Home → simulizi
→ RIWAYA: DAMU YA MWANANGU
SEHEMU YA TATU(03)
*****ILIPOISHIA******
wakati anaangaza angaza macho yake,,akashtuka kumuona Rube akiwa anachota mchanga na kuuweka katika mfuko wa plastiki!
Nyamwela akakumbuka kuwa mganga alimwambia Rube kuwa akishindwa kuwatoa wazazi wake kafara basi alete mchanga wa mtu yeypte ampendaye,,kwa upendo ulioshibana!
Nyamwela akahisi kuchanganyikiwa akapaza sauti,,"Rube unafanya nini hapo?
Rube akaufunga vyema mfuko uliokuwa na mchanga wa unyayo wa Nyamwela,,akaanza kutimua mbio,,,
Nyamwela akaacha kuingia ndani ya nyumba ya Muna akaanza kumkimbiza Rube!
*****ENDELEA*****
Rube alitimua mbio kama kafungwa mota miguuni,,,
alikimbia mfululizo hatimae akatokomea kabisa.
Nyamwela,,,akahisi kuchoka,,ni baada ya kukimbia umbali mrefu pasipo mafanikio ya kumpa Rube! akaamua kusimama akageuza shingo yake,,akatazama ule upande aliotoka,,, wazo likamjia kuwa awahi kule kwenye kijiji anachoishi kwa sasa.....
baada ya masaa kadhaa kupita akawa amefika katika kijiji hicho,,,akaamua kupitiliza mpaka nyumbani kwa Rube...lakini akakuta mlango wa nyumba ya Rube umefungwa kwa nje!
akaamua kumsubiri huenda akarudi...
alibaki hapo kwa masaa kadhaa,,,lakini hakuona dalili zozote za Rude kurudi kwake...
Nyamwela akaamua kurudi nyumbani kwake,,
asubuhi palipokucha Nyamwela akadamka mapema,, ili awahi nyumbani kwa Rube,,,lakini alipofika akaona bado mlango umefungwa kwa nje,,hata apaonyeshi dalili yoyote ya mtu kuwemo ndani ya nyumba!
Nyamwela akazidi kuchanganyikiwa ,,,wazo likamjia aende nyumbani kwake,,akachukue baiskeli akamtafute Rube kona zote za kijiji hicho...
Upande mwingine alionekana Rube akiwa,,, njiani kuelekea kwenye milima ya NZOKA kwa mganga kuupeleka mchanga wa unyayo wa nyamwela,, ghafla akasita,, akajisemea moyoni,,"hapa nilipo sina pesa ya kulipia kwa mganga,,,mbaya zaidi pesa zipo kule nyumbani kwangu,,,akaamua kurudi kule kijijini kwao.
wakati huo huo alionekana Nyamwela akiendelea kumtafuta Rube kwa udi na uvumba,,lakini hakufanikiwa kumpata akaamua kurudi nyumbani kwake...akiwa njiani wazo likamjia,,akajisemea moyoni,,"bila shaka Rube atakuwa kwa mganga wacha niwahi kabla mganga hajaanza kufanya kafala....
bila kuchelewa akapanda kwende baiskeli yake na safari ya kueleke milima ya Nzoka ikaanza.
alipofika kwa mganga,,akastaajabu kutokumkuta Rube,,,,akabaki mdomo wazi! akamuuliza mganga,,"yule rariki yangu ameshafika hapa?
mganga akajibu ,,"bado, pia mbona niliwapa masharti kuwa makafara hayo yatafanyika usiku wa manane,,,mnatakiwa mlete vitu hivyo ussiku huu wa leo,,kwa sababu leo ni jumatano,,au umesahau?
macho yakamtoka Nyamwela,,,akajisemea moyoni,,"nikifanya masihala nitatoleww mimi kafala,,,mbona huyu Rube ni mjinga kiasi hiki!
Nyamwela akaondoka bila kuaga,,,akapanda baiskeli yake akaondoka harakaharaka.
Upande mwingine alionekana Muma akiwa kambeba mwanae,,huku anapika kwenye jiko la kuni..wakati wote Muma alikuwa anaongea peke yake huku akicheka,,,utadhani kunamtu anaongea nae,,,Kumbe Muma huwa kunajambo la kimiujiza analiona mara kwa mara,,hata akiwa anaonge na kucheka peke yake,,wakati mwingine huongea maneno yasiyoeleweka ni kama lugha fulani,,,huwa anatokewa na mzimu wa Mama yake na mzimu huo huwa unaongea na Muna,,lakini jambo hilo hakuna mtu yeyote anayelijua....
baada ya kumaliza kupika akaingia ndani ya nyumba kumlaza mwanae.....
Upande mwingine alionekana Nyamwela akiwa anaendesha baiskeli yake kwa mwendo wa kasi mpaka watu wakawa wanamshangaa!
akiwa njiani akakutana uso kwa uso na Rube,,akiwa anaelekea kwa mganga! Rube akaanza kutimua mbio,,lakini kabla hajafika mbali,,, akakamatwa na Nyamwela....
Nyamwela akaaanza kurusha ngumi nyingi uwoni mwa Rube...kisha akamfunga kamba,,,huku akisisitiza Rube ampe ule mchanga wa unyayo wake!
Rube akakataa katakata akidai kuwa ule mchanga si wa unyayo wa mguu wa Nyamwela....
Nyamwela akaakasirika sana,,,akaamua kumfunga na kamba katika mti mmoja uliokuwa umezungukwa na kichaka kikubwa katika pori dogo akamchinja shingo! kisha akaondoka zake kuelekea nyumbani kwake,,alipofika nyumbani kwake,,akachimba kaburi,,kisha akaingia ndani ya nyumba yake kupumzika.
ilipofika usiku wa saa nne,,Namela akaandaa upanga wake...kisha akaelekea katika kijiji cha tatu,,kule nyumbani kwa Muna.
wakati huo Muna alikuwa kalala usingizi kando ya mtoto wake mchanga.
baada ya lisaa limoja kuoita nyamwela akawa kafika nje ya nyumba ya Muna,,,akavunja mlango na kuingia ndani ya nyumba ya Muna,,
Muna akashtuka kutoka usingizini! alipofumbua macho,,akastaajabu kumuona Nyamwela,,,
bila kuchelewa,Nyamwela akaanza kumshambulia Muna kwa kumkata na upanga aliokuwa kaushikilia mkononi!
alimkata mara nyingi sehemu ya kichwani mpaka Muna akafa papo hapo!
akachukua guni,,na kuweka maiti ya Muna ndani ya gunia hilo akalifunga vyema... akalivuruta na kulipeleka kwenye baiskeli yake,,,,ukiangalia kwa haraka haraka huwezi kugundua kuwa ni maiti,,unaweza kusema ni mzigo wa kawaida!
alipohakikisha kaiweka vyema maiti hiyo,,,akazipiga hatua kurudi ndani ya nyumba ya muna.
akamfuata mtoto wake mchanga aliyekuwa kalala usingizi juu ya kitanda akamchukua mtoto wake,,,akaangaza angaza macho yake akaona khanga..akaamua kuchukua khanga hiyo akamfunga mgongoni! akazipiga hatua kutoka nje ya chumba hicho,,ghafla akasikia hodi,,mtu anagonga mlango!
TAHARUKI!!!!!!!!!
ITAENDELEA..........
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: