Home → ushauri
→ MAPENZI YA KWELI
# Daaaah inasikitisha
Kijana na msichana mmoja walikuwa katika mahusiano. Baada ya miaka kadhaa ya mahusiano yao, kijana alimaliza chuo kikuu na kuamua kujiongezea maarifa kwa kwenda kusoma nje ya nchi.
Kabla ya kuondoka nchini, alitoa mapendekezo ya uchumba kwa yule binti. "Yule kijana alimwambia binti, mimi sio muongeaji, ila ninachojua ninakupenda sana, kama utaniruhusu kukuoa, nitakua mwanaume wa maisha yako yote.
Msichana alikubaliana nae na wakaenda kutambulishana kwa wazazi.
Wazazi wa pande zote walikubaliana vijana wao waoane kwani ni kweli walionesha kupendana sana. Ila kabla ya kuondoka kijana alimvisha pete ya uchumba na kuahidi kufunga ndoa pindi atakaporudi nchini.
Binti aliendelea na kazi yake huku kijana nae akipaa kwenda ng'ambo kujiendeleza kielimu. Walikuwa wakiwasiliana mara kwa mara kupitia emails na kupigiana simu.
Ingawa mapenzi ya mbali yalikuwa magumu kwao, ila kamwe hakuna aliyeonesha kukata tamaa.
Siku moja wakati msichana akielekea kazini, aligongwa na gari lililokua limepoteza mwelekeo. Alipoteza fahamu palepale na siku alipoamka aliwakuta wazazi wake wakiwa karibu yake. Akatambua kwamba yupo hospitali na ameumia vibaya.
Alipomwona mama yake akilia, akataka aongee kitu lakini akagundua hakuna sauti iliyokua inatoka..alipoteza sauti yake. Daktari akatoa ripoti kuwa ubongo umepata madhara na hvyo kupoteza uwezo wa kuongea.
Baada ya kutoka hospitali, binti aliendelea kuuguzwa huku mchumba wake akipiga simu kila siku. Binti hakupokea wala hakutaka mtu yeyote amwambie yule kijana hali yake. Hakutaka awe mzigo kwa yule kijana.
Hivyo alimwandikia barua na kumwambia kua ameshindwa kusubiri hvyo aendelee na maisha yake. Katika barua aliambatanisha na ile pete ya uchumba aliyovishwa kabla yule kijana hajaondoka.
Baada ya kupata ile barua Kijana alijitahidi kutuma barua na kupiga simu mara kwa mara kumbembeleza lakini binti alikuwa akilia tu na kutojibu lolote.
Wazazi wa binti wakaamua kumhamishia mbali wakitaraji kwamba atasahau kila kitu na kuwa na furaha tena.
Katika mazingira mapya, binti alijifunza kuongea kwa vitendo (sign language). Huku akijiambia nafsini mwake atamsahau yule kijana.
Siku moja rafiki yake alimtembelea na kumweleza kuwa yule kijana amerudi nchini. Yule binti alimwomba sana rafiki yake asimwambie yule kijana kwamba yupo pale na asimweleze chochote kuhusiana na yaliyomtokea.
Baada ya hapo hakukua na taarifa tena juu ya yule kijana.
Mwaka mmoja ukapita, na siku moja yule rafiki yake akaja kwa yule binti na kumpa bahasha iliyokua na kadi ya mwaliko wa harusi ya yule kijana. Yule binti aliumia sana moyoni mwake.
Lakini baada ya kufungua bahasha, aliona jina lake kwenye ile kadi. Alipotaka tu kumuuliza yule rafiki yake kwa saini za vitendo, alimuona kijana akiingia ndani.
Yule kijana akatumia lugha ya vitendo na kumwambia "Nimetumia mwaka mzima kujifunza lugha ya vitendo ili niweze kuwasiliana na wewe na kukueleza kwamba, ingawa umepatwa na matatizo makubwa, bado sijasahau ahadi yangu kwako. Nipe nafasi mimi niwe sauti yako. Nakupenda sana..."
Yule binti na Kijana walioana, Mungu amewabariki na watoto watatu, wanaishi kwa upendo huku vicheko na tabasamu ukiwa wimbo wa taifa wa ndoa yao.
TAFAKARI ni vijana wangapi siku ya leo wenye mapenzi ya dhati kama haya, je! Ni vijana wangapi wanaotunza ahadi zao walizowekeana katika uchumba wao? Hakika utagundua mapenzi ya kweli miaka hii yamefifia na kupotea, wengi wanadanganyana, ndio maana kuachana imekua kawaida, john akiwa chuo anatoka na mary, akiwa mtaani likizo anatoka na Catherine na wote kawaahidi ndoa, unafikiri kuna mapenzi ya kweli hapo?
Ni wazi kuwa pale unapofikiri umepoteza matumaini kabisa, ndipo kipindi ambapo msaidizi wako atakapotokea. Haijalishi tatizo gani mwenzio anakumbana nalo, kamwe usimuache peke yake. Kuweni kama timu yenye kiu ya mafanikio.
Kuwa sauti yake pale anapopoteza sauti, kuwa mwanga wake pale anapopoteza matumaini na panapo mafanikio basi furahini pamoja.
Mwenyezi Mungu akubariki wewe uliyesoma ujumbe huu, akujalie mtu ambae utakua nae bega kwa bega katika hatua za kimaisha na kamwe asikuache..!!
AMEN!
Tafadhali SHARE mkasa huu uwafikie watu wengi zaidi katika jamii.
Nakutakia siku Njema, Mungu Akubariki na kukulinda
MAPENZI YA KWELI # Daaaah inasikitisha Kijana na msichana mmoja walikuwa katika mahusiano. Baada ya miaka kadhaa ya mahusiano yao, kijana alimaliza chuo kikuu na kuamua kujiongezea maarifa kwa kwenda kusoma nje ya nchi. Kabla ya kuondoka nchini, alitoa mapendekezo ya uchumba kwa yule binti. "Yule kijana alimwambia binti, mimi sio muongeaji, ila ninachojua ninakupenda sana, kama utaniruhusu kukuoa, nitakua mwanaume wa maisha yako yote. Msichana alikubaliana nae na wakaenda kutambulishana kwa wazazi. Wazazi wa pande zote walikubaliana vijana wao waoane kwani ni kweli walionesha kupendana sana. Ila kabla ya kuondoka kijana alimvisha pete ya uchumba na kuahidi kufunga ndoa pindi atakaporudi nchini. Binti aliendelea na kazi yake huku kijana nae akipaa kwenda ng'ambo kujiendeleza kielimu. Walikuwa wakiwasiliana mara kwa mara kupitia emails na kupigiana simu. Ingawa mapenzi ya mbali yalikuwa magumu kwao, ila kamwe hakuna aliyeonesha kukata tamaa. Siku moja wakati msichana akielekea kazini, aligongwa na gari lililokua limepoteza mwelekeo. Alipoteza fahamu palepale na siku alipoamka aliwakuta wazazi wake wakiwa karibu yake. Akatambua kwamba yupo hospitali na ameumia vibaya. Alipomwona mama yake akilia, akataka aongee kitu lakini akagundua hakuna sauti iliyokua inatoka..alipoteza sauti yake. Daktari akatoa ripoti kuwa ubongo umepata madhara na hvyo kupoteza uwezo wa kuongea. Baada ya kutoka hospitali, binti aliendelea kuuguzwa huku mchumba wake akipiga simu kila siku. Binti hakupokea wala hakutaka mtu yeyote amwambie yule kijana hali yake. Hakutaka awe mzigo kwa yule kijana. Hivyo alimwandikia barua na kumwambia kua ameshindwa kusubiri hvyo aendelee na maisha yake. Katika barua aliambatanisha na ile pete ya uchumba aliyovishwa kabla yule kijana hajaondoka. Baada ya kupata ile barua Kijana alijitahidi kutuma barua na kupiga simu mara kwa mara kumbembeleza lakini binti alikuwa akilia tu na kutojibu lolote. Wazazi wa binti wakaamua kumhamishia mbali wakitaraji kwamba atasahau kila kitu na kuwa na furaha tena. Katika mazingira mapya, binti alijifunza kuongea kwa vitendo (sign language). Huku akijiambia nafsini mwake atamsahau yule kijana. Siku moja rafiki yake alimtembelea na kumweleza kuwa yule kijana amerudi nchini. Yule binti alimwomba sana rafiki yake asimwambie yule kijana kwamba yupo pale na asimweleze chochote kuhusiana na yaliyomtokea. Baada ya hapo hakukua na taarifa tena juu ya yule kijana. Mwaka mmoja ukapita, na siku moja yule rafiki yake akaja kwa yule binti na kumpa bahasha iliyokua na kadi ya mwaliko wa harusi ya yule kijana. Yule binti aliumia sana moyoni mwake. Lakini baada ya kufungua bahasha, aliona jina lake kwenye ile kadi. Alipotaka tu kumuuliza yule rafiki yake kwa saini za vitendo, alimuona kijana akiingia ndani. Yule kijana akatumia lugha ya vitendo na kumwambia "Nimetumia mwaka mzima kujifunza lugha ya vitendo ili niweze kuwasiliana na wewe na kukueleza kwamba, ingawa umepatwa na matatizo makubwa, bado sijasahau ahadi yangu kwako. Nipe nafasi mimi niwe sauti yako. Nakupenda sana..." Yule binti na Kijana walioana, Mungu amewabariki na watoto watatu, wanaishi kwa upendo huku vicheko na tabasamu ukiwa wimbo wa taifa wa ndoa yao. TAFAKARI ni vijana wangapi siku ya leo wenye mapenzi ya dhati kama haya, je! Ni vijana wangapi wanaotunza ahadi zao walizowekeana katika uchumba wao? Hakika utagundua mapenzi ya kweli miaka hii yamefifia na kupotea, wengi wanadanganyana, ndio maana kuachana imekua kawaida, john akiwa chuo anatoka na mary, akiwa mtaani likizo anatoka na Catherine na wote kawaahidi ndoa, unafikiri kuna mapenzi ya kweli hapo? Ni wazi kuwa pale unapofikiri umepoteza matumaini kabisa, ndipo kipindi ambapo msaidizi wako atakapotokea. Haijalishi tatizo gani mwenzio anakumbana nalo, kamwe usimuache peke yake. Kuweni kama timu yenye kiu ya mafanikio. Kuwa sauti yake pale anapopoteza sauti, kuwa mwanga wake pale anapopoteza matumaini na panapo mafanikio basi furahini pamoja. Mwenyezi Mungu akubariki wewe uliyesoma ujumbe huu, akujalie mtu ambae utakua nae bega kwa bega katika hatua za kimaisha na kamwe asikuache..!! AMEN! Tafadhali SHARE mkasa huu uwafikie watu wengi zaidi katika jamii. Nakutakia siku Njema, Mungu Akubariki na kukulinda
Artikel Terkait
UNAJUA KUMWONYESHA MPENZI WAKO KAMA UNAMPENDA????  Kwa upendo wao wote, kwa nguvu zao zote, na uzuri , mahusiano ni kama mmea ambao unahitaji kumwagilia maji na kuwekewa mbolea na kupata jua la kutosha ili uweze kunawiri vizuri Sababu kubwa ambayo watu hukosa kujua kama wanapendwa ni kutohisi upendo. Kwa nini? Kwa sababu hata kama wanasema I love you mwisho wa kuongea kwenye simu au kabla ya kwenda kazini, hayo maneno hayana miujiza bila ya kuwa na mengine yalio rahisi . Kuna vitu vidogo vidogo sana vinavyoonyesha upendo na kumfanya mtu ajisikie kupendwa. 1.Usisahau kumkumbatia kabla ya kusema kwa heri. Uelewa wa kimwili ni wa muhimu kuliko maneno 2.Mwambie jinsi alivyo muhimu kwako. Hii huenda zaidi ya neno i love you. 3.Express understanding panapohitajika kusema. Nimeelewa unachokisema. Kama hujaelewa elezea, kwa kusema hivi , Niambie jinsi unavyojisikia ili nikuelewe. 4.Sema mara nyingi jinsi unavyomkubali anapokuwa amefanya jambo kwako. Husband and wife in park 5.Mwambie jinsi gani unafurahia vipengele vya upekee wake. Kwa mfano , napenda uchangamfu wako, mpongeze. 6.Toka nae siku nzima bila ya kusema kitu chochote zaidi ya kumsifia. 7.Mnunulie chakula anachokipenda bila yeye kusema. 8.Msaidie kupika 9.Kama mna watoto wapeleke kutembea, ili kufurahia michezo ya watoto ili kumwacha awe peke yake kwa utulivu. 10.Tuma ujumbe wa kimapenzi kwa mwenza wako bila sababu . 11.Mtumie email wakati yuko kazini ili kujua anajisikiaje. 12.Mpigie wakati akiwa break kusema tu hujambo 13.Karibia gari, meza, au kochi na umshike mikono yake japo kwa muda kidogo. 14.Mvutie kiti anapotaka kukaa au mfungulie mlango anapotaka kutoka au kuingia. 15.Kumbuka kumpa tabasamu, sio fake, lile ambalo umetunza kwa ajili yake . 16.Badala ya kumweleza jinsi ulivyokuwa na siku mbaya kazini, mwambie kuwa siku hio ulihitaji kuwa na yeye kwa sababu…au nimekuwa na siku mbaya nahitaji unikumbatie. 17.Fanya utani na ucheke nae 18.Nendeni kulala kwa wakati mmoja, ongeeni pamoja au kama kusoma msome pamoja au kama kutulia kwa muda fanyeni pamoja. 19.Kama una watoto mpongeze mwenza wako mbele yao. Watoto watafurahi pia. 20.Mkumbatie mbele za watu, ingawa ataona aibu lakini atafurahia. 21.Tafuta njia nzuri za kuambiana badala ya I love you 22.Muwe na tabia ya kutoka japo mara moja kwa wiki kama mkiweza 23.Mpe zawadi 24.Mpeleke movie 25.mpe massage bila sababu au kwa ajili ya kazi nyingi 26.Mwambie kuwa yeye ni rafiki yako 27.Usiogope kumshirikisha hisia zako, Ni vizuri kufahamu kama una furaha au huna furaha wakati huo na kwa nini 28.Sikiliza anapokuambia jinsi anavyojisikia 29.Kumbuka kila mara unapoweza nunua kitu kidogo kwa ajili yake. 30.Andika ujumbe mdogo wa kimapenzi na kuacha sehemu ambapo atafika 31.Mshike mikono yake mbele za watu 32.Mpate fundisho pamoja, halijalishi ni aina gani 33.Omba msamaha unapokosea 34.Wakati mwingine yeye awe sahihi 35.Mcheze game pamoja 36.Mpe nafasi anapohitaji hivyo.lakini afahamu kuwa upo kama atakuhitaji 37.Mchemshie maji ya kuoga anapokuwa na stress 38.Mwoshee gari yake 39.Jaribu kufanya kitu cha wema kila siku kwa ajili yake 40.Jaribuni kufanya kitu kipya pamoja. Changamoto moja ni bora 41.Mwache alale miguu pako 42.Mtengenezee breakfast, kama inawezekana mpelekee kitandani 43.Mkumbushe kuwa yeye yuko hot au sexy 44.Mkatembee kwenye hewa nzuri pamoja 45.Mnaweza kuvaa nguo za kufanana mnapotoka kupunga upepo 46.Mjitolee pamoja 47.Mtengeneze nywele zake 48.Muweke lengo kama wanandoa, kwa ajili ya fitness, finance, na personal growth 49.Kusafiri pamoja 50.Mpe compani anapoenda mpirani, kwenye game na uwe mmoja wao 51.Chukua muda wa kuwajua rafiki wa mwenza wako 52.Mwache atoke peke yake wakati mwingine 53.Mwekee nyimbo anazozipenda na mcheze pamoja 54.Usiwe serious sana, uwe mcheshi wakati mwingine 55.Mwimbie nyimbo anazopenda 56.Mwambie unampenda zaidi ya jana 57.Kama una siku mbaya , sikiliza kila unachotaka kusema 58.Mwambie kuwa anavutia kuliko wakati mliokutana mara ya kwanza 59.Mwambie unamfikiria kila mara 60.Mwambie kuwa unamsaidia kwa kuwa umemwelewa 61.Mwambie unapenda mwili na akili yake 62.Mwambie unachokifurahia siku hio. Na jinsi gani kinakukumbusha kuhusu yeye. 63.Siku yako imeendaje leo Kila ukiamka mwambie habari za asubuhi kila siku 65.Kila siku ukitaka kulala mwambie usiku mwema 66.Hakikisha anafahamu kuwa yeye ni namba moja kwako 67.Mwonyeshe kuwa unamuheshimu kwa kusikiliza mawazo yake kwenye maamuzi muhimu 68.Onyesha kukubali alichokifikiria na kukiamua hata kama unaona kabisa hukubaliani nacho. 69.Mwambie akuchagulie nguo za kuvaa kazini 70.Nendeni gym pamoja 71.Mnunulie kadi bila sababu , hata kama hakuna sikuku 72.Tamani kumkiss kila mara 73.Mwambie kuwa umepata bahati ya kuwa na yeye na kuwa umebadilika tangu ukiwa nae 74.Kuwa mkweli . mfahamishe makosa uliyoyafanya 75.Kuwa mpole kwake kwa sababu mwanamke ni laini 76.Mwonyeshe kuwa unamwamini ili nae awe wazi kwako 77.Pigeni picha pamoja 78.Fanyeni mambo ya kijinga pamoja 79.Alika familia yake kwenye chakula cha jioni 80.Mwombe mwenza wako mshirikishane ndoto zenu 81.Cheka anapotania,hata kama utani huo hauchekeshi 82.Uwe rahisi ili aweze kukupenda. Utagundua kuwa kumbe ni mkarimu na ana wema. ... Read More
Zoezi lenye kuufanya uume usimame kwa muda mrefu na kuchelewa kukojoa wakati wa kufanya mapenzi  Misuli inayohusika na nguvu za kiume na kuwahi kumaliza wakati wa tendo la kufanya mapenzi huitwa ”puboccugeous Muscle” maarufu inajulikana kama Pelvic Muscle. Misuli hii inapokuwa dhaifu,uwezo wa kusimamisha uume kwa muda mrefu na kuchelewa kukojoa wakati wa kufanya mapenzi huwa mdogo. Zoezi lenye uwezo wa kuongeza nguvu ya misuli ya uume ,linaloweza kuufanya uume kusimama kwa muda mrefu,bila kusinyaa wala kuchoka,hili ni zoezi kama mfano wa zoezi lolote la kunyanyua vyuma vizito ambalo husaidia misuli kuinuka ,kukua na kuongezeka ukubwa na nguvu. ZOEZI LA KWANZA Wataalam wa mambo ya mapenzi wamethibitisha zoezi la misuli ya uume liitwalo ”physiotherapy”ndiyo hurudisha uwezo wa nguvu za kiume za asili,zoezi hili halina madahara yoyote kiafya na linaweza kufanyika wakati wowote. JINSI YA KUFANYA ZOEZI HILI Ukiwa umekaa popote fanya zoezi hili asubuhi na jioni na hali ya kuwa hauna mkojo kabisa(yaani kojoa kwanza) Ukiwa umekaa anza kujibinya kama mtu aliyebanwa na mkojo halafu choo kipo mbali,bana ili mkojo usikutoke kwa kukaza misuli hiyo ya sehemu nyeti,fanya mara 20>25 asubuhi na jioni kila unavyobana hesabu 3 mpaka 5 kisha unaachia,unabana tena hivyo hivyo. Endelea na zoezi hilo kiasi cha wiki,baada ya wiki mbili ongeza ubanaji zaidi kutoka mara 20 mpaka 70. Endelea kufanya zoezi hili kwa wiki 6 na matokeo mazuri huanza kuonekana wiki ya 4 mpaka 6 FAIDA YA ZOEZI HILI 1.Husaidia mzunguko wa damu kuingia kwenye uume na kuufanya uume utanuke na kuwa mgumu zaidi 2. Misuli ya uume itakuwa imara na kuweza kuzuia shahawa na hivyo kukuwezesha kumridhisha mwenza wako kila mara 3. Litakuwezesha kujibana kila unapotaka kukojoa huwapo kwenye tendo la ndoa(usingoje mpaka utamu umezidi utashindwa)jibane kama unajizuia kukojoa mkojo wa kawaida lakini usikate kiuno wakati mwenzio anaendelea kutingisha nyonga. Ikiwezekana hata fikra za utamu huo zihamishe kwa sekunde kadhaa mpaka hali hiyo ya kutaka kukojoa ikiondoka zirudishe fikra ili kuendelea na mwenzio kwa pamoja katika game hilo la kiutu uzima. Kasi iendelee na utaendelea hivyo mpaka uhakikishe mwenzio amekojoa ,na anaweza kukojoa hata mara 3,yaani ukiridhika kuwa mwenzio ameridhika au ukiskia ile sauti “”inatoosha” ndyo sasa nawe ukojoe hapo mwenzio atapata raha zaidi. ZOEZI LA PILI Uinue juu na kuushusha uume wako,uchezeshe juu chini,chini juu mara 5 mpaka 10,fanya mara mbili tatu huku unapumzika kidogo,uwe unaminyaminya kidogo wakati huohuo unavuta hewa kwa pua na kuitoa kwa mdomo. fanya zoezi hili mara kwa mara japo mara 3 kwa wiki linaweza kukusaidia kuimarisha misuli yako ya uume. ZOEZI LA TATU Ufanyaji wa tendo la ndoa mara kwa mara huimarisha moyo,ubongo na misuli ya uume ,wanasayansi wamelithibitisha hili kuwa ufanyaji wa mara kwa mara husaidia uume kupata nguvu(zipo tofauti kati ya uwezo wa mwanamme mwenye mke mmoja na mwenye wake wengi) Mwenye wake wengi anaongeza nguvu zaidi, Mwenyez Mungu anataka wanaume wa kiislam waimarishe misuli hii kwa kutoa fursa ya kufanya tendo la ndoa mara kwa mara pale alipowaamrisha waoe kuanzia wake wawili mpaka wanne wakiweza. Kadri unavyoongeza mke ndivyo unavyojiongezea uwezo kwa aliyeoa wake wawili na zaidi,pima uwezo uliokuwa nao ulipokuwa na mke mmoja kisha zitazame nguvu hizo baada ya kuongeza mke wa pili watatu na wanne Ndiyo maana utakuta mtu mwenye wake wawili akifiwa na mmoja huongeza mke ili kuziba pengo hilo. ... Read More
Tatizo la Ugumba kwa wanawake  Ugumba ni hali ya mwanamke kushindwa kushika ujauzito. Linaweza kuwa tatizo pia kwa mwanaume lakini katika makala hii tutaona nini kinasababisha tatizo hili kwa upande wa wanawake. Nini husababisha ugumba kwa wanawake? Mayai kutokomaa ipasavyo: Tatizo la mayai kutokukomaa vema ndilo chanzo na sababu kuu ya wanawake wengi kushindwa kushika ujauzito na hii inachukua karibu asilimia 30 ya wanawake wote wagumba. Habari njema ni kuwa tatizo hili linaweza kurekebishwa kirahisi ikiwa mwili utapewa vile viinilishe mhimu vinavyokosekana hadi kupelekea mayai kutokomaa vizuri. Vinavyosababisha mayai ya mwanamke kutokomaa vema: (1) Matatizo ya kihomoni Matatizo katika homoni ndicho chanzo kikuu cha mayai kutunga bila kukomaa vizuri. Hatua za ukomaaji wa mayai zinategemea uwiano mzuri wa homoni na namna zinavyotegemeana katika kufanya kazi. Jambo lolote linalovuruga homoni kubaki katika uwiano wake sawa na wa kutegemeana na wenye kufanya kazi ipasavyo linaweza kupelekea utungaji wa mayai ambayo hayajakomaa vizuri. Kuna sababu kuu mbili zinazosababisha matatizo katika homoni: Ufanyaji kazi usioridhisha wa hypothalamus Hypothalamus ni sehemu ya mbele ya ubongo ambayo ina jukumu la kutuma ishara (signals) kwenda katika tezi ya pituitari ambayo yenyewe tena hutuma uchochezi wa kihomoni kwenda kwenye ovari katika mfumo wa F.S.H na L.H ili kuanzisha ukomaaji wa mayai. Ikiwa hypothalamus inashindwa kufanya kazi zake vizuri kutungwa kwa mayai ambayo hayajakomaa ndiyo kutakuwa ni matokeo yake. Tatizo hili linachukuwa asilimia 20 katika kesi za mayai kushindwa kukomaa kiasi kinachohitajika. Ufanyaji kazi usioridhisha wa tezi ya pituitari Kazi kubwa ya tezi ya pituitari ni kuzarisha na kutoa homoni mbili maalumu kwa ajili ya mfumo wa uzarishaji kufanya kazi zake vizuri ambazo zinajulikana kitaalamu kama ‘Follicle-stimulating hormone (F.S.H)’ na ‘Luteinizing hormone (L.H)’. Mayai yatashindwa kukomaa vizuri ikiwa ama L.H au F.S.H zinatengenezwa chache sana au nyingi sana kuliko inavyohitajika. Hili linaweza kutokea kama sababu ya ajari, uvimbe au kama usawa usio sawa wa kikemikali katika pituitari. (2) Kovu katika Ovari Uharibifu au ajari katika ovari unaweza kupelekea kuzalishwa kwa mayai ambayo hayajakomaa. Kwa mfano, upasuaji mkubwa, uvamizi au upasuaji wa mara nyingi wa uvimbe katika ovari unaweza kusababisha kapsuli ya ovari kupata majeraha au makovu na hivyo kwa namna moja ama nyingine kuweza kuzuia utungwaji wa mayai ambayo hayajakomaa vema. Pia maambukizi katika njia ya uzazi yanaweza kupelekea tatizo hili. (3) Dalili za mwanzo za kukaribia kufunga kuzaa (Menopause) Hii huchangia kwa asilimia chache na kwa sasa halielezeki kisawasawa. Kwamba wanawake wengi wanapokaribia umri wa kuacha kuzaa kuanzia miaka 40 kwenda juu baadhi yao hutokewa na tatizo la kutunga mayai ambayo hayajakomaa vema. Baadhi ya wanawake wanaacha kupata siku zao mapema kabla ya umri uliozoeleka yaani miaka 40 kwenda juu. Kwa sababu hiyo inadhaniwa kwamba uwezo wao wa asili katika kuzalisha mayai unakuwa umepunguwa na wengi wao huwa ni wale walikuwa wakijihusisha zaidi na michezo ya kukimbia au wale wenye historia ya muda mrefu ya kuwa na uzito pungufu na wafanyaji sana wa mazoezi. Tatizo hili pia linaweza kuwa ni la kurithi. (4) Matatizo kwenye kijishimo yai (follicle) katika ovari: Ingawa kwa sasa bado hili nalo halielezeki, hiki kijishimo yai kwa kitaalamu kinajulikana kama ‘’follicle’’ ndicho hupasuka na yai kutoka. Kuna baadhi ya kina mama wanapata dalili za kijishimo yai kutokupasuka “unruptured follicle syndrome” na matokeo yake kila mwezi mama anazalisha yai kama kawaida lakini hiki kijishimo yai kinashindwa kupasuka. Hivyo yai linabaki ndani ya ovari na utungaji wa mimba unashindwa kufanyika. Kinachosababisha ufanyaji kazi dhaifu wa mirija ya uzazi (Fallopian Tubes): Magonjwa katika mirija ya uzazi yanahusika na ugumba kwa karibu ya asilimia 25 ya wanawake wote wagumba. Hali yenyewe inatofautiana toka kwa mmoja hadi kwa mwingine kutoka kugandana au kunatana kidogo hadi kuzibika kabisa kwa mirija. Matibabu ya mirija iliyozibika huhusisha upasuaji au usafishaji wa mwili kwa kula vyakula na vinywaji maalum kwa muda wa majuma kadhaa. Sababu kubwa zinazopelekea kuzibika au kunatana kwa mirija ya uzazi ni pamoja na zifuatazo: (A) Maaambukizi Maambukizi katika njia ya uzazi ambayo yamesababishwa ama na bakteria au virusi na ambayo kwa kawaida ni magonjwa ya kuambukizana kwa njia ya tendo la ndoa, maambukizi haya kwa kawaida husababisha muwasho au kuungua na kupelekea makovu na uharibifu. Magonjwa ya zinaa kama vile kisonono na mengineyo yanaweza kuwa chanzo cha ugumba kwa wanawake wengi hasa ikiwa hayatatibiwa mapema. (B) Magonjwa yasiyo ya kawaida Magonjwa yasiyo ya kawaida ni pamoja na ugonjwa wa kidole tumbo (appendicitis) na uvimbe katika utumbo mpana (colitis), magonjwa ambayo husababisha muwasho au kuungua chini ya uvungu wa utumbo mkubwa na kuiathiri mirija ya falopiani na kama matokeo yake makovu na kuzibika kwa mirija ya uzazi hutokea. (C) Upasuaji uliopita Upasuaji una chukua nafasi kubwa katika kusababisha ugumba kutokana na matokeo yake ya kusababisha magonjwa ya mirija ya uzazi na uharibifu utokanao na huo upasuaji. Upasuaji katika utumbo mkubwa unaweza kupelekea kunatana au kugandana kwa mirija ya uzazi kutakakopelekea mayai kushindwa kusafiri kirahisi katika mirija hiyo ya uzazi. (D) Mimba kutungwa nje ya mji wa uzazi: Hii ni wakati mimba inapotungwa katikati ya mirija ya uzazi yenyewe. Katika hali kama hii hata kama kutatokea bahati kiasi gani bado kunaweza kusababisha uharibifu katika mirija na hali hii ni moja ya hali mbaya sana kiafya na kimaisha. (E) Hali ya kurithi Kwa nadra au kwa asilimia fulani ndogo baadhi ya wanawake huzaliwa na hali ya kuwa na mirija isiyo ya kawaida kwa uzazi na kwa kawaida hali hii huambatana na mji wa uzazi usio wa kawaida pia. . (5) Sababu za kitabia: Inajulikana wazi kwamba baadhi ya tabia na namna tunavyoishi kunaweza kupelekea wanandoa wakashindwa kupata mtoto. Kwa bahati nzuri nyingi kama si zote ya hizo tabia zinaweza kurekebishika au kuachwa kabisa na kupelekea siyo tu kuwa na uwezo wa kuzaa bali pia kuwa na afya nzuri kwa ujumla. Sababu hizo za kitabia ni pamoja na zifuatazo: Lishe na mazoezi Ili mfumo wa uzazi uwe na uwezo mzuri unahitaji vitu viwili mhimu, lishe kamili na mazoezi. Wanawake wenye uzito uliozidi sana au wenye uzito pungufu sana wanaweza wakapatwa na tatizo la kutopata ujauzito kirahisi. Uvutaji sigara Uvutaji wa sigara una mchango mkubwa na ugumba. Uvutaji sigara husababisha uzarishwaji wa mbegu chache kwa mwanaume (lower sperm count) kwamba mwanaume anatoa mbegu chache sana ama pungufu wakati huo huo uvutaji sigara huchangia katika tatizo la kutoka kwa mimba, kuzaa kabla ya miezi 9 (njiti), na kuzaa mtoto mwenye uzito mdogo kwa wanawake. Unywaji pombe Unywaji pombe kupita kiasi una mchango mkubwa sana katika ugumba na hii hata ikitokea mama akapata ujauzito kama bado anaendelea kunywa pombe inaweza kupelekea matatizo hata kwa mtoto mtarajiwa. Unywaji pombe pia huchangia uzarishwaji wa mbegu chache kwa wanaume. Madawa ya kulevya Utumiaji a madawa ya kulevya kama bangi na mengine ya kujidunga kwa sindano kunaweza kuwa sababu ya kuzalisha mbegu chache kwa wanaume. Utumiaji wa dawa za kulevya kama ‘Cocaine’ kwa mama mjamzito kunaweza kusababisha mtindio wa ubongo na matatizo katika figo kwa mtoto mtarajiwa. Matumizi ya madawa ya kulevya inafaa yaepukwe wakati wa kutafuta ujauzito na wakati wa ujauzito. Utowaji mimba Utowaji mimba wa mara kwa mara pia unahusika sana na tatizo la ugumba kwa karibu ya asilimia 20. Utowaji mimba unaweza kusababisha makovu katika mji wa uzazi na hata kuharibika kabisa kwa mji wa uzazi ikiwa utowaji huo haukufanyika kitaalamu au unafanyika mara kwa mara. (6) Sababu za ugumba za kimazingira: Uwezo wa kushika ujauzito unaweza pia kuathiriwa kutokana na kuwa karibu na baadhi ya kemikali au sumu katika maeneo ya kazi au makazi. Vitu viwezavyo kusababisha mabadiliko, dosari za kuzaliwa, utokaji mimba, au utasa huitwa ‘Sumu kwa mfumo wa uzazi’. Kamikali zifuatazo zinahusishwa na ugumba au utasa: Risasi (Lead) Kuwa karibu na kemikali au sumu zinazounda risasi kunaweza kuwa sababu ya ugumba. Risasi hupelekea kuzalishwa kwa mbegu zisizo za kawaida kwa wanaume zijulikanazo kwa kitaalamu kama ‘teratospermias’ na inafikirika pia kuhusika na utokaji mimba kusiko kwa asili (artificial abortion). Baadhi ya matibabu na madawa ya hospitalini Kuwekwa kwenye matibabu yanayohusisha mionzi (x-rays), mionzi ya kawaida au hata ile ya kutibia kansa (chemotherapy), kunaweza kusababisha matatizo katika uzarishwaji wa mbegu kwa mwanaume na wakati huo huo kuchangia kwa sababu kadhaa zinazopelekea kutungwa kwa mayai ambayo hayajakomaa vizuri. Pia matumizi ya dawa za kuzuia ujauzito kwa muda mrefu yamekuwa yakihusishwa na ugumba kwa miaka ya hivi karibuni ingawa bado kuna mjadala mkubwa katika hili. Ethylene Oxide Hii ni kemikali inayotumika kusafishia vifaa vya upasuaji, pia hutumika katika kutengeneza baadhi ya sumu za kuua wadudu. Ethylene oxide inaweza kupelekea matatizo katika uzazi hasa katika miezi ya mwanzo mwanzo ya ujauzito na inahusishwa sana na tatizo la utokaji mimba katika miezi ya mwanzo ya ujauzito (early miscarriage). Dibromochloropropane (DBCP) Hii pia ni kemikali au dawa inayotumika katika kuua wadudu, ikiwa unafanya nayo kazi kila mara inaweza kusababisha kutungwa kwa mayai yasiyokomaa vizuri, kuelekea mapema kwa ukomo wa kutokuzaa kabla hata ya miaka 40 au 45 (early menopause) na kadharika. (7) Sababu zingine zinazoweza kusababisha ugumba kwa mwanamke: Karibu asilimia 10 ya ugumba kwa wanawake ni matokeo ya mji wa uzazi usio wa kawaida (abnormal uterus). Hali zingine ni pamoja na uvimbe katika kizazi, kugandana au kunatana kwa mji wa uzazi na mirija ya uzazi. Karibu asilimia 3 ya ugumba kwa wanawake ni matokeo ya matatizo ya ute usio wa kawaida katika mlango wa kizazi (femaleís cervical mucus). Ute ute huu unahitaji kuwa na hali fulani maalumu kwa mbegu za kiume kuweza kuogelea kirahisi katikati yake. Chanzo kikubwa cha tatizo hili ni usawa usio sawa wa homoni za kike ambapo homoni ya uzazi ya kike iitwayo ‘estrogen’ yaweza kuwa ni chache sana au homoni nyingine iitwayo ‘progesterone’ yaweza kuwa ni nyingi sana tofauti na inavyohitajika. Vitu vya kuepuka kwa mtu mwenye tatizo la ugumba: ChipsiVinywaji baridiKaffeinaNyama nyekunduVilevi ... Read More
📶happy birthday you my love 🆗#Najua_Umejifunza_mengi________Tanguu_umekuwa_mtoto_mpaka_now_umekuwaa😘😘😘😘 #____umejionea_mengi_hapa_dunian😧😧 ‼‼‼#___yasikutishe_coz_god_Yuwetu_sote😍😍 #__Amini_UHAI_tu_ndo_muimu_vingine_mapito_tuuu😧😧 #Happy_b_day____ ❇❇my.. Best ❇❇my.. Blood ❇❇rohoo.. Yang.. Kipenz... Changu ❔⁉⁉❔❔⁉MPAKA..Nasahau majina sijui nikuitajeee jamn rohoo ilizikeee 🎂🎁🎁🎂🎊🎊🎇🎉🎀🎂🎂🎂🎆 ... Read More
Utajuaje Kama Mahusiano Uliyonayo Yatadumu.  Dalili 8 zitakuonyesha kama upo kwenye mahusiano ya kudumu au hapana. Afya. Wote tunafikiria kuhusu hili. hasa kwa kadri tunavyoendelea kukua , tunatembelea madaktari, tunakula vizuri wakati mwingine. Tunatafuta dalili na wakati mwingine matokeo yake yanatuambia kuwa hali zetu sio nzuri. Lakini tunapofikiria afya, tunafanya hivyo katika miili yetu tu. mara nyingi tunasahau kufikiria kuhusu afya ya mahusiano na mapenzi. Tunaangalia zaidi afya ya mwili katika maisha ,lakini kuwa na afya nzuri katika mahusiano ni vitu vinavyoungana. Kwa kurahisisha , mahusiano mabaya hayadumu. au ingawa yanaweza kukaa kwa muda fulani.Na kama yakidumu , atakuwepo mtu wa kuumia. Lakini ni nini hasa afya ya mahusiano? Tutajuaje kama mahusiano yetu yatadumu? Utajuaje kama uko na mtu sio sahihi, mtu ambaye mtaishia kwenye kona fulani tu? Hakuna kipimo halisi cha kujua. Hakuna kipima joto kinaweza kupima kiasi cha muda wa mahusiano kuwa ni ya moto au baridi. Kwa bahati kuna hizi dalili 8 ambazo zinaweza kukusaidia kujua afya iliopo kwenye mahusiano yako. 1.Mchumba wako atakuwa na imani na wewe , na wewe utakuwa na imani naye.  Hataongea kwa ajili yake bali ataongea kwa ajili yenu wote. atakukumbusha pale unapokuwa umesahau au unapokuwa na mashaka kwa jinsi ulivyo. Ana maono ya wazi ya muhimu kwako. atalea hali hio na utaiona. Vilevile na upande wako utakuwa kama yeye. hutamsema vibaya kwa marafiki, hutalalamika kitu bali utaongea mbele yake. Utamwamini kuwa yuko kamili , mtu anayeweza kutatua matatizo na kusimama kwa miguu yake. Hata kama haujamsaidia kitu. 2.Unamwamini. Unamwamini katika ukweli wake wote. ahadi zake ni za kweli. utamkubali alivyo. Anahusika katika majukumu yake. 3.Unakubali mambo yake yaliopita na yeye anakubali ya kwako. Jinsi alivyokuwa, alikuwa na wanawake wangapi, wanaume wangapi. hutajali. utamkubali alivyo ili mkue pamoja. hutafikiria kitu chochote kilichopita, bali utakuwa na hamu ya kutaka kujua jinsi gani huyo mtu alivyo. Mahusiano yako yatakuwa yamekusanya, Msamaha na kuachilia yaliopita. 4.Unashukuru kwa vitu vizuri mlivyonavyo Unakubaliana na vitu vidogo vidogo anavyovifanya kwako. unakuwa na matumaini, husubiri kupata kazi, kwa ajili ya mshahara, kwa ajili ya mambo mengine. unashukuru kwa kile mlichonacho sasa na mwenza wako. Mnafuraha wakati huu. hana mchezo wa kijinga. anatengeneza pesa ya kutosha. anafanya kitu akipendacho. Utakuwa unalenga safari sio mwisho wa ndoa, mtoto, sherehe, vitu vinatokea kwa kawaida. 5.Mawasiliano ni ya wazi na ya kueleweka kwa kila mmoja. Hakuna wa kusubiri ni nani atamtafuta mwenzake. kila mtu anakuwa na jukumu la kufanya hivyo. Na kama itatokea mmoja hakuhusika , hakuna lawama, kwa kuwa mnaelewa . utavaa moyo wake. hutahangaika kuyatawala mahusiano kwa sababu hamfanyi mchezo wa kuigiza. 6.Maisha yenu ya sex yataendelea kuwa mazuri na ya kupendeza. Kwa sababu ya urafiki ambao mnao, maisha yenu ya mahusiano yatakuwa rahisi na ya kimapenzi. Ya ukaribu zaidi. sex itakuwa sio kipaumbele chenu bali ni matokeo ya upendo mlionao. mahitaji yenu ya kimwili yatatosheka kwa pamoja. 7.Utamuheshimu na yeye Atakuheshimu wewe. Kila mtu anaheshimu mipaka ya mwenzake na mnaweza kuhimizana katika kutimiza malengo yenu. kama unapenda kucheza , atakuhimiza kufanya hivyo. hutahitaji kukamilisha hisia zako zote. atakuwa na mahusiano mazuri na watu wengine pia. Ni mtu muhimu kwako. anakufanya ujisikie vizuri. 8.Malengo yenu yanafanana. Hutajaribu kumbadilisha. au kujaribu kuomba kuishi na yeye. hutahitaji awe mtu wa kutengeneza kitu chako. ni mtu ambaye ulimtaka awe wako. thamani yake ni muhimu katika maswali hata. Unataka watoto? Unapenda kusafiri? Una hamu ya kupata uzoefu fulani? unakubaliana katika mambo ya pesa? Una furaha unapokuwa naye? Unataka kuishi naye na kuwa naye chumba kimoja? Afya ya mahusiano yako ni muhimu katika maisha ya ndoa utakayoingia. Lakini hakuna kipimo cha kupimia uzima huo. Ni wewe tu na mwenza wako mnajua kama mahusiano yatadumu au yataishia kwenye kona. yatakuwa na matunda au hapana. Mttajua kama ni mazuri au sio. hizo dalili nane zikusaidie kufahamu kama ni ya afya au sio, yatadumu au hayatadumu. ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: