KWANINI WIVU NI HATARI KWA BIN ADAM? Kuna aina nyingi za wivu lakini hapa napenda nitofautishe aina mbili za wivu; 1. WIVU WA MAPENZI 2. WIVU WA MAFANIKIO Nianze na wivu wa Mapenzi, wivu huo ni rafiki kwa Mapenzi ili kuileta maana ya neno NAKUPENDA... Mtu mwenye upendo wa DHATI anao wivu kwa huyo aliyempenda japo nitoe angalizo UKIZIDISHA WIVU UNAHARIBU MAANA YA PENDO LENYEWE maana kuwa na kiasi ni kuitengeneza taswira ya mahusiano husika, Huwezi kumpenda mtu halafu unasikia wivu mpaka UNAMPIGA AMA KUMTUKANA! Jizuie wivu usihame moyoni ukakimbilia akilini nakwambia huwezi kufurahia, Jifunze kuwa na wivu ambao utakulindia penzi lako na kutoingilia UHURU wa mwenzi wako, Mungu ametuumbia UPENDO lakini akatuwekea wivu ili kuutetea moyo ila USIVUKE MIPAKA husika Kwani utaimarisha furaha yako kila siku, Kwa upande wa pili Yaani wivu wa MAFANIKIO hapa ndipo nataka niwakumbushe ndugu zangu, Kila bin adam anao wivu wa mafanikio Kwani ndiyo UBIN ADAM... Kuona wivu wa mafanikio ni chanzo cha mafanikio ikiwa unao uthubutu lakini usipende kutaka kujilinganisha na mwingine Kwani kwa kufanya hivyo UNATENDA DHAMBI! Ukisoma maandiko kitabu cha ZABURI 37:7-8 Biblia inasema; "Ukae kimya mbele za BWANA, Nawe umngojee kwa saburi, Usimkasirikie yeye afanikiwaye katika njia yake, Wala mtu afanyaye hila, Ukomeshe hasira, uache ghadhabu, usikasirike mwisho wake ni kutenda mabaya" Maana kila mtu kwa karama yake, Unayo BARAKA kuwa bin adam ni jukumu lako kujuwa Unataka nini na kwa wakati gani huku ukimtumainia Mungu, Mashindano pamoja na majivuno hudhoofisha Baraka zako, Maandiko katika kitabu cha WAFILIPI 2:3 Biblia inasema; "Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno bali kwa unyenyekevu, Kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake" Na ndivyo utakapoziona BARAKA ZAKO kuliko kuishi kwa wivu kwa mafanikio ya mwenzio, Kama ambavyo Mungu anawanyeshea mvua watu wote Basi ujue jambo moja UMTUMAINIE MUNGU KULIKO CHOCHOTE maana yeye ndiye ajuaye haja yako, Maandiko katika kitabu cha MHUBIRI 7:14 Biblia inasema; "Siku ya kufanikiwa ufurahi, Na siku ya mabaya ufikiri, Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambamba na hiyo ya pili, ili mwanadamu asipate kulijuwa neno lolote litakalofuata baadaye" Kwa hayo nakuasa kujitenga na wivu mbaya ila uwe na wivu ambao una Baraka ndani yake, BARIKIWA KWA NENO HILI.

at 1:47 AM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top