Hapa ndipo ambapo Mwanaume huishusha heshima yake kwa mkewe, Ni kweli MACHO HAYANA PAZIA lakini Yapo mambo ya kutazama na mengine sio ya kutazama uwapo na mwenza wako, Unajuwa macho yanaweza kuona ila usikubari macho yakayumbisha akili yako hata ukajikuta unaaibika mbele ya mkeo, Kwani ni gauni ama viatu alivyovaa mwanamke huyo ndo vikukoseshe UAMINIFU KWA MKEO? Wanaume sisi acha tutukanwe kuwa tuna vichwa viwili na kichwa kimoja hakina ubongo ila kina nguvu ya kuharibu akili ya kichwa kingine ... Maana sio kwa udhaifu huo jamani, Kama umependa gauni ama viatu si uendage kwa duka umnunulie mkeo avae aendane na vile macho yako yanatakagaa? Unakuta umezuzuliwa na nguo pamoja na viatu mwenzio alinunua hata elfu 50 hazifiki, Wewe mkeo pengine hujawahi kumuuliza anapenda mavazi gani ila kulingana na ubabe wako nae anakunyamazia ili kuendana na hali halisi, Unajikuta umehonga laki moja kwa ajili ya mavazi SI MBADILISHIE MAVAZI MKEO kuendana na upendavyo ili akunusuru na kichaa cha macho ulicho nacho? USIONE VYAELEA BABU VIMEUNDWAAAA! Ukitaka kudandia vya wenzio utapaliwa.

at 1:49 AM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top