RIWAYA: DAMU YA MWANANGU DAR ES SALAA SEHEMU YA NNE(04) *****ILIPOISHIA****** akachukua guni,,na kuweka maiti ya Muna ndani ya gunia hilo akalifunga vyema... akalivuruta na kulipeleka kwenye baiskeli yake,,,,ukiangalia kwa haraka haraka huwezi kugundua kuwa ni maiti,,unaweza kusema ni mzigo wa kawaida! alipohakikisha kaiweka vyema maiti hiyo,,,akazipiga hatua kurudi ndani ya nyumba ya muna. akamfuata mtoto wake mchanga aliyekuwa kalala usingizi juu ya kitanda akamchukua mtoto wake,,,akaangaza angaza macho yake akaona khanga..akaamua kuchukua khanga hiyo akamfunga mgongoni! akazipiga hatua kutoka nje ya chumba hicho,,ghafla akasikia hodi,,mtu anagonga mlango! TAHARUKI!!!!!!!!! ****ENDELEA**** Nyamwela akashtuka akaingiwa na wasiwasi,,,akasita kufungua mlango! akabaki kimya! mlango ukaendelea kugongwa mfululizo,,Nyamwela akaamua kufungua khanga aliyokuwa kaifunga mbeleko,,mgongoni,,,akamlaza mtoto kitandani,,kisha akaandaa upanga wake akazipiga hatua kuufuata mlango,akaufungua kisha akauliza kwa sauti ya upole,,"wewe ni nani? ikasikika sauti ikisema,," mimi ni daktari wa kitengo cha wagonjwa wa akili....nimekuja kutazama maendeleo ya mwanamke anayeitwa Muna,,,katika kumbukumbu zangu alikuwa anaishi katika nyumba hii... Nyamwela akajibu kwa sauti ya ukali,,"hapa hakuna kichaa wala chizi,,wote tunaoishi humu ndani tunaakili zetu timamu,,,huenda mtu huyo alihama hapa. baada ya Nyamwela kusema maneno hayo,,yule daktari akaondoka zake... Nyamwela akaendelea kumtazama daktari huyo mpaka akaishilizia.. akaamua kurudi ndani ya nyumba akamchukua mtoto akamfunga mgongoni,,akatoka nje ya nyumba akafunga mlango huo,,akapanda kwenye baiskeli yake akaelekea kijiji cha tatu kule napoishi... baada ya lisaa limoja akawa amefika,,,akashushu gunia lililokuwa na maiti ya muna,,akalivuruta gunia hilo na kuliingiza ndani ya nyumba yake,,akachukua jembe akatokanalo nje ya nyumba,,,kisha akarudi ndani ya nyumba,,,,akamlaza mwanae juu yameza ya mbao,,,akachukua upanga wake akamchinja bila huruma,,kisha akanza kukata viungo vya mwili wa mtoto wake,,ikiwemo mikono na miguu,,kisha akavikusanya na kuviweka kwenye mfuko wa plastiki, akabeba maiti ya mwanae kisha akatoka nje ya nyumba...akarusha maiti hiyo ndani ya lile kaburi alilolichimba nyuma ya nyumba yake,,,,akavuruta maiti ya Muna akaitumbukiza ndani ya shimo,,,kisha akachukua jembe na kuanza kufukia shimo hilo. alipomaliza akarudi ndani kwake asubirie muda ufike aianze safari ya kuelekea kwa mganga,,kupeleka viungo vya mwili wa mwanae.,,,, akaamua kujilaza kitandani,,,,kutokana na uchovu aliokuwanao akajikuta analala masaa mengi,,, aliposhtuka kutoka usingizini,,akatazama saa yake ya mkononi,,akastaajabu kuona ni saa nane kasoro za usiku! akachukua ule mfuko wa plastiki uliokuwa na viungo vya mwili wa mtoto wake,,akazipiga hatua za harakaharaka akatoka nje ya nyumba,, akapanda juu ya baiskeli yake na safari ya kuelekea kwa mganga ikaanza... Nyamwela aliendesha baiskeli yake kwa kasi ya ajabu....hatimae akafika kwenye milima ya Nzoka,,ambapo anapatikana mganga matata.. akatazama saa yake ya mkononi,,ilikuwa ni saa kumi na moja kasoro,,macho yakamtoka,,,akaiacha baiskeli na kuanza kutimua mbio,,huku kashikilia ule mfuko wa plastiki. Alipokaribia eneo la ngome ya mganga huyo,,ghafla ikasikika sauti ikimwambia,,"umechelewa,,huu sio muda wa kufanya kafara,,,rudi ulipotoka! Sauti hiyo ilimshtua Nyamwela,,kwa sababu ilikuwa inatisha kwa mngurumo kama radi,,pasipo kuonekana anayeongea maneno hayo! Nyamwela akautupa ule mfuko akaanza kutimua mbio mpaka kule alipokuwa kaiacha baiskeli yake,,, akaichukua na kuiendesha kwa kasi ya ajabu!!! hatimae akafika nyumbani kwake! akafungua mlango na kuingia ndani,,,,akaiegesha baiskeli yake akazipiga hatua kukifuata kitanda akajilaza,,, baada ya sekunde kadhaa kupita akahisi harufu ya damu ikinuka ndani ya nyumba yake,,,akasema,,"mi ni mjinga kiasi gani? yani nimesahau kufuta zile damu juu ya meza,,pale nilipomchinjia mwanangu! wacha niifanye kazi hiyo sasahivi. Nyamwela akanyanyuka kitandani akawasha koroboi,,akaanza kufuta damu hiyo!! hatimae meza ikawa safi!! akazima koroboi akajilaza kitandani,, baada ya dakika kadhaa kupita,,akahisi tena harufu ya damu ikinuka zaidi ya mwanzo!! akanyanyuka kitandani na kuwasha korobi,,akaangaza angaza macho yake hakuona kitu chochote....akazima koroboi hiyo,,kisha akarudi kitandani,,, harufu ya damu ilizidi kuongezeka kila baada ya dakika kadhaa!! Nyamwela akaanza kuingiwa na wasiwasi!!! hofu ikatawala juu yake,,akaanza kuogopa! wakati anatafakari nini cha kufanya,,gafla kikasikika kishindo cha kitu kizito kudondoka kule nyuma ya nyumba yake!! ni ile sehemu ya kabuli alilomzika Muna pamoja na mwanae.. akachukua koroboi akaiwasha kisha akatoka nje kuelekea kule nyuma ya nyumba,, aone je? ni kitu gani kimedondoka! alipofika akamulika kwenye lile kaburi,,,akashtuka! macho yakamtoka ,,alipotazama juu ya kaburi hilo,,akaona ule mfuko alioutupa kule kwenye milima ya Nzoka,,uliokuwa na viungo vya mwili wa mwanae,,,ukiwa juu ya kaburi hilo!! akatupa koroboi na kutimua mbio akarudi ndani ya nyumba yake,,,akafunga mlango! punde si punde akasikia kishindo cha kitu kikitua juu ya meza!!!! alipotazama kwa makini akaona ni uleule mfuko!!! akafungua mlango haraka akatimua mbio,,,,kabla hajafika mbali,,mara ghafla!! KIZAAZAA!!!!!! ITAENDELEA.......... Tutaendelea usiku sehemu ya tano

at 3:51 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top