Home → ushauri
→ SIMULIZI FUPI :
BUSU KABLA YA KIFO
John alimshika mkono mchumba wake Alice wakitoka nje ya ofisi za Paroko wa kanisa la Mt. Francis Ksaveri la Nyakahoja kuelekea walikoegesha gari lao pembezoni mwa kanisa hilo. Kanisa la Nyakahoja ni moja ya parokia maarufu zaidi mkoani Mwanza na ilijulikana kama parokia ya watu mashuhuri. Mtaani wengine waliita parokia ya mabishoo. Ukienda Nyakahoja siku ya Jumapili usishangae ukipigana vikumbo na Mkuu wa Mkoa, Majaji, Makamanda wa Polisi n.k kwani wakatoliki wengi mashuhuri walikuwa wanasali kanisani hapo. Zaidi ya yote ni parokia pekee iliyokuwa na misa ya kiingereza, na kihindi. Jinsi ilivyo Parokia ya Mt. Petro ya Oysterbay kwa watu wa Dar, ndivyo ilivyo Parokia ya Mt. Francis kwa watu wa Mwanza.
Kanisa hilo lipo pembezoni mwa ziwa Victoria limezungukwa na ukuta uliolitenganisha na ziwa hilo kati yake na ziwa kukiwa na barabara ya kwenda Airport. Upande wa pili wa barabara hiyo kulikuwa kumetanda vibanda kadhaa vya wauza mbao na kwa mbali uliweza kuona eneo la Mwaloni ambako wavuvi na mitumbwi yao walikuwa wakibahatisha bahati zao kwenye hilo ziwa la maji baridi.
Jioni hiyo upepo ulipunga taratibu huku sauti za milio ya gari zikisikika lakini kutokana na ule ukuta basi makali ya sauti hayakuwa makubwa kufika kanisani. Kwenye moja ya vibanda vya kupumzikia vilivyoko nje ya kanisa hilo kulikuwepo na kwaya ya vijana wakifanya mazoezi, huku vijana wengine wakicheza mpira wa nyavu kwenye uwanja ulio upande wa kushoto wa Kanisa hilo.
John na Alice walikuwa ni miongoni mwa wachumba kadhaa waliokuwepo hapo Nyakahoja kwa mafundisho ya ndoa siku hiyo ya Jumamosi. Walitarajia kufunga ndoa mwezi wa nane kwenye Kanisa hilo Katoliki la Kiroma. Kama kawaida baada ya mafundisho wapenzi hao wawili walipata muda wa kukaa na kuzungumza mawili matatu kuhusu maandalizi ya harusi kabla ya kwenda kwenye hoteli ya Victoria katikati ya Jiji kupata chakula cha jioni.
“Baba anataka kuzungumza na wewe” Alice alisema huku akimminya mkono John kwa hali ya mahaba.
Hisia kubwa ya mapenzi ilimuingia John, na dakika ile alijua kuwa uamuzi wa kumuoa Alice ulikuwa ni sahihi na alikuwa tayari kuahidi mbele ya Mungu na wanadamu kufanya lolote kumpa maisha mazuri binti huyo wa watu.
“Kuna tatizo gani?” John aliuliza huku akisimama kwa sekunde chache kumuangalia Koku. Pole pole na kwa mwendo wa kusuasua waliendelea kuelekea walikoegesha gari kwenye ukingo wa ukuta wa barabara, chini ya mti mkubwa. Kulikuwa na magari mengine matatu yameegeshwa eneo hilo. John alikuwa ameshika ufunguo wa gari kwa mkono mwingine huku akiurusha rusha hewani. Ilikuwa ni ajabu kwa Mzee Patrick kutoa mwito wa kumuona John, kwani wakati wowote ule John alikuwa anakaribishwa nyumbani kwa mzee huyo maeneo ya Igoma nje kidogo ya Jiji la Mwanza kwenye barabara ya kwenda Musoma. Nyumbani kwa Mzee Patrick palikuwa ni nyumbani kwa John; alienda bila mwaliko.
Mzee Patrick Rutashobya, alikuwa ni mkimya na asiyependa sana kufuatilia mambo ya vijana wake na katika uzee wake amejikuta anapenda zaidi kukaa nyumbani na kuangalia wajukuu zake. Katika miaka ya utumishi wake aliwahi kuitumikia Tanzania kama balozi katika nchi kadhaa zikiwemo Zimbabwe, Ufaransa, Ubelgiji na Ujerumani. Mwaka 1997 mke wake aliyedumu naye kwa miaka 32 alifariki dunia kitu kilichomfanya mzee Rutashobya kuamua kustaafu toka katika ajira ya serikali. Hata hivyo, mzee huyo hakujifunga na huzuni au kukubali kugubikwa na majonzi bali aliendelea na shughuli zake binafsi ikiwemo kufungua hoteli mpya na ya kisasa iliyoko pembezoni mwa uwanja wa CCM Kirumba, iliyojulikana kwa jina la Paradiso.
“Hakuna tatizo lolote” Alice alimjibu na kumwambia kuwa wakitoka Kanisani kesho basi aende kumuona mzee nyumbani huko Igoma. Walikubaliana kwa hilo na John alimfungulia Alice mlango na akaingia garini huku sketi yake fupi ya kijivu iliyombana mapajani ikijikunja na kuonyesha mapaja yake yaliyopendeza na kunona. John aliangalia kwa sekunde chache na kuombea ile siku ifike ile ale vya “kwake” pasipo kuiba. John alizunguka mbele ya gari na kuingia upande wa dereva. Harufu ya manukato mazuri ya Paradise ya Chanel aliyekuwa amejipulizia Koku ilijaza gari hilo. John alijihisi yuko karibu na pepo.
“Alice, nakupenda sana” John alisema kabla hajawasha gari huku akimwangalia Alice aliyekuwa akijiweka vizuri kwenye kiti na kujifunga mkanda wa usalama. Koku alichukua mkoba wake na kutafuta rangi yake ya mdomoni. Alice alimgeukia John na kumvuta karibu, alimwangalia machoni na kumuambia kuwa na yeye anampenda zaidi. Wakiwa bado wamekaa ndani ya gari hilo aina ya Toyota Sequoia la rangi nyeusi iliyokuwa na vioo vya giza John alimmwagia busu zito tena la nguvu. Alice naye alirudisha busu hilo na kwa dakika chache walipeana busu motomoto; sauti za miguno zikiwatoka. Waliachiana na kuamua kutoka hapo kabla Padre Massawe hajawazukia.
John alirudisha gari nyuma hadi alipopata nafasi ya kuweza kuligeuza kuelekea getini na nje ya eneo la kanisa hilo. Mawazoni alikuwa anamfikiria Alice, mapenzi yake kwake na zaidi ya yote jinsi uhusiano wao ulivyokuwa. Alimshukuru Mungu kuwa amempa mwenzi ambaye atakuwa ni mke mwema na mama wa watoto wake. Kati ya wanawake wote aliowahi kuwa na urafiki nao John hakuwahi kuwa karibu na yeyote kama alivyo kwa Koku. Akiwa na Koku alijihisi yuko huru kusema chochote, na hakuficha hisia zake. Koku alikuwa ni binti anayejua kusikiliza, na ni mcheshi. Wakati mwingie kile kicheko chake tu kilimtuliza John na kumuhakikishia kuwa mambo yatakuwa poa. Alipofika getini akiwa katika dimbwi la mawazo John aliangalia kulia na tena kushoto na kumtazama Koku aliyekuwa anang’aa utadhania malkia. John alisubiri viexpress na magari kadhaa yapite ili apate nafasi ya kuingia barabarani.
“Unakumbuka tulipofanya mapenzi mara ya kwanza” John alimuuliza, huku akiangua kicheko cha kinafiki.
“Nisahau nichekwe!” Alice alijibu. John alijisemea moyoni, “kweli asahau achekwe”. Wakiwa bado hapo, akili ya John na mawazo yake yakazima kuikumbuka siku ile waliyokutana kimwili kwa mara ya kwanza na mpenzi wake. Ilikuwa kinyume kabisa na mafundisho yao ya dini yaliyowataka kusubiri kukutana hadi wawe mume na mke. Ilikuwa ni siku ambayo majaribu waliyafungulia mlango na yakapita hadi chumbani. Bila ya shaka Alice naye alikuwa amepotelea kwenye mawazo hayo hayo. Walishikana mikono huku wakisubiri zamu yao kwani magari yalikuwa yakienda kwa kasi kutoka Uwanja wa CCM Kirumba ambako timu ya Simba ilikuwa imecheza na timu ya SC Villa ya Uganda.
Walizama katika mawazo.
* * *
Ilikuwa siku ya Jumapili jioni John na Alice walielekea eneo la Nyegezi nje kidogo ya Jiji la Mwanza kwenda kuangalia kiwanja ambacho mzee Rutashobya amewanunulia ili wajenge nyumba yao. Barabara ya nyegezi ilikuwa ni ya vumbi kubwa na licha ya mvua iliyonyesha jana yake, ardhi ilikuwa kavu utadhani haijawahi kulowa. John alikata kona kwenye makutano ya barabara ya Shinyanga na ile ya kuelekea kwenye Chuo cha Jamii cha Nyegezi na baada ya mwendo kidogo alikata kona kulia tena kueleke kiliko chuo cha Uvuvi Nyegezi. Eneo hilo zaidi lilikuwa na viunga vya mpunga, na upande wa kulia kulikuwa na viwanja ambavyo vingine vilishaanzwa kujengwa. Kiwanja chao kilikuwa kwenye kona ya vilima viwili vya mawe. Waliegesha gari lao kwenye kibanda cha mafundi, na baada ya dakika chache za kuangalia angalia hapo na kumsalimia mlinzi, waliamua kwenda juu ya vilima vile vya mawe kuangalia jua linavyozama.
Walifika kileleni na waliweza kuona vizuri mandhari ya ziwa Victoria likiangazwa kwa mionzi ya dhahabu ya jua linaloanza kuzama. Mawe makubwa yaliyojipanga utadhani matofali yaliwazunguka wapenzi hao wawili na kuwaficha na mtu yeyote yule huku yakiwapa kivuli kizuri na upepo mwanana wenye harufu ya Sangara toka ziwani ukiwapepea. Ndege aina ya mbayuwayu walikuwa wakiruka huku na kule huku kundi la nyangenyange likipepea angani kama herufi ya v. John alikuwa ameketi chini huku miguu yake ikining’inia kwenye jiwe, Alice aliamua kulala chali huku akiwa amekunja miguu yake, kichwa chake akiwa amekiagamia kwenye mapaja ya John.
“Hivi unafikiri watamaliza kujenga kabla ya harusi?” Alice alimuuliza John huku akimuangalia kwa macho yake yenye upole wa njiwa lakini yenye kuashiria ujanja wa sungura.
“Natumaini hivyo, sitaki kuendelea kupanga tukishafunga ndoa” John alijibu. John aliacha kuzichezea nywele za Alice na kuanza kufungua vifungo vya blauzi yake. Kifua cha Alice kilikuwa kimetuna siyo tu kwa kujaliwa maziwa yapendezayo, bali hata sidiria aliyovaa ni ile inayonyanyua matiti na hivyo kuyafanya yaonekane kama maembe dodo yanayoning’inia mtini. Alice alijinyanyua na kuiteremsha sidiria yake hadi tumboni bila kuifungua. Alirudi na kuendelea kuegama kwenye mapaja ya mpenzi wake. John, huku mkono wake wa kushoto ukiwa unampa egemezo kwenye mwamba, mkono wake wa kulia ulinza kuyachezea matiti ya Alice, na kwa upole kama anayegusa almasi alizichezea chuchu za binti huyo wa Kihaya. Alice hakusema kitu bali alifumba macho na kufurahia mikono migumu ya mpenzi wake iliyompa raha isiyo kifani.
Jua lilikaribia kuzama kabisa na rangi ya mionzi yake ilibadilika toka ile ya dhahabu na kuwa nyekundu ya damu. Ndege walianza kutoweka angani na kurudi kwenye viota vyao.
Alice alikuwa fundi wa mapenzi. Hakumbakishia wala kumpa kwa kibaba alimpa yote huku John na yeye akijibu mapigo kiufundi. Walikuwa wamelowa jasho walipofika kilele kwenye miamba ya jiji la Mwanza. Kwa karibu dakika chache waliendelea kukumbatiana huku wakitaka muda usiende au kesho isije. Walipomaliza kiza kilikuwa kimeshaingia. Bila ya haraka wakavaa nguo zao, kuanza kuteremka kutoka vilele vyote viwili; kuelekea walikopaki gari lao. Mlinzi alisema alianza kuingiwa na wasiwasi lakini John alimhakikishia kuwa walitaka tu kuona jua “linavyozama” kando ya “ziwa Victoria”. Mzee wa Kimakonde hakujua walimaanisha nini. Waliondoka na kurudi nyumbani.
* * *
“John, angalia gari hilo!” Alice alipiga kelele kumzindua John aliyekuwa bado amezama kwenye dimbwi la kumbukumbu ya tendo la mapenzi siku kule Nyegezi. John alishtuka na kuzinduka. Alikuwa ameishaanza kuingia barabarani na hakupata nafasi ya kuliona lori la Scania lilikokuwa linakuja kwa kazi likitokea Pasiansi. Licha ya jitihada zake za kukata kona na kuongeza kasi kuokoa maisha yake na ya mpenzi wake hakuweza kulizidi mwendo lori hilo.
Sauti ya breki zilisikika huku matairi ya gari yakisugua barabara hiyo ya lami. Wapenzi hao hawakuwa na nafasi! Kwani lori la Scani hilo lililokuwa limesheheni magunia ya dagaa liliwaparamia kwa nguvu zote na kusababisha mlio mkubwa wa mgongano uliosika hadi maeneo ya Hospitali ya Sekou Toure. Lori hilo liliwaburuza kwa karibu mita mia moja hadi kwenye lango la shule ya Nyakahoja huku gari lao la Toyota likiwa limekunjwa kunjwa kama karatasi! Magari hayo mawili yalipoweza kusimama, matokeo yalikuwa ni dhahiri. Miili ya wapenzi hao ilikuwa imepondwa pondwa huku baadhi ya viungo vyao vikiwa vimetupwa kando ya barabara na damu ikiwa imesambaa ndani ya gari lao. Ndoto ya maisha yao baada ya ndoa ilifutiliwa mbali kama jani linavyopeperushwa na upepo. Kwa dakika na muda wa karibu miaka miwili tangu wakutane, wapenzi hao wawili wakawa wameiunganishwa milele kwa damu.
Msiba wa John na Alice ulikuwa mkubwa; uliouma wengi na ulioacha kumbukumbu za kudumu katika parokia ya Nyakahoja. Walizikwa pamoja kama wachumba; hawakupata nafasi ya kufunga ndoa katika maisha haya; lakini mauti iliwafunga pingu ya mwisho.
MWISHO
SIMULIZI FUPI : BUSU KABLA YA KIFO John alimshika mkono mchumba wake Alice wakitoka nje ya ofisi za Paroko wa kanisa la Mt. Francis Ksaveri la Nyakahoja kuelekea walikoegesha gari lao pembezoni mwa kanisa hilo. Kanisa la Nyakahoja ni moja ya parokia maarufu zaidi mkoani Mwanza na ilijulikana kama parokia ya watu mashuhuri. Mtaani wengine waliita parokia ya mabishoo. Ukienda Nyakahoja siku ya Jumapili usishangae ukipigana vikumbo na Mkuu wa Mkoa, Majaji, Makamanda wa Polisi n.k kwani wakatoliki wengi mashuhuri walikuwa wanasali kanisani hapo. Zaidi ya yote ni parokia pekee iliyokuwa na misa ya kiingereza, na kihindi. Jinsi ilivyo Parokia ya Mt. Petro ya Oysterbay kwa watu wa Dar, ndivyo ilivyo Parokia ya Mt. Francis kwa watu wa Mwanza. Kanisa hilo lipo pembezoni mwa ziwa Victoria limezungukwa na ukuta uliolitenganisha na ziwa hilo kati yake na ziwa kukiwa na barabara ya kwenda Airport. Upande wa pili wa barabara hiyo kulikuwa kumetanda vibanda kadhaa vya wauza mbao na kwa mbali uliweza kuona eneo la Mwaloni ambako wavuvi na mitumbwi yao walikuwa wakibahatisha bahati zao kwenye hilo ziwa la maji baridi. Jioni hiyo upepo ulipunga taratibu huku sauti za milio ya gari zikisikika lakini kutokana na ule ukuta basi makali ya sauti hayakuwa makubwa kufika kanisani. Kwenye moja ya vibanda vya kupumzikia vilivyoko nje ya kanisa hilo kulikuwepo na kwaya ya vijana wakifanya mazoezi, huku vijana wengine wakicheza mpira wa nyavu kwenye uwanja ulio upande wa kushoto wa Kanisa hilo. John na Alice walikuwa ni miongoni mwa wachumba kadhaa waliokuwepo hapo Nyakahoja kwa mafundisho ya ndoa siku hiyo ya Jumamosi. Walitarajia kufunga ndoa mwezi wa nane kwenye Kanisa hilo Katoliki la Kiroma. Kama kawaida baada ya mafundisho wapenzi hao wawili walipata muda wa kukaa na kuzungumza mawili matatu kuhusu maandalizi ya harusi kabla ya kwenda kwenye hoteli ya Victoria katikati ya Jiji kupata chakula cha jioni. “Baba anataka kuzungumza na wewe” Alice alisema huku akimminya mkono John kwa hali ya mahaba. Hisia kubwa ya mapenzi ilimuingia John, na dakika ile alijua kuwa uamuzi wa kumuoa Alice ulikuwa ni sahihi na alikuwa tayari kuahidi mbele ya Mungu na wanadamu kufanya lolote kumpa maisha mazuri binti huyo wa watu. “Kuna tatizo gani?” John aliuliza huku akisimama kwa sekunde chache kumuangalia Koku. Pole pole na kwa mwendo wa kusuasua waliendelea kuelekea walikoegesha gari kwenye ukingo wa ukuta wa barabara, chini ya mti mkubwa. Kulikuwa na magari mengine matatu yameegeshwa eneo hilo. John alikuwa ameshika ufunguo wa gari kwa mkono mwingine huku akiurusha rusha hewani. Ilikuwa ni ajabu kwa Mzee Patrick kutoa mwito wa kumuona John, kwani wakati wowote ule John alikuwa anakaribishwa nyumbani kwa mzee huyo maeneo ya Igoma nje kidogo ya Jiji la Mwanza kwenye barabara ya kwenda Musoma. Nyumbani kwa Mzee Patrick palikuwa ni nyumbani kwa John; alienda bila mwaliko. Mzee Patrick Rutashobya, alikuwa ni mkimya na asiyependa sana kufuatilia mambo ya vijana wake na katika uzee wake amejikuta anapenda zaidi kukaa nyumbani na kuangalia wajukuu zake. Katika miaka ya utumishi wake aliwahi kuitumikia Tanzania kama balozi katika nchi kadhaa zikiwemo Zimbabwe, Ufaransa, Ubelgiji na Ujerumani. Mwaka 1997 mke wake aliyedumu naye kwa miaka 32 alifariki dunia kitu kilichomfanya mzee Rutashobya kuamua kustaafu toka katika ajira ya serikali. Hata hivyo, mzee huyo hakujifunga na huzuni au kukubali kugubikwa na majonzi bali aliendelea na shughuli zake binafsi ikiwemo kufungua hoteli mpya na ya kisasa iliyoko pembezoni mwa uwanja wa CCM Kirumba, iliyojulikana kwa jina la Paradiso. “Hakuna tatizo lolote” Alice alimjibu na kumwambia kuwa wakitoka Kanisani kesho basi aende kumuona mzee nyumbani huko Igoma. Walikubaliana kwa hilo na John alimfungulia Alice mlango na akaingia garini huku sketi yake fupi ya kijivu iliyombana mapajani ikijikunja na kuonyesha mapaja yake yaliyopendeza na kunona. John aliangalia kwa sekunde chache na kuombea ile siku ifike ile ale vya “kwake” pasipo kuiba. John alizunguka mbele ya gari na kuingia upande wa dereva. Harufu ya manukato mazuri ya Paradise ya Chanel aliyekuwa amejipulizia Koku ilijaza gari hilo. John alijihisi yuko karibu na pepo. “Alice, nakupenda sana” John alisema kabla hajawasha gari huku akimwangalia Alice aliyekuwa akijiweka vizuri kwenye kiti na kujifunga mkanda wa usalama. Koku alichukua mkoba wake na kutafuta rangi yake ya mdomoni. Alice alimgeukia John na kumvuta karibu, alimwangalia machoni na kumuambia kuwa na yeye anampenda zaidi. Wakiwa bado wamekaa ndani ya gari hilo aina ya Toyota Sequoia la rangi nyeusi iliyokuwa na vioo vya giza John alimmwagia busu zito tena la nguvu. Alice naye alirudisha busu hilo na kwa dakika chache walipeana busu motomoto; sauti za miguno zikiwatoka. Waliachiana na kuamua kutoka hapo kabla Padre Massawe hajawazukia. John alirudisha gari nyuma hadi alipopata nafasi ya kuweza kuligeuza kuelekea getini na nje ya eneo la kanisa hilo. Mawazoni alikuwa anamfikiria Alice, mapenzi yake kwake na zaidi ya yote jinsi uhusiano wao ulivyokuwa. Alimshukuru Mungu kuwa amempa mwenzi ambaye atakuwa ni mke mwema na mama wa watoto wake. Kati ya wanawake wote aliowahi kuwa na urafiki nao John hakuwahi kuwa karibu na yeyote kama alivyo kwa Koku. Akiwa na Koku alijihisi yuko huru kusema chochote, na hakuficha hisia zake. Koku alikuwa ni binti anayejua kusikiliza, na ni mcheshi. Wakati mwingie kile kicheko chake tu kilimtuliza John na kumuhakikishia kuwa mambo yatakuwa poa. Alipofika getini akiwa katika dimbwi la mawazo John aliangalia kulia na tena kushoto na kumtazama Koku aliyekuwa anang’aa utadhania malkia. John alisubiri viexpress na magari kadhaa yapite ili apate nafasi ya kuingia barabarani. “Unakumbuka tulipofanya mapenzi mara ya kwanza” John alimuuliza, huku akiangua kicheko cha kinafiki. “Nisahau nichekwe!” Alice alijibu. John alijisemea moyoni, “kweli asahau achekwe”. Wakiwa bado hapo, akili ya John na mawazo yake yakazima kuikumbuka siku ile waliyokutana kimwili kwa mara ya kwanza na mpenzi wake. Ilikuwa kinyume kabisa na mafundisho yao ya dini yaliyowataka kusubiri kukutana hadi wawe mume na mke. Ilikuwa ni siku ambayo majaribu waliyafungulia mlango na yakapita hadi chumbani. Bila ya shaka Alice naye alikuwa amepotelea kwenye mawazo hayo hayo. Walishikana mikono huku wakisubiri zamu yao kwani magari yalikuwa yakienda kwa kasi kutoka Uwanja wa CCM Kirumba ambako timu ya Simba ilikuwa imecheza na timu ya SC Villa ya Uganda. Walizama katika mawazo. * * * Ilikuwa siku ya Jumapili jioni John na Alice walielekea eneo la Nyegezi nje kidogo ya Jiji la Mwanza kwenda kuangalia kiwanja ambacho mzee Rutashobya amewanunulia ili wajenge nyumba yao. Barabara ya nyegezi ilikuwa ni ya vumbi kubwa na licha ya mvua iliyonyesha jana yake, ardhi ilikuwa kavu utadhani haijawahi kulowa. John alikata kona kwenye makutano ya barabara ya Shinyanga na ile ya kuelekea kwenye Chuo cha Jamii cha Nyegezi na baada ya mwendo kidogo alikata kona kulia tena kueleke kiliko chuo cha Uvuvi Nyegezi. Eneo hilo zaidi lilikuwa na viunga vya mpunga, na upande wa kulia kulikuwa na viwanja ambavyo vingine vilishaanzwa kujengwa. Kiwanja chao kilikuwa kwenye kona ya vilima viwili vya mawe. Waliegesha gari lao kwenye kibanda cha mafundi, na baada ya dakika chache za kuangalia angalia hapo na kumsalimia mlinzi, waliamua kwenda juu ya vilima vile vya mawe kuangalia jua linavyozama. Walifika kileleni na waliweza kuona vizuri mandhari ya ziwa Victoria likiangazwa kwa mionzi ya dhahabu ya jua linaloanza kuzama. Mawe makubwa yaliyojipanga utadhani matofali yaliwazunguka wapenzi hao wawili na kuwaficha na mtu yeyote yule huku yakiwapa kivuli kizuri na upepo mwanana wenye harufu ya Sangara toka ziwani ukiwapepea. Ndege aina ya mbayuwayu walikuwa wakiruka huku na kule huku kundi la nyangenyange likipepea angani kama herufi ya v. John alikuwa ameketi chini huku miguu yake ikining’inia kwenye jiwe, Alice aliamua kulala chali huku akiwa amekunja miguu yake, kichwa chake akiwa amekiagamia kwenye mapaja ya John. “Hivi unafikiri watamaliza kujenga kabla ya harusi?” Alice alimuuliza John huku akimuangalia kwa macho yake yenye upole wa njiwa lakini yenye kuashiria ujanja wa sungura. “Natumaini hivyo, sitaki kuendelea kupanga tukishafunga ndoa” John alijibu. John aliacha kuzichezea nywele za Alice na kuanza kufungua vifungo vya blauzi yake. Kifua cha Alice kilikuwa kimetuna siyo tu kwa kujaliwa maziwa yapendezayo, bali hata sidiria aliyovaa ni ile inayonyanyua matiti na hivyo kuyafanya yaonekane kama maembe dodo yanayoning’inia mtini. Alice alijinyanyua na kuiteremsha sidiria yake hadi tumboni bila kuifungua. Alirudi na kuendelea kuegama kwenye mapaja ya mpenzi wake. John, huku mkono wake wa kushoto ukiwa unampa egemezo kwenye mwamba, mkono wake wa kulia ulinza kuyachezea matiti ya Alice, na kwa upole kama anayegusa almasi alizichezea chuchu za binti huyo wa Kihaya. Alice hakusema kitu bali alifumba macho na kufurahia mikono migumu ya mpenzi wake iliyompa raha isiyo kifani. Jua lilikaribia kuzama kabisa na rangi ya mionzi yake ilibadilika toka ile ya dhahabu na kuwa nyekundu ya damu. Ndege walianza kutoweka angani na kurudi kwenye viota vyao. Alice alikuwa fundi wa mapenzi. Hakumbakishia wala kumpa kwa kibaba alimpa yote huku John na yeye akijibu mapigo kiufundi. Walikuwa wamelowa jasho walipofika kilele kwenye miamba ya jiji la Mwanza. Kwa karibu dakika chache waliendelea kukumbatiana huku wakitaka muda usiende au kesho isije. Walipomaliza kiza kilikuwa kimeshaingia. Bila ya haraka wakavaa nguo zao, kuanza kuteremka kutoka vilele vyote viwili; kuelekea walikopaki gari lao. Mlinzi alisema alianza kuingiwa na wasiwasi lakini John alimhakikishia kuwa walitaka tu kuona jua “linavyozama” kando ya “ziwa Victoria”. Mzee wa Kimakonde hakujua walimaanisha nini. Waliondoka na kurudi nyumbani. * * * “John, angalia gari hilo!” Alice alipiga kelele kumzindua John aliyekuwa bado amezama kwenye dimbwi la kumbukumbu ya tendo la mapenzi siku kule Nyegezi. John alishtuka na kuzinduka. Alikuwa ameishaanza kuingia barabarani na hakupata nafasi ya kuliona lori la Scania lilikokuwa linakuja kwa kazi likitokea Pasiansi. Licha ya jitihada zake za kukata kona na kuongeza kasi kuokoa maisha yake na ya mpenzi wake hakuweza kulizidi mwendo lori hilo. Sauti ya breki zilisikika huku matairi ya gari yakisugua barabara hiyo ya lami. Wapenzi hao hawakuwa na nafasi! Kwani lori la Scani hilo lililokuwa limesheheni magunia ya dagaa liliwaparamia kwa nguvu zote na kusababisha mlio mkubwa wa mgongano uliosika hadi maeneo ya Hospitali ya Sekou Toure. Lori hilo liliwaburuza kwa karibu mita mia moja hadi kwenye lango la shule ya Nyakahoja huku gari lao la Toyota likiwa limekunjwa kunjwa kama karatasi! Magari hayo mawili yalipoweza kusimama, matokeo yalikuwa ni dhahiri. Miili ya wapenzi hao ilikuwa imepondwa pondwa huku baadhi ya viungo vyao vikiwa vimetupwa kando ya barabara na damu ikiwa imesambaa ndani ya gari lao. Ndoto ya maisha yao baada ya ndoa ilifutiliwa mbali kama jani linavyopeperushwa na upepo. Kwa dakika na muda wa karibu miaka miwili tangu wakutane, wapenzi hao wawili wakawa wameiunganishwa milele kwa damu. Msiba wa John na Alice ulikuwa mkubwa; uliouma wengi na ulioacha kumbukumbu za kudumu katika parokia ya Nyakahoja. Walizikwa pamoja kama wachumba; hawakupata nafasi ya kufunga ndoa katika maisha haya; lakini mauti iliwafunga pingu ya mwisho. MWISHO
Artikel Terkait
Wanawake: Mumeo akikukera usilale mpaka pakuche hamjasameheana  Usiku kama mumeo kakukera usilale mpaka pakuche hamjasameheana, hata malaika baraka hawawezi shuka kwenu. Huyo ulionae amezaliwa kwao kaja na tabia zake na wewe umezaliwa kwenu una tabia zako. Sasa ukitaka kila kitu kiwe wewe unavyotaka atakuwa mwanao tena huyo sio mumeo samehaneni kwa kila mnalofanyiana. Usiweke vinyongo tena ukajua unamkomoa mana unavyonuna ndo mchepuko unavopata chance ya kuwasiliana na si kila mwanaume anamchepuko wengine washkaji tu sasa ukijitia umenuna kisa umemuona kachat, sijui umekuta meseji sijui nini utakonda uzikwe na presha na unavyotiwa kaburini tu huku wenzio wanamtext pole kazi ya Mungu mpenzi. Gangamala mtoto wa kike sio kidogo kununa kama unga wa ngano ulokosa amira. Tabasamu njia nzuri na sahihi ya kumuua mtu akikosea ukatabasamu ataanza kutafuta mchawi kumbe mchawi mwenyewe, ataanza kutoka kujua kwanini hujakasirika atatulia tu akiamini anakuvizia kumbe anajivizia. ... Read More
MADHARA YA MWANAMKE KUZAA MFULULIZO BILA KUPUMZIKA.  Ni wazi vifo vya uzazi vimekuwa vikisababishwa na sababu mbalimbali ikiwemo ya mwanamke kuzaa mfululizo bila kupumzika hivyo kutokana na hali hiyo ipo haja kwa wakuu wa mikoa ya kanda ya magharibi, kanda ya ziwa na kwingineko kuongeza juhudi zaidi katika kuwaelimisha wananchi wake umuhimu wa kutumia njia ya uzazi wa mpango. Wakuu hao wana kazi ya kuondoa mila na desturi za wananchi wa ukanda huo ili waondokane na mila hizo zilizopitwa na wakati kwa kutumia njia sahihi za uzazi wa mpango katika kuwezesha taifa kukua kiuchumi na kuleta maendeleo kwa wananchi, Takwimu za nchi zinaonyesha kanda ya magharibi inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya kuzaana na kufikiwa asilimia 7.1 ikifuatiwa na kanda ya ya kati na kufuatiwa na kanda ya ziwa hali hii pia inachangia ongezeko la vifo vya uzazi kwa wanawake kutopumzika. Kuna haja wananchi kuelimishwa kuwa matumizi mazuri ya njia ya uzazi hayana madhara mwilini ili waweze kuzaa kwa mpango na kupunguza vifo vya uzazi.  Hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete alizindua mpango mkakati ulioboreshwa wa kuongeza kasi ya kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi na kuwataka watendaji wake katika mikoa yote nchini, ambao ni wakuu wa mikoa kuwa wahakikishe wanapunguza vifo vya watoto na akinamama wanaokufa kwa matatizo ya uzazi. ... Read More
Jinsi ya kumtongoza mwanamke kwa njia 10 muhimu  Mwanamke ni kiumbe anayependa kuonyeshwa mapenzi kila wakati. Kumtongoza mwanamke kunaweza kuwa kazi ngumu sana usipozingatia mambo kadhaa muhimu. Ukitaka kuweza kumtongoza mwanamke lazima ujue anachotaka yeye. Waweza kushangaa kwamba wanachotaka wanawake ni vitu vidogo ambavyo waweza timiza ili kuweza kumfanya akukubali hata kuzungumza na wewe. Waweza kumtongoza mwanamke ukizingatia mambo yafuatayo Msikilize mwanamke unayemtongoza Wanawake hupenda mtu ambaye anawasikiliza kwa kila jambo wanachosema. Ni muhimu unapopatana na mwanamke sharti uwe makini na anacho simulia. Kuwa mtu ambaye anauliza maswali na anaye taka kujua zaidi juu ya huyu mwanamke. Muulize kazi anayofanya, anakoishi, na mwonyeshe kwamba unamsikiliza kwa kuuliza swali unapotaka ufafanuzi. Mwanamke huskia ako huru kwa mwanamme ambaye anamsikiliza kwa maana hii huonyesha mwanamume anamdhamini huyo mwanamke. Kwa kumwonyesha kwamba wewe una nia ya kujua mahitaji yake, kwa matendo yako, si maneno yako, kutakusaidia kumwonyesha kwamba wewe ni mtu anayeweza kuwa naye maishani mwake. Kuweka kipaumbele mahitaji yake na kumsikiza kutakusaidia kwa kumtongoza mwanamke huyo. Mwanamke hupenda mtu mwenye kujiamini Unapomwongelesha mwanamke lazima uwe mtu mwenye kujiamini. Ujasiri na kujiamini ni kitengo kikubwa kinachofafanua mwanamume. Unapomwongelesha mwanamke lazimi uonyeshe ujasiri mbele yake. Kama Warren Farrell, Ph.D., anavyosema “Jambo linalomvutia mwanamke kwa mwanamume ni mwanamume mwenye ujasisiri”. Ujasiri utamvutia mwanamke kwa kujua mwanamume anazungumza na kujibeba kwa ujasiri. Mwanamke hupenda kuwa karibu na mwanamume anayevutia Kuvutia kwa mwanamume huja kwa njia kadhaa. Mwanamke hupenda mwanamume ambaye hachoshi kwa hadithi zake, ni mcheshi, anachangia kwa mazungumzo kati yao na anaye hakikisha kwamba mwanamke anajiskia huru kwa maongezi. Kama mwanamume, hakikisha unatoa mifano inayoendana na maongezi mliyo nayo. Hakikisha mnayoyaongelea yanachangiwa na nyinyi wawili. Mwanamume aliemcheshi na mwenye kumvutia mwanamke kwa anavyoendeleza mazungumzo ndie aliye na nafasi kubwa ya kumpata mwanamke anayetarajia ama aliye na hamu naye. Kumbuka kwamba usiwe ni wewe pekee unayeongea, mwachie pia mwanamke achangie pia. Ukizingatia haya, mwanamke hujiskia yuko huru nawe na anaweza ongelea chochote. Mwanamke hapendi mtu mwenye haraka Haraka hapa ina maana, kwa kutongoza mwanamke lazima uwe mtu mwenye subra sana. Kinachomfanya mtu awe na hamu ya kuwa na mwingine ni matarajio anayopata rohoni. Unapopatana na mwanamke kwa wakati wa kwanza, usimwonyeshe kwa umbele unachotaka, lakini taka kumsikiliza, mjue jina, anachofanya kazini, na mambo mengine kwanza. Kwa kufanya haya mwanamke ataona kwamba unahamu naye na kwamba atajiskia wa maana kwako. Jambo hili litakusaidia sana kwa kutongoza huyo mwanamke. Kitu cha muhimi ni kwanza upate kuwa marafiki na mwanamke yule ili uweze kupata nafasi nzuri ya kumtongoza. Ubinafsi wa kipekee Mwanamke hupenda vitu vya kipekee sio vitu vinavyoigwa kwingine. Usije ukafanya ama ukanena kama mwanamume mwingine ili kumshinda huyo binti. Kuwa na ubinafsi wako, fanya mambo yako kwa kipekee. Kuiga wengine hakutakusaidia kwani mwanamke atakuona kama mtu asiyejiamini. Mwanamke hupenda manamume ambaye ni tofauti na wanaume wengine ambao amewahi kutana nao hapo mwanzo. Ni vizuri kuwa na vitu ambavyo ni vya kipekee kwako. Kama sauti yako, vile wacheka vile wamtizama mwanamke yule, vile wavaa, vile umejipaka manukato mazuri. Upekee huu hukupa nafasi ya mbele kwa mpango wako wa kumtongoza mwanamke yule. Mavazi na usafi Mwanamke hupenda usafi sana. Ukitaka mwanamke aweze kuvutiwa nawe lazima uvae vizuri na uwe safi. Kuvaa vizuri, nguo zinazokufanya upendeze huwa njia moja ya kuvutia wanawake. Pia kuwa makini na usafi. Kuoga vizuri, kujipaka manukato yanayo vutia, kuweka nywele, nguo safi husaidia sana kwa kukupa ujasiri wa kumwendea mwanamke uliye na hamu naye. Sio lazima uvae mavazi ghali, lakini valia kwa kupendeza. Mwanamke hupenda mtu anayejiamini katika alichovalia. Muziki Kwa miaka mingi muziki umejulikana kuwa chombo cha kuonyesha mapenzi ama kama namna ya kumtongoza mwanamke. Mwanamke hupenda kuonyeshwa kwamba ni mtu wa thamani kwa mwanamume. Muziki waweza kukusaidia kuweka mazingira yenye utulivu na yenye riwaya ya mahaba. Kumbuka kumzingatia wakati unaweka muziki ule, jua mbeleni muziki anaopenda na fanya hima kwamba unamtumbuiza na aina hizo kwa kikamilifu. Ukifanya hivyo, mwanamke ataoona kwamba unathamini. Weka muziki wenye utulivu, wenye mahaba na wenye kumsifu mtu wa kike na uzuri wake kwa kumwonyesha mapenzi. Bidii ya kuwa makini kwa mwanamke na kumpa pongezi wakati wowote Mwanamke ni kiumbe anayependa kusifiwa na kupongezwa sana. Kwa mwanamume ni muhimu kwamba kwa kumtongoza mwanamke, kumbuka kila wakati kumpongeza kwa kuvaa kwake, nywele, viatu, anavyong’aa. Ni muhimu kumwonyesha kwamba umefurahia bidii yake ya kuvaa vyema na kuhakikisha anakaa vyema mnapokutana. Mwanamke hujiskia mwenye thamana sana kwa kujua kwamba kuna mwanamume amemwona anakaa sawa. Mwambie wapenda alivyosongwa, anavyotoa busu, anavyocheka, na kila kidogo anachofanya. Utashangaa kwamba yaweza onekana ni mambo madogo lakini huchangia katika kutongoza mwanamke. Mpikie chajio mwanamke unayemtongoza Kama mwanamume hakuna kitu cha muhimu kama kumpikia mwanamke uliye na macho kwake. Mwanamume ajuaye kupika huwa anawavutia wanawake sana. Unaweza kumwalika mwanamke kwako ka chajio. Fanya hima ukajua chakula anachopenda binti unaye mtarajia, ukahakikisha umepika chakula kitamu na kinachovutia kwa kuangalia na harufu tamu. Mwandalie mezani pamoja na kinyuaji. Kuwa umehakikisha kuna mazingira yenye utulivu na pia weka mziki wenye mahaba. Mwanamke hujihisi mwenye thamani sana. Hapa utakuwa umejiongezea pointi kadhaa kwa mpango wako wa kumtongoza binti yule. Zawadi Kila mwanamke hupenda kupata zawadi wakati wowote. Kama mwanamume itakusaidia pakubwa kwa mpango wako wa kumtogoza binti yeyote. Zawadi zaweza kuwa tofauti. Waweza mtumia maua ya waridi kazini, ukakumbuka kumtumia chokoleti wakati wa wapendanao, ukamtumania kahawa asubuhi akiingia kazini. Kwa kufanya vile, mwanamke hujiskia wa dhamana na anayependwa. Wanawake pia hupenda kupelekwa mahali pa zuri ambapo anaweza kujibinjari. Mpeleke densi, mpeleke mahali mkala chajio, mpeleke mbugani kwa wanyama ama kwa safari. Kufanya vile kutakupatia pointi nyingi kwa mtazamo wako wa kumtongoza mwanamke yule. Kama kawaida wanawake na wanaume huwa na hamu ya kujuana na kuishi maisha pamoja. Katika kumtongoza mwanamke lazima kwanza mwanamume afahamu nini mwanamke yule anachopenda. Pia inabidi mwanamume pia kumpa sikio binti yule wakati wowote wanapozungumza na kuuliza mwaswali asipoelewa kitu. Mpe wanamke pongezi wakati wowote mnapopatana, mpe pongezi kwa kusukwa vizuri, kupaka kucha vizuri, kuvaa nguo vizuri, tabasamu lake na anavyocheka. Mara kwa mara mpe zawadi za hapa na pale. La muhimu sana ni mwanamke huvutiwa na mwanamume anaye jiamini. Ukiwa mwanamume ambaye anajiamini, itamfanya mwanamke yule kujiskia huru kuwa karibu nawe na hio itakusaidia katika hali ya kumtongoza. ... Read More
UNAJUA KUMPAGAWISHA MPENZI WAKO????  Kama inavyoeleweka, mapenzi ni sehemu muhimu ya afya ya binadamu. So, katika peruzi zangu, nikakutana na hili somo la "Tantric Sex." Kama inavyoelewaka, mapenzi ni sehemu muhimu ya afya ya binadamu. So, katika peruzi zangu, nikakutana na hili somo la “Tantric Sex.” As if hii duinia, especially hii century haiko overloaded na information kuhusu mambo ya mapenzi, jinsi ya kufanya mapenzi and whats hot in the bedroom, whats in and whats not. So, lately nimeona a lot of tzmoms readers wamekuwa wakitembelea sana na kusoma page ya “mapenzi baada ya ujauzito” na “kufanyamapenzi wakati wa ujauzito.” And I thought well, writing about Tantric Sex will be nyongeza kwa kila mmoja, aliye mama na mbaye bado damu inachemka katika mambo ya mapenzi. Anyhu, kama “SEX/MAPENZI” yangekuwa yanaweza kuyu-nite the world/countries/makabila/people I think hii fani ingeshinda. Well, so kama umeshawahi kujifungua ama kama wewe ni mama, you definitely understand ni jinsi gani ni vigumu kuwa upbeat kuhusu mapenzi ama kumfurahisha mumeo/mpenzio everyday. Well, once in a while maybe but not everyday. Ila kama we ni mdada/binti ambaye hujazaa bado well, damu yako bado inachemka so energy bado ipo nyingi ya kukurupushana na mpenzio. Having said that, si maanishi mtu ukishazaa ndo fani ya kuenjoy mapenzi imekwisha but nguvu zinapungua for sure however, kuna vitu vingi tuu ambavyo vinaweza kusaidia kuleta nguvu ya kutaka kukurupushana chumbani lol. Kukosa nguvu/energy to wanna work it all the time its not because mwanamke ni mvivu but hutokana na kuwa na mambo mengi sana ya kutend nyumbani i.e. kuhakikisha watoto wako taken care of, labda kazini pia unahitajika, etc una kuta hupati muda wa kujifurahisha mwenyewe ama na mpenzi wako. Therefore, mara nyingi before you know mupenzi anaanza kulalamika or hata mwanamke mwenyewe unaweza kufeel like you are not doing enough so mambo ndo hivyo yanaanza kwenda south chumbani. Hivyo basi, lets dig in tuone Tantric Sex inatoa msaada wa aina gani ili kurevamp mapenzi. Kwanza kabisa, FYI tantric sex can be weird at the beginning ila nitajitahidi kutoingia so indepth ili kusave miyoyo ya watu wengine. Kwamaana hii ni soft porn “according to me.” Lol. so usishtuke ama kushangaa sana. Well, anythign “sex” can be unconfortable anyways. Okay, so, kwanza kabisa, with Tantric Sex, mtu na mpenziwe wanatakiwa kuwa; SPIRITUALLY CONNECTED (usishtuke sio kidini lol).. Hii inamaainisha kwamba wewe na patner wako kwa pamoja mnajua mnataka nini emotionally and physically. Kwa kufanya hivi inasaidia kuwafanya kwa pamoja kuwa “FREE” na kuondoa wasiwasi wa labda mwenzangu atanijudge kwamba labda mimi ni malaya ama fuska etc. In other words hii process inaitwa “Dropping the Veil, between “Self” and “Other/patner.” THE ENVIRONMENT/mazingira. Wakati mnapractice tantric sex of course, just like when you are in the bedroom unaweza ukavaa lingerie/kuo za ndani zinazovutia or “kuwa kama mlivyotoka tumboni mwa mama zenu” (you know what i mean). Tatu, wapenzi wanaanza kupapasana lol, but in a way kwamba you are feeling the energy of the other person. Na hii energy unaweza kuifeel kwasababu mko free hamna anayemjudge mwingine/there are no worries. You are just in your own created world. Nne, wakati wa kufeel energy ya mwingine lazima wapenzi wawe wana pumua heavely yaani just feeling every move made but the other person mpaka mnapofikia mahali were you are breathing so hard and you are feeling each other. then you start kissing the lips, and then deeper for minutes even hours. Then mengineyo yanaweza kuendelea. So, all this time kumbuka its not about going straight into sex with your partner rather its about getting high by touching and feeling connected with each other. hivyo basi, once in a while take that time and revamp your intimacy, dress good, feel sexy and heey have fun!!. By 🅱 ... Read More
NIFANYE NINI ILI MUME WANGU AWE NA HAMU NAMI?  Mume wangu anasema ananipenda sana, nami nampenda sana. Tuna watoto wawili wa kiume. Nimejaribu kila kitu cha kumfurahisha, kama vile kuvaa vizuri, kuandaa chakula kizuri akipendacho na kinywaji lakini Lakini mwenzangu haonekani kuridhishwa na jitihada zangu. Baada ya chakula cha usiku huwa tunakaa na kuangalia Luninga huku tukiwa na vinywaji. Lakini cha ajabu nikimsogelea na kutaka niwe karibu naye ananiepuka. Yaani HATAKI hata nimguse ni kama NINANUKA au ninamsumbua vile. Je, tatizo ni nini hasa, Je nanuka? Najiuliza na jibu sipati….Alimalizia kusema huyu mama huko chozi likimdondoka…...... Naam mara nyingi hivyo ndivyo inavyokuwa kwa sisi wanawake pale tukutanapo, si jambo geni sana kwa sisi wanawake kushirikiana kihisia. Ni jambo la kawaida kabisa kukuta mwanamke akimsimulia shoga yake anayemuamini juu ya madhila yake. Yote hiyo ni katika kutafuta nafuu na kuondokana na msongo wa mawazo. Mara nyingi simulizi nyingi zinazowakutanisha wanawake ni zile zinazohusiana na mambo ya Ndoa, mahusiano, watoto au mambo ya kifamilia kwa ujumla, mara nyingi tunatamani kupata mahali pa kulinganishia, ili kutaka kujua kama tatizo nililo nalo lina ukubwa kiasi gani. Ni hivi majuzi nikiwa kazini na mfanyakazi mwenzangu ndipo aliponieleza kile kinachomsibu kwa muda mrefu sasa, inavyoonekana, ni jambo ambalo alikaa nalo muda mrefu akijaribu kupambana nalo kimya kimya huku likiendelea kumtafuna, dada huyu wa Kiswidish. Ili kujiridhisha na kutaka kujua ukweli halisi nikamuuliza kama amemuuliza mume wake jambo hili akajibu amefanya hivyo na jawabu alilolipata ni kwamba, mume wake huwa anachoka. Yaani kazi zake ni nyingi pia malezi ya watoto yanamchosha. Nikamuuliza kama hawawezi wakati wa wikiendi watoke ili kuwa peke yao? Hapo nikapata jibu ambalo sikutegemea. Alidai kwamba akisema hivyo mume wake anaona kama yeye anaamua nini wafanye. Huyu mama akaendelea kusema, mimi ni binadamu Yasinta.,,,,,,,,,, Na nahitaji tendo la ndoa na sitaki kutoka nje kwani nampenda sana mume wangu. Nami sikuachia hapo kama mnavyonifahamu na u-Kapulya wangu nikamuuliza kama tatizo hilo lina muda gani au limeanza siku za karibuni? Mama yule akashusha pumzi, akaniangalia kwa jicho la huzuni, kisha akajibu kuwa inatokea wanafanya tendo la ndoa mara moja kwa mwezi na hapo ni ile ya haraka haraka na halafu baada ya hapo mume wake anampa mgongo na kulala . Hapo….akasita kidogo …nikamuuliza ulitaka kusema nini? Akaendelea unajua Yasinta mwanamke anahitaji kuandaliwa kwanza, mimi huwa siandaliwi kabisa........ Mweh! Nikaona makubwa haya ......nilikosa Jawabu la kumpa kwa kweli, nikabaki kuguna tu. Hata hivyo nilijaribu kumshauri aende kwa washauri nasaha wa masuala ya Ndoa na mahusiano, lakini akadai kuwa mumewe ni mkaidi na hawezi kukubali. Mwenzenu swala hili limenishinda maana sijui nimsaidieje! Je Wewe kama msomaji unaweza kunisaidia ni ushauri gani nimpe mama huyu, ili awe na furaha katika Maisha ya ndoa yake? Ushauri tafadhali........... ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: