Raha ya NGOMA uingie ucheze... Muda mwingine kuona mwenzio akicheza inaleta burudani lakini ili burudani hiyo iukonge moyo hebu ingia kacheze! Kuna wakati unaweza kubaki unacheka tu ukiyawaza MAPENZI😅😅 Yaani waloyaanzisha MAPENZI wao hawakuumizana zaidi ya kumkosea MUNGU lakini sisi vizazi vyao lol👌. Unakuta mwanaume ameoa na kujaaliwa watoto lakini aonapo ndoa yake inamtatanisha hukimbilia kwa marafiki ambao hawana ndoa wala hawajawahi mmiliki mwanamke kwa mwezi mmoja maana wao ni WAZEE WA TAKE AWAY... Ukiyasoma maandiko ya 1 WAKORINTHO 15:33 Biblia inasema; "Msidanganyike, Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema" Ninachoweza kusema katika Swala la mahusiano ama ndoa ni kwamba ZAWADI KUU KATIKA MAISHA YA MWANAMKE AMBAYO UKIMPA NA AKAISHI KWA KUJIAMINI NA AKAFURAHIA UWEPO WAKO NI UPENDO! Zaidi ya hapo hakuna chenye thamani ambacho utamfanya mwanamke wako ajione ni mwanamke kuliko mwanamke mwenzie, Maana kama ni nguo mwanaume yeyote aweza kumnunulia, Je Unadhani ni gari ama nyumba? Vyote hivyo si kipaumbele hasa kwa wanawake wa sasa wanajuwa kujihudumia Kwani wanajituma sana, Ukitaka kumuweza mwanamke wewe bwana WEKEZA UPENDO WA DHATI KWAKE hata ndugu zake watasema sio bure pengine umemroga ndugu yao kumbe MAHABA.

at 9:49 AM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top