Home → ushauri
→ Ni kwamba, kuna njia kadhaa za kitaalamu zinazoweza kutumiwa na wazazi ili kujipatia watoto wanaoweza kujiamulia kuwa wawe wa kiume au wa kike.
Uchunguzi wa Nipashe uliohusisha mahojiano na madaktari kadhaa wakiwamo mabingwa wa masuala ya uzazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, umebaini kuwa sasa wazazi wanaweza kufanikisha ndoto ya kupata watoto wa kiume au wa kike kadri watakavyo kwa njia rahisi inayotoa matokeo chanya kwa asilimia 80 au nyingine ya kitaalamu zaidi inayopatikana pia nchini na ambayo matokeo yake huwa na uhakika wa takribani asilimia 100.
Kupitia mahojiano hayo na wataalamu, Nipashe imebaini kuwa karibu wote humtanguliza Mwenyezi Mungu katika kufanikisha jambo hilo.
Akizungumza na Nipashe katika mahojiano maalum yaliyofanyika Alhamisi, Daktari Bingwa wa Wanawake katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Living Colman, alisema jambo hilo linawezekana lakini kuna mambo muhimu ya kuzingatia kabla wazazi kupata mtoto wa jinsia waitakayo.
Alisema wahusika ni lazima wawe na afya njema na pia mbegu kutoka kwa mwanaume lazima ziwe na ubora unaotakiwa katika kufanikisha utungaji wa mimba.
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Tanzania ina watu milioni 45, huku wanawake wakiwa milioni 23, sawa na asilimia 51.
NJIA KUPATA MTOTO WA KIUME, KIKE
Wakizungumza na Nipashe, baadhi ya madaktari waliitaja njia ya upandikizaji wa mbegu kuwa ndiyo kubwa na ya uhakika zaidi kufanikisha utungaji wa mimba ya mtoto wa jinsia waitakayo wazazi.
Hata hivyo, Dk. Colman aliiambia gazeti hili kuwa mbali na njia hiyo inayohusisha matumizi ya maabara, ipo njia nyingine rahisi inayotokana na ufuatiliaji makini wa kalenda ya mzunguko wa hedhi wa mama.
“Hii ni rahisi zaidi na haihusishi upandikizaji wa mbegu kwenye maabara… hata hivyo, njia hii inahitaji wahusika kuwa makini zaidi katika kufuatilia mzunguko wa hedhi wa mama kwa sababu kinyume chake matokeo huwa hafifu,” alisema Dk. Colman.
Akieleza zaidi, Dk. Colman alisema wengi hujaribu kufuata njia hiyo ya kalenda na kupata matokeo hasi kwa sababu ya kutozingatia maelekezo, lakini ukweli ni kwamba yenyewe hutoa matokeo ya uhakika kwa asilimia 80.
“Kati ya watu 10 wanaokuja kwangu na kuomba ushauri wa namna ya kupata watoto wa jinsi waitakayo, nane wamefanikiwa… kwa hiyo hii inawezekana kabisa,” alisema Dk. Colman.
UFAFANUZI NJIA YA KALENDA
Wakati baadhi ya madaktari wakitilia shaka njia ya kalenda, Dk. Colman anasisitiza kuwa huleta mafanikio chanya kwa kiasi kikubwa na kwamba, lililo muhimu ni kwa wazazi kuwa na utimamu wa kiafya na kubwa zaidi ni kuzingatia muda sahihi wa kushiriki tendo la ndoa kwa nia ya kupata mtoto.
Akifafanua, Dk. Colman alisema daima, mwanamke huzalisha mbegu aina moja zinazotambulika kama ‘XX’ na hizo huendeleza ukike. Kwa wanaume, mbegu zinazozalishwa huwa ni za aina mbili ambazo ni ‘X’ (kike) na ‘Y’ (kiume).
Alisema kuwa mbegu yoyote ya mwanamke (X) ikichavushwa na mbegu ‘X’ ya mwanaume hutengeneza muunganiko wa ‘XX’ ambao mwishowe huwa ni kutungwa kwa mimba ya mtoto wa kike. Hata hivyo, inapotokea mbegu ya mwanamke ikakutana na mbegu ‘Y’ hutokea muunganiko wa ‘XY’ ambao mwishowe huwa ni mimba ya mtoto wa kiume.
Akieleza zaidi, Dk. Colman alisema kuwa sifa ya mbegu ‘X’ huwa ni uimara wake kulinganisha na mbegu ‘Y’, lakini pia huwa na mwendokasi mdogo kulinganisha na mbegu ‘Y’ ambazo zenyewe huwa hazidumu muda mrefu kabla ya kuharibika kwa vile siyo imara kulinganisha na ‘X’, na zina mwendokasi mkubwa zaidi.
“Mbegu X ipo imara lakini inapotoka huenda taratibu wakati mbegu Y ni dhaifu, lakini mwendo wake huwa ni wa kasi zaidi,” alisema.
Kwa sababu hiyo, Dk. Colman alisema wazazi wanapaswa kuzingatia kalenda ya mzunguko wa hedhi ili kufanikisha mimba ya mtoto wa kiume au wa kike kulinga na na vile watakavyo.
“Ni lazima ujue mzunguko wa mwanamke husika ni wa aina gani… kwa maana kuna mizunguko ya wastani wa siku 28 ambayo hii yai lake hutoka siku ya 14, kuna mzunguko mfupi wa siku 21 na yai hutoka siku ya 10 na pia wale wa mzunguko mrefu wa siku 36 ambao yai hutoka katika siku ya 18,” alisema.
"Kwa kawaida, yai hutoka katikati ya mzunguko wa mwanamke kulingana na mzunguko wake. Hivyo, mbali ya kujua hilo la mzunguko, ni lazima wazazi watambue tabia za mbegu X inayosafiri taratibu na Y inayosafiri haraka… hilo ni muhimu kwa sababu ndilo husaidia katika kufanikisha ndoto ya kuchagua jinsia ya mtoto," alisema.
Aliongeza kuwa wahusika wakishiriki tendo la ndoa siku mbili au tatu karibu na yai la mama kutoka, maana yake kutakuwa na uwezekano mkubwa wa kutungwa kwa mimba ya mtoto wa kiume kwa vile kutokana na tabia ya mbegu Y ya kusafiri kwa kasi, maana yake ndiyo itakayotangulia na hivyo kukutwa na mbegu ya mama wakati nyingine ya X ikiwa imeachwa kwa vile kasi yake ni ndogo.
Alisema kwa sababu hiyo, wazazi wanaoota kupata mtoto wa wa kiume watalazimika kushiriki tendo la ndoa wakati zikiwa zimebaki siku mbili au tatu kabla ya yai la mama kutoka.
Aidha, Dk. Colman alisema ikiwa wazazi watakuwa na ndoto ya kupata mtoto wa kike, watalazimika kushiriki tendo la ndoa siku nyingi, kati ya 9, 10 au 11 kabla ya siku inayotarajiwa kuwapo kwa yai la mama katika mzunguko wake.
Alisema hilo ni muhimu kuzingatiwa kwa sababu kutokana na tabia ya mbegu X (kike), maana yake mwendo wake utakuwa wa taratibu na itadumu kwa siku hizo nyingi kabla ya kukutwa na kukutana na mbegu itokayo kwa mama huku mbegu Y ikiwa tayari imeshaharibika kutokana na kutangulia kwake mbele haraka na kukosa uimara wa kusubiria siku zote hizo.
“Mkishiriki tendo la ndoa mapema kidogo, kama siku mbili au moja hivi karibu na yai kutoka, mtapata mtoto wa kiume. Lakini ikiwa ni siku nyingi kabla ya hapo kuna uwezekano mkubwa wa kupata mtoto wa kike,” alisema Dk. Colman kabla ya kutahadharisha kwa kuongeza:
“Ila hizi zote siyo kanuni za kudumu maana mwili wa binadamu hubadilika… lazima hili lifanyike kwa kuzingatia mzunguko wa mwanamke na hiyo ni kwa mujibu wa matokeo ya tafiti.”
Aidha, Dk. Colman alisisitiza kuwa msingi wa mafanikio ya mpango huo wa kuchagua jinsia ya mtoto kwa kuratibu mzunguko wa hedhi ya mama ni kujua kwa usahihi siku za mzunguko huo.
“Kikubwa ni mwanaume na mwanamke kujua yai linatoka lini ili mbegu X au Y zikutane na yai la mwanamke na kufanikisha utungwaji wa mimba ,” alisema Dk. Colman.
Aliongeza kuwa, endapo kuna wazazi wanapenda kuwa na watoto wa jinsia tofauti, ni vyema wakazingatia njia hiyo isiyogharimu chochote ya kuzingatia vyema mzunguko wa hedhi wa mwanamke kama ni wa kawaida, mrefu au mfupi.
Alisema eneo hilo ndilo huwashinda wengi na kupata matokeo tofauti na yale wanayoyatarajia.
“Hapa wengi huchanganya sana. Unakuta mwanamke mzunguko wake ni wa siku 28 na hivyo yai hutoka siku ya 14, lakini wawili hao wanatumia kanuni nyingine ya mzunguko mfupi wa siku 21 ambayo yai hutoka siku ya 10.
Ni lazima pia kuzingatia muda wa kushiriki tendo la ndoa kulingana na tabia nilizozitaja za X na Y,” alisema Dk. Colman.
“Hadi sasa, katika watu 10 walionifuata na kuniomba ushauri wa kupata watoto wa jinsia waitakayo, nane wamefanikiwa (asilimia 80). Kwa hiyo utaona kwamba jambo hilo linawezekana, ila muhimu ni kuzingatia masuala hayo ya mzunguko wa mama na siku ya kushiriki tendo la ndoa,” alisema.
NJIA YA UPANDIKIZAJI
Mbali na njia ya kuzingatia mzunguko wa mama kabla ya kushiriki tendo la ndoa ambayo haileti mafanikio kwa asilimia 100, Dk. Colman aliitaja njia nyingine inayotoa fursa kwa wazazi kuchagua jinsia ya mtoto kuwa ni ile ya upandikizaji mbegu kwa mama kuwa ndiyo ya uhakika zaidi katika kuchagua jinsia ya mtoto.
Hata hivyo, Dk. Colman alisema teknolojia hiyo ya upandikizaji ni ghali na kwa hapa Tanzania bado ni ngeni na haipo katika hospitali za Serikali.
“Upandikizaji mbegu unaanzia kwa kutolewa mbegu mwanaume na baadaye kupelekwa maabara. Huko hupimwa magonjwa yote ili kujua ubora wake. Pia ni huko maabara ndipo wazazi wanapoweza kujua jinsia ya mtoto wao kwa asilimia 100. Na hii ndiyo njia sahihi na ya uhakika zaidi,” alisema Dk. Colman.
Aliongeza kuwa katika siku zijazo, anaamini kuna wakati hospitali yao (Muhimbili) itatimiza lengo la kuanzisha Kitengo Maalum cha Matatizo ya Ujauzito na Uzazi ambako humo, watakuwa na fursa ya kuwasaidia watu wanaohitaji huduma ya upandikizaji wa mbegu kwa ajili ya kupata watoto.
KLINIKI YA UPANDIKIZAJI DAR
Katika uchunguzi wake, mwandishi wa Nipashe alipata bahati ya kutembelea kituo cha tiba kilichoanzishwa miaka ya hivi karibuni katika maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushughulikia matatizo ya uzazi huku pia kikiwa na teknolojia ya kupandikiza mbegu kiitwacho Dar IVF and Fertilizing Clinic.
Mkurugenzi wa Tiba wa kituo hicho, Dk. Tamale Sali, alizungumzia pia uwezekano wa wazazi kupata watoto wa jinsia watakayo kwa kutumia teknolojia ya upandikizaji na kuleta matokeo sahihi ya asilimia 100.
“Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa hii njia ya kuchagua jinsia ya mtoto kwa mzunguko wa hedhi hutoa matokeo ya asilimia 50 kwa 50. Siyo ya uhakika sana kwa sababu wazazi wanaweza wanaweza kufanikiwa au wasifanikiwe.
Lakini ya upandikizaji maabara ina uhakika zaidi katika kupata mtoto wa jinsia wanayoitaka wazazi,” alisema Dk. Sali.
Akieleza zaidi, Dk. Sali alisema kinachoweza kufanyika kwa wale wanaotaka kuwa na watoto wa kiume au wa kike kadri watakavyo ni kuchukuliwa kwa mbegu za mwanaume, kupelekwa maabara na huko ndiko uamuzi kuhusu jinsia ya mtoto unaweza kutolewa na wahusika.
Aidha, Dk. Sali aliongeza kuwa mbali na uamuzi kuhusu jinsia ya mtoto, wazazi hupata fursa pia ya kupata mtoto asiyesumbuliwa na maradhi kama ya kisukari na moyo.
“Mbali ya kupimwa jinsia ya mtoto, mbegu ya baba hupimwa pia magonjwa mengine kama ya moyo na kisukari… kama itabainika kuwa mbegu ina tatizo, inaachwa na kuchukuliwa mbegu nyingine,” alisema.
Dk. Sali alisema kuwa hadi sasa, tangu waanze kutoa huduma zao nchini, tayari wameshasaidia wazazi tofauti 15 kupata watoto wa jinsia waitakayo kwa njia ya upandikizaji huku wastani wa watoto wanaozaliwa nchini Uganda kwa mwaka kupitia njia hiyo katika kliniki yao iliyopo nchini humo ni 30.
Alisema wanaopaswa kutumia njia ya upandikizaji katika kupata watoto ni wanawake ambao mirija yao ya uzazi imeziba, wale walio na utasa na baadhi ya wagojwa wenye uvimbe kwenye ‘ovari’, vivimbe vya vimeleo kuzunguka mfuko wa uzazi, wanawake waliomaliza hedhi na bado wanahitaji mchango wa mayai, waliotolewa mfuko wa uzazi lakini ovari zao zimebaki na sababu nyingine za kijamii ikiwamo mume kusafiri kwenda masomoni au vitani.
Alisema kwa kawaida, wao hutoa matibabu kwa njia ya upandikizaji pale tu inapowalazimu wanandoa kufanya hivyo ikiwa ni njia ya mwisho baada ya njia nyingine zote za kupata mtoto kugonga mwamba.
MSIMAMO WA SERIKALI KUHUSU JINSIA ZA WATOTO
Baadhi ya watu hutamani kuwa na mchanganyiko wa jinsia katika orodha ya watoto wao na hivyo huwa tayari kufuata njia mbalimbali ili kuwapata watoto wa jinsia waitakayo ili kukidhi matakwa yao.
Hata hivyo, Nipashe imebaini kuwa baadhi ya njia haziruhusiwi nchini ikiwamo ile ya kukatisha uhai wa mimba ya mtoto wa jinsia wasiyoitaka wazazi wakati wa kutungwa kwake.
Mkurugenzi wa Uhakiki wa Ubora wa Huduma katika Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mohamed Mohamed, alisema ni kosa kisheria kwa mama kutoa mimba baada ya kujua jinsia ya mtoto anayetarajia kumzaa.
Kuhusu upandikizaji alisema sheria inatambua wale wenye matatizo ya uzazi, wenye umri mkubwa na ukomo wa hedhi kuwa hawakatazwi kupandikiza lakini siyo wanandoa wenye afya njema na uwezo wa kupata watoto kwa njia ya kawaida.
Ni kwamba, kuna njia kadhaa za kitaalamu zinazoweza kutumiwa na wazazi ili kujipatia watoto wanaoweza kujiamulia kuwa wawe wa kiume au wa kike. Uchunguzi wa Nipashe uliohusisha mahojiano na madaktari kadhaa wakiwamo mabingwa wa masuala ya uzazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, umebaini kuwa sasa wazazi wanaweza kufanikisha ndoto ya kupata watoto wa kiume au wa kike kadri watakavyo kwa njia rahisi inayotoa matokeo chanya kwa asilimia 80 au nyingine ya kitaalamu zaidi inayopatikana pia nchini na ambayo matokeo yake huwa na uhakika wa takribani asilimia 100. Kupitia mahojiano hayo na wataalamu, Nipashe imebaini kuwa karibu wote humtanguliza Mwenyezi Mungu katika kufanikisha jambo hilo. Akizungumza na Nipashe katika mahojiano maalum yaliyofanyika Alhamisi, Daktari Bingwa wa Wanawake katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Living Colman, alisema jambo hilo linawezekana lakini kuna mambo muhimu ya kuzingatia kabla wazazi kupata mtoto wa jinsia waitakayo. Alisema wahusika ni lazima wawe na afya njema na pia mbegu kutoka kwa mwanaume lazima ziwe na ubora unaotakiwa katika kufanikisha utungaji wa mimba. Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Tanzania ina watu milioni 45, huku wanawake wakiwa milioni 23, sawa na asilimia 51. NJIA KUPATA MTOTO WA KIUME, KIKE Wakizungumza na Nipashe, baadhi ya madaktari waliitaja njia ya upandikizaji wa mbegu kuwa ndiyo kubwa na ya uhakika zaidi kufanikisha utungaji wa mimba ya mtoto wa jinsia waitakayo wazazi. Hata hivyo, Dk. Colman aliiambia gazeti hili kuwa mbali na njia hiyo inayohusisha matumizi ya maabara, ipo njia nyingine rahisi inayotokana na ufuatiliaji makini wa kalenda ya mzunguko wa hedhi wa mama. “Hii ni rahisi zaidi na haihusishi upandikizaji wa mbegu kwenye maabara… hata hivyo, njia hii inahitaji wahusika kuwa makini zaidi katika kufuatilia mzunguko wa hedhi wa mama kwa sababu kinyume chake matokeo huwa hafifu,” alisema Dk. Colman. Akieleza zaidi, Dk. Colman alisema wengi hujaribu kufuata njia hiyo ya kalenda na kupata matokeo hasi kwa sababu ya kutozingatia maelekezo, lakini ukweli ni kwamba yenyewe hutoa matokeo ya uhakika kwa asilimia 80. “Kati ya watu 10 wanaokuja kwangu na kuomba ushauri wa namna ya kupata watoto wa jinsi waitakayo, nane wamefanikiwa… kwa hiyo hii inawezekana kabisa,” alisema Dk. Colman. UFAFANUZI NJIA YA KALENDA Wakati baadhi ya madaktari wakitilia shaka njia ya kalenda, Dk. Colman anasisitiza kuwa huleta mafanikio chanya kwa kiasi kikubwa na kwamba, lililo muhimu ni kwa wazazi kuwa na utimamu wa kiafya na kubwa zaidi ni kuzingatia muda sahihi wa kushiriki tendo la ndoa kwa nia ya kupata mtoto. Akifafanua, Dk. Colman alisema daima, mwanamke huzalisha mbegu aina moja zinazotambulika kama ‘XX’ na hizo huendeleza ukike. Kwa wanaume, mbegu zinazozalishwa huwa ni za aina mbili ambazo ni ‘X’ (kike) na ‘Y’ (kiume). Alisema kuwa mbegu yoyote ya mwanamke (X) ikichavushwa na mbegu ‘X’ ya mwanaume hutengeneza muunganiko wa ‘XX’ ambao mwishowe huwa ni kutungwa kwa mimba ya mtoto wa kike. Hata hivyo, inapotokea mbegu ya mwanamke ikakutana na mbegu ‘Y’ hutokea muunganiko wa ‘XY’ ambao mwishowe huwa ni mimba ya mtoto wa kiume. Akieleza zaidi, Dk. Colman alisema kuwa sifa ya mbegu ‘X’ huwa ni uimara wake kulinganisha na mbegu ‘Y’, lakini pia huwa na mwendokasi mdogo kulinganisha na mbegu ‘Y’ ambazo zenyewe huwa hazidumu muda mrefu kabla ya kuharibika kwa vile siyo imara kulinganisha na ‘X’, na zina mwendokasi mkubwa zaidi. “Mbegu X ipo imara lakini inapotoka huenda taratibu wakati mbegu Y ni dhaifu, lakini mwendo wake huwa ni wa kasi zaidi,” alisema. Kwa sababu hiyo, Dk. Colman alisema wazazi wanapaswa kuzingatia kalenda ya mzunguko wa hedhi ili kufanikisha mimba ya mtoto wa kiume au wa kike kulinga na na vile watakavyo. “Ni lazima ujue mzunguko wa mwanamke husika ni wa aina gani… kwa maana kuna mizunguko ya wastani wa siku 28 ambayo hii yai lake hutoka siku ya 14, kuna mzunguko mfupi wa siku 21 na yai hutoka siku ya 10 na pia wale wa mzunguko mrefu wa siku 36 ambao yai hutoka katika siku ya 18,” alisema. "Kwa kawaida, yai hutoka katikati ya mzunguko wa mwanamke kulingana na mzunguko wake. Hivyo, mbali ya kujua hilo la mzunguko, ni lazima wazazi watambue tabia za mbegu X inayosafiri taratibu na Y inayosafiri haraka… hilo ni muhimu kwa sababu ndilo husaidia katika kufanikisha ndoto ya kuchagua jinsia ya mtoto," alisema. Aliongeza kuwa wahusika wakishiriki tendo la ndoa siku mbili au tatu karibu na yai la mama kutoka, maana yake kutakuwa na uwezekano mkubwa wa kutungwa kwa mimba ya mtoto wa kiume kwa vile kutokana na tabia ya mbegu Y ya kusafiri kwa kasi, maana yake ndiyo itakayotangulia na hivyo kukutwa na mbegu ya mama wakati nyingine ya X ikiwa imeachwa kwa vile kasi yake ni ndogo. Alisema kwa sababu hiyo, wazazi wanaoota kupata mtoto wa wa kiume watalazimika kushiriki tendo la ndoa wakati zikiwa zimebaki siku mbili au tatu kabla ya yai la mama kutoka. Aidha, Dk. Colman alisema ikiwa wazazi watakuwa na ndoto ya kupata mtoto wa kike, watalazimika kushiriki tendo la ndoa siku nyingi, kati ya 9, 10 au 11 kabla ya siku inayotarajiwa kuwapo kwa yai la mama katika mzunguko wake. Alisema hilo ni muhimu kuzingatiwa kwa sababu kutokana na tabia ya mbegu X (kike), maana yake mwendo wake utakuwa wa taratibu na itadumu kwa siku hizo nyingi kabla ya kukutwa na kukutana na mbegu itokayo kwa mama huku mbegu Y ikiwa tayari imeshaharibika kutokana na kutangulia kwake mbele haraka na kukosa uimara wa kusubiria siku zote hizo. “Mkishiriki tendo la ndoa mapema kidogo, kama siku mbili au moja hivi karibu na yai kutoka, mtapata mtoto wa kiume. Lakini ikiwa ni siku nyingi kabla ya hapo kuna uwezekano mkubwa wa kupata mtoto wa kike,” alisema Dk. Colman kabla ya kutahadharisha kwa kuongeza: “Ila hizi zote siyo kanuni za kudumu maana mwili wa binadamu hubadilika… lazima hili lifanyike kwa kuzingatia mzunguko wa mwanamke na hiyo ni kwa mujibu wa matokeo ya tafiti.” Aidha, Dk. Colman alisisitiza kuwa msingi wa mafanikio ya mpango huo wa kuchagua jinsia ya mtoto kwa kuratibu mzunguko wa hedhi ya mama ni kujua kwa usahihi siku za mzunguko huo. “Kikubwa ni mwanaume na mwanamke kujua yai linatoka lini ili mbegu X au Y zikutane na yai la mwanamke na kufanikisha utungwaji wa mimba ,” alisema Dk. Colman. Aliongeza kuwa, endapo kuna wazazi wanapenda kuwa na watoto wa jinsia tofauti, ni vyema wakazingatia njia hiyo isiyogharimu chochote ya kuzingatia vyema mzunguko wa hedhi wa mwanamke kama ni wa kawaida, mrefu au mfupi. Alisema eneo hilo ndilo huwashinda wengi na kupata matokeo tofauti na yale wanayoyatarajia. “Hapa wengi huchanganya sana. Unakuta mwanamke mzunguko wake ni wa siku 28 na hivyo yai hutoka siku ya 14, lakini wawili hao wanatumia kanuni nyingine ya mzunguko mfupi wa siku 21 ambayo yai hutoka siku ya 10. Ni lazima pia kuzingatia muda wa kushiriki tendo la ndoa kulingana na tabia nilizozitaja za X na Y,” alisema Dk. Colman. “Hadi sasa, katika watu 10 walionifuata na kuniomba ushauri wa kupata watoto wa jinsia waitakayo, nane wamefanikiwa (asilimia 80). Kwa hiyo utaona kwamba jambo hilo linawezekana, ila muhimu ni kuzingatia masuala hayo ya mzunguko wa mama na siku ya kushiriki tendo la ndoa,” alisema. NJIA YA UPANDIKIZAJI Mbali na njia ya kuzingatia mzunguko wa mama kabla ya kushiriki tendo la ndoa ambayo haileti mafanikio kwa asilimia 100, Dk. Colman aliitaja njia nyingine inayotoa fursa kwa wazazi kuchagua jinsia ya mtoto kuwa ni ile ya upandikizaji mbegu kwa mama kuwa ndiyo ya uhakika zaidi katika kuchagua jinsia ya mtoto. Hata hivyo, Dk. Colman alisema teknolojia hiyo ya upandikizaji ni ghali na kwa hapa Tanzania bado ni ngeni na haipo katika hospitali za Serikali. “Upandikizaji mbegu unaanzia kwa kutolewa mbegu mwanaume na baadaye kupelekwa maabara. Huko hupimwa magonjwa yote ili kujua ubora wake. Pia ni huko maabara ndipo wazazi wanapoweza kujua jinsia ya mtoto wao kwa asilimia 100. Na hii ndiyo njia sahihi na ya uhakika zaidi,” alisema Dk. Colman. Aliongeza kuwa katika siku zijazo, anaamini kuna wakati hospitali yao (Muhimbili) itatimiza lengo la kuanzisha Kitengo Maalum cha Matatizo ya Ujauzito na Uzazi ambako humo, watakuwa na fursa ya kuwasaidia watu wanaohitaji huduma ya upandikizaji wa mbegu kwa ajili ya kupata watoto. KLINIKI YA UPANDIKIZAJI DAR Katika uchunguzi wake, mwandishi wa Nipashe alipata bahati ya kutembelea kituo cha tiba kilichoanzishwa miaka ya hivi karibuni katika maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushughulikia matatizo ya uzazi huku pia kikiwa na teknolojia ya kupandikiza mbegu kiitwacho Dar IVF and Fertilizing Clinic. Mkurugenzi wa Tiba wa kituo hicho, Dk. Tamale Sali, alizungumzia pia uwezekano wa wazazi kupata watoto wa jinsia watakayo kwa kutumia teknolojia ya upandikizaji na kuleta matokeo sahihi ya asilimia 100. “Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa hii njia ya kuchagua jinsia ya mtoto kwa mzunguko wa hedhi hutoa matokeo ya asilimia 50 kwa 50. Siyo ya uhakika sana kwa sababu wazazi wanaweza wanaweza kufanikiwa au wasifanikiwe. Lakini ya upandikizaji maabara ina uhakika zaidi katika kupata mtoto wa jinsia wanayoitaka wazazi,” alisema Dk. Sali. Akieleza zaidi, Dk. Sali alisema kinachoweza kufanyika kwa wale wanaotaka kuwa na watoto wa kiume au wa kike kadri watakavyo ni kuchukuliwa kwa mbegu za mwanaume, kupelekwa maabara na huko ndiko uamuzi kuhusu jinsia ya mtoto unaweza kutolewa na wahusika. Aidha, Dk. Sali aliongeza kuwa mbali na uamuzi kuhusu jinsia ya mtoto, wazazi hupata fursa pia ya kupata mtoto asiyesumbuliwa na maradhi kama ya kisukari na moyo. “Mbali ya kupimwa jinsia ya mtoto, mbegu ya baba hupimwa pia magonjwa mengine kama ya moyo na kisukari… kama itabainika kuwa mbegu ina tatizo, inaachwa na kuchukuliwa mbegu nyingine,” alisema. Dk. Sali alisema kuwa hadi sasa, tangu waanze kutoa huduma zao nchini, tayari wameshasaidia wazazi tofauti 15 kupata watoto wa jinsia waitakayo kwa njia ya upandikizaji huku wastani wa watoto wanaozaliwa nchini Uganda kwa mwaka kupitia njia hiyo katika kliniki yao iliyopo nchini humo ni 30. Alisema wanaopaswa kutumia njia ya upandikizaji katika kupata watoto ni wanawake ambao mirija yao ya uzazi imeziba, wale walio na utasa na baadhi ya wagojwa wenye uvimbe kwenye ‘ovari’, vivimbe vya vimeleo kuzunguka mfuko wa uzazi, wanawake waliomaliza hedhi na bado wanahitaji mchango wa mayai, waliotolewa mfuko wa uzazi lakini ovari zao zimebaki na sababu nyingine za kijamii ikiwamo mume kusafiri kwenda masomoni au vitani. Alisema kwa kawaida, wao hutoa matibabu kwa njia ya upandikizaji pale tu inapowalazimu wanandoa kufanya hivyo ikiwa ni njia ya mwisho baada ya njia nyingine zote za kupata mtoto kugonga mwamba. MSIMAMO WA SERIKALI KUHUSU JINSIA ZA WATOTO Baadhi ya watu hutamani kuwa na mchanganyiko wa jinsia katika orodha ya watoto wao na hivyo huwa tayari kufuata njia mbalimbali ili kuwapata watoto wa jinsia waitakayo ili kukidhi matakwa yao. Hata hivyo, Nipashe imebaini kuwa baadhi ya njia haziruhusiwi nchini ikiwamo ile ya kukatisha uhai wa mimba ya mtoto wa jinsia wasiyoitaka wazazi wakati wa kutungwa kwake. Mkurugenzi wa Uhakiki wa Ubora wa Huduma katika Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mohamed Mohamed, alisema ni kosa kisheria kwa mama kutoa mimba baada ya kujua jinsia ya mtoto anayetarajia kumzaa. Kuhusu upandikizaji alisema sheria inatambua wale wenye matatizo ya uzazi, wenye umri mkubwa na ukomo wa hedhi kuwa hawakatazwi kupandikiza lakini siyo wanandoa wenye afya njema na uwezo wa kupata watoto kwa njia ya kawaida.
Artikel Terkait
HIVI UNAIJUA MAANA YA MAPENZI VIZURI AMA.......???  Jina mapenzi limeweza kupewa maana nyingi kulingana na maongezi yanayozunguka jina hilo. Mapenzi yaweza kusemwa kwamba ni jina linaloonyesha hisia za mtu iwe mahaba, pendo kwa mtu ama upendo wa Mungu. Mara nyingi watu wengi hukosea kwa kuchambua mapenzi katika mahaba pekee. Watu wengi hudhania mapenzi huwa yanahusisha moyo wa binadamu, lakini hakika ni kwamba huhusisha ubongo wa mwanadamu. Kuna aina nyingi za mapenzi ambazo binadamu huonyesha katika maisha yao wanapoendelea na shughuli zao za kila siku. Kama binadamu sisi husahau aina nyingine za mapenzi kwani wengi wetu hawajui neno mapenzi lina maana nyingi. Kwa kufafanua mapenzi yapo na aina zifuatazo Mapenzi ya kimwili (Eros) Aina hii ya mapenzi ni ya kimahaba. Kwa mfano mwanamume kumtamani mwanamke ama vile vile mwanamke kumtamani mwanamume kwa hamu ya ngono. Hapa mapenzi huwa yanayoendelezwa na hisia za kumtaka yule mwingine kimapenzi. Hii ndio aina ambayo watu wengi duniani hudhani ndio maelezo kamili ya mapenzi ill hali hii ni moja yapo ya zingine nyingi. Aina hii ya mapenzi ni muhimu kwa watu wanaoanza kutongozana ama watu wanaofikiri kuwa katika uhusiano. Mapenzi ya Urafiki (Philia) Aina hii ni ambayo inavutiwa na mtu kukufanyia kitendo kizuri ama kukusaidia ama ni mtu mzuri kwa ujumla. Mapenzi hapa yaweza kuwa kwa ndugu ama rafiki yako mzuri. Mapenzi haya huwa sana ambapo mtu wanashiriki maadili sawa na mwenzake na kwamba hisia zao sinaambatana ama mmoja anapokea matendo sawia na yale anamwelekezea yule mwenzake. Mapenzi ya aina hii yanaenziwa sana duniani. Wataaluma huamini kwamba mapenzi ya urafiki husaidia kutoa tamaa ya mwili na kuzingatia kufahamiana zaidi kwa marafiki na dunia kwa jumla. Mapenzi ya Familia(Storge) Aina hii ya mapenzi ni inayoonekana na wazazi kwa watoto wao na pia kutoka kwa watoto kwa wazazi. Aina hii hutofautiana na ya urafiki kwani haizingatii kile mtu anachokutendea bali uhusiano wa kidamu na vile wazazi na watoto wao wanavyotegemeana. Sifa za binafsi hazizingatiwi hapa ili wazazi waonyeshe wanao hisia hizi. Uhusiano wao huchangia kwa mapenzi haya. Mapenzi haya huhusishwa na mtu kujiskia yuko huru na salama. Mapenzi ya Kujitolea(Agape) Aina hii ya mapenzi inazingatia asili, mapenzi kwa Mungu au miungu na mapenzi kwa usiowajua. Hii ni mapenzi ya kujitolea kwa ubinafsi ama mapenzi ya ubinadamu. Aina hii inahusishwa na kuto tarajia malipo au kitu chochote kwa matendo unayoyafanya. Yaani ni mapenzi yakujitolea mhanga. Aina hii ya mapenzi hutusaidia kuwapenda watu tusiowajua na kusaidiana kibinadamu kwa hali yoyote ile. Dunia yastahili kuwa na aina hii kwa wingi ili tukaweza kukaa kwa amani na furaha. Mapenzi kwa Mungu ama niungu pia huwa katika aina hii. Kumwabudu Mungu aliye binguni ni mfano mmoja wa kueleza aina hii. Mapenzi Changamfu (Ludus) Aina hii ya mapenzi ni mapenzi yasio na dhamira yoyote na ma mzaha tu. Mapenzi haya hayana masharti hata kidogo. Mfano wa aina hii ya mapenzi ni kama mtu anovyomtongoza mwingine, kupinga densi na kucheza. Aina hii ya mapenzi haina mambo mengi kwani huwa ni kawaida tu. Aina hii huwa sawa kwa watu wanaojitosheleza kimaisha. Aina hii ya mapenzi huwa gumu wakati mtu mmoja hufasiri kwamba mwingine ana hamu ya kimwili. Inafaa watu waweze kuelewa kama wanahamu zaidi na raha na kufurahi tu. Mapenzi Madhubuti(Pragma) Aina hii ni mapenzi ambayo yako na msingi wa wajibu wako kwa mwingine na wa kuzingatia maslahi ya mwingine ya siku za usoni. Mfano mwema ni kwa wapenzi ambao wako katika ndoa. Aina hii inahusishwa na uvumulivu na maelewano kati ya walio katika ndoa. Aina hii ya mapenzi hukuzwa kwa muda wa miaka kadha na ndio maana yaitwa madhubuti ya ka kudumu. Mvuto wa kimwili sana hauzingatiwi katika aina hii ya mapenzi bali kujengana kimawazo na kufanya maisha yao kuwa bora zaidi. Kinyume na aina zingine za mapenzi mapenzi madhubuti huzingatia pande zote mbili za wapenzi wawili. Lazima wewe wanapendana ama kuwa na mafikira na dhamira sawia. Mapenzi ya Kibinafsi (Philautia) Mapenzi haya ni ya mtu binafsi. Aina hii ya mapenzi huwa ina matokeo mawili, yaweza kuwa nzuri ama ya kudhuru. Upande mbaya wa aina hii huwa kwa ile hali ya ubinafi, kutafuta umaarufu na kutafuta utajiri na hufanya mtu kujiona ana dhamana kuliko mtu mwingine yeyote. Upande huu hufanya mtu akajiona yuko mkubwa kuliko mungu. Pia kuna upande mzuri wa aina hii ya mapenzi ambao inahusiana na mtu kujijua, kwa kufahamu uwezo wako na kujidhamini kwa uzuri wako na unachoweza kufanya. Kwa uhusiano wowote, huwezi kumpenda mwingine kama wewe mwenyewe hauna mapezi ya kibinafsi. Kwa kujipenda kwanza ndio tunaweza kupenda wengine na kuwatunza vizuri maishani. Aina hii ni muhimu sana kwa maisha ya kila mwanadamu. Mapenzi ya kibinafi humsaidia mtu kujua mazuri na mabaya na kupanga maisha yake kwa nji inayostahili. Mapenzi ya kibinafsi humwongezea mtu hali ya kujiamini na kujidhamini. Watu waliyo na mapenzi ya kibinafsi huweza kuelewana sana na watu wengi kwa vile kwa kujidhamini watu pia hukudhamini. Hii husaidia kwa vile mnaelewana na watu kazini, nyumbani na mahali pengine ambapo mnapatana. Watu waliyo na mapenzi ya kibinafsi hawahitaji kujigamba ili watu wawajue ama kujionyesha kwa watu. Uzuriwao hujionyesha kwa wanayofanya na wanavyoongea. Watu wanaojipenda kibinafsi huwa wako huru kwa mambo mapya na uwazi. Uchambuzi na ufahamu wa mapenzi ni nini husaidia kila mwanadamu kutambua aina gani anafaa kuwapa watu kwa kila wakati na aina gani ya mapenzi kutupilia mbali. Mwanadamu anaweza penda ila kwa hiari yake. Haina maana lazima mtu akupende ndio umpende nawe. Kila mwanadamu anauwezo wa kumpenda mwingine ama kitu anachotaka hata kama yeye mwenyewe hajapatiwa mapenzi hayo. Lazima kama mwanadamu kufanya mapenzi kama kitu cha kawaida kwa kila tunachofanya maishani. Iweke iwe sehemu ya maisha yako na utu wako. Pia ni muhimu kuwa na aina hizi zote za mapenzi kwa uhusiano kwa kila siku na watu wengine ilituweze kuishi maisha marefu. Kama binadamu, mapenzi ya muhimu sana ni yale ya kujitolea na yale ya kibinafsi. Unapokuwa na mapenzi yasiyo tarajia kitu chochote na mapenzi yako mwenyewe ndio utaweza kuwapa watu mapenzi hayo mengine. Tukiweza kushikilia aina zote zingine za mapenzi kwa mahusiano yetu basi tutakuwa na maisha marefu na yenye kufana. Mapenzi ni kitu muhimu maishani na ni sharti yaenziwe na kila mwanadamu. ... Read More
Majina Ya Watoto Wa Kiume (26)  Katika tamaduni nyingi, majina ya watoto wa kiume hutokana na majira au matukio ya wakati wanapozaliwa. Kwa mfano, wakati mmoja, mwanamke Mwethiopia alijifungua mtoto wa kiume. Shangwe yake ikageuka kuwa majonzi alipoona mtoto wake akiwa amelala bila kusonga. Nyanya yake alipomchukua mtoto huyo ili amwoshe, kwa ghafla mtoto akaanza kusonga, kupumua na hata kulia. Hali hii ikawa chanzo cha jina la mtoto na hiyo wazazi wake wakaunganisha jina muujiza na neno linguine la Kiamhara na kumwita mvulana huyo Muujiza Umefanyika. Nchini Burundi, majina memgin yalitokana na wakati wa vita vilivyokuwemo mwanzo wa miaka ya tisini. Mtoto aliyezaliwa huku mzazi akijifichakutokana na machambulizi angepatiwa jina kama Manirakiza amabalo maana yake ni’Mungu Ndiye Anayeokoa’. Majina mengine ya wakati ule ni kama Twagirimana na Mwana wa Imana ambayo pia humaanisha mwana wa Mungu au mtu aliyeponea vita kwa muujiza wa Mungu. Desturi hii ya majina ya watoto wa kiume imeenea kote ulimwenguni ambapo kuna majina mengi yaliyo na maana ya nyakati kam wakati wa vita, njaa, shjrehe, makumbusho au tukio amabalo watu hupenda kukumbuka kwa kuwapa watoto majina. Kuna majina kadhaa amabyo ni mashuhuri sana ulimwenguni ;Noah, Liam, Mason, Jacob, William, Ethan, Michael, Alexander, James, Daniel na mengine. MAANA MAJINA TUKIZINGATIA HERUFI YA JINA LA KWANZA (KIUME) HERUFI A Watoto wenye jina linaloanza kwa herufi hii hupenda mambo makubwa,hujiamini sana na huwa na uwezo wa kutimiza malengo yao. Ni watoto wenye tahadhari,wachangamfu na hupenda matukio. Kwa kawaida hupenda kuheshimiwa,hupenda mamlaka,na ana kiburi,watoto wapenda hasira.Kidesturi herufi hii huwakilisha nyota ya punda. HERUFI B Mwenye jina linaloanziana na herufi hii ni watoto wakarimu,waaminifu na hupenda kazi sana. Ni wajasiri, shujaa na wakatili katika vita au popote pale anapotaka kulinda vilivyo katika himaya yake.Herufi hii huwakilisha nyota yangombe. HERUFI C Mwenye jina linaloanzia na herufi hii ni motto wa kubadilikana,ni washindani na hupenda kupigania malengo yao wanayopenda.Ni watu wabunifu na wanapenda mawasiliano,herufi hii huwakilisha nyota ya mapacha. HERUFI D Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni anayependa usawa,biashara ni watu wanaopenda kuamrisha na mwenye kupenda usafi.Ni wajeuri na wenye msimamo. Herufi hii huwakilisha nyota ya kaa. HERUFI E Mwenye jina linaloanza na herufi ni mtu mwenye roho nzuri,mwenye mapenzi na huruma,mwenye kupenda uhuru katika mapenzi na mchangamfu. Ubaya wake ni mtu asiyetegemewa na ni kigeugeu.Herufi hii huwakilishwa na nyota ya samba. HERUFI F Mwenye jina linaloanza na herufi hii n mtu mwenye mapenzi,huruma,roho nzuri na ana uwezo wa kuwafariji watu,ni mtetezi wa watu na mwenye huzuni lakini ni mzito wa kufanya maamuzi.Herufi hii huwakilisha nyota ya mashuke. HERUFI G Mwenye jina linaloanzia na herufi hii ni mtu mwenye imani ya kidini na nguvu za kiroho,ana kipaji cha kubuni na uwezo wa kutatua matatizo ya watu. Ni mtu mwenye hisia kali,msomi,mpweke na mkaidi wa kukubali ushauri kutoka kwa watu.Herufi hii huwakilisha nyota ya mizani. HERUFI H Mwemye jina linaloanzia na herufi hii ni mtoto mwenye ubunifu na nguvu katika biashara,hupata faida kubwa katika anayopenda kutokana na bidii, ni mwenye mawazo mengi,mchoyo na mbinafsi.Herufi hii huwakilisha nge. HERUFI I Mwenye jina inayoanzia na herufi hii ni mtoto mwenye kupenda sharia,ana huruma na utu mzuri.Wakati mwingi ni mtoto mwenye kujiamini sana na mwenye hasira za haraka. Herufi hii huwakilisha nyota yam shale. HERUFI J Mwenye jina inayoanzia na herufi hii ni mtoto mwenye matamanio,mkweli,mkarimu na mwerevu.Huwa asiyekubali kushindwa na hupata mafanikio makubwa,wakati mwingine anakuwa ni mtoto mvivu na anayekosa mwelekeo. Herufi hii huwakilisha nyota ya mbuzi. HERUFI K Mwenye jina linaloanza ha herufi hii ni mtoto mjeuri,mwenye msimamo thabiti,mpenda umashuhuri na mwenye uwezo wa kushawishi na kuamsha hisia za watu, ana uwezo wa utambuzi ambao watu wengi hawana,ni mtoto asiyeridhika. Herufi hii huwakilisha nyota ya ndoo. HERUFI L Mwenye jina linaloanza ha herufi hii ni mtoto wa vitendo,mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha,hupatwa na misiba mara kwa mara.Herufi hii huwakilisha nyota ya samaki. HERUFI M Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye kujiamini sana,mchapakazi na hupata mafanikio,ni mropokaji,mwenye haraka na mwepesi kukasirika. Herufi hii huwakilisha nyota ya punda. HERUFI N Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mbunifu, mwenye hisia kali,hupenda kuwasiliana lakini ana wivu sana.Herufi hii huwakilisha nyota ya ngombe. HERUFI O Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye subira,mvumilivu,na mwenye bidii ya kusoma.Ni mtoto mwenye kupenda kutumikia jamii na mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia.Herufi hii huwakilisha nyota ya mapacha. HERUFI P Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye uwezo wa kuamuru na ana hekima kubwa.Ana nguvu za kiroho lakini anapenda sana kujitumbukiza kwenye mambo ya watu. Herufi hii huwakilisha nyota ya kaa. HERUFI Q Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtotto mwenye kupenda mambo ya asili,ni watu wasioelezeka,wako na uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulikana hata hivyo ni mtu aliyepooza sana.Herufi hii huwakilisha nyota ya samba. HERUFI R Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mtulivu,mwenye huruma lakini mwenye hasira za haraka.Muda mwingi yeye ni mpenda amani. Herufi hii huwakilisha nyota ya mashuke. HERUFI S Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye mvuto kali wa kuleta utajiri,ni mtoto mwenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi makubwa. Herufi hii huwakilisha nyota ya mizani. HERUFI T Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye kupenda ushauri wa kiroho,anatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio baada ya muda mrefu, ni watoto wenye hisia kali na wepesi sana kushawishika.Herufi hii huwakilisha nyota ya nge. HERUFI U Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye bahati kwa ujumla,anapenda uhuru katika mapenzi,ni mbinafsi,mwenye tama na anayekosa maamuzi. Herufi hii huwakilisha nyota yam shale. HERUFI V Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mchapakazi,mwenye bidii asiye choka lakini ni watu wasiotabirika. Herufi hii huwakilisha nyota ya mbuzi. HERUFI W Mwemye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye mawazo sana,mchangamfu sana,mwenye uwezo wa kutambua watu wabaya na wema, ni wenye tama na hufanya mambo hatari sana.Herufi hii huwakilisha nyota ya ndoo. HERUFI X Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto asiyependa kuwekewa vizuizi hasa katika anasa na ni rahisi kwake kujiingiza kwenye uzinzi na kujitoa uaminifu. Herufi hii huwakilisha nyota ya punda. HERUFI Y Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mpenda uhuru na hapendi kupingwa katika jambo lolote,ni watoto wanaokosa uamuzi na husababisha kupoteza bahati katika maisha. Herufi hii huwakilisha nyota ya punda. HERUFI Z Mwenye jina linaloanza na herufi hii ni mtoto mwenye kupenda matumaini na amani,ni wenye msimamo mkali japo ni wenye kukubali ushauri . Herufi hii huwakiisha nyota ya ngombe. ... Read More
UNAJUA KUMPAGAWISHA MPENZI WAKO????  Kama inavyoeleweka, mapenzi ni sehemu muhimu ya afya ya binadamu. So, katika peruzi zangu, nikakutana na hili somo la "Tantric Sex." Kama inavyoelewaka, mapenzi ni sehemu muhimu ya afya ya binadamu. So, katika peruzi zangu, nikakutana na hili somo la “Tantric Sex.” As if hii duinia, especially hii century haiko overloaded na information kuhusu mambo ya mapenzi, jinsi ya kufanya mapenzi and whats hot in the bedroom, whats in and whats not. So, lately nimeona a lot of tzmoms readers wamekuwa wakitembelea sana na kusoma page ya “mapenzi baada ya ujauzito” na “kufanyamapenzi wakati wa ujauzito.” And I thought well, writing about Tantric Sex will be nyongeza kwa kila mmoja, aliye mama na mbaye bado damu inachemka katika mambo ya mapenzi. Anyhu, kama “SEX/MAPENZI” yangekuwa yanaweza kuyu-nite the world/countries/makabila/people I think hii fani ingeshinda. Well, so kama umeshawahi kujifungua ama kama wewe ni mama, you definitely understand ni jinsi gani ni vigumu kuwa upbeat kuhusu mapenzi ama kumfurahisha mumeo/mpenzio everyday. Well, once in a while maybe but not everyday. Ila kama we ni mdada/binti ambaye hujazaa bado well, damu yako bado inachemka so energy bado ipo nyingi ya kukurupushana na mpenzio. Having said that, si maanishi mtu ukishazaa ndo fani ya kuenjoy mapenzi imekwisha but nguvu zinapungua for sure however, kuna vitu vingi tuu ambavyo vinaweza kusaidia kuleta nguvu ya kutaka kukurupushana chumbani lol. Kukosa nguvu/energy to wanna work it all the time its not because mwanamke ni mvivu but hutokana na kuwa na mambo mengi sana ya kutend nyumbani i.e. kuhakikisha watoto wako taken care of, labda kazini pia unahitajika, etc una kuta hupati muda wa kujifurahisha mwenyewe ama na mpenzi wako. Therefore, mara nyingi before you know mupenzi anaanza kulalamika or hata mwanamke mwenyewe unaweza kufeel like you are not doing enough so mambo ndo hivyo yanaanza kwenda south chumbani. Hivyo basi, lets dig in tuone Tantric Sex inatoa msaada wa aina gani ili kurevamp mapenzi. Kwanza kabisa, FYI tantric sex can be weird at the beginning ila nitajitahidi kutoingia so indepth ili kusave miyoyo ya watu wengine. Kwamaana hii ni soft porn “according to me.” Lol. so usishtuke ama kushangaa sana. Well, anythign “sex” can be unconfortable anyways. Okay, so, kwanza kabisa, with Tantric Sex, mtu na mpenziwe wanatakiwa kuwa; SPIRITUALLY CONNECTED (usishtuke sio kidini lol).. Hii inamaainisha kwamba wewe na patner wako kwa pamoja mnajua mnataka nini emotionally and physically. Kwa kufanya hivi inasaidia kuwafanya kwa pamoja kuwa “FREE” na kuondoa wasiwasi wa labda mwenzangu atanijudge kwamba labda mimi ni malaya ama fuska etc. In other words hii process inaitwa “Dropping the Veil, between “Self” and “Other/patner.” THE ENVIRONMENT/mazingira. Wakati mnapractice tantric sex of course, just like when you are in the bedroom unaweza ukavaa lingerie/kuo za ndani zinazovutia or “kuwa kama mlivyotoka tumboni mwa mama zenu” (you know what i mean). Tatu, wapenzi wanaanza kupapasana lol, but in a way kwamba you are feeling the energy of the other person. Na hii energy unaweza kuifeel kwasababu mko free hamna anayemjudge mwingine/there are no worries. You are just in your own created world. Nne, wakati wa kufeel energy ya mwingine lazima wapenzi wawe wana pumua heavely yaani just feeling every move made but the other person mpaka mnapofikia mahali were you are breathing so hard and you are feeling each other. then you start kissing the lips, and then deeper for minutes even hours. Then mengineyo yanaweza kuendelea. So, all this time kumbuka its not about going straight into sex with your partner rather its about getting high by touching and feeling connected with each other. hivyo basi, once in a while take that time and revamp your intimacy, dress good, feel sexy and heey have fun!!. By 🅱 ... Read More
Kwanii Wanaume Waaminifu Kwenye Uhusiano Huachwa.....  Kuachwa na mpenzi kwa sababu umekuwa ni muaminifu sana yaonekane ni jambo lisiloingia akilini lakini linatokea. Moja ya mambo ya ajabu unayoweza kuwa ushawahi kuyasikia ni kwamba mara nyingine uamuzi wako wa kuwa mwanaume mwema sana na unayejitahidi kufanya uhusiano wako wa kimapenzi uwe mzuri muda wote unaweza kukugharimu na kujikuta unaachwa kabisa. Haitakiwi kuwa hivyo lakini mara nyingine inatokea, na inatokea kwa sababu wazo la mwenza wako kuhusu uhusiano wa kimapenzi laweza likawa tofauti na ulionao wewe. Wengine wana mawazo hasi kuhusu jinsi uhusiano/ndoa inavyotakiwa kuwa. Hii ndio sababu hutakiwi kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mtu asiye na vipaumbele sawa na vya kwako au asiye na mtazamo mmoja wa kimaisha kama ulionao wewe. Usipozingatia hilo, utajikuta unaingia kwenye uhusiano na mtu ambaye hatakujali vya kutosha kwakuwa labda humfokei au kumpiga anapokukosea – au utajikuta ameshakupanda kichwani na kuanza kukudai mambo ambayo huwezi kuyatimiza lakini ukajikuta unajitutumua kumtimizia kwa sababu unataka kumfurahisha mpenzi wako na analijua jambo hilo. Kwa sababu baadhi ya wanaume wanapenda kulinda siri na kuwaachia uhuru wapenzi wao, wanajikuta wakiwapa ruhusa wanawake zao kwenda popote wanapojisikia bila kuwafatilia wanachofanya. Nini kinafata baada ya hapo? Mwanamke anatoka, anatafuta mchepuko na kukusaliti. Mwisho inakufanya wewe mwanaume uonekane mjinga mbele ya wengine. Tatizo ni kwamba tabia hii inaibuka kutokana na mazoea ya watu kuingia kwenye uhusiano wakiwa wameficha tabia zao halisi na kuja kufungua makucha yao baada ya kuona ameshaishi na wewe kwa muda mrefu kiasi kwamba huwezi tena kumuacha. Hii inasababisha wanaume walioathirika kutokana na tabia kama hizi kutoka kwa waliokuwa wapenzi wao wasiweze kuwaamini wanawake wengine tena kwa kuona kwamba wote ni sawa na wale waliowaumiza na kusababisha wasiweze kuwaonesha wenza wao wapya mapenzi kwa kiwango cha juu wakihofia kuumizwa tena. Kuwa mpole, mkarimu na mwenye upendo wa hali ya juu kwa mpenzi wako ndio jambo linalotarajiwa kwenye uhusiano. Mtu hatakiwi kufanywa ajisikie vibaya kwa kumuonesha mapenzi ya kweli mwenza wake. Kama wewe unakuwa muaminifu na mwema kwa mpenzi wako lakini umekuwa unadharauliwa au ukaachwa kutokana na tabia hiyo, kaa ukiwa na amani kabisa kwamba lawama za kuvunjika kwa uhusiano huo hazikuhusu wewe – lawama ni za mpenzi wako aliyeshindwa kujua wewe umekuwa mwema kiasi gani kwake. ... Read More
Kanuni Kumi '10' Muhimu za Kuwa Mke Mwema Katika Ndoa....Ikizishindwa Imekula Kwako  UHALISI WA MAISHA: Maisha halisi ya mwanamke anayetarajia kuwa mke/ mke tayari hii ni kumaanisha kuwa wanawake mashujaa tunapaswa kuishi maisha ambayo yanatutambulisha kama mfano wa kuigwa ili tunapozungumza na kufundisha mabadiliko tuwe tunazungumza uhalisia wa maisha yetu ambao unajengwa na haya yafuatayo; UVUMILIVU: Kuwa mvumilivu katika maisha yake ya kila siku hasa ukizingatia kuwa tunakutana na mambo mbali mbali yasiyotuvutia katika mahusiano yetu, mengine ni magumu na yanayokwenda kinyume kabisa na matakwa yetu au mazoea yetu ya binafsi. Ifahamike kwamba wewe kama mwanamke shujaa inapotokea umekutana na mambo kama haya hupaswi kuonyesha hasira zako wazi wazi kama vile; chuki, kulaumu, ugomvi, vurugu, malalamiko, manung’uniko, machafuko, kulipa kisasi au aina yoyote ya uharibifu kutokea kwako au ndani mwako. Hivyo mwanamke shujaa huwa ni heri kila anapokuwa kwani hutunza amani ya eneo alipo. UPENDO WA DHATI: Maisha ya upendo wa halisi na sio wa kinafki kwa jamii inayomzunguka. Tabia ya upendo wa halisi ina thamani kubwa sana kuliko mali nyingi, pesa, elimu ya juu n.k. wewe unaweza kabisa kuwa na elimu ya juu sana na pesa nyingi sana lakini pasipo upendo wa halisi ni sawa na kusema kopo zuri kwa nje na ndani hamna kitu. Nguzo kuu ya maisha ya mwanamke shujaa ni Upendo wa dhati na uhalisia. UTII KWA KWA JAMII: Maisha halisi ya utii katika jamii inayokuzunguka ili kuweza kuyafanyia kazi yale yote uliyojifunza na pia kuyatenda kwa ufasaha pasipo kupita kona yoyote. Utii kwa jamii ni ufunguo mmoja wapo utakaokusaidia kufanikisha mambo yako na malengo yako kama mwanamke shujaa. UAMINIFU KATIKA JAMII: Kuishi maisha ya uaminifu wa kweli na uhalisia katika jamii inayomzunguka. Uaminifu wa kweli huonekana nyakati zote na siyo tu wakati mtu anapokuwa mbele za watu wanaomjua bali hata wale wasiomjua na hata anapokuwa mahali peke yake aweze kutunza uaminifu wake kwa faida ya jamii nzima. Mwanamke shujaa hujitahidi sana kutunza uaminifu wake katika sekta zote. UNYENYEKEVU WA KWELI: Kuishi maisha halisi kabisa ya unyenyekevu kwa jamii inayomzunguka, unyenyekevu ni kinyume kabisa na kiburi, majivuno, kujigamba, kujikweza, kujiinua, kujiona,na hata kjitanguliza mbele kwa kila jambo. Mwanamke shujaa huwa ni mnyenyekevu wakati wote na hana makuu daima. UWAJIBIKAJI WA DHATI: Maisha halisi ya uwajibikaji akiangalia majukumu yake yote yanayomkabili na kuhakikisha anafanya kwa moyo bila kuwa na tabia ya kusaidiwa majukumu yake. Mwanamke shujaa ni mfano wa kuigwa kutokana na uwajibikaji wake. USHIRIKIANO WA DHATI: Ushirikiano katika jamii inayomzunguka. Sisi wanawake mashujaa yatupasa kujua dhahiri kuwa kazi ya kubadili tabia na kufanya wengine wabadilike kwa lengo la kupata familia bora ni lazima kuwa na ushirikiano wa kweli ambao utajenga tabia ya kuaminiana na kunai mamoja katika harakati hizi za kuandaa/ kujenga familia bora. UTARATIBU WA KAZI/MPANGILIO: Katika utaratibu wa maisha yake, pamoja na mpangilio mzuri wa mambo yanayomzunguka hii itakusaidia kuwa na muda mzuri wa kufanya shughuli zako na pia kutekeleza majukumu yako ya kila siku kama mwanamke shujaa. Hakuna njia yoyote ya kukuwezesha kukua na kuendelea katika maisha yako bila kuwa na utaratibu na mpangilio wa mambo yako. KUFANYA TATHIMINI: Kuweza kufanya tathimini ya yale yote anayoyafanya katika maisha yake ya kila siku, pengine ni mfanyabiashara, mfanyakazi, mkulima n.k kama mwanamke shujaa yakupasa kutathimini shughuli zako kama zina leta faida/hasara kwa familia na jamii yako inayokuzunguka. Ukiona faida ni kubwa unaendelea na hiyo shughuli lakini kama hasara ni kubwa unajiweka katika nafasi ya kubadilisha aina ya shughuli mara moja bila kupoteza wakati. ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: