FUNGULIWA NA KISA HIKI CHA NDEGE Kulikuwa na ndege aliyekua akiishi Jangwani; ndege huyo alikuwa mgonjwa, manyoya yamepukutika, hakuna chakula, maji ya kunywa wala kiota. Siku moja malaika alipita hapo jangwani, ndege yule akamsimamisha malaika na kumuuliza, "unaelekea wapi?" malaika akamjibu "naenda kuonana na Mungu" Hivyo ndege akamwambia malaika, 'tafadhali sana muulize Mungu, ni lini matatizo yangu yataisha' Malaika akamwambia 'sawa nitamuuliza na akamuaga. Malaika alipofika kwa Mungu akamshirikisha Mungu ule ujumbe alopewa na yule ndege . Malaika akamuelezea Mungu ni jinsi gani alivyomkuta yule ndege akiwa na hali mbaya. Mungu akamjibu malaika na kumwambia "Kwa muda wa wiki saba ndege huyo ataendelea kuhangaika hivyo hivyo, hatakuwa na furaha mpaka atakapofariki". Malaika akasema ndege atakaposikia haya ataumia sana roho, unaweza ukamsaidia kupata suluhisho la matatizo yake? Mungu akajibu: Mwambie awe anarudia rudia maneno haya " Asante Mungu kwa kila kitu". Malaika akaonana na yule ndege na kumueleza ni nini Mungu anahitaji. Baada ya wiki saba, malaika alipita tena na kumuona ndege akiwa na furaha, manyoya yamemuota, nyasi zimeota ktk sehemu ya jangwa lile, kijito kidogo cha maji, na kiota ktk mti uliopo pembeni, na ndege alikuwa akiruka ruka kwa furaha huku akiimba. Malaika alishangaa imekuaje kuaje, 'Mungu alisema kwa wiki saba ndege hatakuwa na furaha, sasa hii imekuaje tena' huku akiwa na maswali haya malaika akapita na kwenda kumuuliza Mungu. Mungu akamjibu malaika kwamba, "imeandikwa kwamba ndege hatakuwa na furaha kwa wiki saba, lakini ndege huyo amejawa na shukrani kwa kusema Asante Mungu kwa kila hali anayopitia, pale alipoanguka ktk mchanga wa moto wa jangwani alishukuru, pale aliposhindwa kuruka alishukuru, alipokosa kabisa chakula alishukuru kwa kusema Asante Mungu kwa kila kitu. Kwa hizo wiki saba niliingiwa na huruma na kumtengenezea mazingira mazuri ikiwemo na kuihuisha afya yake ndege huyu mwenye uvimilivu aliejaa shukrani. SOMO KWETU SOTE katika hali yoyote unayopitia usishau kumkumbuka Mungu wako. Mshukuru Mungu ktk mahusiano yako, uchumi wako, biashara yako, rafiki zako, wafanyakazi wenzako na kwa kila hali unayopitia. Lengo la ku share nanyi story hii ni kukumbusha jinsi gani Shukrani zilivyo na nguvu. Acha kulalamika, tengeneza furaha yako huku ukimshukuru Mungu Namalizia kwa kusema, kuwa na shukrani ushuhudie kubadilika kwa attitude yako, kuwa na subira na baraka zako. Nashukuru sana kwa kusoma! Asante Mungu kwa kila kitu. Ijumaa njema yenye Baraka! share

at 1:35 PM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top