SIRI ZA GIZANI 3 Shemeji alilia sana pale hospitalini, maana alihisi kukatwa mguu wake itakuwa ni kama kapoteza kitu kikubwa sana katika maisha yake na isitoshe alikuwa ni mwanamke mrembo alie vutia sana na alipenda kupendeza mda wote, hivyo ilikuwa inamuuma sana. Kaka akamwambia, "mke wangu, naomba ukubali tu ukatwe huo mguu, kwani wewe hujioni mguu ulivyo kuwa, kila siku mguu unaoza, kila siku unauma, usiku hatulali mke wangu unalia tu ndani, naomba ukubali tu kukatwa, mimi siwezi kukuacha nitakuwa na wewe kwenye changamoto zozote za dunia" huwezi kuamini shemeji alikataa kabisa kukatwa ule mguu, sasa kutokana na ule ugonjwa ikabidi kaka amuite mama kutoka kijijini aje kukaa nyumbani kwake ili amuuguze mke wake, maana biashara zao zilianza kuyumba kutokana na kukosa mda wa kuziangalia, maana walitumia mda mwingi kumuuguza shemeji. Mama yetu alisafiri kutoka kijijini akaenda kukaa pale nyumbani kwa kaka kumuuguza shemeji. mama alienda na kuku wawili moja jogoo nyingine kuku wa kutaga kawaida. Watoto wa kaka yaani Ibra na Nasra walifurahi sana kumuona bibi yao. Ila kumbe bibi yao alikuwa mchawi na alitoka amefungasha dawa za kutosha kutoka kijijini akaja nazo mjini, kuisumbua familia ya kaka, sisi hatukujua kama ni mchawi maana alitulea vizuri tu tangu tukiwa wadogo. Alafu na wale kuku wawili, kumbe jogoo alikuwa ni Ibra, alafu kuku wakutaga kawaida alikuwa ni Nasra, hivyo kuku ambayo ingechinjwa kwanza basi mtoto wa kaka mmoja angekufa na kama zinge chinjwa zote pia wangefariki wote. Hakuna alie fahamu kabisa kama mama angeweza kufanya mambo kama yale, maana tulikuwa tuna muheshimu sana sisi. kaka alipo kuwa anaenda kazini, mama alikuwa anaonyesha upendo sana mchana kwa mkwe wake, wakawa marafiki sana, lakini kumbe mama hakupenda ata mkwe wake apone alitamani kuona ata anakufa tu, Sasa kwa sababu ya ule mguu kumuuma sana shemeji, hivyo ata kujisaidia kwake ilikuwa ni ngumu sana, sasa bibi alicho kuwa anafanya ni kuchukua kopo kisha analiweka karibia na sehemu nyeti za shemeji ili aweze kujisaidia, lakini ilikuwa aisadii kabisa maana mkojo wake wote ulikuwa unaishia chini. Shemeji alikuwa analia tu, maana hakuamini kama angeweza kujikojolea na utu uzima wake wote, USIKOSE_4

at 10:53 PM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top