'CHOMBEZO YA MAPENZI' 'INAITWA' 'NANII TAMU!?'. KUTOKA;DSM TZ EPISODE;06 Ilipoishia iliishia pale... Baba akiinhia ndani na mimi niliingia ndani kitendo cha kuingia na kushika simu yangu mara ilianza kuita mara kadhaa 'Davi, pokea hiyo simu kwani usikii inaita'?. Sasa endelea nayo.. Baba aliongea huku akionekana kuchukizwa na hicho cha kutokupokea simu, mawazo yalinitawala kichwani mwangu baada ya kuona jina la mtu ambaye nilijua wazi ni mlalamikaji, atanilalamikia kwa sana. Jina la suzi lilionekana kwenye screen ya simu yangu, 'Davi, nimekwambia uipokee hiyo simu haraka sana'. Safari hii Baba aliongea akiwa kama kachukizwa sana. Ilinibidi nijifanye naipokea kumbe nakata simu, na kweli niliweza kufanikiwa kufanya hivyo baada ya kukata simu. Suzi akupiga tena 'Sijui amekata simu maana nimejaribu kumpokea akuongea neno lolote lile'. Nilijiongelesha kwa Baba ili asiweze kuhisi kitu chochote mara nikiwa hapo najua kuwa nimemfunga kamba ya futi kumi na mbili lo!. Kumbe nilikuwa najisanganya kabisa. 'Naomba simu yako niitazame hiyo namba ambayo ilikuwa inakupigia'!?. Baba aliongea akiwa amenyoosha mkono wake, nilitetemeka sana baada ya kusikia kauli ya Baba ikiwa inahitaji simu yangu. 'Baba, devi yaani toka umekuja ujamiita mkeo uko sebuleni tu, kwani uko kumetokea nini!?'. Mama aliongea huku akiwa anajifunga khanga yake vizuri kiunoni. Kitendo cha mama kuja nilijihisi nafuu sana. Na kweli kwa jinsi nilivyokuwa nikitegemea ilikuwa hivyo, baada ya mamaangu kuja sebuleni Baba akufatilia tena mimi na simu yangu. Nilienda moja kwa moja hadi chumbani, baada ya kufika niliwasha simu yangu baada ya kuizima kipindi Baba anahitaji kuitazama. Ilipowaka nilikuta ujumbe ukiwa umetoka kwa suzi na mwingine ukiwa umetoka kwa Merry. Nilipokuta kuna ujumbe wa Merry, ilinibidi nianze kusoma wa Merry ujumbe wa Merry uliandikwa kwa maneno matatu tu na kwa herufi kubwa, yalikuwa yanasomeka hivi 'NAOMBA NANII YAKO'?. Ujumbe wa Merry ulikomea hapo, pasipo kuwepo na mwendelezo mwingine wowote ule wa ujumbe huo. 'Davi,davi!?'. Nikiwa bado niko nawaza la kufanya mara nilisikia sauti ikiinita kutoka sebuleni na ilikuwa sauti ya mamaangu. Nilitoka kwa haraka mpaka sebuleni 'Mwanangu vipi umeanza kubadilika mpaka Baba ako ameanza kukutilia mashaka kwaaasa ila keshokutwa unaenda shule kwamaana Baba ako kwasasa amehenda Benki kulipa na pia kununua vifaa vya shule ila mwanangu husiruhusu shetani akutawale umesikia mwanangu'. Mama aliongea huku akionekana mwenye simanzi kubwa usoni mwake. 'Ndio mama sitamruhusu shetani anitawale mimi mama na pia na nyie mniombee'. Ilinibidi na mimi nijitetee japo kwa mama. 'Mwanangu sisi tunakuombea ufanikiwe salama kwa ili'. Mama aliongea huku akiwa ananitazama kwa umakini wa hali ya juu sana. SIKU YA KWENDA SHULE. Siku ya kwenda shule iliwadia, nikiwa najipaka mafuta mara simu yangu iliita, nilipojaribu kuitazama nilifurahia sana baada ya kuona Merry akiwa ananipigia, niliipokea ile nataka kuongea mara mlango ulifunguliwa kwa ghafla sana. Nilizima simu yangu na kuiweka mfukoni. 'Mwanangu unafanya nini muda wote huo ujamaliza kuvaa na unajua kuwa mwisho wa kupokea wanafunzi ni saa kumi. 'Ndio mama nafahamu ila nilikuwa napanga vitu hivyo usiwe na shaka kwa hilo'. Nilimjibu mama huku nikiwa nakuja baadhi ya nguo zangu na kuziweka kwenye mtoma wangu. Mama alitoka kwenye chumba changu baada ya kutoka ilinibidi niwashe simu yangu. Kitendo cha kuwasha nilikuta sms nyingi zikiwa zimetoka kwa Merry. Nilifungua ya mwisho ili niweze kuisoma na kweli nilifanikiwa kuisoma na ilikuwa inasomeka hivi; 'USINIACHE NA PIA UKIFIKA BARABARANI UNIAMBIE NIJE NA MIMI NA PIA KUMBUKA OMBI LANGU'. Nilipomaliza kuisoma nilitabasamu kidogo na huku nikijing'ata kidole na kujisemea 'Huyu binti niwa kula tu maana ana kila sifa'. Nilijisemea nikiwa natoka chumbani kwangu huku nimeishaa nguo za sale za shule. Baada ya kutoka nje Mama na Baba walinisindikiza mpaka kwenye kituo cha magari. 'Hivi mtoto wa jirani yuko wapi ngoja nijaribu kumpigia jirani ili watoto waende wote'. Baba aliongea akiwa anabofyabofya simu yake. Kipindi anajaribu kupiga na mara wazazi wa Merry waliwa wameongozana na Merry walikuja mpaka kwenye kituo cha magari. Wazazi waliamkiana na mimi niliamkia wazazi wa Merry baada ya kuamkiana wazazi wote walitusii kusoma kwa bidii sana. Na mwisho wa maneno ni pale mwongeaji anapokuwa anaongea lakini hakuna mtu, hivyo umfanya kunyamaza tu na kufanana bubu. Ni pale baada ya kupanda gari wazazi wangu na wazazi wa Merry walinyea sana na kutuaga kwa imshara za mikono na sisi tuliwajibu kwa kuwaaga. Safari ilianza na Merry alikuwa pembeni yangu, tuliongea maneno ya hapa na pale mpaka tulipofika shule, baada ya kufika tulishuka kila mtu alibeba mzigo wake. Ilitubidi twende moja kwa moja katika ofisi ya mkuu wa shule baada ya kufika. Mkuu wa shule alitupokea kwa furaha sana na mara alipoga simu na watu wawili walikuja na mmoja akiwa ni mwanaume na mwingine mwanamke. Mwanaume alinibebea mtoma wangu na mwanamke alimbebea mtoma Merry. Baada ya kutoka nje kila mtu alifuata jinsia yake kwamaana kila mtu alipita njia yake. Mwanaume huyo alionekana si mwongeaji kabisa kwani hakuweza kuongea na mimi mpaka tulipofika kwenye dom la kulala. Alinionesha kitanda ambacho nitakuwa ninakitumia baada ya kunionesha alinishika mkono na kunipeleka moja kwa moja mpaka kwenye hospitali iliyokuwa karibu na hapo. Baada ya kuingia nilipimwa kila ugonjwa hakuna ugonjwa niliokuwa nao, japokuwq kwenye fomu yao, ilikuwa imeandikwa kuwa 'Yampasa mwanafunzi kuja shuleni akiwa amepima na pia asiwe na kasoro yoyote ile'. Hivyo ilionekana wazi kuwa wanahakiki watu. Baada ya kuonekana sina ugonjwa wowote ule nilipelekwa mpaka darasani, kitendo cha kufika darasani nilihisi aibu sana baada ya kwenda mbele ili nijitambulishe na darasa ilo lilionekana wazi kuwa na wasichana wengi na pia walionekana wazuri kuwatazama. Nilijitahidi kujitambulisha baada ya kumaliza yule mwanaume niliyekuwa nae aliondoka na kuniacha mbele. Na mara hiyohiyo aliingia mtu akionekana wazi kuwa ni mwalimu kwani alikuwa ameshika daftari mkononi mwake, baada ya kufika nilipokuwa alininyoshea kidole kuwa niende nikae sehemu fulani, Moyo ulidunda mara kadhaa pasipokuwa kawaida yake. JE; Ni kwanini moyo ulinidunda na pia Merry alikuwa wapi!?. Usikose kipande hata kimoja cha chombezo yetu ya NANII TAMU!?.

at 4:42 PM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top