Home → ushauri
→ FANGASI SEHEM ZA SIRI. (Vaginal candidiasis)
Maambukizi ya Fangasi katika Sehemu za SIRI.
Share na like page hii. Nimekuwa nipoa sim nyingi na kuwasaidia watu wengi haswa wanawake katika tatizo hili nimeona kunahaja kubwa ya kuongelea swala hili kiundan ili watu wote mpate elimu hii iwasaidie na kwa ambao hawafaham nini chakufanya wapate mwanga sasa endelea. Kati ya maambukizi yanayowasumbua
wanawake na wanaume wengi duniani ni maambukizi ya
fangasi. Inakisiwa asilimia 75 ya wanawake
wote duniani hupata maambukizi haya
katika kipindi cha uhai wao.
Maambukizi ya fangasi katika sehemu za siri
za mwanamke husababishwa na uwepo wa
fangasi wanaojulikana kitaalamu kama
Candida albicans. Maambukizi haya pia
hujulikana kama yeast infection au thrush.
Fangasi hupatikana kama vimelea vya
kawaida katika mdomo, mpira wa kupitisha
chakula sehemu inayojulikana kama
pharynx, katika kibofu cha mkojo, uume na
hata kwenye uke.
Mfumo mzuri wa kinga wa mwili pamoja aina
fulani za bakteria wanaoishi pamoja na
fangasi hawa husaidia sana katika kuthibiti
maambukizi yanayoyosababishwa na aina hi
ya fangasi.
Nini hutokea?
Kwa kawaida, Candida albicans huishi
kwenye uke na sehemu nyingine (kama
zilivyoelezewa hapo juu) bila kusababisha
madhara yoyote yale isipokuwa pale
mazingira ya eneo husika yanapobadilika
kama vile mabadiliko katika hali ya pH ya
eneo husika (ifahamike ya kwamba pH ya
kawaida ndani ya uke ni 4.0 - 4.5) au
uwiano wake na vimelea (microorganisms)
wengine unapoharibiwa kutokana na sababu
mbalimbali kama vile matumizi ya madawa
aina ya antibiotics, kupungua kwa kinga
mwilini kutokana na magonjwa mbalimbali.
Maambukizi haya ya fangasi yanaweza
kugawanywa katika sehemu kuu mbili
Maambukizi yasiyo makali yaani
uncomplicated thrush: Katika kundi hili,
mgonjwa hupatwa na maambukizi mara
moja hadi nne kwa mwaka na dalili zake
huwa si mbaya sana na maambukizi haya
husababishwa na fangasi wa jamii hii ya
Candida albicans.
Maambukizi makali yaani complicated
thrush: Katika kundi hili, mgonjwa
hupatwa na maambukizi zaidi ya mara
nne kwa mwaka, dalili zake kuwa mbaya
zaidi au kama maambukizi yatakuwa
yametokea kipindi cha ujauzito, ugonjwa
wa kisukari, upungufu wa kinga mwilini.
Aina hii kusababishwa na vimelea vya aina
nyingine tofauti na Candida albicans.
Vihatarishi
Watu walio katika hatari ya kupata
maambukizi ya fangasi hawa ni wale wenye
• Kutumia sana dawa aina ya detergents
kwenye sehemu za siri au douches (vifaa
vinavyotumiwa kusafishia uke kwa kutumia
maji yaliyochanganywa na siki au antiseptic
yoyote ile) kwa sababu hali husababisha
kuharibika kwa uwiano wa fangasi na aina
nyingine ya vinyemelezi kama bakteria aina
ya lactobacilli
• Kutumia sana madawa aina ya antibiotics,
steroids ambayo yana tabia ya kushusha
kinga ya mwili
• Mabadiliko ya mfumo wa homoni mwilini
ambayo husababisha mabadiliko katika sehemu za siri na hivyo kufanya kuwepo kwa
ukuaji wa kasi wa fangasi hawa
• Ujauzito (kutokana na kubadilika kwa
mfumo wa homoni mwilini na kupungua kwa
kinga ya mwili). Hata hivyo ieleweke hapa
kuwa si kila mjamzito hupatwa na
maambukizi haya.
• Matumizi ya dawa za kupanga uzazi
(vidonge vya majira)
• Upungufu wa kinga mwilini kutokana na
magonjwa sugu kama kisukari, saratani aina
yoyote ile, ugonjwa aina ya mononucleosis
na nk.
• Ugonjwa wa ukimwi (HIV/AIDS)
• Matibabu ya homoni (hormonal
replacement therapy) kutokana na sababu
mbalimbali
• Matibabu ya kusaidia kushika mimba kwa
wale wenye matatizo ya uzazi (infertility
treatment)
• Msongo wa mawazo (stress)
• Utapia mlo (malnutrition)
• Kuvaa nguo au mavazi yanayoleta joto
sana sehemu za siri kwa muda mrefu kama
nguo za kuogelea (swimwear), nguo za ndani
(chupi) zilizotengenezwa kwa kitambaa aina
ya nylon, nguo za ndani zinazobana sana
nk.
• Kujamiana kwa njia ya kawaida mara tu
baada ya kujamiana kupitia njia ya haja
kubwa (anal sex) au matumizi ya vilainishi
venye glycerin wakati wa kujamiana pia
yamehusishwa na maambukizi haya.
• Kuvimba kwa tezi la koo (goiter)
• Saratani ya tezi la koo (thyroid cancer)
• Wanawake wenye umri wa miaka kati ya
ishirini na thelathini wapo kwenye hatari
kubwa ya kupata maambukizi haya wakati
wale ambao wameshaacha kupata hedhi au
wale ambao hawajaanza kupata hedhi kabisa
hawako kwenye hatari kubwa.
Kwa wanaume vihatarishi vya maambukizi
haya ni
• Kujamiana na mwanamke mwenye tatizo
hili au maambukizi haya
• Upungufu wa kinga mwilini
• Matumizi ya madawa aina ya antibiotics
kwa muda mrefu bila ushauri wa daktari
• Magonjwa sugu kama kisukari, saratani ya
aina yoyote ile na nk.
Dalili na viashiria kwa wanawake
• Kuwashwa sehemu za siri (kwenye tupu ya
mwanamke)
• Kuhisi kuwaka moto sehemu za siri (burning
sensation)
• Kufanya kama vidonda katika sehemu za
siri (soreness)
• Maumivu wakati wa kujamiana (superficial
dyspareunia)
• Maumivu au usumbufu wakati wa kujisaidia
haja ndogo (wakati mtu anakojoa)
• Kuvimba na kuwa rangi nyekundu kwa
mdomo wa nje wa tupu ya mwanamke (labia
minora)
• Kutokwa na uchafu wa rangi nyeupe au
nyeupe kijivu, unaoweza kuwa mwepesi,
majimaji au mzito na ambao umefanana na
jibini (cottage cheese like discharge) wenye
muonekano unaojulikana pia kama curd-
like appearance. Kwa kawaida, uchafu huu
haumbatani na harufu yoyote isipokuwa
panapokuwa na tatizo la ziada kama
ugonjwa wa zinaa aina ya Bacteria vaginosis.
Uchafu huu unaotoka hapa unaweza kuenea
kwenye maeneo mengine yaliyokaribu na
tupu ya mwanamke kama kwenye mitoki
(groin area) au perineum na kusababisha
kuharibika kwa ngozi katika sehemu hizo.
Dalili na viashiria hivi huwa mbaya zaidi
wakati mwanamke anapokaribia kupata
hedhi.
Dalili na viashiria kwa wanaume ni
• Kuwashwa sehemu za siri
• Kuvimba na kuwa rangi nyekundu kwenye
ncha ya uume
• Kuwepo kwa uchafu wa rangi nyeupe (kama
nilivyoeleza hapo juu) kwenye sehemu ya juu
ya uume.
• Kuwa na vidonda vidogo kwenye uume (sore
on the glans)
Hata hivyo, mara nyingi wanaume
hawaoneshi dalili zozote zile, ni vizuri kwa
mwanamke kumueleza mwenza wake pale
anapopata maambukizi haya ili naye pia
apate kutibiwa.
Vipimo vya uchunguzi
Kabla ya vipimo vya uchunguzi, ni muhimu
kwa daktari kuchukua historia ya mgonjwa
kwa usahihi kabisa. Vipimo vitahusisha:
Uchunguzi wa uke (per Vaginal Examination
(PV exam)
Daktari huvaa gloves, na kuzilainisha gloves
hizi kwa jelly maalum, mgonjwa hulala
kwenye kitanda na kutanua miguu yake ili
njia itanuke na kumrahisishia daktari
kumfanyia uchunguzi, wakati akiwa tayari,
daktari ataingiza vidole vyake viwili (cha
shahada na cha kati) ukeni kwa dhumuni la
Kuhisi kama kuna uvimbe wowote ndani ya
tupu ya mwanamke
Kuangalia kama anapata maumivu wakati
wa kujamiana
Kuangalia kama kuna uchafu wowote
unaotoka, wingi wake, rangi yake, harufu
yake, uzito wake (mwepesi, majimaji au
mzito), na aina ya uchafu unaotoka kama
ni sahihi kutokana na maelezo ya
mgonjwa au ni tofauti
Kuangalia kama sehemu ya siri ipo
kawaida
Kuangalia kama kuna uvimbe wowote wa
tezi za sehemu ya siri (mitoki)
Kuangalia nywele za sehemu za siri zilivyo
na jinsi zilivyokaa
Kuangalia shingo ya kizazi, bartholin
glands nk.
Kuangalia sehemu ya haja kubwa kama
kuna skin tags, bawasiri (haemorrhoids)
nk.
Kuangalia kwenye kinembe (clitoris) kama
kuna tatizo lolote lile.
Hayo ni baadhi tu ya malengo na faida za
kipimo hiki kwa vile humuwezesha daktari
kugundua tatizo au maradhi mengine ya
ziada ambayo hayajaanza bado kuonesha
dalili zake kwa mgonjwa au mgonjwa
mwenyewe hafahamu kama hali aliyo nayo
ni tatizo. Hata hivyo inashauriwa sana kabla
ya kufanya kipimo hiki, daktari amjulishe
mgonjwa aina ya kipimo, lengo lake na jinsi
kitakavyofanyika ili kumuandaa mgonjwa
kisaikolojia. Aidha ni muhimu pia
kumtaarifu wakati anapoanza kuingiza
vidole.
Kuchunguza uchafu unaotoka kwa kutumia
hadubini (microscope).
Mara tu baada ya kuchukua sehemu ya
uchafu kwa kutumia swab, kipimo hicho
humwagiwa tone la 10% potassium hydroxide
ambayo huyeyusha chembechembe za ngozi
na kubakisha seli za Candida albicans.
Kuwepo kwa pseudohyphae (mfano wa aina
fulani ya mizizi au miguu ya fangasi hawa)
pamoja na budding yeast cells (yaani seli za
fangasi zinazojigawa kwa ajili ya kuzaliana)
ni uthibitisho wa maambukizi ya fangasi aina
ya Candida albicans.
Kuchukua kipimo na kuotesha kwenye
maabara
ili kuangalia aina ya uoto huo kama ni wa
fangasi aina ya Candida albicans, ama la.
Kipimo cha mkojo (Urinalysis)
Vipimo vingine hufanyika kulingana na dalili
zinazoashiria uwepo wa magonjwa mengine
kama vile ugonjwa wa kisukari, HIV/AIDS,
ugonjwa wa kuvimba tezi la koo (goiter),
saratani ya tezi koo (thyroid cancer) nk.
MATIBABU
Kama umeshapitia vipimo hivyo au hata vipimo mbali mbalI na bado tatizo linaendelea au linajiludia mara kwa mara wakati mwingine linaweza kuwa sugu unashauliwa kutumia njia za asili.
kwa maelezo zaidi na msaada wa kimatibabu piga 0767421678 au 0655148030 unaweza kutuma sms za aina zote utajibiwa kupitia 0767421678. ASANTE. Share na like page yetu AFYA KWA WANAUME na AFYA YA WANAWAKE Facebook. https://www.facebook.com/hamad1199/
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: