusi au kahawia chenye harufu mbaya sana. Hii humaanisha mgonjwa anapata haja kubwa au choo kilichochanganyika na damu kwa mbali Uwepo wa dalili kama kiungulia cha muda mrefu, kucheua na kutapika baada ya kula na historia ya kutumia dawa za kupunguza maumivu ( kwa muda muda mrefu bila kufuata ushauri wa daktari ni ishara tosha ya kumfanya mgonjwa kumuona daktari kumpima na kumfanyia uchunguzi ili kujiridhisha kuwa hana tatizo la vidonda vya tumbo. Vipimo vya kutambua Ugonjwa wa vidonda vya tumbo Vipimo vinavyotumika katika kutambua tatizo la vidonda vya tumbo ni pamoja na 1. Vipimo vya kuangalia ndani ya utumbo ambavyo ni pamoja na Kipimo cha au au . Kwa kutumia kipimo hiki, daktari huangalia moja kwa moja ndani ya utumbo wa mgonjwa kuona sehemu iliyo na vidonda pamoja na ukubwa wa tatizo lake. Aidha vipimo hivi humuwezesha daktari kuchukua sehemu ya utumbo iliyoathiriwa kwa ajili ya kuchunguza zaidi maabara ili kutambua uwepo wa vidonda au tatizo jingine linalomsumbua mgonjwa tofauti na vidonda vya tumbo. Kipimo kingine kijulikanacho kama kina uwezo pia wa kuthibitisha uwepo wa ugonjwa wa vidonda vya tumbo. 2. Vipimo vya kutambua uwepo wa uambukizi wa bakteria aina ya kama Kipimo kiitwacho Kipimo cha kuotesha kinyama kilichochukuliwa kutoka katika kipimo cha ( Kipimo kinachoitwa ambacho hufanywa kwa kutumia kinyama kilichochukuliwa kutoka kwenye utumbo wakati wa kufanya . Kipimo hiki huangalia tabia ya vimelea hawa wa Kipimo cha damu kwa ajili ya kutambua kiwango cha maambukizi ya vimelea wa ). Kipimo cha haja kubwa kwa ajili ya kutambua kama bacteria wapo hai au wamekufa ( ). Kipimo hiki ni cha uhakika zaidi na nafuu kuliko kipimo cha Kipimo cha kimaabara cha kuchunguza kinyama kilichochukuliwa wakati wa kipimo cha 3. Vipimo vingine maalum vya kitaalamu zaidi kama Kiwango cha homoni ya katika damu Kipimo cha kuangalia uzalishaji wa homoni ya ambayo uhusika katika uchocheaji wa homoni ya Kupima kiwango cha tindikali inayozalishwa katika tumbo. Hata hivyo vipimo hivi ni vya gharama zaidi na ni aghalabu hutumika mara kwa mara. Matibabu ya Ugonjwa wa vidonda vya tumbo Habari nzuri ni kuwa ugonjwa huu wa vidonda vya tumbo unatibika. Hata hivyo tabia ya baadhi ya wagonjwa wengi kuacha kumalizia dawa au kutumia dawa chini ya kiwango tofauti na walivyoshauriwa na madaktari husababisha kujirudia kwa tatizo au kufanya tatizo kuwa sugu zaidi. Iwapo itagundulika uwepo wa tiba inayotumika ni kuchanganya dawa za antibayotic ( ) za aina tofauti kama au na dawa zenye uwezo wa kupunguza uzalishaji wa tindikali kwa wingi au kwa kitaalamu Wakati mwingine daktari anaweza pia kuongeza dawa ya . 1. Kwa wagonjwa sugu, dawa za antibioc za aina tatu tofauti zinaweza kutumika. Dawa hizi ni pamoja na ambazo hutumika sambamba na dawa yeyote moja kutoka kundi la kama vile au pamoja na . 2. Kwa mgonjwa wa kawaida ambaye si sugu tiba bora inayoshauriwa ni kuchanganya dawa za antibiotic za aina mbili kama sambamba na dawa yeyote moja ya jamii ya kama 3. Iwapo hakuna ushahidi wa kuwepo kwa uambukizi wa bacteria, dawa yeyote moja ya jamii ya yaweza kutumika kwa muda mrefu zaidi bila kuchanganya na antibiotic yeyote. Kwa kawaida kitendo cha kutibu na kuwaondoa humaliza na kuponyesha kabisa vidonda vya tumbo. Hata hivyo, inawezekana kabisa ugonjwa huu kujirudia tena, hali ambayo hulazimisha kurudiwa tena kwa matibabu kwa kutumia aina nyingine ya antibiotics. Aidha msomaji, inashauriwa si vyema kwa mgonjwa kujitibu mwenyewe bila kufuata ushauri wa daktari ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea iwapo dawa hazitatumiwa inavyopaswa. Ni kweli Maziwa ya ng’ombe yanaponyesha vidonda vya tumbo? Kinyume na dhana iliyozoeleka ndani ya jamii, maziwa ya ng'ombe hayaponyeshi vidonda vya tumbo, bali huongeza madhara yatokanayo na ugonjwa huu. Hii ni kwa sababu, maziwa huwa na tabia ya kutengeneza aina fulani ya kinga au ukuta ( ) kwa vimelea vya ambayo huvikinga vimelea hivi dhidi ya mashambulizi ya dawa na hivyo kufanya dawa kushindwa kuwaua na kuwaondoa kabisa vimelea hivi. Kinachotokea ni kuwa, maziwa huondoa tu kwa muda maumivu ya tumbo kwa kupunguza makali ya tindikali iliyopo tumboni. Pindi maziwa haya yanapoisha, maumivu hurejea tena na kuwa makali kama hapo awali. Matibabu ya vidonda vya tumbo kwa njia ya upasuaji Zipo aina nyingi ya upasuaji unaofanywa ili kutibu ugonjwa huu. Kuvuja damu ndani ya mwili kupitia vidonda vya tumbo ni sababu mojawapo ya kufanyiwa upasuaji kwa vile ni hatari sana hata kupelekea kifo iwapo mgonjwa hatapata tiba haraka. 1. ni njia inayotumika kutibu uvujaji wa damu unaotokana na vidonda vya tumbo. Aina hii ya tiba hutegemea sana aina na sehemu vilipo vidonda vya tumbo. Tiba hii yaweza kufanyika kwa kuchoma sehemu inayovuja damu ndani ya tumbo au utumbo kwa lengo la kusitisha uvujaji wa damu ( ) au kwa kuvifunga vidonda kwa kutumia vifaa maalum ( ). Aidha tiba hii ni nzuri na haina madhara yeyote yale. 2. Madaktari wengi hupendelea upasuaji ujulikanao kitaalamu kama sambamba na tiba ya kuondoa bakteria. Aidha, mgonjwa pia hushauriwa kuacha matumizi ya dawa za kwa ajili ya kuondoa uwezekano wa damu kuendelea kutoka kwa vile kama ilivyoonekana hapo awali, matumizi ya dawa hizi huweza kusababisha uvujaji wa ndani kwa ndani ya mwili. 3. Wagonjwa sugu, hufanyiwa baadhi ya upasuaji ambao huitaji utaalamu wa hali ya juu katika kuondoa neva na mishipa ya fahamu yenye kuhusika na uzalishaji wa tindikali katika tumbo. Madhara ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo 1. Uvujaji wa damu ndani ya utumbo: Hali hii yaweza kusababishwa na vidonda kuenea hadi kwenye mishipa ya damu na hivyo kufanya damu kuanza kuvuja. Hali hii ni hatari sana na inahitaji tiba ya dharura. 2. Vidonda vya tumbo huweza kusababisha tundu (kutoboka kwa ukuta wa tumbo) na kufanya vitu vilivyo ndani ya utumbo kutapakaa katika tumbo ( ) Hali hii huitwa na ni hatari sana na inahitaji matibabu ya dharura. Aidha, kuenea huko kunaweza pia kuathiri tezi kongosho na kusababisha madhara katika tezi hiyo, ugonjwa unaojulikana kama . 3. Vidonda vya tumbo vinaweza pia kuenea na kuathiri pia viungo vya jirani kama vile ini au kongosho ( ) 4. Kuvimba kwa kuta za tumbo pamoja na makovu yasababishwayo na vidonda hivi huweza kusababisha kuziba kwa njia ya kupitishia chakula kutoka kwenye tumbo ( ) kwenda sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo ( ) hali ambayo kitaalamu huitwa 5. Iwapo vidonda vya tumbo vimesababishwa na , kuna uwezekano wa kati ya mara tatu hadi ya sita ya mgonjwa kupata kansa ya tumbo ( PEPTIC ULCERS Ulcers of the stomach (gastric ulcers) and the duodenum (the first part of the intestines after the stomach) are together known as peptic ulcers. Symptoms Although most peptic ulcers are quite small, they can be incredibly painful. This pain tends to be: A constant gnawing or burning pain. Located in the upper, central abdomen (but may penetrate into the back). Worse at night or in the early morning. Worse if you miss a meal. Relieved by food or 'white medicine' such as antacids or milk. Other symptoms include: Tiredness. Nausea and vomiting. Indigestion or heartburn, vomiting blood or passing blood in the stools (this may be the only sign of an ulcer). Anaemia, caused by blood loss, resulting in paleness and shortness of breath. However, some people have no symptoms at all. If left untreated, peptic ulcers may cause rapid internal bleeding, which can be very dangerous, or a perforation or obstruction in the intestines. Causes and risk factors Peptic ulcers occur when the membrane lining the digestive system breaks down or erodes. This membrane normally stands up to some fairly tough challenges, containing and churning up food particles while resisting the effects of the stomach's powerful digestive juices. The discovery that the bacteria is the main cause of these ulcers has been one of the great success stories of modern medicine. Several mechanisms protect the digestive membrane, but under certain conditions these fail, allowing acid and digestive enzymes to cause damage. These conditions include: Infection with - many people carry this bacteria, and while not everyone with develops an ulcer, almost everyone with an ulcer has . Non-steroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs) - these include aspirin, ibuprofen and many painkillers used for conditions such as arthritis. Ulcers and haemorrhage are a common problem with these drugs. Smoking. Excessive amounts of alcohol. Other factors that increase the risk of an ulcer include a family history of ulcers and being blood group O. It used to be thought that high levels of stress could cause ulcers, but many doctors now think emotional stress simply accentuates the pain of an existing ulcer and may interfere with healing. Events that put mmense physical stress on the body, such as severe burns, major surgery or a major trauma, do seem to be linked to peptic ulcers. Tests to confirm the diagnosis of an ulcer include: Gastroscopy - a thin tube or endoscope is passed into the stomach to look at the digestive membrane. Barium studies - a substance called barium is swallowed and then highlights ulcers on an x-ray. Tests will also look for the presence of . These may involve a blood test, breath test or biopsy of the digestive membrane. Treatment and recovery If is detected, The main treatment is eradication therapy. This usually means taking a combination of two antibiotics and a drug that suppresses stomach acid production for a week. It's commonly known as 'triple therapy'. It's also important to cut down on factors that can aggravate an ulcer, such as smoking, and stop taking any NSAIDs. Although medical treatments usually cure the ulcer, an operation is still required in some cases. This may involve cutting the main nerve that controls acid production in the stomach (the vagus nerve) or removing part of the stomach itself. Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi. Version: Mobile Web Helicobacter pylori Non Steroid Anti-inflamatory Drugs Aspirin Diclofenac stomach duodenum. (Gastric ulcers) (Duodenal Ulcers) (Oesophageal ulcers) Merckel’s Diverticulum ulcer

at 11:48 AM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top