Home → ushauri
→ DAWA ZA FANGASI NA JINSI YA KUZITUMIA VIZURI
Fangasi ni miongoni mwa vijidudu vya magonjwa vinavyosumbua watu wengi. Magonjwa ya fangasi ni mengi sana na mengine ni hatari sana kiasi cha kuweza kusababisha vifo, hususan kwa watu wenye kinga ndogo ya mwili. Magonjwa yao huwa kwenye ngozi, kwenye damu, kwenye kucha, kichwani, kwenye ubongo na viungo vingine vya mwili.
Tatizo kubwa zaidi kwa watu walio wengi ni fangasi wa kwenye ngozi, kucha na nywele. Husababisha mapunye, mashilingi, muwasho, michubuko, vidonda, vipele, harufu mbaya, nywele kutoota vizuri, kucha kukatika au kutoota nk
Tatizo la fangasi ni kubwa zaidi kwa watoto, wanawake na wakazi wa maeneo yenye joto na unyevu unyevu.
DAWA ZA KUTIBU MAGONJWA YA FANGASI
Tuna dawa nyingi za kutibu magonjwa ya fangasi. Dawa hizi zinatofautiana sana kwa uwezo na aina ya fangasi zinazoweza kuwadhibiti vizuri. Kwa hiyo, sio kila aina ya fangasi inaweza kutibiwa kwa dawa yoyote ya fangasi.
Dawa za fangasi ni pamoja na
1. Clotrimazole
2. Fluconazole
3. Ketoconazole
4. Griseofulvin
5. Nystatin
6. Itraconazole
7. Econazole
8. Terbinafin
9. Tolnaftate
Dawa hizo zipo katika mitindo mbalimbali kama vile vidonge, krimu, losheni, poda, sindano, kimiminika nk.
Muhimu : Dawa hizi zinatakiwa kutumika baada ya uchunguzi wa daktari na kushauriwa na daktari na mfamasia. Pia hapa tumeziorodhesha kwa lengo la kukuelimisha tu, kwa hiyo usiende kununua dawa yoyote wala kutumia dawa yoyote kati ya hizo bila kupata ushauri wa daktari.
Ni muhimu kutambua kwamba ushauri wa daktari na mfamasia ni muhimu sana kabla ya kununua na kutumia dawa yoyote. Na ukitaka matokeo mazuri hakikisha unatumia dawa vizuri.
JINSI YA KUTUMIA VIZURI DAWA ZA FANGASI
Fangasi wana tabia ya kuondoka pole pole. Kwa hiyo unaweza ukahisi umepona baada ya kuona muwasho, harufu, majimaji, michubuko, mapunye au mashilingi yamepungua au kupotea. Ukweli ni kwamba inawezekana fangasi bado wapo na ukiwahi kuacha dawa wanajitokeza tena baadae.
Fangasi wanaweza kuwepo nje ya mwili na ndani ya mwili. Ni vyema kupata matibabu yanayosaidia kuondoa fangasi sehemu zote ili ukipona upone kabisa na ugonjwa usijirudie au kuwa sugu.
Kwa dawa za kupaka na fangasi wa kwenye ngozi hakikisha unaendelea kupaka dawa kwa wiki moja hadi mbili baada ya dalili za fangasi kupotea na kuhisi umepona. Hii inakusaidia wewe kuwamaliza kabisa na kuwazuia wasije wakaibuka tena.
Kwa ugonjwa unaohitaji vidonge basi hakikisha unatumia vidonge na unatumia vizuri. Ukitumia ya kupaka peke yake unaweza usipone vizuri, tumia vidonge kama utakavyoshauriwa na daktari na mfamasia wako.
Baadhi ya fangasi matibabu yake huchukua muda mrefu. Mifano ni fangasi wanaoathiri kucha na nywele, matibabu yake huweza kuchukua mwezi mmoja au zaidi. Kuwa mvumilivu na maliza dawa zote.
Kama una ujauzito ambao ni ngumu kujulikana na daktari au mfamasia wafahamishe kwamba wewe ni mjamzito. Hii itasaidia kukukinga wewe na mtoto dhidi ya dawa ambazo hazifai kwenu.
Kama una matatizo ya ini, figo, magonjwa mengine au unatumia dawa zingine ni vyema ukamfahamisha daktari na mfamasia wako pia. Hii ni kwa sababu kuna muingiliano mkubwa sana kati ya dawa za fangasi na magonjwa na dawa zingine kiasi cha kuweza kukuathiri wewe, afya yako na matibabu yako.
Tumia dawa zote kama utakavyoshauriwa. Hii ndiyo tiketi ya kupona kwako.
DAWA ZA FANGASI NA JINSI YA KUZITUMIA VIZURI Fangasi ni miongoni mwa vijidudu vya magonjwa vinavyosumbua watu wengi. Magonjwa ya fangasi ni mengi sana na mengine ni hatari sana kiasi cha kuweza kusababisha vifo, hususan kwa watu wenye kinga ndogo ya mwili. Magonjwa yao huwa kwenye ngozi, kwenye damu, kwenye kucha, kichwani, kwenye ubongo na viungo vingine vya mwili. Tatizo kubwa zaidi kwa watu walio wengi ni fangasi wa kwenye ngozi, kucha na nywele. Husababisha mapunye, mashilingi, muwasho, michubuko, vidonda, vipele, harufu mbaya, nywele kutoota vizuri, kucha kukatika au kutoota nk Tatizo la fangasi ni kubwa zaidi kwa watoto, wanawake na wakazi wa maeneo yenye joto na unyevu unyevu. DAWA ZA KUTIBU MAGONJWA YA FANGASI Tuna dawa nyingi za kutibu magonjwa ya fangasi. Dawa hizi zinatofautiana sana kwa uwezo na aina ya fangasi zinazoweza kuwadhibiti vizuri. Kwa hiyo, sio kila aina ya fangasi inaweza kutibiwa kwa dawa yoyote ya fangasi. Dawa za fangasi ni pamoja na 1. Clotrimazole 2. Fluconazole 3. Ketoconazole 4. Griseofulvin 5. Nystatin 6. Itraconazole 7. Econazole 8. Terbinafin 9. Tolnaftate Dawa hizo zipo katika mitindo mbalimbali kama vile vidonge, krimu, losheni, poda, sindano, kimiminika nk. Muhimu : Dawa hizi zinatakiwa kutumika baada ya uchunguzi wa daktari na kushauriwa na daktari na mfamasia. Pia hapa tumeziorodhesha kwa lengo la kukuelimisha tu, kwa hiyo usiende kununua dawa yoyote wala kutumia dawa yoyote kati ya hizo bila kupata ushauri wa daktari. Ni muhimu kutambua kwamba ushauri wa daktari na mfamasia ni muhimu sana kabla ya kununua na kutumia dawa yoyote. Na ukitaka matokeo mazuri hakikisha unatumia dawa vizuri. JINSI YA KUTUMIA VIZURI DAWA ZA FANGASI Fangasi wana tabia ya kuondoka pole pole. Kwa hiyo unaweza ukahisi umepona baada ya kuona muwasho, harufu, majimaji, michubuko, mapunye au mashilingi yamepungua au kupotea. Ukweli ni kwamba inawezekana fangasi bado wapo na ukiwahi kuacha dawa wanajitokeza tena baadae. Fangasi wanaweza kuwepo nje ya mwili na ndani ya mwili. Ni vyema kupata matibabu yanayosaidia kuondoa fangasi sehemu zote ili ukipona upone kabisa na ugonjwa usijirudie au kuwa sugu. Kwa dawa za kupaka na fangasi wa kwenye ngozi hakikisha unaendelea kupaka dawa kwa wiki moja hadi mbili baada ya dalili za fangasi kupotea na kuhisi umepona. Hii inakusaidia wewe kuwamaliza kabisa na kuwazuia wasije wakaibuka tena. Kwa ugonjwa unaohitaji vidonge basi hakikisha unatumia vidonge na unatumia vizuri. Ukitumia ya kupaka peke yake unaweza usipone vizuri, tumia vidonge kama utakavyoshauriwa na daktari na mfamasia wako. Baadhi ya fangasi matibabu yake huchukua muda mrefu. Mifano ni fangasi wanaoathiri kucha na nywele, matibabu yake huweza kuchukua mwezi mmoja au zaidi. Kuwa mvumilivu na maliza dawa zote. Kama una ujauzito ambao ni ngumu kujulikana na daktari au mfamasia wafahamishe kwamba wewe ni mjamzito. Hii itasaidia kukukinga wewe na mtoto dhidi ya dawa ambazo hazifai kwenu. Kama una matatizo ya ini, figo, magonjwa mengine au unatumia dawa zingine ni vyema ukamfahamisha daktari na mfamasia wako pia. Hii ni kwa sababu kuna muingiliano mkubwa sana kati ya dawa za fangasi na magonjwa na dawa zingine kiasi cha kuweza kukuathiri wewe, afya yako na matibabu yako. Tumia dawa zote kama utakavyoshauriwa. Hii ndiyo tiketi ya kupona kwako.
Artikel Terkait
Je Wajua Kwanini Wanawake Hula Vyakula vya Ajabu Ajabu Wakiwa Wajawazito?  Tabia hii inayojulikana kwa Kiingereza kama “Pica” inatokana na mtu kutamani kula vitu vyenye virutubisho kidogo sana au visivyo na virutubisho vya aina yoyote kwa mwili. Tamaa hizi huwa zinawapata watoto au mama mjamzito kutafuna vitu ambavyo kimsingi si chakula – kama udongo au chaki. Jina hili la pica ni aina ya ndege ambaye anajulikana kwakuwa anakula kitu chochote, hana anachochagua. Ni kweli kwamba wajawazito wengi hupata hamu ya kula vitu ambavyo si vyakula walivyozoea kula mara kwa mara wakiwa si wajawazito; wengi wao ni rahisi kuwaelewa kwa sababu hukimbilia mchele, barafu na vinginevyo ambavyo si vitu vibaya kula. Kwa watoto, hii ni tabia iliyozoelekakwakuwa inawatokea watoto wengi ambao ni kati ya asilimia 25 na 30% ya watoto wote; lakini kwa wanawake wajawazito, inatakiwa iwe kwa kiwango cha chini zaidi. Nini kinasababisha tabia hii kwa wajawazito? Sababu ya baadhi ya wanawake kuwa na tabia hii wakati wa ujauzito haijulikani hasa. Kwa sasa hakuna sababu maalumu, lakini kwa mujibu wa Jarida la Chama cha Watu Wanaoishi na Ugonjwa wa Kisukari nchini Marekani, tabia hii yawezekana ikasababishwa na upungufu wa madini ya chuma mwilini. Baadhi wanadai kwamba hali hii inaashiria kwamba mwili unajaribu kupata vitamini na madini mengine yanayokosekana kwenye chakula cha kawaida ambacho mtu anakula. Muda wingine tabia hii yawezaikatokana na kuumwa viungo au akili kwa muda mrefu. Baadhi ya vitu vya ajabu ambavyo wajawazito hupenda kula Vitu vinavyopendwa zaidi na wajawazito wengi ni udongo, uchafu. Vitu vingine ni njiti za kiberiti zilizochomwa, mawe, mkaa, barafu, dawa ya meno, sabuni na mchanga. Mjamzito anapokula vitu hivi hujisikii raha kana kwamba amekula chakula chenye faida kubwa kwake na kwa mtoto aliye tumboni. Kuna hatari yoyote kwa mtoto aliye tumboni? Kula vitu ambavyo si vyakula kimsingi ni jambo linaloweza kusababisha madhara kwa mjamzito mwenyewe na mtoto aliye tumboni. Kula vitu hivi kunaweza kuharibu mfumo wa kawaida wa kunyonya virutubisho kutoka kwenye vyakula na kusababisha mwili wako upungukiwe na madini muhimu unayoyahitaji kwa afya yako na ya ukuaji wa mtoto vilevile. Tabia hii ni hatarishi sana kwakuwa vitu ambavyo si vyakula vinaweza kuwa na viambata ambavyo ni sumu au vyenye vijidudu vinavyoathiri mwili. Kudhibiti tabia hii Usihamaki unapojikuta unatamani vitu vya ajabu ajabu wakati wa ujauzito: inatokea sana na si jambo la kushangaza kwako pia. Jambo la muhimu ni kumjulisha muuguzi wako au wahudumu wa kliniki unayohudhuria kujua maendeleo yako ya mtoto tumboni ili akuelimishe na ahakikishe kwamba una uelewa kuhusu hatari zinazoambatana na tabia hiyo. Baadhi ya mbinu za kutumia kushinda tamaa hizo Mtaarifu mhudumu wako wa afya kwenye kliniki unayohudhuria na muangalie kumbukumbu za ukuaji wa mtoto tumboni pamoja na hali yako ya kiafyaFatilia kiwango chako cha madini ya chuma mwilini pamoja na kiwango cha vitamini na madini mengine unayotakiwa kulaOmba ushauri kuhusu kitu gani uwe unakula ili kubadili ili kuepuka vitu vya ajabu (waweza kumung’unya/ kutafuna vitu kama pipi au ‘big g’ isiyo na sukariMwambie hata rafiki yako mmoja kuhusu hamu hizi na umtake awe anakukataza unapokula vitu vya ajabu ... Read More
Kanuni Kumi '10' Muhimu za Kuwa Mke Mwema Katika Ndoa....Ikizishindwa Imekula Kwako  UHALISI WA MAISHA: Maisha halisi ya mwanamke anayetarajia kuwa mke/ mke tayari hii ni kumaanisha kuwa wanawake mashujaa tunapaswa kuishi maisha ambayo yanatutambulisha kama mfano wa kuigwa ili tunapozungumza na kufundisha mabadiliko tuwe tunazungumza uhalisia wa maisha yetu ambao unajengwa na haya yafuatayo; UVUMILIVU: Kuwa mvumilivu katika maisha yake ya kila siku hasa ukizingatia kuwa tunakutana na mambo mbali mbali yasiyotuvutia katika mahusiano yetu, mengine ni magumu na yanayokwenda kinyume kabisa na matakwa yetu au mazoea yetu ya binafsi. Ifahamike kwamba wewe kama mwanamke shujaa inapotokea umekutana na mambo kama haya hupaswi kuonyesha hasira zako wazi wazi kama vile; chuki, kulaumu, ugomvi, vurugu, malalamiko, manung’uniko, machafuko, kulipa kisasi au aina yoyote ya uharibifu kutokea kwako au ndani mwako. Hivyo mwanamke shujaa huwa ni heri kila anapokuwa kwani hutunza amani ya eneo alipo. UPENDO WA DHATI: Maisha ya upendo wa halisi na sio wa kinafki kwa jamii inayomzunguka. Tabia ya upendo wa halisi ina thamani kubwa sana kuliko mali nyingi, pesa, elimu ya juu n.k. wewe unaweza kabisa kuwa na elimu ya juu sana na pesa nyingi sana lakini pasipo upendo wa halisi ni sawa na kusema kopo zuri kwa nje na ndani hamna kitu. Nguzo kuu ya maisha ya mwanamke shujaa ni Upendo wa dhati na uhalisia. UTII KWA KWA JAMII: Maisha halisi ya utii katika jamii inayokuzunguka ili kuweza kuyafanyia kazi yale yote uliyojifunza na pia kuyatenda kwa ufasaha pasipo kupita kona yoyote. Utii kwa jamii ni ufunguo mmoja wapo utakaokusaidia kufanikisha mambo yako na malengo yako kama mwanamke shujaa. UAMINIFU KATIKA JAMII: Kuishi maisha ya uaminifu wa kweli na uhalisia katika jamii inayomzunguka. Uaminifu wa kweli huonekana nyakati zote na siyo tu wakati mtu anapokuwa mbele za watu wanaomjua bali hata wale wasiomjua na hata anapokuwa mahali peke yake aweze kutunza uaminifu wake kwa faida ya jamii nzima. Mwanamke shujaa hujitahidi sana kutunza uaminifu wake katika sekta zote. UNYENYEKEVU WA KWELI: Kuishi maisha halisi kabisa ya unyenyekevu kwa jamii inayomzunguka, unyenyekevu ni kinyume kabisa na kiburi, majivuno, kujigamba, kujikweza, kujiinua, kujiona,na hata kjitanguliza mbele kwa kila jambo. Mwanamke shujaa huwa ni mnyenyekevu wakati wote na hana makuu daima. UWAJIBIKAJI WA DHATI: Maisha halisi ya uwajibikaji akiangalia majukumu yake yote yanayomkabili na kuhakikisha anafanya kwa moyo bila kuwa na tabia ya kusaidiwa majukumu yake. Mwanamke shujaa ni mfano wa kuigwa kutokana na uwajibikaji wake. USHIRIKIANO WA DHATI: Ushirikiano katika jamii inayomzunguka. Sisi wanawake mashujaa yatupasa kujua dhahiri kuwa kazi ya kubadili tabia na kufanya wengine wabadilike kwa lengo la kupata familia bora ni lazima kuwa na ushirikiano wa kweli ambao utajenga tabia ya kuaminiana na kunai mamoja katika harakati hizi za kuandaa/ kujenga familia bora. UTARATIBU WA KAZI/MPANGILIO: Katika utaratibu wa maisha yake, pamoja na mpangilio mzuri wa mambo yanayomzunguka hii itakusaidia kuwa na muda mzuri wa kufanya shughuli zako na pia kutekeleza majukumu yako ya kila siku kama mwanamke shujaa. Hakuna njia yoyote ya kukuwezesha kukua na kuendelea katika maisha yako bila kuwa na utaratibu na mpangilio wa mambo yako. KUFANYA TATHIMINI: Kuweza kufanya tathimini ya yale yote anayoyafanya katika maisha yake ya kila siku, pengine ni mfanyabiashara, mfanyakazi, mkulima n.k kama mwanamke shujaa yakupasa kutathimini shughuli zako kama zina leta faida/hasara kwa familia na jamii yako inayokuzunguka. Ukiona faida ni kubwa unaendelea na hiyo shughuli lakini kama hasara ni kubwa unajiweka katika nafasi ya kubadilisha aina ya shughuli mara moja bila kupoteza wakati. ... Read More
MASWALI 60 YA KUMUULIZA MPENZI WAKO , YANAWEZA KUWA YA KUCHEKESHA& KUFURAHISHA:  Mawasiliano hujenga mahusiano mazuri, bila hivyo kutakuwa na tofauti fulani kati ya wawili wapendanao .watu wengi wanaamini kuwasiliana kunajenga uhusiano mzuri, hebu fikiria kama una rafiki yako mnaopendana hakutafuti hata kama umekuwa mbali kwa muda mrefu , si inaboa sana? nikupe mfano mmoja , wanandoa wakiwa pamoja nyumbani , siku hiyo wameamua wasiende mahali popote, unafikiri wangekalia kufanya tendo la ndoa siku nzima? jibu ni hapana. lakini wanakuwa na mawasiliano ya aina yake , Hapa nakuletea maswali unayotakiwa kumuuliza mpenzi wako mkiwa mko mmekaa jioni , au katika mapumziko yenu, lakini uwe makini hapa kuna wengine hawapendi umdadisi, ile kuna wengine ni waelewa na watakuelewa. mwanaume mwenye kukupenda atakuelewa. MASWALI YA KUMUULIZA KIJANA UMPENDAE. 1.Unakumbuka nini cha utotoni ambacho uliwahi kufanya? 2.kwenye hii tamthilia unampenda mwigizaji gani? 3.nafikiri nimepoteza namba yangu ya simu , naweza chukua ya kwako? 4.ni kipi kinachoweza kukufanya ucheke zaidi katika maisha yako? 5.kwa mfano wewe ungekuwa muhudumu ungechagua watu wa jinsia gani wa kuwahudumia ? 6.umewahi kutuma maombi ya urafiki kwa rafiki wa kike? 7.kabla ya mimi umewahi kuwa na nani? 8. je unaweza kukosa kitu unachokipenda kwa ajili yangu? 9.kama ukijikuta umeangukia kwa mwanamke , utaitumiaje hio siku wewe kama wewe? 10.wewe ni wangu? 11.unampenda nani? 12. unaamini kama kuna mungu? 13.unawezaje kumjua mtu kama ni rafiki wa kweli? 14.Unapenda kuwa smart au ni vyovyote tu? 15.je unweza kukaa na mtu usiempenda? 16.Unajisikiaje unapokuwa na mimi? 17. Utamjuaje mchumba wa kweli? 18.Unatafuta kitu gani kwa msichana? 19.Utajielezeaje wewe mwenyewe? 20.je, utaweza kunielezea mimi? 21.Kuna tatizo gani umewahi kukumbana nalo? 22.ni mzuri au ni mbaya? 23.umewahi kumwacha msichana? 24.umewahi kujihusisha na kitu chochote kibaya? 25.busu la kwanza kabisa ulimbusu nani? 26.ulifanikiwa? 27. Unapenda staili ipi ya mapenzi?kitandani. 28. Tamthilia ipi unaipenda? 29.Unapenda chakula gani? 30.unapenda rangi gani? 31.unapenda mziki gani ? 32.ukiwa mtoto ulikulia wapi? 33.Ulipendelea kucheza mchezo gani wakati wa utoto? 34. unashangilia timu gani ya mpira? 35.mwigizaji gani unamkubali sana duniani? 36. tamthilia ipi ni nzuri? 37.unawafurahia marafiki zangu? 38.unaipenda kazi yako? 39.unategemea kubadilisha nininkatika maisha yako? 40.Kuna kitu chochote ambacho huwa nakuudhi hata kama ni cha kijinga ambacho hujawahi kujaribu kuniambia? MASWALI MENGINE YA KINDANI ZAIDI YA KUULIZA UNAPOKUWA NA MTU ANAYEKUTHAMINI. 41.Ukipoteza nguvu zako wakati wa usiku , je ni kitu kipi utanieleza ili niridhike? 42.Ni sehemu gani ya mwili wangu , macho yako yakiona utashangaa kama hujawahi kuniona nikiwa uchi? 43.Umewahi kusikia mwili wangu ukinuka? 44.kama nakuhitaji, natupo pamoja wakati huo, unawezaje kunielewa, wengine husema unawezaje kunisoma,je unafikiri utajua dalili? 45.umewahi kuota uko na mwanamke ukifanya mapenzi? 46.umewahi kucheza kama dactari wakati wa utoto? 47. ni aina gani ya mapenzi ungependa kuwa nayo katika maisha yako? 48.Umewahi kufumwa ukiwa uchi? 49.je una uzoefu gani katika mahusiano? 50.unaweza kuniambia vitu vya kuchekesha ulivyofanya wakati wa utoto? 51.Kama ungetaka kubadili jinsia ni sehemu ipi ungependelea,na kwa nini? 52.Kuna siri yeyote hujaniambia? 53.UTU. je unafikiri umbo la mtu lina tatizo katika mahusiano? 54.tukipata watotro mimi na wewe ungependa watoto wetu wafuate tabia zetu? 55.unapenda staili ipi ya chini au ya juu? 56. umewahi kumpiga mtu kofi? 57.je wewe ni mkweli? 58.kitu gani unachokipenda ambacho hujawahi kuniambia? 60 .Nikimwangalia mwanaume mwingine na kumsifia utaudhika?je kuna tabia yeyote ya udanganyifu ambayo hujaipenda kwangu?unaweza kuacha kitu unachokipenda kwa kumsaidia rafiki? fuatilia maswali mengine mengi yatakuja. toa maoni yako katika maswali haya. ... Read More
NI JINSI GANI UNAMWOMBA MPENZIO MSAMAHA, JE NI KWA KUMPA ZAWADI? Msamaha una nafasi kubwa sana katika mapenzi. Hamna mtu aliyemkamilifu ndiyo maana neno samahani lipo. Ila neno hili linaweza kutumika sahihi au isiwe sahihi. Hivyo ni vizuri ukawa makini katika matumizi ya neno hili. Kuna baadhi ya watu hawawezi kabisa kutamka hilo neno na badala yake hutumia maneno yafuatayo (mbadala) kama ; yaishe,basi samahani,umeshinda,sorry(kama njia yakupunguza makali na wakati lugha iliyokua ikitumika ni kiswahili). Jinsi yakutumia samahani kiusahihi Unapotoa samahani kutoka katika kilindi cha moyo wako ina maana sana zaidi ya chochote. Samahani itumike tu pale unapotenda kosa moja kwa mara ya kwanza, hapo ni rahisi kusamehewa na kuaminiwa zaidi.Heshima, pendo na mapenzi yatakuwa kama awali na utaheshimika nakuonekana unajali. Hakikisha hauombi samahani zaidi ya mara moja kwa kosa moja ndo mana wanasema, “kosa sio kosa ila ukirudia kosa ndio kosa’’. Kama ulikua haufahamu ni vizuri ujifunze na ikiwezekana rudisha kumbukumbu zako katika matukio yanayohitaji msamaha kwenda kwa mpenzi wako na ulinganishe na hatua ulizozifanya. Kiri kosa ndiyo msamaha wako uweze kukubalika.Usiombe msamaha huku unasema lakinii…… ila……. Siamini kama haya yangetoa……… aina hizi za midokezo inapotumika katika kuomba msamaha ujue unataka kuonesha ulichokifanya sio kosa… Its simple, admit your mistake for the heartest forgiviness .Utapelekea upande wa pili (uliokosewa kukuamini tena na ni rahisi kusamehe na kusahau) tofauti na kuwa na maneno meeengi yakujitetea ilihali umetenda kosa. Sasa nije kwenye suala la zawadi, Jamani zawadi isiwe ndiyo silaha ya kudai msamaha. Zawadi inatumika wakati wowote kuimarisha mapenzi kwa kuonesha unamjali mwenzi wako nakumfanya ahisi faraja wakati wote na uwepo wake katika maisha yako. Epuka tabia ya kutoa sana zawadi wakati unamplease mpenzi wako.Kwa wakati mwingine utamjengea fikra za kosa pindi tu unapomletea zawadi. Hivyo asiifurahie ile zawadi na badala yake atakua na shauku kufahamu msamaha wa siku hiyo ni wa kitu gani au umetenda kosa gani tena. Wakati mwingine zawadi inapotumika katika kuomba msamaha itakua ni kama KUMBUKUMBU YA KOSA ulilomfanyia mwenzi wako, hivyo kumfanya akumbuke mara kwa mara kosa ulilolifanya. Kuwa makini sana katika njia za kuomba msamaha. Njia nzuri ya kuomba msamaha na ukubaliwe kwa upesi Kubali kosa pale ambapo umetenda,(note; Usikiri kosa kwa sababu tu unampenda na hutaki kumpoteza ,au hutaki malumbano. Ukifanya hivo ndo unaweza haribu uhusiano wako kabisa) Badili mazingira ya maongezi yaani tofauti na eneo la nyumbani/mlilozoea kukaa Omba msamaha wakati hasira zimepungua na ukiwa sio mlevi (hasa kwa wale wenye hasira au wanywaji wa pombe) Usilazimishe kusamehewa ,yaani mwenzako anapokua haridhii tumia njia nyingine mfano kumshirikisha mtu wenu wa karibu saana (kwa wote wawili) ila hapa uwe makini kwa sababu sio wote wanapenda siri zao za uhusiano kujulikana na wengine.Hapa itategemea na jinsi mlivyo Anayeomba msamaha ahakikishe sio mtu wa kukumbuka makosa ya mwenzie yaliyofanyika kipindi cha nyuma.Hapa na maanisha wale wenye tabia yakusamehe wenzao ila niwakukumbuka, endapo atakosewa kwa kitu kingine hata kwa bahati mbaya.Mfano akikosewa huwa ni mtu wakusema; ''hiyo ni kawaida yako'' that means anashikilia vitu moyoni.Itamuwia vigumu mwenzako kukubalia msamaha kwa urahisi, kutokana na tabia yakumshikilia bango kwa kumkumbusha yaliyopita endapo yeye atakukosea. Ni vizuri kujitahidi katika kufanya mambo mazuri kwenye uhusiano wako.Usitegemee zawadi kuwa ni kitu kizuri katika kuomba msamaha. Timiza malengo yako,jiheshimu,kuwa mwaminifu na kumthamini mwenzio na kumpenda kwa dhati. Bila kusahau kusikilizana na kufanya maamuzi kwa pamoja. ... Read More
📶happy birthday you my love 🆗#Najua_Umejifunza_mengi________Tanguu_umekuwa_mtoto_mpaka_now_umekuwaa😘😘😘😘 #____umejionea_mengi_hapa_dunian😧😧 ‼‼‼#___yasikutishe_coz_god_Yuwetu_sote😍😍 #__Amini_UHAI_tu_ndo_muimu_vingine_mapito_tuuu😧😧 #Happy_b_day____ ❇❇my.. Best ❇❇my.. Blood ❇❇rohoo.. Yang.. Kipenz... Changu ❔⁉⁉❔❔⁉MPAKA..Nasahau majina sijui nikuitajeee jamn rohoo ilizikeee 🎂🎁🎁🎂🎊🎊🎇🎉🎀🎂🎂🎂🎆 ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comments:
Mi natumia ya kupaka wakati unanifanyia usafi wa sehem z a sili nikajijeruhi me nikiendelea kupaka kuna máscara ikiingia nilipojichanja