Nakuuliza Mwanamke "NI KWANINI WANAUME HAWARIDHIKI NA MWANAMKE MMOJA?" Nakuona unavyojitengeneza usome UDAKU Wanaume kwa asilimia 75 hawaridhiki na mwanamke mmoja, Na katika hili naomba niseme kuwa HAWARIDHIKI KWAKUWA HAWAJUI NINI HASA HITAJI LAO KWA MWANAMKE ndo maana wanaume wa aina hiyo hata awe na mwanamke mzuri na mkamilifu kama BIKRA MARIAM kamwe hawezi kuishi bila kuchepuka, Sina maana nawatukana ama nawatolea siri zetu laa hasha! Ni katika kuweka uwiano wa furaha katika mahusiano na Mapenzi kwa ujumla, Asilimia 25 ni wanaume wajuao mahitaji yao kwa mwanamke, Wanaume hawa huzitunza familia zao lakini pia wanayo bidii kuzijenga ndoa zao. NINI KIFANYIKE KATIKA HILI? Hakuna bin adam awezaye kumbadilisha bin adam mwenzie ila mamlaka na nguvu zipo kwa MUNGU... Waweza kuwa mzuri na mwenye mvuto hata wanawake wenzio wakakutamani lakini kwa mwanaume mzinzi wewe ni PITIO TU maana hajui haja yake kwako, Amini nakwambia ndo maana hata mtume Paulo katika kitabu cha 1 WAKORINTHO 7:8-9 Biblia inasema; "Lakini nawaambia wale wasiooa Bado na wajane, Ni heri wakae kama Mimi nilivyo, Lakini ikiwa hawawezi kujizuia na waoe, Maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa" Mungu awasaidie wanawake maana mko na changamoto.

at 1:46 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top